Hukumu ya Mgomo wa Chakula kwa Leng...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Mgomo wa Chakula kwa Lengo la Kutaka Dhuluma Iondoshwe.

Question

Katika zama hizi, suala hili limeenea, nalo ni baadhi ya watu kugoma kula chakula na kunywa mgomo kamili. Na mgomo wao huo ni kwa lengo la kuelezea upingaji wao wa kitu fulani, au wakitaka dhuluma iliyopo iondolewe au ili kulifikia lengo maalumu. Na wanauendeleza mgomo huo mpaka dola au serikali au Taasisi fulani au hata wizara iyakubali matakwa yao. Je? Ni ipi hukumu ya Kisheria ya Jambo hili? Na je? Anayepoteza maisha katika wafanyao Mgomo anazingatiwa amejiua? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya hayo:
Mgomo katika lugha ya kiarabu ni asili ya kitenzi cha amegoma (Adhraba). Husemwa nimegomea kitu fulani yaani nimejizuia na kitu hicho na kujiepusha nacho. [Tazama: Lisaanu Al Arab ya Ibn Mandhuur, kidahizo cha Dharaba 547/1, Ch. Dar Swader Bairut].
Na kinachokusudiwa hapa kwa maana ya Mgomo wa Chakula ni: Mtu kujizuia kula chakula na kujiepusha nacho kwa lengo la kuonesha upingaji wa jambo na kumshinikiza mwingine akitaka aondoshewe dhuluma aliyotendewa au kwa lengo la kuyapata masilahi fulani.
Na tunayoyachagua kwa kutoa Fatwa katika jambo hilo ni; Kwamba aina hii ya Mgomo wa Chakula inajuzu kwa sharti kwamba Mgomo huo usimsababishie Mgomaji madhara ya kiafya, au kuleta madhara makubwa zaidi kwake au hata kumwangamiza kabisa. Masharti haya ya madhara yakipatikana au hata sharti moja kati ya hayo basi mgomo huo utazingatiwa kuwa haufai, kwani kuacha chakula na maji ni katika kuacha vya halali nalo ni jambo linalosihi kwa masharti yaliyotajwa hapo mwanzo (ya kutokuwepo madhara).
Ama anaposhurutisha kutoleta madhara kwa muhusika yanayoweza kumwangamiza, ni kwa kuwa Sheria ya Kiislamu inakataza Madhara; Basi imepokelewa kutoka kwa Abi Said Al Khudriy kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Hakuna kudhuru au kujidhuru", Imamu Nawawiy amesema katika kitabu chake: [Al Arbai'n (Hadithi arobaini za Kinabii) kuhusu Hadithi hiyo Uk. 97 na 98, Ch. Dar Al Menhaaj kwa uchapishaji na usambazaji vitabu, Lebnan]: "Hadithi Hasan", Ilipokelewa na Ibn Majah, Ad Darqutwniy na wengineo (Musnad), Malik akaipokelea katika kitabu chake: [Al Muwatwa] (Mursal) kutoka kwa Amru Bin Yahya kutoka kwa baba yake kwamba Mtume S.A.W. basi akamwondoshea Abi Said. Na Hadithi hiyo ina njia zinazojiongezea nguvu zenyewe kwa zenyewe.
Na Mwislamu haruhusiwi kumsababishia mtu mwingine yeyote au yeye mwenyewe madhara.
Imetajwa katika kitabu cha: [Al Inswaaf, kwa Al Mardawiy wa Kihanbali 330/8, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]; "Na asipunguziwe chakula ambapo atajidhuru nafsi yake". (Imekwisha)
Ama kushurutisha kitendo hicho kisilete madhara makubwa zaidi, kama vile kumfanya mtu apitwe na jambo la Faradhi kwa udhaifu wa mwili unaompata mtu aliyegoma kula chakula au hata kunywa maji, basi kwa wakati huo hakuna zingatio lolote la kuwapo masilahi yanayotazamiwa dhidi ya madhara yaliyotajwa. Na hiyo ni kwa kuwa kuzembea katika Kilichofaradhishwa hakukubaliki isipokuwa kwa udhuru unaotambulika kisheria, na Mgomo wa Chakula sio katika nyudhuru za kisheria ambazo ni halali kwazo kuacha Faradhi.
Na baadhi ya wanachuoni wa Fiqhi waliyaeleza hayo. Basi katika kitabu cha: {Majma' Al Anhaar kwa Mtaalamu wa Kifiqhi; Damaada Al Hanafiy, 524/2, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]; (Sura katika kula): yaani katika kueleza hali za kula; (miongono mwake), yaani baadhi ya vyakula na pia vinywaji, (ni faradhi, nayo ni kwa kiwango kinachoepusha maanganizi), na katika kuacha kwake ni kujitupia katika Maangamizi, na ikiwa mtu ataangamia basi atakuwa amemuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kula, Mja huweza kutekeleza Ibada za Faradhi na hulipwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufanya hivyo.
Na inaongezewa juu ya hayo, kwamba imepokelewa katazo la Funga ya Usiku na Mchana katika Saumu; kutokana na mtu kujitumbukiza yeye mwenyewe katika uzito na kuudhoofisha mwili wake. Na Maana ya (Wiswaalu) ni kufululiza kufunga usiku na mchana bila ya kula na kunywa.
Basi Imamu Al Bukariy na Imam Muslim wamepokea kutoka kwa Abi Hurairah R.A. amesema: Mtume S.A.W. amesema: "Jiepusheni na Kufunga Usiku na Mchana. Wakamuuliza Mtume: Hakika yako wewe unafunga hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu! Akasema: hakika nyinyi hamfanani na mimi katika jambo hilo, hakika mimi ninalala na Mola wangu Mlezi ananilisha na kuninywesha, kwa hivyo fanyeni ibada mnazoziweza".
Na katazo la kufunga Usiku na Mchana - pamoja na kuwa kwake ni ibada ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu - ni kwa lengo la kumzuia mtu asijiingize katika ugumu, na akaudhoofisha mwili wake na kushindwa kutekeleza yanayomlazimu, na anajiadhibu yeye mwenyewe na kujitesa, na iwapo maana hizi zitapatikana katika Mgomo basi utakuwa ni wenye kukatazwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma,isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Walamsijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.} [AN NISAA 29] Na Amesema pia: {Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, walamsijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.} [AL BAQARAH 195]
Na Sheria imemuhalalishia Mtu ale kilichoharamishwa kuliwa katika hali ya dharura kwa lengo la kuilinda nafsi yake na kwa lengo la kukinga maangamizi. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: { Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake,jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi,yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [AL BAQARAH] Na Mgomo unapingana na hili. Kwa hivyo, mtu kujizuia na kula chakula cha halali mpaka akaangamia ni Haramu kwa njia ya kwanza.
Imamu Abu Bakr Aj Jaswasw mwanazuoni wa kihanafi alisema katika kitabu cha: [Ahkaamu Ak Qur'aan 157/1, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy] Mtu atakayejizuia jambo la Halali mpaka akafariki dunia atakuwa ni mwenye kujiua mwenyewe na ni mwenye kuiangamiza nafsi yake kwa mtazamo wa Wanachuoni wote na wala haitofautiani kwao Hukumu ya Asi au Mtiifu, bali inakuwa wakati huo kutokula kwake chakula ni nyongeza tu ya kuasi kwake. Na imewajibika kuwa sawa Hukumu yake na Hukumu ya Mtiifu, katika kuhalalisha chakula wakati wa dharura, je wewe huoni kwamba yeye kama angelijizuia kula chakula halali alichonacho mpaka akafariki dunia angelikuwa amemuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na imetaja katika kitabu cha: [Al Furuuq kwa Imamu Al Qarafiy, 183-184/4, Ch. Alam Al Kutub]: katika utofauti wa Mia mbili , arobaini na saba, baina ya Msingi wa kuharibu kwa Uadui na baina ya kuharibu bila ya Uadui, Hakika mwenye kunyamaza kwa kutojitetea mpaka akauawa hakuzingatiwi kuwa ni mwenye dhambi wala hakuzingatiwi kajiua mwenyewe kinyume kama angelijizuia kula chakula na kunywa maji yake mpaka akafariki dunia hakika yeye ni mwenye makosa na ni mwenye kujiua.
Na tofauti kati ya kuacha kumzuia adui na kuacha kula chakula na maji mpaka afikwe na umauti, kwamba kuacha kula chakula ni sababu kuu inayopelekea kifo hakuongezea nyingine, na lazima paongezwe kitendo cha Adui ili kuwezesha.
Na tofauti iliyopo baina ya kuacha kula chakula na kuacha kunywa dawa haiwi Haramu Kwamba Manufaa ya dawa hayadhibitiki. Dawa inaweza kuponya au kutoponya, wakati ambapo chakula ni Manufaa ya lazima.
Kutokana na hayo yaliyotangulia; Hakika kugoma kula chakula kwa lengo la kutaka kupinga Jambo na kumshinikiza mwingine kutaka dhuluma iondoshwe masilahi maalumu yapatikane, inajuzu kwa sharti la kutosababisha Mgomaji kupata madhara yanayoweza kupelekea yeye mwenyewe kujiangamiza. Na kusipelekee madhara makubwa zaidi, na wala kusipelekee maangamizi. Na ikiwa masharti haya yatatekelezwa au moja wapo katika hayo basi Mgomo huo utakuwa haufai na utazuiliwa, na anaekufa kwa mgomo huo anazingatiwa amejiua.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

 

Share this:

Related Fatwas