Hukumu za Mwenye Matatizo Akilini

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu za Mwenye Matatizo Akilini

Question

1- Hukumu ya kuoa mwenye matatizo ya akili, na kuzaa kwao baada ya ndoa.
2- Je inafaa mwenye matatizo ya akili kutoa talaka?
3- Ni kipindi gani cha usimamizi wa msimamizi wa mlemavu wa akili kwa mke wa mlemavu na watoto wake
4- Ikiwa ndoa ya mwenye ulemavu wa akili inaficha lengo la kupata manufaa ya kitu nyuma yake je wakati huo ndoa inakuwa ni batili?
 

Answer

Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, sala na salamu ziende kwa Nabii wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na watu wake na Masahaba wake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Jambo la Kwanza: Kuoa ni haki miongoni mwa haki za mlemavu wa akili, haki hii imethibiti kwake kwa mujibu wa ubinadamu na asili, kwa sababu ni mwanadamu mwenye matamanio na mwenye kuhitaji utulivu uangalizi na usimamizi, alivyo ni sawa na wanadamu wengine pamoja na kuongezeka kwake hitajio la usimamizi kutokana na hali yake maalumu aliyonayo.
Kama ilivyo katika hilo haki iliyothibiti kwake, pia imetihibiti kisharia, ikiwa sharia imeruhusu kwa mwendawazimu mwenye wazimu wa kiwango cha juu kuoa basi aliyekuwa chini ya huyu – kama vile mlemavu wa akili kwa kiwango kidogo – kufaa kuoa kwake ni bora zaidi, wala hakuna ubaya wowote katika hilo madamu huyu mwenye ulemavu wa akili anapata usimamizi na ulezi.
Ndoa ni makubaliano miongoni mwa makubaliano, wakati wowote nguzo zake na sharti zake zinapokamilika basi ni makubaliano sahihi na kukubaliana na athari zake, miongoni mwa sharti za kufaa kwa makubaliano: Ni kufikia umri wa kujitambua kwa kukubaliana, ikiwa litakosekana hilo kwa uwendawazimu basi haifai kwa mwendawazimu – na mtu wa mfano wake – kuoa yeye mwenyewe, ikiwa atafanya hivyo basi makubaliano hayo hayatazingatiwa, na hilo ni kwa sababu ndoa ni hatua inayosimama kwenye makusudio sahihi, ambapo hayapatikani isipokuwa kwa kuwa na akili.
Amesema mwanachuoni Al-Kasaniy katika kitabu cha: [Badaai swanaai 2/232 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]: “Haifungwi ndoa ya mwendawazimu na mtoto mdogo asiye na akili, kwa sababu akili ni miongoni mwa sharti la haki ya kutumia”.
Kwa sababu ya kosoro hii ya kutokuwa na sifa ya haki ya kutumia au kuamua sharia imethibitisha mamlaka ya usimamizi wa mwendawazimu yapo kwa mtu mwingine, ili kufikia kumlinda, na kwa mujibu wa mamlaka haya msimamizi wake atakuwa na jukumu la kusimamia mambo yake yote.
Katika vitendo ambavyo vinafaa msimamizi kusimamia: Ni kumuolea mwendawazimu ambaye yupo chini ya usimamizi wake kwa masilahi ya kumlinda na kumkinga.
Amesema Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Raudhwa 5/435 Ch. ya Dar Aalam Al-Kutub]: “Akiwa mwendawazimu ni mtu mzima hakuozeshwa pasina haja, na akaozeshwa kwa haja, na hilo kwa kuonekana utashi wake katika hilo, au kwa kuhitaji mtu wa kumuhudumia na wala hakuna katika watu wake wakaribu mwenye kumsimamia katika hili...au kwa matarajio ya kupona kwake kwa kuoa, ikiwa itafaa kuoa basi baba ndio atakayesimamia kisha babu kama baba hayupo kisha kiongozi mkuu kwa watu wa nje ya ukoo wake, kama vile kwenye usimamizi wa mali, ikiwa huyu mgonjwa wa akili ni mtoto mdogo haifai kumuozesha kwa kauli sahihi.
Amesema mwanachuoni Al-Buhuty katika kitabu cha: [Kas-shafu Al-Qinaai” 5/45 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Ama mwendawazimu wa kike basi wasimamizi wake wote wanaweza kumuoza ikiwa ataonekana ana mwelekeo wa kutaka wanaume, kwa sababu ni mwenye haja ya ndoa, ili kuondoa madhara ya matamanio na kumlinda na uovu na kupata mahari kugharamiwa na kulindiwa heshima yake, hakuna sababu ya kupata ruhusa yake ni halali kumuoza, na hufahamika mwelekeo wake wa kutaka wanaume kupitia maneno yake na kufuata wanaume na mfano wa hayo miongoni mwa dalili za hali hiyo, vile vile ikiwa wamesema watu wenye kuaminika miongoni mwa madaktari – ikiwa itashindikana kwa wengine, au watu wawili – kuwa matatizo yake yataondoka kwa kuozwa, basi kila msimamizi anaweza kumuoza, kwa sababu hilo ni miongoni mwa masilahi yake makubwa, kama vile dawa, ikiwa mwendawazimu mwenye matamanio na mfano wake hana msimamizi basi kiongozi atamuoza”.
Undani wa maelezo ni kuwa makusudio ya usimamizi wa wasimamizi ni masilahi tu kwa anayesimamiwa, na wala sio kugeuzwa jambo hilo na kuwa biashara ya kitumwa katika sura ya kuwatumia hawa wenye ulemavu wa akili kwa matumizi yasiyokuwa ya kibinadamu na yasiyokuwa ya kimaadili.
Asili ni wazazi wawili au mmoja wao kutathmini matendo yake kwa mlemavu wa akili yanafungamana na masilahi yanayomzunguka, ikiwa kuna masilahi kwake kwa upande wa nafsi au afya au masilahi ya kitu kwenye ndoa basi haifai kwake kuzuia kati yake na hayo masilahi, bali inawezekana kuunganisha hali zinazofanana au zilizo karibu na kufanana kwa kukamilisha ndoa kati yake kupitia Jumuiya na taasisi ambazo zinasimamia watu wa mfano wa hawa walemavu wa akili, na kuchelewa kwa wasimamizi kwenye masilahi yake kuna kuwa na mapungufu na makosa kwa kiasi cha kuchelewa kwao kufikisha heri hii ambayo inadhaniwa kupatikana kwa walemavu wa akili.
Ama kuhusu kuzaa baada ya ndoa: Marejeo ya hilo ni kwa watu wazoefu na wale wenye weledi, nao ni wenye kufahamika kupitia watu hao kujua kwao kiwango cha masilahi na uharibifu katika yale yanayofungamana na kuzaa au kutozaa au kuchelewa kwa mujibu wa masilahi ya kila hali kivyake, na hawa ndio ambao wanaweza kusimamia uwezo wa mgonjwa wa akili katika kulea watoto katika umri wa rika mbalimbali, je nafasi ya kutokea kurithi kwa mgonjwa wa akili bado ipo? Na kwa kiwango gani kinawezekana kupatikana? Na je kuzaa kuna athiri vibaya katika hali ya baba au mama? Na mengine katika mitazamo ya kiweledi ambayo yanakuwa na nguvu katika kuzaa au kutozaa, na hayo yanakuwa chini ya ulezi na usimamizi wa msimamizi wa mgonjwa wa akili.
Jambo la Pili: Kuhusu talaka ya mgonjwa wa akili: Asili katika talaka ni haki inayomilikiwa na mume peke yake, kwa Hadithi iliyopokelewa na Ibn Maja kutoka kwa Ibn Abbas R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Hakika ya talaka ni kwa mume” hakuna yeyote anayemiliki tofauti na mume talaka ya mke wake isipokuwa akipewa msimamizi wa hilo, kwa wakati huo inafaa, kwa sababu asili ni mtu kufanya mwenyewe, lakini asili hii ni kwa yule mwenye upungufu wa kimajukumu haifai kwake talaka, imepokelewa na watu wanne kutoka kwa Ally na Bi. Asha R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Kalamu imeondolewa kwa watu watatu: Kwa mtu aliyelala mpaka atakapo amka, kwa mtoto mdogo mpaka atakapo kuwa mkubwa, na kwa mwendawazimu mpaka atakapo pata akili au kuzinduka”.
Wanachuoni wametofautiana: Je kwa msimamizi anaweza kutoa talaka kwa mke wa mgonjwa wa akili – kwa maana ya mlemavu wa akili – ambaye yupo chini ya usimamizi wake? Jopo la wanachuoni wa Imamu Abu Hanifa, Imamu Shafi na Imamu Hanbal wanasema kuwa hana mamlaka hayo, angalia kitabu cha:: [Al-Mabsuut 25/24 Ch. ya Dar Al-Maarifa – Beirut], kitabu cha: [Raddu Al-Mukhtar 3/25 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], kitabu cha: [Asnaa Al-Matwaleb 2/212 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Islamy], sharhe ya kitabu cha:: [Muntaha Al-Iraadaat 3/59 Ch. ya Aalam Al-Kutub].
Imenukuliwa kutoka kwa baadhi ya wanachuoni waliotangulia kuwa inafaa, angalia: [Musannaf Ibn Aby Shaibah 4/27], na katika hilo wamesema pia wanachuoni wa Imamu Malik, angalia: [Sharhe ya Al-Kharashy Mukhtasar Khalil 4/17 Ch. ya Dar Al-Fikr].
Wamehusishwa baadhi ya wanazuoni wafuasi wa Imamu Hanbal na kauli ya kufaa kutoa talaka baba pasi na mwingine miongoni mwa wanaosimamia ndoa katika jumla ya wasimamizi, kitabu cha: [Al-Mughniy, 7/41].
Na sheria ya Misri haikuweka wazi katika vipengele vyake hukumu ya kutoa talaka msimamizi wa mgonjwa wa akili aliye chini ya usimamizi wake, isipokuwa fiqhi ya sheria imekwenda sawa na madhehebu ya jopo la wanachuoni, angalia: Ansaikolopidia ya fiqhi katika hali za ndoa cha mwanasheria Muhammad Azmy Al-Bakry [4/20 Ch. ya Dar Mahmuod], imekuja kwenye waraka wa ufafanuzi baadhi ya mabadiliko ya sheria ya hali ya ndoa namba 100 ya mwaka 1985, kuwa hukumu maalumu za sheria za maisha ya ndoa ikiwa haijatamkwa basi huchukuliwa hukumu kwa kauli yenye nguvu zaidi za madhehebu ya Abi Hanifa ukiacha yale yaliyovuliwa katika hayo.
Nayo ni katika Fatwa zilizotolewa na ofisi ya Mufti wa zamani wa Misri, zama za Sheikh Bakry as-Sudfy, mfungo nane 1328, na mfano wake katika Fatwa zengine za Sheikh Hassan Maamun, za mwezi mosi Ramadhani 1378H, sawa na tarehe 10/March/ 1959.
Kwa Fatwa hizo: Hapaswi msimamizi wa mambo ya mgonjwa wa akili kutoa talaka kwa mke wa mgonjwa wa akili, ikiwa ataona hivyo basi anapaswa kulifikisha suala hilo kwa kadhi ili kuangaliwa, kadhi peke yake ndio mwenye kumiliki utoaji talaka katika hali kama hii ikiwa itabainika kwake yanayopasa kisharia kutolewa talaka.
Jambo la Tatu: Ama yanayofungamana na mipaka ya usimamizi ya msimamizi wa mlemavu wa akili kwa mke wa mlemavu na watoto wake: Msimamizi husimama nafasi ya mgonjwa wa akili ambaye yupo chini ya usimamizi wake katika kusimamia mambo ya mke wake na watoto, sababu ya kuwepo msimamizi hapa: Ni kumlinda huyu mwenye mapungufu, na kumfanyia yale yenye masilahi kwa mgonjwa wa akili, kwa sababu hiyo ni kuwa msimamizi anakuwa kwa niaba yake kwa yale ambayo angepaswa kuyafanya mgonjwa wa akili ikiwa ni pamoja na maamuzi na mambo yanayo muhusu yeye mwenyewe na familia yake kama angekuwa na akili.
Maelezo ya wanachuoni yameonesha juu ya uwazi huu na wajibu unaomuhusu huyu mgonjwa wa akili, hakuna tofauti kati ya mwendawazimu na mlemavu wa akili kwani wote wana mapungufu ya kimajukumu:
Waliyoyasema kuhusu mke wa mgonjwa wa akili kuanzia kumgharamia chakula mavazi ni kwamba yatasimamiwa na mlezi wa mgonjwa wa akili, kama vile yeye ndiye anayesimamia mgao wa huyu mgonjwa wa akili kama atakuwa na mke zaidi ya mmoja, imekuja kwenye kitabu cha: [Mukhtasar Khalil” na sharhe yake] [Manhu Al-Jalil cha Sheikh Muhammad] Aliish miongoni mwa vitabu vya wanachuoni wa Imamu Malik [3/536 Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Ni lazima kwa msimamizi wa mume aliye na matatizo ya akili ambaye ana wake wawili au zaidi ya wawili kusimamia mambo ya wake zake kwa kumuingiza kwa mmoja wa wake zake nyakati za jioni baada ya kuzama kwa jua, na kubakia huko mpaka kuzama kwa jua jioni ya siku ya pili, atamtoa kwa mke wake huyo na kumpeleka kwa mke mwingine, na ataendelea kufanya hivyo, kama vile msimamizi anawajibu wa kugharamia chakula chao na mavazi yao, kwa sababu hayo ni katika haki za mwili ambazo msimamizi atazisimamia”.
Miongoni mwa maelezo mengine: Ni yale aliyoyasema Sheikh Al-Islaamu Zakaria Al-Answariy katika [sharhe ya Minhaaj at-Twullaab 2/548 – 549 Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Ikiwa mtumwa atahirimia ibada ya umra hata kama atakuwa ameandikiwa uhuru wake au kuhirimia mke pasi na ruhusa kwa kile alicho kihirimia basi msimamizi wa mambo yake akiwa bwana wake au mume wake atavua nia hiyo kwa kumtaka kujivua kwenye nia yake, kwa sababu maamuzi yao ya kuhirimia yanakwamisha manufaa yao ambayo wanayastahiki, hivyo wanapaswa kujivua nia hiyo kwa wakati huo”.
Amesema mwanachuoni Al-Jamal akifafanua katika kitabu chake 2/548 kwenye kauli yake “Basi msimamizi wa mambo yake... mpaka mwisho” ndio, ikiwa atasafiri naye na akahirimia ambapo hakupitwa naye na kitendo cha ndoa kwa kuwa kwake ni mwenye kuhirimia, wala muda wa kuhirimia kwake mke au mtumwa haukuwa mrefu zaidi ya muda aliyohirimia mume au bwana wa mtumwa, katika hali hiyo hakuna sababu ya kujivua kwenye nia yake, vile vile akiwa mke au mtumwa wa kike amehirimia kwa kutekeleza nadhiri fulani kabla ya kuolewa au baada ya kuolewa kwa ruhusa yake, au kwa utelekezaji wa haraka basi msimamizi wa mume au bwana wa mtumwa anapaswa kumzuia moja kwa moja” tamko hili kutoka kwa mwanachuoni Al-Jamal akibainisha kuwa ikiwa mtu atasimamia yale anayopaswa kusimamia kwa ajili ya mtu mwingine – kama vile katika hali ya uwendawazimu au ulemavu wa akili – basi huyu msimamizi anatakiwa kuingilia kati kwa kumzuia mke anayemsimamia kutokamilisha kunuia kwake katika sura iliyotajwa, haliwi hilo ni kwa sababu yeye anasimama nafasi ya anayemuwakilisha kwenye usimamizi katika ruhusa na kuzuia.
Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi wamezungumzia pia masuala haya kuwa je mke wa mume mwenye matatizo ya akili atajizuia kutekeleza ibada ya funga ya sunna kwa kuwepo mume mwenyewe au yule anayemsimamia katika kutoa ruhusa? Au pakasemwa: Ikiwa kustarehe kwa tendo la ndoa kunamletea madhara kutoa ruhusa msimamizi wa mume wake, na ikiwa kuna manufaa au hakuna madhara je hakuna kizuwizi? Amesema mwanachuoni Shihab Ramly katika kitabu chake cha: [Asnaa Al-Matalib” 3/435 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Islamiy], baada ya kutaja hili: “Ndani yake inategemea, ameyasema hayo pia Al-Adharaii”.
Kana kwamba shaka yao kati ya kumzingatia msimamizi wa mgonjwa katika kutoa ruhusa na kutotoa ruhusa na kati ya hukumu yao ya kutofaa kufunga mke wa mume mgonjwa wa akili funga ya sunna kwa kuwepo mume wake, shaka inatokana na mambo mawili:
Jambo la Kwanza: Ni kuwa asili katika usimamizi ni kama vile anachukua unaibu kwa mgonjwa wa akili katika kuendesha mambo yake vile vile anachukua unaibu katika yale yanayohusu usimamizi wa familia yake.
Jambo la pili: Ni kuwa mgonjwa wa akili hafai kutoa ruhusa, hali inaweza kujirudia ya kutaka kukutana kimwili na mkewe, jambo hili halina kuingiliwa na msimamizi wa mgonjwa katika kupangiliwa kwake, hivyo haiwezekani kujibu ruhusa ya mke ya kufunga (Funga ya Sunna) kwa kupata ruhusa ya msimamizi wa mume wake, au inaweza kuzingatiwa ruhusa ya msimamizi wa mume wake ikiwa huyu mgonjwa wa akili anadhurika kwa kukosa kuingilia, kwa sababu ruhusa katika hali hii sababu yake ni kuzuia madhara kwa mgonjwa wa akili, ni maamuzi yanayoangalia masilahi ya mgonjwa, tofauti na ikiwa kunamfaa au kutodhurika, kwa uwezekano wa kujirudia kwa hali ya matamanio kwa mke wake, na wakati huo kudhurika kwa kuzuia.
Miongoni mwa kauli: Ni pamoja na aliyosema mwanachuoni Al-Buhuty katika sharhe ya: [Muntaha Al-Iraadaat 3/147 Ch. ya Aalam Al-Kutub]:”Msimamizi wa mgonjwa wa akili ametoa talaka bila ya kitu mbadala kile anachomiliki akiwa na akili kisha akachanganyikiwa (akiwa ndani ya eda ya talaka akamrudia hata kama mke amechukia) hilo, kwa msimamizi wa mgonjwa kuchukua nafasi ya mume wake kwa kuhofia isije kwisha muda wa eda yake” na hii ni ruhusa yake kuwa msimamizi wa mgonjwa wa akili ana chukua nafasi ya mgonjwa ambaye yupo chini ya usimamizi wake.
Jambo la Nne: Ama swali kuhusu hukumu ya ndoa ya mlemavu wa akili ikiwa linafichwa lengo la kupata manufaa nyuma yake, tunasema: Hakika nia na kukusudia ni katika mambo ya ndani zaidi hawezi mtu yeyote kuyapitia, mazingatio katika makubaliano ni kwa matamshi yake na mjengo wake na wala sio makusudio yake wala maana zake, makubaliano yanakuwa ni sahihi madamu yameanzishwa yakiwa yamekamilika nguzo zake na sharti zake za wazi, nia ya kutumia vibaya makubaliano na kuiba nyuma yake ikiwa ndio kusudio la makubaliano yake hayo basi atapata dhambi kwa hilo, lakini upande wa dhambi ni tofauti na upande wa makubaliano, kwani upande wa dhambi si wenye kuathiri uhalali wa makubaliano, kama vile mtu aliyepora ardhi kisha akaswali kwenye ardhi hiyo, swala yake ni sahihi – ikiwa itakamilika nguzo zake na sharti zake - lakini wakati huo huo ana dhambi kwa sababu ya kupora kwake ardhi, na jukumu litaendelea kuwa naye wakati wote mpaka arudishe ardhi aliyopora, upande wa amri ya kuswali sio upande wa kukataza kupora.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas