Kuheshimu Bendera na Kusimama kwa a...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuheshimu Bendera na Kusimama kwa ajili ya Wimbo wa Taifa.

Question

Natarajia kupata ufafanuzi wa hukumu ya kuheshimu bendera na kusimama kwa ajili ya wimbo wa amani wa Taifa, ambapo baadhi ya watu wanadai kwamba jambo hili ni haramu kisheria; kwa sababu ya kuitukuza bendera, na utukufu hauruhusiwi kwa kiumbe yeyote, na haswa ikiwa kitu hakina uhai, basi kwa wakati huo ni ushirikina au ni sababu ya kuuelekea ushirikina. Vile vile hii ni kujifananisha na tabia mbaya za makafiri, pia inazingatiwa kuwa ni uzushi, kwa sababu haikuwepo katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala katika zama za makhalifa wake R.A.. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Bendera ina maana kadhaa katika lugha, ikiwa ni pamoja na: upambanuzi wa nchi mbili, na pia ina maana ya kitu kilichowekwa katika njia kinachoongoza, mlima, mchoro katika mavazi, na bendera [Rejea: Taji Al-Arus kwa Al-Zubaidi 33/131, 132, Ch. Dar Al-Hidaya]. Inayomaanisha hapa: ni bendera, ambayo sasa ni alama ya nchi na alama ya serikali.
Kuzingatia bendera ni alama iliyokuwa inajulikana kwa Waarabu kabla ya Uislamu, haswa katika vita. Na imepokewa kwamba Mtume S.A.W. amechukua bendera, na wanavyuoni wa Hadithi wameandika katika vitabu vyao kuhusu bendera; walisema: “Sura katika bendera” [Sunan Abu Dawud], “Yaliyotajwa kuhusu bendera” [Sunan Al-Tirmidhiy], “Yaliyotajwa kuhusu bendera na mabango” [Sunan Al-Baihaqiy], na kadhalika.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas, R.A. amesema: “Bendera ya Mtume S.A.W. ilikuwa nyeusi na nyeupe”. Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud kutoka kwa Sammak kutoka kwa mtu wa watu wake kutoka kwa mwingine wao R.A. amesema: “Nimeiona bendera ya Mtume S.A.W. ilikuwa rangi yake ni manjano”. Imepokelewa vile vile kutoka kwa At-Tirmidhiy kutoka kwa Jabir R.A. kwamba Mtume S.A.W. aliingia Makka na bendera yake ilikuwa nyeupe, na imepokelewa kutoka kwa Ahmad na Ibn Majah kutoka kwa Al-Harith Bin Hassan Al-Bakriy R.A. alisema: “Tumekuja Madina wakati ambapo Mtume S.A.W. alikuwa juu ya mimbari na Bilal akisimama mbele yake Mtume akiwa kavaa upanga wake, na zikiwa bendera nyeusi, niliuliza: Je! Ni bendera gani hizi? Wakasema: Amr Bin Al-Aas amekuja kutoka vitani”.
Al-Haafiz Ibn Hajar alisema huko kwenye kitabu cha: [Fath Al-Bariy 6/127, Dar Al-Maarifa] kuwa: “Mtume S.A.W. alikuwa katika vita akampa mkuu wa kila kundi bendera ili wapigania vita chini yake”.
Kuhusu maana ya bendera, ni kawaida kwamba adui hulenga kumpiga mtu anayebeba bendera kabla ya mwingine, ili kukatisha tamaa jeshi; wakati bendera ilipoinuliwa hiyo ilikuwa ishara ya kiburi, nguvu, uthabiti, na wakati ilipoanguka ilikuwa ishara ya kushindwa na kufedhehesha na kukataliwa, vile vile anayebeba bendera huwa na hamu kubwa sana ya kuifanya bendera iinuke, hata akiwa atatoa roho yake mwenyewe, sio kwa ajili ya kutukuza kitambaa, lakini kwa ajili ya maana yake.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhaariy katika Sahihi yake kutoka kwa Anas Bin Malik R.A. kwamba alisema: Mtume S.A.W. alisema: Zayd alichukua bendera na akajeruhiwa - hiyo ni, katika vita vya Muutah – kisha Jaafar akaichukua na akajeruhiwa, halafu Abdullah Ibn Rawaha akaichukua na akajeruhiwa, na macho ya Mtume S.A.W. yakamiminika machozi - Khalid bin Al-Walid akaichukua bila amri -kutoka kwa Mtume- basi akafungua).
Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim katika Al-Mustadrak kutoka kwa Ibn Abbas, R.A., amesema: Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alipokuwa amekaa na Asmaa Bint Umais akiwa karibu yake pindi alipoitikia salamu, kisha akasema: "Ewe Asmaa, huyu ni Jaafar bin Abi Talib na Jibril na Mikail na Israfil wametusalimia uitikie salamu yao. Akaniambia kuwa amekutana na washirikina siku fulani na fulani kabla ya kupita kwa Mtume S.A.W. kwa siku tatu au nne. Akasema: nimekutana na washirikina nikajeruhiwa mwilini mwangu kutoka upande wa mbele kati ya mapigo na kuchomwa mara sabini na tatu, kisha nikachukua bendera kwa mkono wangu wa kulia, ukakatwa, nikaichukua kwa mkono wangu wa kushoto ukakatwa. Basi Mwenyezi Mungu alinilipa mabawa mawili ili niruke na Jibril na Mikael ili nishuke peponi mahala ninapotaka, na kula matunda yake kama nitakavyo", Asmaa alisema: Hongera sana kwa Jaafar kwa yale mema ambayo Mwenyezi Mungu amemruzuku, lakini ninaogopa kwamba watu hawaamini, Mtume S.A.W. akapanda mimbari ili kuwambia watu habari ile, akapanda mimbari akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifu halafu akasema: "Enyi watu, hakika Jaafar pamoja na Jibril na Mikael ana mabawa mawili ambayo Mwenyezi Mungu alimpa badala ya mikono yake, na Jaafar akanisalimia". Kisha akawaambia jinsi alivyokuwa alipokutana na washirikina, baada ya siku ile watu walijua kama alivyowaambia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwamba Jaafar R.A. alikutana nao; kwa hivyo aliitwa arukaye peponi.
Kuhusu kuitolea heshima bendera kwa mkono kwa njia fulani, au kwa kuomba dua wakati wa kuinuliwa kwa kusema idumu nchi, ni kama harakati au maneno tu, na kuizoea hali hii na kukaririwa - kama ilivyotokea - inafanya hali ile miongoni mwa mambo ya mila; kwani mila ni: mambo yanayokubalika kufanywa na watu wa jamii fulani na yanakaririwa [Al-Mufradat kwa Raghib Al-Aswfahaniy Uk. 594, Dar Al-Qalam]. Asili ya hali ile inaruhusiwa, isipokuwa kama kuna dalili ya kuizuia; Mwenyezi Mungu amesema: (naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni) [AL ANAAM: 119], na imepokelewa kutoka kwa At-Tirmidhiy kutoka kwa Salman, R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: "Halali ni ile aliyoihalilisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake, na haramu ni ile aliyoharimisha Mwenyezi Mungu, na yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa msamaha wake).
Kuhusu mazoea na vitendo hivi ndivyo vimehusishwa na upendo wa nchi, vitendo hivyo vilikuwa njia ya jumla ya kuelezea upendo wa nchi na kuonesha undugu na kuthibitisha uaminifu, iliamuliwa katika misingi ya Sharia kuwa njia zina hukumu za makusudi, ikiwa upendo wa nchi ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kama ilivyoelekezwa katika dalili za Sheria, basi njia yake inayoruhusiwa katika asili yake pia inatakiwa, na hii inathibitishwa ikiwa kutosimama kwa watu kunamaanisha kutoheshimu.
Kuhusu wimbo wa taifa, ni wimbo wa kimuziki ambao ni wimbo wa nchi au wa nyumbani, ambao ni ishara ya nchi au ya nyumbani, hucheza katika matamasha ya jeshi na hafla kadhaa za umma.
Na rai iliyochaguliwa ni kwamba kusikia au kucheza muziki si haramu; kwani ni sauti; nzuri yake ni nzuri na mbaya yake ni mbaya, na kile kilichoelezewa katika kuharimishwa kwake ni: ukweli wake sio wazi, na uwazi wake sio kweli.
Na kutoa hukumu ya kutoharimisha imepokelewa kutoka kwa Abdullah bin Omar, Abdullah bin Zubair, Amr Bin Al-Aas, na masahaba wengine, R.A., na kutoka kwa wafuasi: Kharjah Bin Zaid, Saeed Bin Al-Musayyib, Ataa, Ashaabi, na wengi wa wanavyuoni wa fiqhi wa Madina, na miongoni mwa walio baada yao ni: Abu Mohammed Bin Hazm, Sheikh Abu Ishaq Al-Shirazi, Sheikh Abdul Ghani Al-Nabulsi, na wengine wengi. Wakati Sheikh Izz Al-Din Bin Abd Al-Salam alipoulizwa kuhusu zana zote za muziki, alisema, “Inaruhusiwa.” Sheikh Sharaf Al-Din Al-Tilmisani alisema, "Sheikh Izz Al-Din Bin Abd Al-Salam anakusudia kwamba hakuna dalili sahihi kutoka Sunna kuwa zana hizi ni haraamu”. Sheikh Izz Al-Din Bin Abd Al-Salam amesikia maneno haya akasema: “Hapana, nakusudia zana hizi inaruhusiwa.” [Imepokewa kutoka kwa Farah Al-Asmaa Birukhsi Samaa, kwa Abu Al-Mawahib Ash-Shazliy Uk. 12, India].
Baadhi ya wanavyuoni wengine walisema pia kuwa zana za muziki zinaruhusiwa miongoni mwao ni: Ibn Hazm, Ibn Al-Samaani, Ibn Al-Qaysrani, Ad-Adfawiy, Abu Al-Mawahib Ash-Shazliy Al-Maliki na wengineo.
Hukumu ya wimbo wa taifa ni ile ile hukumu ya bendera; ambapo zote ni alama tu, na kusimamia wakati wa kuibwa kusudio lake ni kuonesha tu heshima na kuthamini kwa kile kinachowakilisha nchi.
Na kupenda nchi ni jambo ambalo binadamu alilozoea; hata baadhi ya wanafalsafa walisema: “Silika ya mwanadamu huwa na upendo wa nchi yake” [Al-Haniin lelawtaan kwa Al-Jahidh, Uk. 10, Dar Al-Kitab Al-Arabiy].
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhaari kutoka kwa Hamid Al-Taweel kwamba amesikia Anas R.A. akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alikuwa akirudi kutoka safari, akiona daraja za Madina, huenda haraka kwa ngamia wake na kama akipanda mnyama humharakisha. Al-Bukhaari alisema: “Al-Harith Bin Omair aliongezeka kutoka kwa Hamid: (humharakisha mnyama kwa sababu ya upendo wake kwa Madina).”
Al-Haafiz ibn Hajar alisema katika kitabu cha: [Fath Al-Bariy 3/621, Ch. Dar Al-Marifa]: “Hadithi hii ina ishara ya... uhalali wa upendo wa nyumbani na hamu yake”.
Imam Ibn Batwal alisema katika maelezo yake [4/453, Maktabat Ar-Rashiid]: "Kauli yake: (kwa sababu ya upendo wake kwa Madina); inamaanisha: kwa sababu ni nchi yake, na ndani yake familia yake na mtoto wake ambao ni watu anaowapenda zaidi, Mwenyezi Mungu ameziumba roho kwa kupenda nchi na ameweka ndani yao hamu ya nyumbani, na hivyo ndivyo Mtume S.A.W. alivyofanya naye ni mfano mzuri wa kuigwa”.
Na kuelezea kwa upendo huu uliomo kwenye Hadithi una kazi na udhihirisho, pamoja na kile kilicho katika maneno na kile kilicho katika vitendo.
Asili ya yote hayo inaruhusiwa hadi dalili inapofika, na kati ya vitendo vingine vinavyoonesha upendo kusimama kwa ishara ya nchi na nembo yake, ambayo ni bendera au ni wimbo wa taifa; mpenzi anashughulikia kila kitu kinachohusiana na mpendwa wake, na haizingatiwi ni ubaya isipokuwa ambao umezingatiwa ni umbaya na Sheria.
Kuhusu madai kwamba hii ni haramu, kwa sababu ya utukufu wake, na utukufu hauruhusiwi kwa kiumbe, haswa kikiwa hakina uhai, inajibiwa kuwa huu ni utukufu, lakini kusema kwamba utukufu kabisa hauruhusiwi kwa kiumbe huo ni uongo, lakini kisicho halali ni kumwabudu kiumbe anayetukuzwa, kama watu wa Jahiliya walivyotukuza masanamu yao, wanafikiri kuwa wao ni miungu na wanadhuru na kunufaisha bila Mwenyezi Mungu, na huu ni ushirikina. Kama ni kwa jambo lingine lolote, ambalo linaonesha heshima, Utukufu, linaruhusiwa, ikiwa kinachotukuzwa kinastahili kutukuzwa, hata kikiwa hakina uhai. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Urwa Bin Az-Zubayr, R.A., akielezea masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akasema: “Masahaba walikuwa hawamwangalii Mtume S.A.W. kwa kumtukuza kwake.”
Imepokelewa kutoka kwa Ahmad na Al-Hakim kwamba Aisha, R.A. amesema: “Nimeona katika Utukufu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwa mjomba wake - yaani: Abbas - ni ajabu.”
Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika Musnad yake kwamba Mtume S.A.W. alikuwa akiona Kaaba huinua mikono yake, na kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu, iongezee nyumba hii heshima, utukufu, ukarimu na mapenzi".
Imepokelewa kutoka kwa Ad-Darmiy kutoka kwa Ikrima ibn Abi Jahl R.A. kwamba alikuwa akiweka Mus-haf (Qur`ani) usoni mwake akisema: “Kitabu cha Mola wangu, Kitabu cha Mola wangu”.
Imam Malik alisema katika kitabu cha: [Muwatwa' 1/265, Emirates]: "Inasemekana: kutoka Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumtukuza mzee ambaye ni Muislamu".
Hii inamaanisha kuwa kuna tofauti kubwa kati ya njia na ushirikina. Njia iliyoamriwa na Sharia ni: kumkaribia Mwenyezi Mungu na yote ambayo ameyaamuru, na kila kinachotukuzwa na Mwenyezi Mungu kinaingia katika Utukufu huu pamoja na mahali, nyakati, watu na hali; kwa mfano, Muislamu hutafuta kussali katika Msikiti Mtakatifu na kuomba dua kwenye kaburi la Mtume S.A.W. na kuomba dua vile vile kwenye Al-Multazam (Kikuta cha Kaaba baina ya Hajaril Aswad na Mlango wa Kaaba) kwa ajili ya kutukuza kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu amekitukuza kutoka mahali. Na Muislamu hutafuta kuswali katika usiku wa Qadar, na hujitahidi kuomba dua katika saa ya kujibiwa dua siku ya Ijumaa, katika thuluthi ya mwisho ya usiku kwa ajili ya kutukuza kile kinachotukuzwa na Mwenyezi Mungu kutokana na wakati. Pia Muislamu humkaribia Mwenyezi Mungu kupitia kuwapenda waja wema kwa ajili ya kutukuza wale wanaotukuzwa na Mwenyezi Mungu kutokana na watu. Aidha hujitahidi kuomba dua wakati wa kuonyesha mvua na wakati mwingine kwa ajili ya kutukuza ile inayotukuzwa na Mwenyezi Mungu kutokana na hali.. Na hivyo; yaani, ni kutukuza kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kutukuza kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: {Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.} [AL HAJJ: 32] Kama kwamba kumtii Mtume S.A.W. ni kama kutii kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyemtuma: {Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu} [AN NISAA: 80], na kufungamana na Mtume ni kufungamana na Mwenyezi Mungu Mtukufu Mtukufu: {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu} [AL FATHU: 10].
Kuhusu “Shirki” ni utukufu wa kitu pamoja na Mwenyezi Mungu au utukufu bila Mwenyezi Mungu, kwa hivyo, Malaika waliposujudu kwa Adamu R.A. hali hii ilikuwa imani na kupwekesha. Lakini wenye kusujudia masanamu hali yao ni ukafiri na ushirikina, ingawa aliyesujudiwa kwake katika hali hizi mbili ni kiumbe. Wakati sujudu ya Malaika kwa Adam ilipokuwa ni kwa ajili ya kutukuza Amri ya Mwenyezi Mungu ilikuwa njia halali ambayo mwenye kuifanya anastahiki kulipwa thawabu, na wakati sujudu ya wanaoabudu masanamu ilikuwa kwa ajili ya kutukuza kama kumtukuza Mwenyezi Mungu, basi hali hii ilikuwa ushirikina na mwenye kuifanya anastahiki kuadhibiwa.
Kwa msingi huu, kuna tofauti kubwa kati ya kusimama kwa ajili ya ibada na kusimama kwa heshima. Ya kwanza ni marufuku isipokuwa kwa Allah, na ya pili imetajwa katika Sunna ambayo inashuhudia kwa kuruhusiwa kwa mfano wake kwa viumbe. Katika Sahihi mbili kutoka kwa Hadithi ya Abi Saeed Al-Khudri R.A. kwamba Saad bin Muaadh wakati alipokuja Mtume S.A.W., Mtume akasema kwa Al-Answaar: "Simameni kwa bwana wenu".
Al-Khatib Al-Sherbiniy katika kitabu chake: [Al-Mughniy Al-Muhtaaj 4/219, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] alisema: “Inaruhusiwa kusimamia watu wenye fadhila pamoja na elimu au wema au heshima au hivyo; kuheshimu sio kwa unafiki. Alisema katika kitabu cha Ar-Rawdhah: “Imethibitishwa katika suala hili Hadithi sahihi”.
Wanazuoni wamesema kwamba inapendekezwa kusimama kwa ajili ya Qur`ani; Imam Al-Nawawi alisema katika kitabu chake: [Al-Tibian fi Adaab Hamalatil Qur`ani” Uk. 191, Ch. Dar Ibn Hazm] kuwa: “Inapendekezwa kusimama kwa ajili ya Qur`ani, kwa sababu inapendekezwa kusimama kwa wenye fadhila pamoja na wenye elimu na watu wema, hivyo, Qu`rani ni muhimu zaidi”.
Wanavyuoni walisema kwamba kufuatana na mila kusimama ni ishara ya heshima, hali hii inafanya kuacha kusimama kwa kile kinachostahiki kuheshimiwa zaidi ni karibu na kulaaniwa; Sheikh Taqi Al-Din Ibn Taimiyah Al-Hanbaliy alisema katika kitabu cha: [Al-Fatwa Al-Kubra 1/49, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kwamba: “Ikiwa watu walizoea kusimama kwa kila mmoja, inaweza kusemwa: Ikiwa wataacha kufanya hali hiyo kwa Qur'ani haikuwa vizuri, watakuwa karibu na kulaaniwa; ambapo wanasimamiana, na hawafanyi hali hii kwa Qur`ani, ambayo inastahiki zaidi ya hivyo; Ambapo ni lazima iheshimiwe na kuongeza ile ambayo haifai kwa nyingine ... Wanavyuoni wakubwa wametaja mara nyingi hali ya kusimama watu kwa ajili ya Qur`ani pasipo na kukataa”.
Na hali ya kusimamia elimu au unaposikia wimbo wa taifa ina mfano wake katika kazi ya Waislamu wa zamani, baadhi ya wanavyuoni wamesema kwamba miongoni mwa adabu nzuri ni hali ya kusimama wakati wa kusikia jumbe za mwenye mamlaka. Walichukua kutokana na hivyo kipaumbele cha kusimama kwa ajili ya Qur`ani, na kuacha kusimama kwa ajili ya heshima ilikuwa zamani tu. Watu walipozoea kusimamiana na ilikuwa kuiacha hali hii inaonekana kuwa na wasiwasi, hukumu yake ilikuwa kupendekeza badala ya kuruhusiwa; imetajwa katika kitabu cha: [Ghayatul Muntaha] kwa Sheikh Marei Al-Karmiy na maelezo yake [Matalibu Uli Nuha kwa Sheikh Mustafa Ar-Rahibani kutoka vitabu vya mabwana wanaofuata madhehebu ya Imam Ahmad bin Hanbal [1/157, 158, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy]: “(Na) inaruhusiwa (kusimama kwake - yaani: kwa Qur`ani) - Sheikh Taqi Al-Din alisema: Ikiwa watu walizoea kusimamiana, basi kusimama kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur`ani) ni muhimu zaidi. Katika kitabu cha: [Al-Futruu] na kitabu cha: [Al-Mubdiy]: inachukuliwa kutoka kwa kitendo cha Ahmad kuruhusiwa; hivyo, Ibrahim Bin Tahman ametajwa jina lake wakati alikuwa akijinyoosha, akaketi sawasawa, akasema: haiwezekani kutajwa watu wema wakati wa kujinyoosha. Ibn 'Aqil alisema: Nilifahamika kutoka maneno haya tabia nzuri ambayo watu hufanya wakati wa kutaja maimamu au kusikia jumbe zao. Alisema katika kitabu cha: [Al-Furuu]: inajulikana kwamba suala letu ni muhimu zaidi. Ibn Al-Jawziy alisema hali ya kuacha kusimama ilikuwa zamani iliyopita, kisha wakati ilipokuwa hali ya kuacha kusimama ni kama kupuuza kwa mtu, ilikuwa inapendekeza kusimama kwa yule anayestahiki hivyo.
Kusimama kwa Qur`ani au kwa anayekuja ambaye ni mwenye shani sio isipokuwa kuonesha heshima, na wanavyuoni walisema hivyo. Si vibaya kusimama wakati wa kuinua bendera au wimbo wa taifa, kwani sababu ni moja.
Kuhusu madai kwamba kufanana na makafiri katika tabia zao mbaya, hatukubali kuwa hii ni moja ya tabia ya makafiri ambayo inahusiana nao, bali madai hayo hayana dalili, na kama ni kweli tutajibu kuwa tabia hii haijahusiana nao siku hizi, lakini ilikuwa ni tabia ya Waislamu na waliizoea mpaka ikawa inaingia katika msingi usemao: “Inasamehewa kwa kitu kinachozoeleka lakini haisamehewi kwa kitu mwanzoni” [Al-Manthur kwa Az-Zarkashi 3/375, Ch. Wizarat Al-Awqaf nchini Kuwait].
Ikiwa ni kufanana nao, kuiga tu sio haramu isipokuwa kwa mambo yanayohusiana na itikadi yao ya kidini, na dalili nyingi zimetajwa kuhusu suala hilo; zikiwemo: kwamba Mtume S.A.W. aliamuru kubadilishwa kwa nywele kijivu, alisema kama ilivyopokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi na wengine kutoka kwa Abu Hurairah R.A.: "Zibadilini mvi kwa kuzipaka (hina n.k), wala msijifananishe nao Mayahudi", na Masahaba wengi walikuwa hawazipaki, na hakuna Hadithi yoyote inayosema kwamba waliozipaka wamewakanusha kwani wamefanya mwiko kwa kutopaka kwa sababu ya ufananisho uliokatazwa.
Imepokelewa kutoka kwa Imam At-Tabari katika kitabu cha [Tahdhibul Athaar Uk. 518, Ch. Dar Al-Mamuun Lel Turaath] makubaliano kuhusu kubadilisha kwa mvi na kukataza ufananisho hapa ni kwa kuchukiza sio kwa kuharimisha.
Zikiwemo Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Dawood kutoka kwa Shaddad Bin Aws R.A. kwamba Mtume wa Allaah S.A.W. alisema: “Tofautianeni na Wayahudi, hawasali wakivaa viatu vyao, wala wakivaa khofu zao.” Lakini haikupokelewa kutoka kwa mmoja wa wanavyuoni kwamba ni lazima kuswali kwa kuvaa viatu, bali walitofautiana kuhusu hukumu yake ikiwa inapendekeza au inaruhusiwa au inachukiza [Faidh Al-Qadiir 4/67, Ch. Al-Maktabah Al-Tujariyah Al-Kubra].
Zikiwemo Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Amr Bin Al-Aas, R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: "Tofauti baina ya saumu yetu na saumu ya watu wa kitabu (Mayahudi na Manasara) ni kula daku.). Na inapendekeza kula daku, ilipokelewa kutoka kwa Imam Ibn Al-Mundhir makubaliano juu ya hilo katika kitabu chake "Al-Ijmaa" [Uk. 49, Ch. Dar Al-Muslim].
Zikiwemo Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Saad katika kitabu cha: [Al-Tbaqaat 1/159, 160, Ch. Dar Swadir] kutoka kwa Ibn Abbas, R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alimwambia Jaafar Bin Abi Talib, R.A.: "Ewe Jaafar, wewe unanifananisha katika tabia na sura", Jaafar akamzunguka Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akicheza, Mtume S.A.W. akamwambia: "Hii ni nini, ewe Jaafar?". Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, An-Najashi alikuwa kama akimridhisha yeyote akiruka juu ya mguu mmoja kumzunguka.
Inavyoonekana, hii ilikuwa mila ya Wakristo wa uhabeshi, hii ni idhini ya Mtume S.A.W., kwa sababu hakukataa kwa Jaafar hali yake ya kujifananisha na Wakristo wa uhabeshi, hii ni matini wazi kwamba ukiukaji huo sio lazima.
Na zikiwemo Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Hakim katika Al-Mustadrak kutoka kwa Ibn Abbas, R.A. akasema: Fatima, R.A., alikuwa mgonjwa sana, alimwambia Asmaa binti Umais, R.A.: Je! Hauoni kwamba ninabebwa kitandani? Asmaa R.A. alisema: naapa nitakufanyia jeneza, kama nilivyoona katika uhabeshi, alisema: nioneshe. Ibn Abbas akasema: alimtuma Asmaa kwa ajili ya kuleta makuti yenye maji, akakata kwa panga, na kutengeneza jeneza juu ya kitanda, ambayo ilikuwa jeneza la kwanza, Fatima R.A. alitabasamu, na sikumwona akitabasamu baada ya kufa kwa baba yake isipokuwa siku hiyo tu, kisha tukambeba na kumzika usiku. Wakati huu Masahaba Wenye Heshima, R.A. walikuwa wakihudhuria na hawakukana mmoja wao kwa alivyofanya Fatima, R.A. kwamba kwa hali hii anajifananisha na Wakristo wa uhabeshi, basi ilikuwa makubaliano yao kupitia kunyamaza nayo ni hoja.
Alisema katika kitabu cha: [Jamil Jawami] na maelezo yake kwa mwanachuoni Al-Mahali [2/221 – pamoja na Hashiyatul Atwar-, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kuwa: “(na sahihi) ni kwamba makubaliano ambayo kupitia kunyamaza ni - (hoja) kabisa”.
Na miongoni mwa wanavyuoni walioashiria kuwa kujifananisha na wasio Waislamu sio marufuku ni: Al-Hafiz Ibn Hajar katika kitabu cha: [Fathul Bari 10/98, Ch. Dar Al-Maarifa] Aliposema juu ya sababu ambazo kwa ajili yao yalikatazwa matumizi ya vyombo vya dhahabu na fedha, alisema: “Ilisemwa: sababu ya kukatazwa ni kujifananisha na Uajemi. Na suala hilo lina wasiwasi, kwa uthibitisho wa onyo kwa mtendaji wake. Na kwamba kujifananisha nao tu hakufiki kwa hivyo.
Imam Al-Muwaq Al-Maliki alisema katika kitabu cha: [Sunan Al-Muhtadin fi Maqamat Addin Uk. 249 Ch. Muasasat Sheikh Murabih Rabah katika Moroko]: “Maimamu ninaowaamini walisema kuwa sio kila kitu kilichofanywa Uajemi kilikatazwa kufanywa, isipokuwa kama sheria ikikikataza na misingi ilibainisha kukiachwa ... Na kukataza kule kunahusiana na wanachofanya kinyume na makusudi ya sharia yetu, na walichokifanya kulingana na kupendekeza au kulazimisha au kuruhusiwa katika sharia yetu, tusikiachie kitu hiki kwa sababu wale wanakifanya; kwani Sharia haikukataza kuiga wale wanaofanya kile kilichoidhinishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mtume alichimba Khandaki mjini kujifananisha na Uajemi, hadi wakashangaa Al-Ahzaab, kisha waligundua kuwa hiyo ni ishara ya Salman Al-Farsi”.
Halafu, kama tukikubali kuwa kuwaiga wasio Waislamu ni marufuku katika aina zote, tukio la kawaida la kile ambacho ni sawa na kazi ya watu wa kitabu haziitwi kuiga isipokuwa kama mwigizaji akitarajia kupata kujifananisha nao.
Miongoni mwa misingi ya Sharia kuzingatia kwa makusudi ya aliyekalifishwa, na hii pia inathibitishwa na: iliyopokelewa kutoka kwa Imam Muslim kutoka kwa Jaber bin Abdullah, R.A., akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa mgonjwa tukaswali nyuma yake alipokuwa akiketi, akatugeukia akatuona tukisimama, akatuashiria, tuketi, alipomaliza swala yake akasema: "Mmekaribia kufanya kitendo cha Uajemi na Warumi; walikuwa wanaketi juu ya wafalme wao ambapo wameketi, msifanye hivyo, wafuateni Maimamu wenu; anaposwali amesimama swalini mmesimama. Na aliposwali ameketi, basi swalini mmeketi" Lakini Masahaba wakati wasipokusudia kujifananisha sifa ile ileondolewa kwa mujibu wa Sharia. Muislamu ambaye anaiheshimu bendera au anasimama kwa ajili ya wimbo wa taifa hakukusudia kuiga wasio Waislamu.
Imam Al-Twahtawiy alisema katika kitabu cha: [Hashiyat Maraqi Al-Falah 1/336, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Hali ya kuiga watu wa kitabu haikuchukiza hata kidogo; tunakula kama wanavyokula na kunywa kama wanavyokunywa, lakini ni marufuku kuwaiga wakati ilikuwa na lawama na nia ya mwenye kuiga, alisema rai hii Qadhikhan katika Sharul Jamii As-Saghiir”.
Mwanachuoni Ibn 'Abdiin alisema katika kitabu cha: [Radul Muhtaar 1/624, Ch. Dar Al-Fikr] - akitoa maoni yake juu ya maneno ya mwenye kitabu cha: [Ad-Durr Al-Mukhtar]: “(Hali ya kuwaiga - yaani: watu wa kitabu – haikuchukiza kabisa) - tunakula na kunywa kama wanavyofanya ... Na inathibitishwa kwa iliyotajwa katika kitabu cha: [Adh-Dhakhirah] kabla ya kitabu cha: [At-Tahariy]. Hisham alisema: Nimeona Abu Yusuf akivaa viatu viwili vimeshonwa na misumari nikamwuliza: huoni misumari hii ni mibaya? Akasema: Hapana, nikasema: Sufyan na Thaur Bin Yazid wanaona kuwa inachukiza, kwa sababu ni kujifananisha na watawa. Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amevaa viatu vyenye nywele, navyo ni vya watawa. Hadithi hii imeonesha kuwa hali ya kujifanana inayohusiana na maslahi ya watu haina madhara; kuna ardhi ambayo haiwezekani kusafiri umbali wa mbali tu isipokuwa kwa aina hii ya viatu.
Kuhusu madai kwamba huu ni uzushi, kwa sababu haikuwa katika wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., wala katika enzi ya makhalifa wake wazima, R.A. Tunasema: "Tukikubali kuwa huu ni uzushi, lakini hailazimishi kuharimisha, kwani uzushi una hukumu tano za Sharia, na uzushi hauhusiani na vitu vilivyozuiliwa, bali uzushi ni sehemu na vitu vilivyozuiliwa ni sehemu nyingine".
Sheikh wa Uislamu Imam Izz Al-Din Bin Abd As-Salam alisema katika tasnifu yake: [Qawaid Al-Ahkam fi Masalih Al-Anaam 2/204, 205, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kuwa: Uzushi ni: Kufanya kile kisichozoeleka katika enzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. Uzushi umegawanywa katika: uzushi wa lazima, uzushi marufuku, uzushi unaopendekeza, uzushi unaochukiza, na uzushi unaoruhusiwa, na njia ya kujua aina ya uzushi ni kulingana uzushi na Sheria. Kama uzushi huu umeingia katika misingi ya lazima, basi ni lazima, ukiwa umeingia katika misingi ya kukataza, basi ni haramu, ukiwa umeingia katika misingi inayopendeza, basi inapendeza, ukiwa umeingia katika misingi inayochukiza, basi unachukiza, na ukiwa umeingia katika misingi inayoruhusiwa, basi unaruhusiwa. Uzushi unaolazimishwa una mifano mingi; miongoni mwake: kushughulikia elimu ya sarufi ambayo maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume wake S.A.W. yanaeleweka kupitia elimu hii, na uzushi huu ni lazima; kwani kuhifadhi Sheria ni wajibu, wala haihifadhiwi isipokuwa kufahamu elimu hii, kwa hivyo, jambo linalosaidia kutekeleza jambo lingine ambalo ni wajibu hukumu yake ni wajibu pia. Kuhusu uzushi unaokatazwa una mifano; ikiwemo: Swala ya Tarawih… uzushi unaochukiza una mifano; ikiwemo: kuweka mapambo juu ya Mushaf. Na uzushi unaoruhusiwa una mifano; ikiwemo: kushikana mikono baada ya Swala ya Asubuhi na Swala ya Al-Asiri.
Suala letu hili linafanana na suala lingine; nalo ni suala la kuubusu mkate kwa nia ya kuheshimu neema, na uhusiano uliopo kati ya masuala hayo mawili: Ni nia ya kuheshimu bila ya kuzingatia kitu kinachoheshimiwa, lakini kinazingatiwa kile kinachowakilisha, Al-Jalal As-Suyuti aliulizwa je, suala hilo ni uzushi? Alisema katika kitabu chake cha: [Al-Hawi Lilfatawa” 1/221, Ch. Dar Al-Fikr] kuwa: ni sahihi kwamba kuubusu mkate ni uzushi, lakini hukumu ya uzushi siyo haramu tu, bali uzushi umegawanywa kwa hukumu tano. Hakuna shaka kwamba hii haiwezikani kuwa haramu kwa sababu hakuna dalili inayothibitisha uharamu wake, au inachukiza; kwani jambo linalochukiza ni lile linalohusiana na katazo maalumu, na suala hilo halikukatazwa. Na jambo linaloonesha kwamba uzushi huu unaruhusiwa ni kwamba unatendwa kwa nia ya kuheshimu, na kwa ajili ya Hadithi zilizopokelewa kuhusu kuheshimu, basi suala hili ni nzuri.
Mwanachuoni Ibn Abdiin alitaja hukumu hiyo katika maandishi yake [6/384, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kutoka kwa wanavyuoni wanaofuata madhehebu ya Shaafi kwa ujumla, halafu akasema: “Na Sharia yetu hailikatazi suala hilo”.
Ikiwa imeamuliwa kutoka kwa yaliyotangulizwa kwamba suala linaloulizwa linaruhusiwa katika Sharia kwa asili yake, na ukweli wa jambo linaloruhusiwa ni kwamba inaruhusiwa kulifanya au kuliacha, basi wakati watu walipofahamu kuwa kuheshimu bendera ni ishara ya kuiheshimu nchi na ishara ya kuipenda na njia ya kuonesha hivyo katika maswala ya kitaifa na uhusiano kati ya nchi, hukumu yake ilikuwa sawasawa na nia yake. Ikiwa inaongezwa kwa hiyo kwamba kuiacha kunamaanisha kutoheshimu na husababisha shida na mgogoro na mgawanyiko wa safu na ubadilishanaji wa mashtaka kati ya washirika au hali ya kupinga uhusiano wa kimataifa, basi inapaswa kuheshimu bendera; ili kuepukana tahadhari hizi, na miongoni mwa wanavyuoni waliotaja hukumu hii ni Imam Shihab Al-Din Al-Qarafiy katika kitabu chake cha: [Al-Furuuq 4/430, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], kutoka kwa Sheikh Al-Izz Bin Abdul Salam aliyekuwa mmoja wa wanavyuoni wakuu, wakati alipoombwa kutoa Fatwa kuhusu Swala ya Qiyam (ambayo ni Swala inayosaliwa baada ya isha) ambayo watu waliizusha siku hizi ingawa haikuwepo katika wakati wa watu wema waliotangulia inaruhusiwa au hairuhusiwi? Akaandika akisema kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: "Msibughudhiane [msichukiane], wala musihusudiane wala msipeane Tmgongo, wala msikatane, kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ni ndugu", na kuacha Swala ya Qiyam katika wakati huu husababisha na kukatana na kupeana mgongo, ikiwa ikisemwa kuwa ni wajibu basi ni sawa.
Kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia hapo juu, inaruhusiwa kuheshimu bendera au kusimama kwa ajili ya wimbo wa Taifa, hakuna kuchukiza wala kukataza katika mambo mawili haya kama walivyosema watu wasio na elimu. Ikiwa hali hii ni kwenye vikao vya umma ambapo kufanya hivyo ni ishara ya kuheshimu na kuacha kunamaanisha kutoheshimu: basi kusimama huko kunathibitishwa; ili kuepukana na sababu ya mzozo, na kwa ajili ya kutumia tabia nzuri na maadili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas