Kuhukumu kwa Kutumia Sheria za Kutu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhukumu kwa Kutumia Sheria za Kutunga.

Question

Je, inafaa kwa Mwislamu kuhukumu kwa kutumia sheria za kutengenezwa kama vile sheria za kutunga?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Maana ya kuhukumu kwa upande wa lugha: Ni mtu kupewa jukumu la kutoa hukumu, na kwa upande wa sheria : Ni wagomvi wawili kumpa mtu wanayemridhia jukumu la hukumu katika yale wanayogombania ili kumaliza mzozo na madai yao (Kitabu cha Durar Al-Hukkam, 4/578, mada ya 1790, Ch. Dar Al-Jeel).
Na neno hukumu asili yake ni kuzuia, kwa mfano inasemwa: Amehukumiwa kwa hukumu fulani, maana yake: amezuiliwa na hakuweza kutoka katika hilo.
Amasema Ibn Faris katika vipimo vya lugha, [2/91, Ch. Dar Al-Fikr]: Herufi ya Ha, Kaf na Mim ni asili moja nayo ni kuzuia kutokana na dhuluma.
Katika kitabu cha [Mukhtar As-Sih-hah, 1/78, Ch. Maktabat Al-Asriah]: Amehukumu mtu katika mali yake, pindi anapoitolea hukumu, na kuhukumiwa katika hilo, na kutakiwa kutolewa hukumu kwa hakimu kwa maana wakahukumiana, na usikilizwaji wa kesi ya wagombanao kwa hakimu.
Hakuna tofauti sana ya maana ya kisamiati na maana ya kilugha, angalia kitabu cha: [Al-Bahri Al-Raaiq, sherhe ya Kanz Daqaaiq, 7/24, Ch. Dar Al-Kitab El-Islamiy], na kitabu cha: [Tabsirat Al-Hukkam cha Ibn Farhuon, 1/62, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Katika gazeti la hukumu za uadlifu kipengele 1790 kinasema: Kutoa hukumu ni ibara ya hatua ya wagomvi wawili kumfanya mtu mwengine kuwa ni hakimu kwa ridhaa yao ili kuondoa ugomvi wao na madai yao, Kitabu cha: [Durar Al-Hukkam sherehe gazeti la hukumu, 4/578 Ch. Dar Al-Jeel].
Kuhukumu kwa kufuata kanuni au kuhukumu kwa kanuni hizo maana yake ni kutoa usimamizi kwa atakaye hukumu kesi ya kumaliza ugomvi na mvutano na pande husika kuwajibika.
Neno kanuni kwa asili si neno la Kiarabu, na kusudio lake katika misamiati ya kisiasa na kimahakama pamoja na viongozi wa nchi: “Ni mkusanyiko wa sheria ambazo zinasimamia mwenendo wa watu ndani ya jamii ambapo kila mtu anapaswa kuzifuata kwa hiyari au kwa nguvu, na wakati wowote mtu akipinga kuzifuata na kuzitii, basi nchi itamlazimisha kuziheshimu” kitabu cha: [Utangulizi wa sayansi ya sheria cha Dkt. Taufiq Faraj, uk. 15].
Na sheria za kuwekwa inamaanisha kuwa mwanzo wake unategemea zaidi fikra ya mwanadamu, hivyo ni katika vitu vinavyowekwa na mwanadamu na kuvitengeneza, ambapo mwekaje wake anaweza kuwa na mtazamo unaokwenda sawa na maumbile safi ya mwanadamu au kukubaliana na nadharia za Dini za mbinguni, hivyo hizo sheria haziwi ni moja kwa moja au kufanya kazi muda wote sehemu yoyote wala kwa mtu kila mtu, lakini ufanisi wake ni kiwango na mabadiliko kwa mujibu wa maendeleo ya jamii na asasi zake.
Maelezo yaliyopita yameweka wazi kuwa si katika sharti za sheria za kuwekwa kuwa zinapingana na Sheria au kukubaliana, isipokuwa wakati mwengine huwa zinakubaliana au kutokubaliana kwa ujumla wake au sehemu sawa na kukubaliana kwa jamii kwa makundi yake yaliyopewa jukumu la kuweka sheria na kutengeneza mada zake na vipengele vyake.
Kazi za uanzishaji sheria na kuzipitisha kwa pande maalumu husika ndani ya nchi hukubaliana kisheria kuwa ni kazi ya kuanzisha mikataba kati ya pande za watu wanaozingatiwa ambao ni viongozi na wanaoongozwa au mamlaka iliyochaguliwa na wananchi, kwani wananchi ndio wanaochagua mamlaka hiyo ili iwe wakili wake katika kulinda na kudhibiti mahusiano ya jamii kupitia utengenezaji wa sheria na utekelezaji wake, na asili katika makubaliano ni halali ikiwa tu haipingani na Sheria katika kuhalalisha haramu au kuharamisha halali, na kwa maelezo haya katika wigo wa makubaliano wamesema wanachuoni kama vile Ahmad na Malik pamoja na Ibn Taimiyah na Ibn Al-Qayyim na wengine, amesema Ibn Taimiyah baada ya kutaja tofauti za wanachuoni katika asili hii [“Kitabu cha mkusanyiko wa fatwa 29/132 Ch. Taasisi ya Mfalme Fahd]: “kauli ya pili: Ni kuwa asili katika makubaliano na masharti ni kufaa na kuwa sahihi, wala haiharamishwi lakini hubatilishwa kile kitakachooneshwa na Sheria juu ya uharamu wake na kubatilishwa kwake kwa tamko la wazi au la kipimo kwa yule anayesema hilo, na asili inayotamkwa kwa upande wa Imamu Ahmad mara nyingi hukabaliana na kauli hii, na Imamu Malik yupo karibu na hilo lakini Imamu Ahmad ni mwingi wa marekebisho ya masharti wala hakuna kwa wanachuoni wote wanne mwenye kufanya marekebisho mengi ya masharti zaidi ya Imamu Ahmad...”.
Kisha akasema [29/137–138]: “Na katika hili wapo waliosema: sharti hili linakwenda kinyume na mahitaji ya makubaliano. Akaulizwa: Ni kuwa inakwenda kinyume tu na makubaliano au kwenda kinyume moja kwa moja, ikiwa anakusudia sura ya kwanza: basi ni sharti zote ipo hivyo. Ikiwa anakusudia sura ya pili: hakufuata isipokuwa ni kuharamisha kutokubaliana makusudio ya makubaliano kama kuweka sharti ya talaka katika ndoa au kuweka sharti la kuvunja makubaliano. Ima ikiwa kutakuwa na sharti linalokusudia makubaliano, basi inakuwa haijapingana na makusudio yake, kauli hii ni sahihi kwa dalili ya Qur'ani na Hadithi pamoja na kauli za wanachuoni na kutokuwepo kwa dalili inayopingana nayo.
Anasema Ibn Al-Qayyim ndani ya kitabu cha: [Ilamul Waqqin, 1/259, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: ikiwa ni kuunga mkono mtazamo huu: “Kosa lao la nne: Ni kuamini kwao kuwa makubaliano ya Waislamu na masharti yao pamoja na mashirikiano yao vyote hivyo vipo kwenye ubatilifu mpaka pale itakapokuwepo dalili ya usahihi, na kwao ikiwa hakuna dalili ya kufaa kwa sharti au makubaliano au mashirikiano hufungamanishwa na ubatilifu wake, kwa mtazamo huo wamebatilisha mambo mengi ya mashirikiano ya watu na mikataba yao pamoja na sharti zao pasi na dalili yoyote toka kwa Mwenyezi Mungu ni kutokana tu na kufanyia kazi msingi huu, na jopo la wanachuoni wapo tofauti na mitazamo hii, na kuwa asili katika mikataba na makubaliano pamoja na masharti ni usahihi isipokuwa yale yaliyobatilishwa na Sheria au kukatazwa, kauli hii ndio kauli sahihi, kwani hukumu ya kubatilika kwake ni hukumu ya kuharamisha na kumfanya mtu kupata dhambi, kinachofahamika ni kuwa hakuna kilicho haramu isipokuwa ni kile kilichoharamishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na Mtume wake, wala hakuna dhambi isipokuwa lile kilichotiwa dhambi na Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume wake kwa mtendaji wa jambo hilo, kama vile hakuna la lazima isipokuwa ni lile lilifanywa lazima na Mwenyezi Mungu, wala hakuna lililo haramu isipokuwa lililoharamishwa na Mwenyezi Mungu, wala hakuna dini isipokuwa ni ile iliyowekewa Sheria na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani asili katika ibada ni kuwa batili mpaka pale panapokuwa na dalili ya amri ya ibada hiyo, na asili katika mikataba na makubaliano pamoja na mashirikiano ni uhalali mpaka pale panapokuwa na dalili ya kubatilika au uharamu wa makubaliano na mashirikiano hayo....
Ama kwa upande wa makubaliano na masharti pamoja na mashirikiano ni vitu vilivyo na msamaha kufanzika kwake mpaka pale Sheria inapoharamisha, na kwa haya Mwenyezi Mungu Amewakemea washirikina kwa kwenda kinyume na asili hizi mbili nazo ni kuharamisha yasiyoharamishwa na Mwenyezi Mungu na kujiweka kwao karibu na Mwenyezi Mungu kwa mfumo usiowekwa na Sheria zake, naye Mwenyezi Mungu lau Angenyamazia uhalali wa hayo na uharamu wake basi hayo yangekuwa ni katika mambo yaliyosamehewa hivyo haifai kuyaletea hukumu ya kuharamishwa kwake na kubatilika kwake”.
Na inaonesha kuwa hakika asili ni usahihi na kufaa katika kila kisichopingana na Sheria ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na mikataba na makubaliano pia na kanuni au sheria zilizowekwa kwenye jamii, ni kutokana na Hadithi iliyopokelewa na Imamu Tirmidhiy na Ibn Majah katoka kwa Salman Al-Farisy R.A. amesema: “Siku moja aliulizwa Mtume S.A.W. kuhusu samli jibini na ngozi za kusimbikwa Mtume S.A.W. akasema: Halali ni ile iliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu ndani Kitabu chake na haramu ni iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu chake, na aliyoyanyamazia, basi hayo ni katika aliyoyasamehe”.
Kutoka kwa Tabaraniy Hadithi inayotokana na Abu Ad-Dardai kutoka kwa Mtume S.A.W. kuwa amesema: “Alichokihalalisha Mwenyezi Mungu hicho ni halali, Alichokiharamisha, basi hicho ni haramu, na Alichokinyamazia, basi hicho ni msamaha, hivyo pokeeni msamaha utokao kwa Mwenyezi Mungu kwani Mwenyezi Mungu hakuwa ni mwenye kusahau chochote” ameipitisha Hadithi hii As-Seyutwiy ndani ya kitabu cha: [Al-Ash-bah wa An-Nadhair, uk. 60, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kutokana na maelezo hayo inaonesha wazi kuwa inafaa kutumia sheria zilizotungwa katika kutolea hukumu katika yale yasiyopingana na Sheria ya Kiislamu kwa kuzingatia kuwa sheria hizo ni mikataba au makubaliano yaliyotengenezwa ili kulinda masilahi ya kijamii, kutokana na yale yaliyoteuliwa na baadhi ya wanachuoni kuwa hakika asili ya makubaliano ni sahihi na kufaa isipokuwa kitakachooneshwa na Sheria juu ya ubatili wake na kuharamishwa kwake.
Na kuhusu hukumu za sheria za kutunga zenyewe wakati mwengine hupelekea kutokea mvutano kati ya nchi mbalimbali kwa mfano mivutano ya ardhi maji petrol ya vinavyofanana na hivyo, basi watu hukimbilia kwenye sheria hizo za kimataifa ambazo zina kanuni zake zisizotokana na Sheria za Kiislamu.
Na sheria ambazo zinalinda uhusiano wa Waislamu na wasiokuwa Waislamu wakati wa amani na hata wakati wa vita huitwa na wanachuoni wa wazamani kwa jina la Seer, wanachuoni wa sasa wakaziita sheria za kutunga.
Na hukumu katika musuala ya kuwa ikiwa sheria za kimataifa katika masuala haya hazipingani na Sheria hasa katika yale yanayofungamana na utu na heshima, bali ni masuala ya kifedha kama tulivyotolea mfano, ni kuwa hakuna ubaya wa sheria hizo katika hali hii, kwa sababu Waislamu hawaishi peke yao mbali kabisa na ulimwengu, hivyo ni lazima kwao kushirikiana na wenzao wasio kuwa Waislamu katika yale yanayopelekea kukubaliana na kutofautiana kama ilivyo kawaida kati ya watu, ikiwa kila kundi halikubaliana na utashi wa kundi lengine au kukubaliana na sheria zake au mtazamo wa mwenzake katika kadhia basi ni lazima kutumika hukumu za atakayeondoa mvutano huu, wala hakuna sharti katika makubaliano haya kuwa msingi wake unatokana na Sheria , bali ni kuwa sawa na vile aonavyo kiongozi miongoni mwa masilahi ya Waislamu.
Miongoni mwa dalili ya hayo ndani ya Qur'ani Tukufu ni kauli ya Mola Mtukufu:
{Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmehirimia Hija. Na miongoni mwenu atakayemuuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu}[AL MAIDAH, 95].
Sura ya dalili ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Amefanya kitendo cha kuwinda wanyama kinarejeshwa kwenye hukumu ya jitihada katika mambo ya kuwinda wanyama hali ya kuhirimia hija, imejengwa hoja kwa Aya hii juu ya kuleta hukumu kati ya Ally na Muawiyah pindi kundi la Khawarij walipoleta mjadala.
Vile vile kauli ya Mola Mtukufu: {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari} [AN NISAA, 35].
Amesema Al-Qurtwubiy: “Katika Aya hii kuna dalili ya kuthibiti kutolewa hukumu na sio kama wanavyosema kundi la Khwarij: ni kuwa hakuna hukumu inayotoka zaidi ya kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, neno hili ni haki lakini wanakusudia ndani yake batili”. [Kitabu Al-Jamii Ahkam Al-Quran cha Imamu Al-Qurtubiy, 5/179 Ch. Dar Al-Kutub Al-Masriya]
Miongoni mwa dalili ya hilo katika Hadithi ya Mtume S.A.W.
Ni kuchunga kwake Mtume S.A.W. mambo yanayokubalika kwenye nchi mbalimbali ya kutouwa Mitume au kuwafunga, kutoka kwa Abi Rafii amesema: “Makuraishi walinituma kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. nilipomwona Mtume S.A.W. moyo wangu ukawa na hamu ya Uislamu, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika yangu sitorudi kabisa kwao. Akasema: Hakika yangu sivunji makubaliano wala kumkamata mjumbe aliyetumwa, isipokuwa rudi ikiwa ndani ya nafsi yako yapo uliyonayo hivi sasa ndani ya ndani ya nafsi yako basi rudi. Akasema: basi nikarudi, kisha nikaenda kwa Mtume S.A.W. na nikasilimu”. Imepokelewa na Abu Dawud.
Amesema Al-Qurtwubiy: “Kusudio la ahadi hapa ni yale mambo ya kawadia yanayofanyika na kufahamika kati ya watu kuwa Mitume hawapaswi kupatwa na mambo yanayochukiza na kauli ya Mtume S.A.W. inayaonesha haya katika Hadithi ifuatayo: “Ama naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wajumbe hawauwawi...... ni hadithi” kitabu cha: [Mirkat Al-Mafatih sherehe ya Mishkat Al-Masabih, 6/2564 Ch. Dar Al-Fikr].
Kutoka kwa Naeem Ibn Msoud amesema kuwa Mtume S.A.W. aliwaambia watu wawili ambao walikuja kwa Musailamah: “Ama naapa kwa Mwenyezi Mungu lau wajumbe wangekuwa wanauwawa basi ningewakata shingo zenu”. Imepokelewa na Ahmad pamoja na Abu Dawud.
Kutoka kwa Abi Said Al-Khudhriy R.A. amesema: “Pindi ilipoteremka kwa watu wa Quraidhah hukumu ya Saad Ibn Muadh, Mtume S.A.W. alimtuma na alikuwa yupo karibu naye sana basi akaja akiwa amepanda punda alipokaribia ndipo Mtume S.A.W. aliposema: Simameni waheshimiwa, akaja na akakaa kwa Mtume S.A.W. na Mtume akamwambia: Hakika ya hawa wamekuja kutokana na hukumu yako, akasema: Hakika yangu nimetoa hukumu ya kuuawa wapiganaji na kuachwa kizazi, akasema: Hakika umewahukumu kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu”.
Sura ya dalili ipo wazi ambayo ni kule kukubali kwa Mtume S.A.W. kutolewa hukumu kwa Wayahudi.
Pia alifanya hivyo kwa watu wengine, imetokana na Ibn Shaaheen kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Watu wa koo la Banu Hambar walipatwa na damu kwa watu wao waliamua kwenda kwa ndugu zao koo la Khuzaa, Mtume S.A.W. alimpelekea mjumbe kwa watu wa Khuzaa na watu wa Al-Ambar, watu wa koo la Hambar pindi walipomuona mujumbe wakamzuia, kuna watu wakafika kwa Mtume S.A.W. na kumwambia kuwa mjumbe aliyepelekwa kwa watu wa Hambar wamemzuia, ndipo Mtume S.A.W. akampeleka kwao Ayeenah Ibn Husnu na watu mia moja sabini na kuwakuta watu wakiwa na mambo yao ya kurithi, na kuwaongoza watu tisa na wanawake kumi na mmoja pamoja na watoto, habari hiyo ikawafikia watu wa Ambar ndipo walipokwenda kwa Mtume S.A.W. kiasi cha watu sabini akiwemo na Aqraa Ibn Haabis pia akiwepo Al-Awar Ibn Bishamah Al-Ambary akiwa ndio kijana wao zaidi, pindi walipofika Madina wamawake pamoja na watoto wakaanza kuwacheka, walifika kwa Mtume S.A.W. na kuanza kumuita: Ewe Muhammad Allaam ametutenganisha na wake zetu na wala hatujawahi kwenda kinyume na wewe, ndipo Mtume S.A.W. akatoka na kuwaambia: Basi tuweke muamuzi kati yangu mimi na nyinyi, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu awe Al-Aawar Ibn Bishaamah. Akasema: Isipokuwa kiongozi wenu ni Ibn Amru, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Al-Aawar Ibn Bishaamah, Mtume S.A.W. akampa nafasi Aawar ya kutoa hukumu basi akahukumu kundi moja litoe fidia na kundi lengine liachwe huru”. [Rejea kitabu: Al-Isabah fi Tamyeez Sahaba cha Ibn Hajar 1/95, Ch. Dar Al-Jeel]
[Rejea kitabu: Al-Isabat fi Tamyeez As-Sahabah cha Ibn Hajar 1/95 Ch. Dar Al-Jeel.
Waarabu katika zama za ujinga walikuwa wakihukumiana wao kwa wao, na walikuwa na mahakimu waliokuwa wanafahamika kwa kazi hiyo, na mahakimu wa Kiarabu ndani ya zama za ujinga ni pamoja na Akthum Ibn Saify, Hajib Ibn Zarrarah, Aqraa Ibn Habis, Rabiia Ibn Makhashin, Dhamrah Litameem, Aamir Ibn Ad-Dharb, Ghailan Ibn Salamah Laqees, Abdulmutwalib, Abu Twaalib, Al-Aaswy Ibn Waail, Al-Allaa Ibn Haarithah, Rabiia Ibn Hadhar, Yaamur Shaddakh, Safwan Ibn Umayah na Salamy Ibn Noofal. Angalia Kamusi ya Al-Muheetw, na Taj Al-Arus kipengelea cha HKM.
Miongoni mwa visa vyao katika hilo ni babu wa Mtume S.A.W. mzee Abdulmutwalib kuchimba kisima cha zamzam, amekitaja Ibn Ishaq kuwa, mzee Abdulmutalib alitoka akiwa na kijana wake Haarith Ibn Abdulmutalib –na hakuwa na mtoto mwengine wakati huo– na kuanza kuchimba kisima, ilipoonekana kwa mzee Abdulmutalib kukuwa kwa kisima ndipo Makuraishi wakafahamu hitajio lake ndipo walipomuendea na kumwambia: Ewe mzee Abdulmutalib hiki ni kisima cha baba yetu mzee Ismail, na sisi tuna haki kwenye kisima hiki basi tushirikishe kwenye kisima hiki, akasema: sikuwa mimi wa kufanya hivyo, kwani jambo hili limehusishwa na wengine na kupewa miongoni mwenu, wakasema kumwambia:
Tuelezee kwani sisi hatutakuacha mpaka tutavutana na wewe katika hili, akasema: Basi mtafuteni mumtakaye awe hakimu kati yangu na nyinyi, wakasema ni kiongozi wa ukoo wa Bani Saad Ibn Hudheym, akasema: ndio. Na alikuwa na wakuu wa Sham ndipo mzee Abdul Muttalib alipopanda kipando akiwa na kundi la watu wa bany Umayyah, na akapanda na kila mtu mmoja kutoka kabila la Kikuraishi wakatoka na ardhi ilikuwa ni kavu mzee AbdulMuttalib na watu wake walipokosa maji na kushikwa na kiu kikali mpaka wakawa na uhakika kuwa wanakufa, wakaomba maji ya kunywa kwa wenzao lakini walikataa kuwapa maji, na wakasema: hakika sisi ni kuhitaji, na sisi tunaogopa kufikwa kama yanayokufikeni nyinyi, mzee AbdulMuttalib akasema:
Mimi naona kila mmoja wenu achimbe kisima chake yeye mwenyewe hii kutoka na nguvu mulizokuwa nazo hivi sasa, ikawa kila anapokufa mtu watu wake humtumbukiza kwenye shimo lake mpaka akabakia mtu wa mwisho ndipo mzee AbdulMuttalib akasema kuwaambia watu wake kuwa: Kujitupa sisi wenyewe kwenye umauti hatusongi mbele wala haitakiwi sisi kushindwa kwani huenda Mwenyezi Mungu akaturuzuku maji ndani ya nchi zengine, hivyo wakaondoka mpaka mzee Abdulmuttalib anapotembea mnyama wake chini ya mguu wa mnyama kukawa kunachimbuka chemchem ya maji matamu ndipo mzee AbdulMuttalib alipotoa takbeera pamoja na watu wake pia, kisha akateremka na kunywa maji yeye na watu wake wakajaza vifaa vyao maji mpaka vikajaa, kisha wakawaita makabila ya Kikuraishi, hali ya kuwa wakiwaangalia wao katika hali zote na akasema: Njooni kwenye maji kwani Mwenyezi Mungu ametunywesheleza maji, ndipo wakaja na wakanywa wote, kisha wakasema kumwambia mzee AbdulMuttalib: Tunaapa kuwa Mwenyezi Mungu amehukumu kwake juu yetu, tunaapa kuwa hatutagombana na wewe katika maji ya zamzam, hakika yule aliyekunywesha haya maji ndio yule aliyekunywesha maji ya zamzam basi rudi kwenye kinywaji chako, ndipo akarudi na wakarudi pamoja nao pasi ya kufika kwa makuhani. Rejea kitabu: Al bidayah wan-nihaayah 3/336 Ch. Dar Hijr.
Kutoka kwa Aly R.A. amesema: Pindi ilipobomoka nyumba baada ya Jurham ndipo Makuraishi walipojenga pindi walipotaka kuweka jiwe la msingi ndipo walipojenga pindi walipotaka kuweka jiwe la msingi ndipo walipovutana juu ya nani atakayeweka wakakubaliana juu ya muwekaji wa jiwe hili ni yule atakaye kuwa wa kwanza kuingia mlango huu, ndipo Mtume S.A.W. akaingia kwenye mlango wa watu wa Sheibah, ndipo Mtume akaamrishwa kuletwa nguo na akawekea katikati ya nguo jiwe na kutoa amri kila mmoja kila mmoja ashike ncha ya nguo na kulinyanyua, kisha Mtume S.A.W. akalichukua na kuliweka sehemu yake. Imetokana na Abu daud na wengine.
Haya ikiwa ameyafanya kabla ya kutumwa kuwa Mtume lakini hiyo ni hiyari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, bali pia imepokelewa yanayoonesh juu ya kukubali kwake jambo hili baada ya kutumwa kwake, kutoka kwa Sharyh Ibn Haanii toka kwa baba yake, pindi alipomtuma kwenda kwa Mtume S.A.W. akasikia wakimwita kwa pongezi kuwa ni baba wa hukumu ndipo Mtume S.A.W. akamwita na kumwambia: “Hakika Mwenyezi Mungu mwingi wa hekima na hukumu inatoka kwake, basi ni kwanini unaitwa baba wa hukumu? Akasema: Hakika watu wangu wanapotofautiana katika kitu basi huja kwangu na huwa natoa hukumu kati yao na kuridhia kila upande. Akasema: Ni uzuri ulioje wa jambo hili, je una mtoto? Akasema: Ninaye Shariyh, Abdillah na Muslim, Mtume akauliza: Ni nani mkubwa wao? Akasema: Ni Shariyh. Akasema Mtume: Basi wewe ni baba Shariyh, akamwita kwa jina la mtoto wake”. Ni Hadithi imetokana na Abu Dawud na An-Nisaai.
Dalili hapa ni kutopinga kwake Mtume hukumu kusimamiwa na kuendeshwa na baba Shariyh lakini alibadilisha kuitwa kwa jina la baba wa hukumu, lau jambo hili lingekuwa si lenye kufaa basi asingebadilisha kuitwa kwake na kuacha lililomuhimu zaidi ya hilo.
Kiongozi wa Waumini Aly aliridhia hukumu iliyotolewa na watu wa Sham, na kupinga kwake hukumu iliyotolewa na watu kundi la Khawarij kwa yale tuliyotaja miongoni mwa Aya za Qur'ani , kutoka kwa Abdillah Ibn Abbas amesema: Nilipotoka Huruuriyah watu walikusanyika kiasi cha elfu sita nikaenda kwa Ally R.A na nikasema: Ewe Kiongozi wa Waumini hakika yangu huenda nikaenda kwa hawa watu na kuzungumza nao, akasema: Hakika yangu nina hofu kwako, nikasema: Hapana, kisha nikatoka kuwaendea nikiwa nimevaa vazi zuri zaidi kwa watu wa Yemen, nikawafuata wakiwa kwenye nyumba huku wanazungumza, basi nikawasalimia na wakasema: Karibu sana ewe baba Abbas, ni vazi gani hili? Nikasema ni vazi muliloniuzia kwani nimeona kwa Mtume S.A.W. akiwa na vazi zuri na ikashuka Aya ya Mwenyezi Mungu: {Sema ni nani anayeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu kwa waja wake pamoja na kuzuia riziki iliyo nzuri} [Al-Araaf, 32], wakasema: Umekuja kwa lipi? Nikasema nimekuja kwenu nikitokea kwa Sahaba wa Mtume S.A.W. miongoni mwa wahamiaji na wenyeji lengo ni kukufikishieni yale wanayosema na kutoa habari ya yale munayosema, juu yao imeteremka Qur'ani na wao ndio wenye kujuja zaidi mambo ya ufunuo kuliko nyinyi, na kwao imeteremshwa na wala hakuna miongoni mwenu hata mmoja, baadhi yao wakasema: Wala musigombane na Makuraishi, kwani Mwenyezi Mungu Anasema: {Bali hao ni watu wagomvi} [AZ ZUKHURUF 58], amesema Ibn Abbas: Nimekwenda kwa watu sijapatapo kuona watu wenye jitihada kuliko wao, nyuso zao zikiwa na alama kana kwamba mikono yao na magoti yao yamekuwa na alama, wakiwa wamevaa nguo zilizo safi, baadhi yao wakasema: Tuzungumze naye na tusubiri atakachosema, nikasema: Niambieni kitu gani munachokipinga kwa Aly mtoto wa baba mdogo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mkwe kwake pamoja na wahamiaji na wenyeji? Wakasema mambo matatu, nikauliza ni yepi hayo?
Wakasema la kwanza, ni kuwa watu wametoa hukumu katika jambo la Mwenyezi Mungu, kwani Mola Mtukufu Amesema: {Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu} [AL AN'AAM, 57] hakuna hukumu itolewayo na watu, nikasema hili la kwanza, wakasema ama lengine, ni kuwa amepigana bila ya kutukana wala kuchukuwa mali za ngawira, lau ingekuwa wale ambao wamepigwa ni makafiri basi ingehalalika kuwatukana na kuchukuwa mali za ngawira, na kama ni Waumini isingekuwa halali kuwapiga, nikasema: Hili la pili la tatu ni lipi? Wakasema ni kufutwa jina lake kutoka Kiongozi wa Waislamu na kuwa ni Kiongozi wa makafiri, nikasema: Je kuna mambo mengine yasiyokuwa haya? Wakasema:
Yanatutosha haya tu, ndipo nikawaambia: Munaonaje ikiwa nitawasomea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake S.A.W. katika yale yanayojibu maneno yetu je mutaridhia? Wakasema: Nido, ama kauli yenu ya watu kuhukumu katika jambo la Mwenyezi Mungu mimi ninawasomeeni andiko hukumu yake imejibu kuhusu wale watu wa thamani ya robo ya dirham ya kuuza sungura na mfano wake katika wanyama wa kuwindwa, nikasoma: {Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mkiwa mumehirimia Hija} [AL MAIDAH, 95] mpaka kauli yake Mola Mtukufu: {Kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu} [AL MAIDAH, 95]. Na peni wito kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwahukumu watu kuhusu sungura na mfano wake katika wanyama wa kuwindwa ni bora zaidi au hukumu yao kwenye damu zao na kuleta suluhu katika yale yenye masilahi kweo, na mufahamu kuwa Mwenyezi Mungu lau angetaka angetoa hukumu na wala isingekuwa hukumu inatoka kwa watu, na kuhusu mwanamke na mumewe Mola Mtukufu Amesema: {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha} [AN NISAA, 34] Mwenyezi Mungu Akafanya hukumu za watu ndani ya kipindi cha mwaka uliopita zilitokana na hili? Wakasema ndio: Nikasema ama kuhusu kauli yenu, amepigana bila ya kutukana wala kuchukuwa ngawira, je munaweza kumtukana Mama yenu Bi Aisha kisha mukahalalisha kwake yale yanayo halalishwa kwa wanawake wengine? Ikiwa mutafanya hivyo basi mutakuwa mumekufuru, kwani Yeye ni Mama yenu, na ikiwa mutasema: Si Mama yetu pia mutakuwa mumekufuru, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao} [AL AHZAAB, 06]. Basi nyinyi munazunguka kati ya potofu mbili, yeyote mutakayo kuwa nayo basi mutakuwa mupo kwenye upotovu, wakaanza kuangaliana wao kwa wao, nikasema: Mumelielewa hili? Wakasema ndio, nikasema, ama kauli: Limefutwa jina lake kutoka Kiongozi wa Waislamu, basi mimi ninakuleteeni yule munaye mridhia naona mutakuwa mumesikia kuwa Mtume S.A.W. siku ya Hudaibiyah waandishi wa washirikina akiwemo Suhail Ibn Amru na Aba Sufyaan Ibn Harb, Mtume S.A.W. akasema kumwambia Kiongozi wa Waislamu: “Ewe Ally andika: Haya ndio aliyoandika Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, washirikina wakasema: Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu hatufahamu kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, lau tungefahamu kuwa wewe ni Mtume wa Mwneyezi Mungu basi tusingepigana nawe, Mtume S.A.W. akasema: Ewe Mwenyezi Mungu Hakika yako Unafahamu kuwa mimi ni Mtume wako, andika ewe Ally: Haya ndio aliyoandika Muhammad Ibn Abdillah”, basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna aliyebora kwa Mtume zaidi ya Ally, lakini Ally hakumtoa Mtume kwenye Utume wake pale alipofuta jina lake, anasema Abdillah Ibn Abbas: Watu elfu mbili walikubali na kurudi na waliobaki wakabaki kwenye ujinga wao. [Kitabu As-Sunan Al-Kubra cha Al-Baihaqiy, 8/310]
Kutoka kwa Abdillah Ibn Shidad Ibn Al-Haad, amesema: Nilifika kwa Bi Aisha R.A. wakati tukiwa tupo kwake ndio siku ilisemekena Ally aliua, pale aliposema Bi. Aisha kuniambia: Ewe Abdillah Ibn Shidad, je wewe ni mkweli kwa yale nitakayo kuuliza? Ebu niambie kuhusu hawa watu waliouwawa, nikasema: Nina nini mimi nisikuamini? Akasema: Basi nifahamishe kuhusu kisa chao, nikasema: Hakika Ally baada ya kumwandikia Muawiyah, na kutoa hukumu mbili, basi kiasi cha watu elfu nane miongoni mwa wasomi wa Qur'ani walikuja maeneo ya Kufah, sehemu inayoitwa Harruraa, wakiwa wanampinga, wakasema vua kanzu uliyoveshwa na Mwenyezi Mungu na kukuita nayo, umeondoka na kuhukumu katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwani hakuna hukumu isipokuwa ni ya Mwenyezi Mungu, baada ya Ally kufahamu yale waliyokuwa wanalalamika na kutengana na amri ndipo alipoita muitaji: Asiingie mtu kwa Kiongozi Mkuu wa Waumini isipokuwa yule aliyebeba Qur'ani , baada ya wale wasomi wa Qur'ani walipojaa ndipo Ally alipotaka msahamu mkubwa na kuuweka mbele yake na akawa anafungua kurasa zake kwa mkono wake na anasema: Ewe msahafu wazungumzishe watu, ndipo watu wakasema: Ewe Kiongozi wa Waumini hicho unachokiuliza ni ibara ya karatasi na wino, na sisi tunazungumza kile tulichopokea, hivyo ni kitu gani unahitaji? Akasema: Wenzenu ambao walioachana na mimi na wao kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mtukufu Anasema kuhusu mke na mume: {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke} [AN NISAA, 35],
Kwani Umma wa Muhammad S.A.W. ni wenye utukufu mkubwa zaidi ya mke na mume, na wakachukia kuwa mimi nimemuandikia Muawiyah, wakati wa uhai wa Mtume S.A.W. aliwahi kuja Suheil Ibn Amru na sisi tukiwa pamoja na Mtume S.A.W. huko Hudaibiyah pindi watu wake Mtume walipoingia makubaliano na Makuraishi, Mtume S.A.W. aliandika: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu” Suheil akasema: Usiandike: Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, nikasema niandike vipi? Akasema andika: Kwa jina lako Ewe Mola, Mtume S.A.W. akasema andika, kisha akasema Mtume: “Andika kutoka kwa Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu” akasema: Lau tungekuwa tunafahamu kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu basi tusingekupinga, andika hivi: “Haya yaliyofikiwa na Muhammad Ibn Abdillah Mkuraishi”. Mwenyezi Mungu Anasema kwenye Kitabu chake: {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho}[Al-Ahzaab, 21]. Ally alimtuma kwao Abdillah Ibn Abbas, nami nikatoka pamoja naye mpaka tulipofika eneo lao Ibn Kawwaa alisimama na kuwaambia watu kwa kusema: Enyi wabeba Qur'ani hakika huyu ni Abdillah Ibn Abbas, kwa yule aliyekuwa hamfahamu basi mimi ninamfahamisha kutokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, huyu ndiye iliyomteremkia na kwa watu wake kauli ya Mungu: {Bali hao ni watu wagomvi} [AZ ZUKHURUF, 58], basi rudisheni kwa mwenyewe na wala musimdharau kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: Akasimama mzungumzaji wao wakasema: Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu kwa hakika tunamuheshimu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, pale anapotujia na jambo la haki basi tunalifahamu na kulifuata, lakini akitujia na jambo batili tunamuacha na ubatili wake, na kuurudisha ubatili huo kwa mwenyewe, kwa muda wa siku tatu watu elfu nne walirejea wakiwa wote wametubu, Ibn Kawwaa akawapokea na kuwapeleke kwa Ally R.A. kisha Ally akatuma kwa wale wengine waliobakia, akasema, hakika mumeona amri yetu na amri za watu, simameni mtakavyo na kutaneni na watu mtakavyo kwani kati yetu na nyie ni lazima kuepusha mikuki yetu maadam haijakata njia na kutaka kumwaga damu, kwani nyinyi mukifanya hivyo basi tumejiepusha mapigano na nyinyi kwani Mwenyezi Mungu hapendi watu wasaliti.
Bibi Aisha R.A. akasema: Ewe Ibn Shidad, je Ally aliwaua? Anasem: Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakupeleka mjumbe kwao mpaka walipokata njia na kumwaga damu pamoja na kumshambulia Ibn Khabban na kuhalalisha kushambuliwa watu wa dhimma, akasema Bi Aisha: Ni kweli? Nikasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu ndivyo ilivyokuwa, akasema Bi. Aisha: Yaliyonifikia kutoka kwa watu wa Iraq wanamzungumzia Ally wanasema: Mwenye maziwa mwenye maziwa, nikasema: Hakika wamemuona Ally akipigana na kuwaita watu na kuwaambia je huyu munamfahamu? Wengi waliokuja walisema: Hakika tulimuona ndani ya Msikiti wa watu wa fulani akiwa anaswali, tumemuona Misikiti wa watu wa ukoo fulani akiwa anasali hawakuja kuthibitisha yasiyokuwa haya, akasema Bi Aisha: Ni ipi kauli ya Ally pale alipodhaniwa na watu wa Iraq? Nikasema: Nimemsikia anasema: Amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake, akasema Bi Aisha je wewe umemsikia akisema tofauti na haya? Nikasema: Hapana, akasema ndio amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu ampe huruma Ally hayo ndio maneno yake: Kwani alikuwa haoni kitu kinachomshangaza isipokuwa husema: Amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake. [Kitabu As-Sunan Al-Kubraa cha Al-Baihaqiy, 8/311]
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, ni wazi kuwa inafaa kutoa hukumu kwa kutumia sheria za kutungwa ni sawa sawa sheria hizo ziwe ni za kimataifa au za ndani kwa sharti tu la kutopingana na Sheria za Kiislamu na misingi yake pamoja na madhumuni yake.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas