Msemo wa (Hakuna Dini kwenye Siasa,...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msemo wa (Hakuna Dini kwenye Siasa, wala hakuna siasa kwenye dini)

Question

Je! Msemo wa (Hakuna Dini kwenye Siana, wala hakuna siasa kwenye dini) ni sahihi?

Answer

Ikiwa tunazungumzia katika kazi za kisiasa za kichama, basi msemo huu ni sahihi, na ni wajibu kwa vyama vya kisiasa kuondoa nembo za kidini katika programu zao za kampeni ambazo wanajipamba nazo dhidi ya vyama vingine, na kinyume na hivyo, basi hilo linakuwa ni aina miongoni mwa aina ya kuitumia Dini ya Mwenyezi Mungu kibiashara na kuvituhumu vyama vingine, na kusababisha fitina katika jamii. Na hapa ndipo yalipofikia makundi ya itikadi kali ambayo yemeingia katika maisha ya kisiasa. Ni wajibu kwa mtu wa dini kujiweka mbali na siasa kwa maana yake ya siasa ya kichama ili iwe milki ya wote, na ajishughulishe na kuwafundisha watu misingi ya juu katika nyanja mbalimbali ili kufikia masilahi yanayotarajiwa kwake kama Mwanzuoni wa sharia.

Ama siasa kwa maana yake kiujumla, ikiwa na maana ya kusimamia mambo ya nchi ndani na nje, kwa maana hii haijuzu kuitenganisha na Dini, Dini ipo pamoja nayo katika njia moja, Dini na siasa vinafanya kazi ili kufanikisha lengo moja. Pia misingi ya kisheria inawakilisha siasa- kwa maana hii- ambayo haijuzu kuikengeuka katika kazi, sawasawa kazi za kisharia au kijamii au nyinginezo.

Share this:

Related Fatwas