Umaarufu na Udhibiti wake

Egypt's Dar Al-Ifta

Umaarufu na Udhibiti wake

Question

Je! Ni ipi hukumu ya umaarufu? Na ni upi udhibiti wake? Na je, kuna moja kati ya aina zake iliyo mbaya zaidi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na Maswahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu;
Umaarufu ni kjulikana sana; ni sawa na umashuhuri [Qamus Al-Muhiit uk. 412, Muasaatur Risalah].
Ibn Mandhur alisema: [Lisaan Al-Arab, 4/332, Kidahizo cha SH H R]: “Ash-Shuhrah (Umaarufu) ni: kujitokeza kwa kitu kinachojulikana ili watu wakieneze. Al-Jawahri alisema: umaarufu ni uwazi wa jambo, na Ash-Shahr ni: mwezi. Umaarufu ulipewa jina hilo kwa sababu ya umaarufu wake na kuonekana kwake. Az-Zajaj alisema, Ash-Shahr ni (mwezi): Umaarufu ulipewa jina hilo kwa sababu ya kujulikana na kuonekana kwake.”
Na umaarufu, ukitokea kwa mtu kuuomba, basi ni jambo linalochukiza. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bayhaqi katika Ash-Shuab kutoka kwa Anas – R.A - kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu – S.A.W -, alisema: (Imetosha kwa mtu kuhesabika kuwa ni mja wa shari pale ambapo watu humwashiria kwa vidole kwenye dini yake na dunia yake isipokuwa aliyelindwa na Mwenyezi Mungu tu.) Imepokelewa pia kutoka kwa Al-Bayhaqi na At-Tabarani kutoka kwa Abu Hurayra R.A kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: “Imetosha kwa mtu kuhesabika kuwa ni mja wa shari isipokuwa aliyelindwa na Mwenyezi Mungu tu kutokana na ubaya pale ambapo watu humwashiria kwa vidole kwenye dini yake na dunia yake.”. Watu wema waliotangulia walikuwa wakichukia kuutaka umaarufu kwa kuuomba. Ayoub Al-Sukhtiani alisema: “Naapa kwa Allah, hakuna mja aliye mkweli kwa Mwenyezi Mungu na akapenda umaarufu.” Ishaq Ibn Banan alisema, kwamba Ahmed alisema: “Nilimsikia akisema - ninamaanisha Bishran:- Ibrahim Ibn Adham alisema: Mwenyezi Mungu hufurahihswa na mja asiyependa umaarufu.”
Ikiwa umaarufu unatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu sio kwa mtu kuuomba kwa Watu kwa ajili ya kueneza dini yake basi hilo ni jambo zuri.
Abu Hamid Al-Ghazali alisema katika kitabu chake [Al-Ihyaa, 10/1830, Dar Al-Shaab]: “Ujue Mwenyezi Mungu akuongoze kuwa asili ya ufahari ni kuenea kwa sifa na umaarufu, na jambo hili ni baya, lakini jambo zuri ni hali ya kutokuwa na umashuhuri, isipokuwa aliyejulikana kwa ajili ya kueneza dini yake bila ya kuutafuta umaarufu.”
Kisha akasema: “Lakini kile kinachohitajika kwa umaarufu na kuenea kwa sifa ni hadhi katika mioyo, na upendo wa ufahari ndio asili ya ufisadi wote, kama ukisema kwa mfano: Ni sifa gani inayozidi kuliko umaarufu wa manabii na makhalifa na maimamu katika wanavyuoni, namna gani walikosa fadhila ya kutokuwa na umaarufu. Ujue kwamba jambo baya ni kuomba na kuusaka umaarufu, lakini kuwepo kwake pasipo mtu kuuomba kwa Watu ni jambo lisilo baya. Ndiyo kuna fitna juu ya watu ambao ni dhaifu sio wenye nguvu nao ni kama mwenye kuzama ambaye ni dhaifu akiwa pamoja na watu wenye kuzama, ni bora kwake iwe kwamba hakuna yeyote kati yao anayemjua, kwani watamkamata na ataangamia pamoja nao, lakini kwa mwenye nguvu ni bora kwake kuwajua wenye kuzama ili wamkamate na atawaokoa kisha atalipwa thawabu kwa kazi hii.
Al-Khademi Al-Hanafi alisema baada ya Hadithi ya Anas [Bariqah Mahmoudiyah fi Sharhi Tariqah Muhammadiyah, 2/52, Al-Halabi]: “Kwa hivyo, umaarufu ulikuwa janga, ama kuhusu dini ni kuwa kwake chanzo cha mafano wa mshangao huo, na kutegemea kazi na unafiki nao ni chombo cha ukusanyaji wa ulimwengu. imesemekana kuwa: Umaarufu katika dini ni kufanya uzushi mkubwa kwa siri, lakini kuhusu umaarufu katika dunia ni chanzo cha udhalimu, kiburi na kuacha kutii na kuyaongeza malengo ya kidunia.”
Kwa hivyo, mtu kuuomba na kuusaka umaarufu kwa nafsi yake ni jambo baya na inachukiza kile kinachopelekea ombi hili pia. na kama hakuuomba umaarufu kama akivaa mavazi ya umaarufu, au mavazi yanayojulikana kwa watu na anaashiriwa kwa vidole, imepokelewa kutoka kwa Al-Bayhaqi kutoka kwa Abu Huraira – R.A.- akasema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu. S.A.W. ameukataza umaarufu maradufu akaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je! umaarufu maradufu ni upi? Akasema: “Ni kuvaa Nguo nyembamba inayoonesha rangi ya mwili, unene, ulaini, ukali, urefu na ufupi wa mwili wa mtu, lakini hata kama ni moja kati ya hizo hali zote.” Na imepokelewa kutoka kwa Abu Dawood kutoka kwa Ibn Omar – R.A. – alisema kuwa: “Yeyote aliyevaa mavazi ya umaarufu Mwenyezi Mungu atamvalisha mavazi ya fedheha Siku ya Kiyama.”
Al-Bhuti Al-Hanbali alisema katika kitabu cha [Kashaf Al-Qinaa, 1/278, Dar Al-Fikr]: “Inachukiza kuvaa nguo inayojulikana yaani ambayo ina umaarufu kwa watu, na kuashiriwa kwa vidole, ili isiwe sababu ya kuwapelekea watu kumsengenya mtu, akawashirikisha Watu hao dhambi ya kusengenya. Na miongoni mwa mavazi ya umaarufu ni mtu kuyageuza mavazi yake ya kawaida, kama vile kuvaa mavazi ya juu au kugeuzwa, kama wanavyofanya baadhi ya watu waovu. Al-Hassan alikuwa akisema: Hakika watu walifanya unyenyekevu wao katika mavazi, na wakajitambulisha kwa kuvaa nguo za sufi, hata akiwa mmoja wao ni mwenye kiburi kwa kuvaa nguo za sufi zaidi kuliko anayevaa nguo za anasa. Ibn Rushd alisema: elimu ilikuwa ndani ya mioyo ya watu lakini ilikuwa katika ngozi za kondoo. Pia inachukiza kuvaa vinginevyo kinyume na mavazi ya wenyeji; kwa sababu ni mavazi ya umaarufu. Kama mtu akikusudia kuonyesha unyenyekevu basi mavazi haya ni haramu kwa sababu hali hii ni unafiki.”
Miongoni mwa udhibiti wa umaarufu ni kuwa na maadili na tabia nzuri, kwa sababu mtu maarufu ni mfano wa kuigwa na hairuhusiwi kwake kushuka kwa kiwango cha watu wa kawaida ili asiwafitini watu katika dini yao.
Umaarufu mbaya ni ule unaoombwa kwa ajili ya yeyote asiye Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya ufahari na sifa tu, imepokelewa kutoka kwa Al-Bayhaqi na At-Tabarani (R.A) walisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (S.A.W.) anasema: “Yeyote anayejionesha watu kwa kazi yao Mwenyezi Mungu atamwonesha thawabu ya kazi hii kisha atamzuia thawabu hiyo, na mwenye kuuomba umaarufu Mwenyezi Mungu atawajulisha watu ubaya wake”'. Ni bora zaidi kutoomba umaarufu kabisa, lakini mtu anaombwa kwa umaarufu. Abu Hamid Al-Ghazali alisema katika kitabu cha [Ihyaa Ulumud Din, 10/1830, Dar Al-Shaab]: “Jambo zuri ni kutokuwa na umaarufu, isipokuwa wale ambao wanajulikana kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kueneza dini yake bila ya kuuomba umaarufu.”
Hali hii haipingani na kuonesha mtu haki mbele ya watu au kikundi au vinginevyo, hata ikiwa hali hii inamsababishia umaarufu, kwa sharti asikusudie kwa maneno yake umaarufu wowote, au kutaka ufahari, au sifa, umaarufu hapa sio kawaida na haukusudiwi wala hauhitajiki wala anautamani.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu: hali ya kuuomba na kuutaka umaarufu ni jambo baya, na hii haiyazuii mambo halali, lakini inawezekana kwa umaarufu ukawa jambo la lazima au la kuhitajika, kama vile kuionesha haki pasipo na kutarajia umaarufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas