Matibabu ya Kasoro za Ngozi.

Egypt's Dar Al-Ifta

Matibabu ya Kasoro za Ngozi.

Question

Je! Nini hukumu ya kutibu hali ya Kasoro za ngozi ambayo mwanadamu huzaliwa nayo, au zile zinazojitokeza katika ngozi yake kwa sababu ya ajali za barabarani, au mfano wake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya hayo:
Hakika matibabu ya kuungua kwa aina yoyote yanaingia kiasili ndani ya uhalali wa kujitibu, na hayatoki nje hadi kutafutwe dalili mpya.
Upendo wa uzuri na kuondoshwa kinachoaibisha ni jambo la kimaumbile, ambalo linalokubalika Kisheria. Katika Hadithi ya wale Watu watatu waliokimbilia Pangoni, "Mwenyezi Mungu Mtukufu, Akawatumia Malaika. Akamwendea mwenye mbalanga akamuuliza: Kitu gani ukipendacho zaidi? Akajibu: Rangi na ngozi nzuri [ya mwili], na uniondokee ugonjwa wa [mbalanga] niliokuwa nao kwani ugonjwa huu unawakera watu. Akasema: [Malaika] Akamgusa ukamuondokea ugonjwa akapewa rangi na ngozi nzuri". [Imepokelewa kutoka kwa Imamu Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abu Huraira].
Dalili katika Hadithi hii ni kukubali Malaika na kumjibu ombi lake.
Katika Sunnah Tukufu, Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Dawood kutoka kwa Abdul Rahman Ibn Tarfah kwamba babu yake Arfajah Ibn Asaad alikatwa pua yake katika siku ya Al-Kilaab na kuchukua pua iliyotenenezwa kwa karatasi, ikawa inanuka basi Mtume S.A.W. akamwagiza achukue pua iliyotenenezwa kwa dhahabu.
Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Imamu Tirmidhi na amesema: Hii ni Hadithi yenye hadhi ya Hasan na Ghariib... Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa zaidi ya mwanazuoni mmoja kwamba watu waliweka meno ya dhahabu kwa sababu hiyo, na Hadithi iliyotajwa hapo juu ni hoja kwao.
Nayo ni hoja kwenye sehemu hii, na masahaba waliifuata kama alivyosema Imamu Trmidhi kutoka kwa baadhi yao.
Katika sehemu hii pia ni kwamba Qatadah Ibn Nu'man wakati alipojeruhiwa katika jicho lake katika moja ya vita, Mtume S.A.W. akalirudisha kwake bora kuliko lilivyokuwa na akamwombea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hadithi hii imepokewa kwa njia kadhaa kama katika Al-Isabah, Kitabu cha Al-Hafiz Ibn Hajar [5/318, 319, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Katika Hadithi hiyo dalili ya ruhusa ya kuondoa sehemu iliyoharibika, ambayo inamuathiri mwanadamu, na dalili hapa ni kuondoa dosari inayosababisha kitu hata kutoka nje ya mwili. Ikiwa ni kutokana na mwili wa mwanadamu mwenyewe, kuchukuliwa kutoka katika ngozi yake isio dhahiri ili kuwekwa mahali pa ngozi iliyoharibika, hali hii inaruhusiwa kisheria, na mtu anaweza kuchukua ngozi yake mwenyewe akizingatia masilahi yaliyochaguliwa na wanavyuoni mwanzoni, basi yeyote akipigwa usoni mwake na kitu ambacho kinaweza kumwua au kumvunja; anaweza kujikinga kwa mikono yake katika hali zote, ingawa mikono yake itajeruhiwa. Ikiwa hali ni kama ilivyo hivyo, basi inaruhusiwa pia kuondoa nywele kutoka katika baadhi ya sehemu za mwili na kuzipandikiza katika sehemu nyingine mwilini.
Ibn Najim Al-Hanafiy amesema: "Ikiwa madhara mawili yanakinzana basi yatazingatiwa madhara yaliyo makubwa zaidi kwa kufanya yaliyo mepesi zaidi. Az- Zilai amesema kwamba: chimbuko la suala hili ni kuwa yule anayejaribiwa kwa shida mbili zinazolingana, anaweza kuchukua yoyote anayoitaka, na kama zitakuwa tofauti anaweza kuchagua iliyo nyepesi zaidi kati ya mbili." [Al-Ashabh Wal Nadhair uk. 76, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Baraza la Fiqhi ya Kiislamu –lililo chini ya Mkutano wa Kiislamu huko Jeddah - limetoa maamuzi yakiwemo yafuatayo: Inaruhusiwa kubadilisha kiungo kutoka sehemu moja ya mwili wa binadamu kwenda sehemu nyingine ya mwili wake, kwa kuzingatia na kuhakikisha kuwa faida inayotarajiwa ya mchakato huu ina uwezekano mkubwa wa kuleta manufaa kuliko uharibifu uliojitokeza, ikizingatiwa kuwa kufanya hivyo ni kwa ajili ya kurekebisha kiungo kinachopotea, kurejesha sura yake au kazi yake, kurekebisha kasoro, au kuondoa ngozi ambayo husababisha shida ya kisaikolojia au ya kiungo kwa muhusika. [Maneno haya yametajwa katika: Ahkaam Ash-Shir fi Al-Fiqhi Al-Islami, Kitabu cha Taha Muhammad Faris, Uk. 184, Ch. Dar Al-Buhuuth led Drasat Al-Islamiyah wa Ihyaa At-Turarth].
Madaktari wa Kiislamu bado wanatibu ngozi iliyouungua, bali wanatafuta kile kinachootesha nyama nzuri katika mwili wa mgonjwa:
Ibn Sina alisema: “Sehemu katika sheria ya matibabu ya kuungua kwa moto: kusudi katika matibabu ya kuungua kwa moto kuna madhumuni mawili: moja ni kuzuia mafuta, na pili ni kurekebisha kile kilichoungua” [Al-Qanun 5/260, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Alisema pia: “Ikiwa kilichoungua ni nyama ya mwili kama vidonda, hatupaswi kuchukua hatua ya kufanya chochote, lakini lazima tutunze na kuotesha nyama mwanzoni.” [1/307]
Pia alisema: “Kama kwa bustani ina ardhi nzuri ikapata maji ya wastani ... vidonda hujazwa kwa nyama nzuri ya asili yake inayofaa pahala palipounguzwa na maji ya moto; kwa sababu imekaushwa kiasi.” [1/590].
Utunzaji wa uzuri wa viungo vya mwili wa binadamu una athari katika maneno ya wanavyuoni wa Fiqhi katika sehemu mbali mbali za Fiqhi, zikiwemo:
Katika mlango wa Kutayamamu: Wanavyuoni wameruhusu mgonjwa kutayamamu, hata katika maeneo ya Mijini, ikiwa matumizi ya maji yanaweza kukidhuru kiungo cha mwili wake:
Zakaria Al-Answariy As-Shafiy alisema juu ya sababu zinazopelekea kuruhusiwa kutayamamu: “(ugonjwa) hata katika maeneo ya mjini kwa mujibu wa Aya hii [Na mkiwa wagonjwa] [AN-NISAA: 43] yaani mkiogopa kutumia maji yaliyozuiwa basi ukusudieni mchanga safi ... (au) hofu ya (kupata madhara mabaya (katika kiungo kinachoonekana) kwa sababu huharibu uumbaji na hali hiyo hudumu." [Asna Al-Matwalib 1/80, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Katika mlango wa makosa ya Jinai (Ta'zir) Wanavyuoni walionya chochote kinachoharibu kiungo cha mwili kilichobora:
Al-Bahwatiy alisema: :(auepushe uso) kwa heshima yake (na) aepushe (tumbo na sehemu za hatari) akiogopa kuua. (Na) huepukana na sehemu (zilizobora) ili asiziharibu.” [Kashaf Al-Qinaa 5/209, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu inajulikana kuwa hukumu ya matibabu ya kuungua, na kubadilisha ngozi nyingine inaruhusiwa kufanya hivyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas