Kuthibitisha Nasaba kwa Maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuthibitisha Nasaba kwa Maiti

Question

Swali la Kwanza: Ni muda gani wa mwisho kwa mtu aliyefariki kuthibitisha nasaba?
Swali la Pili: Ni njia zipi za kuthibitisha nasaba kwa mtu aliyefariki?
Swali la Tatu: Je inafaa nasaba kwa mtu aliyefariki pasina kuwepo kifungu cha sharia?
Swali la Nne: Je inafaa nasaba kwa mtoto wa zinaa?
Swali la Tano: Je alama za vidole inazingatiwa ni dalili ya mwisho ya kuthibitisha nasaba? Na ipi hoja ya hilo?
Swali la Sita: Je ni lazima kwa mtu yeyote kufanya uchunguzi wa alama za vidole na ni nani anayelazimisha hivyo? Je nasaba inayotakiwa kwake ni kama vile baba au mwingine, kwa maana je kuna ulazima kwa kile kinachoitwa kuwa wao ni ndugu yao kwa uthibiti wa alama za vidole?
 

Answer

Shukrani zote za Mwenyezi Mungu peke yake, sala na salamu ziwe kwa yule ambaye hakuna utume tena baada yake naye ni Mtume wetu Muhammad pamoja na watu wake na Masahaba wake na wale wote wanaomfuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Wanachuoni wa Sharia wamekubaliana kuwa inathibiti nasaba ya mtoto aliyekuwa tumboni kwa kukutana kimwili ikiwa ndani ya muda unaozingatiwa uwezekano wa mimba, na muda mchache wa mimba ni miezi sita kwa kuwepo tamko lake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili} [LUQMAAN, 14], ina maana kumaliza miaka miwili, na katika Aya nyingine inasema: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} [AL-AHQAAF, 15], jumla ya muda wa chini wa ujauzito kwenye Aya hizi mbili ni miezi sita ikiwa tutatoa kwenye muda wa pili muda wa kwanza, hiyo ni dalili ya tafsiri ya Ibn Abbas, wala hakuna tofauti kati hili kwa wanachuoni.
Ama muda wa mwisho wa mimba hakuna andiko linaloainisha, hivyo imekuwa muda wa mwisho ni wenye kufahamika kwa ufuatiliaji wa karibu ili kufikia uelewa, kwa sababu kila chenye kufaa kutokea kwake na kutotokea kwake hakiwezekani kufahamika isipokuwa kwa hisia au kwa kunukuu – kama alivyosema Imamu Al-Raazy katika kitabu cha: [Maalim Usuul Ad-Ddin Uk. – 23 – 24], ikiwa itakosekana nukuu basi hakuna kinachobakia isipokuwa ni hisia ya kuonekana kwake, amesema Ibn Khuweiz Mindaad: Uchache wa muda wa damu ya hedhi na nifasi na uwingi wake, na uchache wa muda wa ujauzito na uwingi wake huchukuliwa kwa njia ya kufanya jitihada, kwa sababu elimu ya hilo ipo kwa Mwenyezi Mungu tu, hivyo haifai kuhukumu kitu isipokuwa kwa kiwango ambacho tumeonesha, ni imekutwa wazi kwa wanawake katika hali chache au ya kawaida, pindi tulipomkuta mwanamke amekuwa na ujauzito kwa muda wa miaka minne na miaka mitano tukahukumu kwa muda huo, kwa upande wa damu ya hedhi na nifasi pindi tulipokosa uelewa sahihi tukarejea katika hali inayokuwepo kwa nadra sana kwa wanawake [Tafsiri ya Imamu Qurtuby 9/288 - Ch. ya Dar Ash-sha’ab], kwa sababu hii wanachuoni wametofautiana kuhusu muda wa mwisho wa mimba kutokana na kilichothibiti kwao kwa kufuatilia hali iliyopo kwa ukaribu, wametaja kutokana na uelewa wao muda wa mimba miaka miwili mitatu na minne, na hii ikiwa ni katika hali chache sana kutokea lakini hata hivyo imewahi kutokea, na linakuja hilo ni pale mwanamke anapokuwa katika hali hiyo basi alikuwa anaachwa mpaka anapojifungua hata kama utavuka muda wa ujauzito, hili likawa linapelekea kutokea hali nyingi za vifo kwa wanawake wajawazito ambao wamevuka muda, na wala hawakuwa wanasalimika isipokuwa ni katika hali chache sana, na sababu ya kutotokea hali hiyo hivi sasa ni kuwa kanuni na sheria za tiba zinazosimamia hali hii zinamzuia daktari kuruhusu kuendelea kubakia mtoto tumboni mwa mama yake zaidi ya muda maalumu, hii ni kwa sababu ya mara chache sana mtoto kuwa salama kwa kutofariki ikiwa mimba itavuka muda wa wiki 45, na kutotokea kwake sababu ni kuwa hilo linazuiliwa kuonekana, wala hayapingwi maelezo ya wanachuoni na Maimamu kwa kutotokea kwake hivi sasa, kwa sababu kutotokea hakuna maana ya kutokuwepo.
Sehemu ya maelezo ya wanachuoni kuhusu muda wa mwisho wa mimba na katika uhalisia ambao wamechukulia ushahidi wa kutokea kwake: ni kwa mwanamke ambaye unaonekana ujauzito na muda wake kuwa ni mrefu, na hivi sasa kudai uwepo wa mimba za muda wa zaidi ya muda wake pasi na kuonekana hizo mimba na alama zake basi haikubaliki kwa kudai tu, pamoja na wepesi wa kufikiwa kwa madai haya kupitia majaribio ya kitiba yanayoonesha idadi ya wiki za ujauzito.
Yaliyoteuliwa na kanuni za maisha ya ndoa nchini Misri miongoni mwa kauli za wanachuoni ni pamoja na yaliyoelezewa kwenye kipengele nambari 15 cha sheria namba 25 ya mwaka 1929 kuwa, haitosikilizwa wakati wa kukanwa madai ya nasaba kwa mtoto kwa yule aliyefiliwa na mume wake ikiwa madai hayo yatakuja baada ya muda wa mwaka mmoja tokea kutolewa talaka au kutokea kwa kifo.
Ama kuhusu swali la njia na namna ya kuthibitisha nasaba kwa mtu aliyefariki: Hilo linachukuliwa kisharia ni kuwa asili katika nasaba ni jambo la akiba, limeangaliwa na sharia kuthibiti kwake ni kwa njia yoyote inayowezekana, na miongoni mwa njia zenye kuzingatiwa katika kuthibiti nasaba kwa mtu aliyefariki: Ni kuthibiti hali ya ndoa iliyopo kati ya mume na mke wakati wa kuanza kwa ujauzito na sio wakati wa kuzaa, imepokelewa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Bibi Aisha na Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mtoto wa kitandani” kwa maana: Mtoto hunasibishwa kwa mwenye ndoa naye ni mume.
Na huthibiti nasaba pia kwa dalili ya wazi, nayo ni ushahidi wa wanaume wawili au mwanaume mmoja na wanawake wawili, na ushahidi wao unakuwa kwa uwepo wa ndoa kwa maana yake ya kisharia.
Wala hakuhusishi kuthibiti kwa nasaba kwenye ndoa sahihi tu, bali kunathibiti pia kwa ndoa mbaya na kuingilia kunako fananishwa, kama vile inafaa katika dalili ya ushahidi wa nasaba kwa kusikia na hayo yote ndio kauli yenye nguvu na kufanyiwa kazi katika Fiqhi ya Imamu Abu Hanifa, amesema katika kitabu cha: [Al-Hidaya na sharhe ya mwanachuoni Al-Baabarty]: “Haifai kwa shahidi kutoa ushahidi kwa kitu asichokiona isipokuwa kwenye nasaba kifo ndoa kuingilia na utawala wa kadhi, ambapo ananafasi ya kutoa ushahidi kwa vitu hivi ikiwa ameambiwa na mtu anaye muamini, kwani ikiwa ushahidi wa kusikia hautokubalika basi itapelekea uzito na kukwama kwa hukumu [7/388, 389 Ch. ya Dar Al-Fikr].
Vipengele viwili cha kwanza na cha pili katika mada ya nne ya sheria nambari 12 ya mwaka 1996 ikiwa imebadilisha sheria nambari 126 kuwa, mtoto ana haki ya kuwa na nasaba ya wazazi wake halali na kupata malezi yao, na ana haki katika kuthibitisha nasaba yake halali kwao kwa njia zote za kuthibitisha ikiwa ni pamoja na njia halali za kisayansi.
Miongoni mwa njia za kielimu za hivi sasa katika kuthibitisha nasaba ni pamoja na maumbile ya alama za vidole, maelezo yake ya kina yatakuja.
Sharia ya hali ya maisha ya ndoa ya mwaka 2000 katika kipengele nambari 7 pia kinasema: Haikubaliki wakati wa kukana madai ya kukubalika nasaba au ushahidi wa kukubali baada ya kufariki kwa mwenye kurithiwa isipokuwa ikiwa kutapatikana nyaraka rasmi au zimeandikwa zote kwa hati ya marehemu na kuwa na saini yake au dalili ya wazi inayoonesha uhalali wa madai haya.
Haya yote yamewekewa sharti la kuzaliwa kutokuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja wa kumalizika kwa ndoa sahihi kwa kifo au talaka au baada ya kumalizika kwa ndoa ya kufananishwa kwa kuacha, sawa na ilivyoelezewa na sheria ya Misri inayotokana na mitazamo ya wanachuoni wa Fiqhi katika masuala ya kutoa fursa katika hali chache kutokea, yote hayo ni pamoja na uwezekano wa kukutana kati ya mzazi wa kiume na wa kike, na uwezekano wa kuleta taswira ya ujauzito wa mzazi wa kike kutoka kwa mzazi wa kiume na kutokanusha mzazi wa kiume mtoto wakati wa kufahamu kwake, imekuja katika mada ya 15 ya sheria ya hali ya ndoa nambari 25 ya mwaka 1929 kuwa, haisikilizwi wakati wa kukanushwa madai ya nasaba kwa mtoto wa mama imethibiti kutokutana kati ya mke na mume wake tokea kufungwa kwa ndoa, wala kwa mtoto wa mama aliyekuja baada ya mwaka tokea kutoweka kwa mume, wala mtoto kwa aliyefiliwa na mume wake ikiwa atakuja kwa zaidi ya mwaka tokea kutoka kwa talaka na kifo.
Ama kuhusu nasaba ya mtoto wa zinaa: Wanachuoni wamekubaliana kuwa mtoto wa zinaa nasaba yake ni kwa upande wa mama yake ambaye amemzaa, na hilo ni kwa sababu upande wa mama ni uhusiano asili tofauti na upande wa baba ni uhusiano wa kisharia, hivyo haithibiti baba mzinifu kwa kuweka tone la maji kwa njia ya uzinzi.
Dalili ya hayo ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Mtoto ni wa kitandani na mzinifu hana haki ya kuwa na mtoto” inafahamika kuwa mtoto hunasibishwa kwa mume ambaye mwenye ndoa, na kutokana na ndoa hiyo ndio huthibiti sifa ya ubaba kisharia.
Kutokana na hilo wanachuoni wa Fiqhi katika wafuasi wa Imamu Abu Hanifa, Imamu Malik, Imamu Shafiy na Imamu Hanbali wamesema kuwa haithibiti nasaba ya mtoto wa zinaa kwa baba mzinifu, kitabu cha: [Tabyeen Al-Haqaaiq cha Zailai’i 6/241 – Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Islaamy], na kitabu cha: Sherh Saqhir cha Ahmad Dardir pamoja na Hashiyat As-Saawy 3/540 – Ch. ya Dar Al-Maarif, kitabu Kashaf Al-Qanaai 4/424 – Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kwa maelezo hayo, haifai kunasibishwa mtoto wa zinaa na baba yake tofauti na kunasibishwa kwa mama yake, wala kwa kukubali kuwa ni mtoto wake anayetokana na zinaa, kwa sababu maji ya zinaa huharibu, kunasibishwa kwa baba ni unasibishaji wa kisharia, haufikiwi isipokuwa kwa mujibu wa njia za kisharia ili kuthibitisha nasaba, maelezo yametangulia kuhusu njia ya kuthibitisha nasaba kwa mtu aliyefariki.
Ama kuhusu kuthibitisha nasaba kwa kutumia maumbile ya ncha za vidole kuna faa, kwa sharti la kuthibiti ndoa, na hili linakubaliana na madhehebu ya sharia katika kuangalia uthibiti wa nasaba, lakini haifai kisharia kutegemea hilo katika kukanusha nasaba, kwa sababu mtu inawezekana kukosea kwenye kuchambua, hivyo kutumika dhana katika njia ya kuthibitisha kwake inapelekea taarifa ya maumbile ya ncha za vidole kutokuwa na uwezo wa kukanusha nasaba iliyothibiti kwa njia ya kisharia, ama kuthibiti nasaba kwa vidole hivi kunaweza kukimbiliwa katika hali ya kuwepo ndoa sahihi au ndoa mbaya – kwa maana ile ndoa ambayo haijakamilika sharti zake na nguzo zake – au katika hali ya kuingilia kunako fananishwa, kama vile kumuingilia mwanamke kwa kudhania kuwa ni mke wake, vile vile inawezekana pia kutumia maumbile ya ncha za vidole katika hali ya mvutano wa kutofahamika kwa nasaba kwa sababu ya kukamilika kwa dalili au kuwa sawa, au kwa sababu ya kushiriki katika kuingilia kunako fananishwa na mfano wa hilo, na mfano wake: Ni pamoja na hali ya kufanana kwa watoto hospitali na vituo vya kulelea watoto na mfano wake, vile vile kufanana watoto wa bomba, na katika hali pia ya kupotea watoto na kuchanganyika kwao kwa sababu ya matukio au majanga au vita na kuwa ngumu kufahamika wazazi wao, au kuwepo miili ya wafu haikufahamika walikotoka, au kwa kukusudia kuchunguza utaifa wa mateka wa vita na wale waliopotea.
Kisharia hakuna kizuizi kulazimika mwenye kupinga kwa njia ya mahakama kufanya uchunguzi wa maumbile ya ncha za vidole ni sawa sawa kwa mwanamme au mwanamke au upande mwingine kama vile msimamizi na mlezi kwa mfano, na hilo ni pale mmoja wao au wote wawili anapodai kuwa na uhusiano wa mume na mke pamoja na kutokuwepo kizuizi cha kisharia cha kuzuia kuwepo kwa ndoa kati ya mwanamume na mwanamke, ikiwa haujathibiti uhusiano huo wa ndoa kati yao basi kutatakiwa ushahidi au shahada ya ndoa au mfano wa hayo, vile vile hali inapotokea uingiliaji wa mfanano au ndoa mbaya kati yao, uthibiti huu wa nasaba ya mtoto ukadaiwa na mmoja wao au wote wawili kuwa amezaliwa na wao, katika hali ya kukataa mwenye kudai kufanya uchunguzi uliotajwa basi kupinga kutazingatiwa ni dalili yenye nguvu ya kuthibiti nasaba ya huyu mtoto kwake, pamoja na kutoangalia kubakia kwa maisha ya ndoa na athari zinazo tokana, kwani kuthibitisha nasaba hakuna maana ya kuendelea kuwepo kwa maisha ya ndoa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi


 

Share this:

Related Fatwas