Udhuru wa Kutojua.

Egypt's Dar Al-Ifta

Udhuru wa Kutojua.

Question

Je, kutojua kunazingatiwa ni udhuru wa kisharia kwa yule aliyetoa hukumu inayopingana na Uislamu ambapo hahukumiwi kwa ukafiri wake? Na vipi vigezo vya ujinga ambao unazingatiwa ni udhuru? 

Answer

Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, sala na salamu ziwe kwa Mtume wa mwisho naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W. na kwa Masahaba wake na kila mwenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya malipo na baada ya hayo:
Masuala ya Imani na ukafiri ni katika masuala ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa maneno ya kina zaidi, hii ni kutokana na yanayopelekea miongoni mwa hukumu za kidunia na kiakhera, kwa sababu maana ya kuthibiti kwa mtu kuritadi hupelekea kupotea kwa damu, mali na uharamu wa kuwa karibu na mke wake Mwislamu, na ushahidi kwake kuingia motoni milele ikiwa atakufa katika hali hiyo, kwa sababu ya ukubwa wa jambo lenyewe na hatari yake ndipo wanachuoni wametahadharisha mitazamo isiyo na ujuzu kwenye suala la ukafiri na kufanya haraka kutoa hukumu, kwani mwenye kuwa na haraka ya kutoa hukumu ya ukafiri basi fahamu kuwa huyo mtu hakunusa harufu ya elimu, na hasa ni kuwa hukumu ya ukafiri inasimama kwa kuimarika masharti na kuondoka viziwizi, kwa mfano mtoto mdogo na mwendawazimu haifai kuzingatiwa kuritadi, kwa sababu hiyo ni lazima ubainifu na uchunguzi mkali ufanyike kabla ya kutolewa hukumu ya ukafiri na hasa kwa watu waliothibitika kuwa na Uislamu wao, na hasa ikiwa Uislamu wake ni wenye dalili yenye nguvu inayomlinda na hukumu ya ukafiri.
Imamu Al-Ghazaliy anasema katika kitabu cha: [Al-Iqtisad” Uk. 157, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Jambo ambalo anapaswa kuliendea mchunguzi: Ni kujikinga na hukumu ya ukafiri kadiri anavyoweza kupata njia ya hilo, ikiwa kuahalalisha mali na damu ya wenye kuswali wakielekea Kibla huku wakipaza sauti kwa kusema: Hakuna Mola wa haki isipokuwa ni Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kosa, na kosa la kuacha kuwakufurisha makafiri elfu moja katika maisha ni jepesi zaidi kuliko kumwaga damu ya Mwislamu, na anasema pia ndani ya kitabu kilichotajwa Uk. 93: Katika watu wenye vitendo viovu zaidi ni kundi la wazungumzaji waliokufurisha Waislamu wote, na wakadai kuwa asiyefahamu maneno ya uelewa wetu na wala hakufahamu Imani yetu ya kisharia kwa dalili zetu ambazo tumezichambua basi huyo ni kafiri, basi watu hawa wameibana rehema ya Mwenyezi Mungu iliyo pana kwa waja wake kwanza, na wakaifanya Pepo kuwa ni wakfu kwa uovu mchache wa wazungumzaji. Anasema Sheikh Ibn Taimiyah: “Hakika jambo la kukufurisha lina masharti na vizuwizi vinaweza kukosekana kwa mtu, na kukufurisha hakulazimiki isipokuwa yakitimia masharti na kukosekana vizuwizi”.
Kitabu cha: [Majmu’ Al-Fatawa 12/187].
Kauli ya Sheikh Ibh Tayimiah ndani yake kuna uelewa wa kanuni muhimu, nayo ni kuwa kuna tofauti kati ya kukafirisha kwa sifa na kukafirisha kwa vitu, kwani si kila mwenye kuongea neno au kufanya kitendo cha ukafiri na anakuwa kafiri moja kwa moja kwa kufanya hivyo tu, na hili ndio tulilomaanisha hapa mwanzo kwa kusema: Ni lazima masharti yatimie na kutokuwepo kwa vizuwizi, na kutokana na sharti hizo ndipo hufikiwa kigezo cha kuhukumiwa hivyo, kwani miongoni mwa vigawanyo vya vigezo hivi ni pamoja na uhalali wa kutenda, nayo ni uhalali wa mwanadamu kwa kila anachokifanya kuzingatiwa kiishara, na kuwa na akili nacho, hivyo basi vitendo ambavyo vinatokana na msongamano wa makusudio na utashi kuna sharti kwa mtendaji wake kuwa na akili timamu na ufahamu kamili, mgawanyo huu ni miongoni mwa vigawanyo vya vigezo na uhalali ambapo vinaweza kutokea athari kwa kupungua au kuondoka kabisa, ambapo huitwa “vinavyo zaliwa kwenye vigezo” na athari zake ima kwa kuondoa au kupungua, au kubadilika baadhi ya hukumu kwa upande wa yule aliyetokewa pasina kuathiri uhalali wake.
Vinavyozaliwa kwenye vigezo miongoni mwake ni vile vinavyofanywa, kwa maana mwanadamu anakuwa ni sehemu ya hiyari na hilo ni kama vile ujinga, lakini - ujinga wowote - haupingani - na uhalali - anasema Zarkashiy katika kitabu cha: [Manthuur 2/16 Ch. ya Wizara ya Waqfu na mambo ya Uislamu nchini Kuwait]: Udhuru wa mjinga ni kwa upande wa kumfanyia wepesi na wala sio upande wa ujinga wake”. Kwa maana athari ya ujinga katika uhalali ni kuondoshwa kwa baadhi ya hukumu zake kwa mfano kama vile dhambi, lakini sio kila ujinga unazingatiwa ni udhuru ambapo hauna dhambi, na kama ni hivyo basi ujinga ungekuwa ni bora kuliko uelewa kama anavyo sema Imamu Shaafi katika kile kilichonukuliwa na Zamarkashy katika kitabu cha: [Manthur 2/17] ambapo amesema:
Lau utazingatiwa udhuru wa mjinga kwa sababu ya ujinga wake basi ujinga utakuwa ni bora kuliko elimu, ambapo mja anakumbana na uzito wa utekelezaji majukumu na kuupumzisha moyo wake na matatizo mbalimbali hivyo hakuna hoja kwa mtu kwa ujinga wake wa kutofahamu hukumu baada ya kufikishwa na kuwezeshwa ili watu wasiwe na hoja kwa Mwenyezi Mungu baada ya kufikiwa na Mitume. Na anasema Ar-Ramly katika sherehe yake ya [Al-Minhaj 3/164 Ch. ya Dar al-Fikri]: Na akaegemea baharini kuwa ndio udhuru tosha wa mjinga, lakini kinyume ndio sahihi, kwa sababu hiyo wanachuoni wameweka vigezo vya ujinga ambao unaruhusiwa kuwa ni udhuru na ule ambao hauruhusiwi kuwa ni udhuru, kabla ya kuzungumzia vigezo hivi tunapenda kubainisha kuwa tutaelezea masuala haya yenyewe tu mbali kabisa na mifano inayogusa wengi, kwa sababu maandishi ya wengi katika masuala haya – yaani: Udhuru kwa sababu ya kutokujua – yamechukuwa sura nyingi kama mifano, nasi hatuoni kuwa ni sahihi katika kutolea mfano, na imejengeka kwa uelewa mbali mbali unaokwenda kinyume na sisi kama ufahamu wa Imani na ukafiri, hivyo tumeona mgongano wa kutaja mifano ambayo ndio sehemu ya chimbuko la tofauti sehemu nyingi.
Na wengi waliotaja masuala haya ni watu wa Abu Hanifa, na hilo linakuja kutokana na umuhimu wao wa kuweka somo kamili la masuala ya uhalali na vinavyo zaliwa kwenye uhalali huo ndani ya vitabu vyao, na kuzingatia ujinga ni miongoni mwa vinavyo zaliwa, ukweli ni kuwa mengi yaliyo elezewa na watu wa Abu Hanifa na wengineo katika vigezo vya udhuru wa kutojua inawezekana kujibiwa kwa mambo mawili, kwa sababu ima vigezo vinarejea kwa mwenye kupewa jukumu au vinafungamana na ujinga.
Jambo la Kwanza: Vigezo ambavyo vinarejea kwa mtu mwenyewe:
Kusudio letu hapa la mtu mwenye kupewa jukumu ni yule mwenye uhalali kamili wa utekelezaji, kwa maana hajatokewa na kitu chochote katika vinavyo zaliwa kwenye uhalali tofauti na ujinga, wala haizingatiwi ni udhuru katika hili tofauti na watu wa aina mbili:
Wa Kwanza: Mtu mgeni katika Uislamu, na aliyekulia eneo lililombali na wanachuoni, mfano wao ni sawa na yule mwenye kuishi kwenya mji wenye uzushi mwingi wa dini, na mwenye kuishi kwenye eneo limejaa sana ukafiri, asili katika hilo ni Hadithi ya Abi Waqid Al-Laithy ambayo imepokelewa na Ahmad pamoja na Tirmidhy kwa mapokezi sahihi: “Kuwa Mtume S.A.W. pindi alipotoka kwenda Hunain alipita kwenye mti wa washirikina unaitwa: Mti mkubwa, ambapo makafiri huweka hapo silaha zao, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nasi tuwekee sehemu ya kuhifadhi silaha zetu kama wao wanavyofanya, Mtume S.A.W. akasema: Utakasifu ni wa Mwenyezi Mungu, haya ni sawa na maneno yaliyosemwa na watu wa Nabii Mussa: Tufanyie na sisi mungu kama wao walivyokuwa na mungu wao, ninaapa kwa yule nafsi yangu ipo mikononi mwake mtafuata mwenendo wa wale waliokuwa kabla yenu” imepokelewa na Abdurazaq na Ibn Aby Shaibah katika vitabu vyao, na amepokea pia An-nisaai na Baihaqy pamoja na Twabrany na wengine kwa upokezi wa maelezo tofauti, imekuja pia katika baadhi ya mapokezi ya Twabrany: “Tulitoka na Mtume S.A.W. kuelekea Hunain na sisi tukiwa wageni na ukafiri....”.
Mti huu mkubwa wenye ukijani unapatikana karibu na mji wa Makkah, katika zama za ujinga watu walikuwa wanakuja kila mwaka kwenye mti huu na kuutukuza pamoja na kuweka silaha zao na kuchinja kwenye mti huu, na kauli iliyokaribu zaidi ni kuwa hawa watu walikuwa wakiuabudia mti huu, kama ilivyoelezwa na baadhi ya wapokezi wa Hadithi kama vile Tabarany katika kitabu cha: [Al-Kabiir], kutokana na hilo kauli ya kuwa mti huu watu walikuwa wakitambika kwa kutafuta baraka tu ni kutoa hukumu bila ya dalili, sehemu ya ushahidi katika Hadithi ni kauli yake: “Na sisi wageni na ukafiri” ambapo hakuna shaka kuwa ombi la baadhi ya Masahaba kwa Mtume S.A.W. awafanyie na wao mfano wa mti huo kwa ukafiri, lakini haikuwa kwao wao kuwa ni wageni katika Uislamu.
Anasema mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haitamiy katika kitabu chake cha: [Al-Iilaam Bi Kawaatwii Al-Islam, Uk. 242] ni katika jumla ya kitabu kilichokusanya matamshi ya ukafiri chapa ya Dar Ilaf ya kimataifa nchini Kuweit, “Kwetu sisi ikiwa nchi ipo mbali na Waislamu ambapo hainasibishwi kuna uzembe wa kuacha kuja ili kujifunza au mji ukawa mgeni na Uislamu basi huwa udhuru wa kutojua kwake, na atafahamishwa usahihi” na akasema pia uk 282 akikamilisha kauli ya msemaji: “Hakuna udhuru kwa yeyote katika ukafiri kwa ujinga”: na alichosema kwa uwazi kinakubaliana na madhehebu yetu, ambapo kipimo cha hukumu ya ukafiri ni kwa sura ya nje, hakuna sababu ya kuangalia makusudio na nia, wala kuangalia dalili ya hali yake, ndio unazingatiwa ni udhuru kwa mwenye kudai kutojua ikiwa ni mgeni wa Uislamu au yupo mbali na wanachuoni. Na katika kitabu cha: [Al-Ashbah wa An-Nadhair cha Imam Suyuuty Uk 200 Ch. ya Mustafa al-Halaby]: “Kila mwenye ujinga wa uharamu wakitu miongoni mwa vitu vinavyotumiwa na watu wengi basi haukubaliki udhuru wake isipokuwa akiwa ni mgeni katika Uislamu au amekulia maeneo yaliyo mbali hakuna vitu vya mfano huo”.
Wa Pili: Ni yule isiyawezekana kujifunza, ambapo katika hali hii ujinga unakuwa miongoni mwa mambo magumu kuwa nayo mbali, na hilo ni kama mfano wa watu wa kipindi cha matatizo ya kupotea kwa athari ya Mtume, pindi inapotokea yanayopelekea ukafiri hakufurishwi mtu, kwa sababu uwezekano wa kujifunza huenda upo kwa kuwauliza watu wa elimu au kufanya juhudi kubwa ya kusoma na kupata elimu, kama vile - hali yoyote ya kukosekana uwezekano wa kujifunza - ni katika mambo ya kukadiriwa ambayo huachiwa mtu na ukweli wake.
Anasema Samarkandiy katika kitabu cha: [Mizani al-Usuuli Uk 171 Ch. Doha Mpya]: “Kuwa kinachoamrishwa ni chenye kufahamika kwa mwenye kuamrishwa kwa maana inawezekana kujifunza kwa kuzingatia ni sababu tosha” na anasema mwanachuoni Ibn Al-Luhham Al-Hanbaly katika kitabu cha: [Kawaaid Uk 58 Ch. ya Sunnat Al-Muhammadiya]: “Sharti la kufaa kupewa jukumu ni kuwa na uelewa wa kile anachotakiwa kukitekeleza...ikiwa litakuwa hili basi hapa kuna masuala yanayofungamana na ujinga wa hukumu: Je huo ni udhuru au hapana inafungamana na kanuni hii, ikiwa tutasema: unakubalika kuwa udhuru, basi sehemu yake ikiwa hakuna uzembe katika kujifunza hukumu, ama kukiwa na uzembe basi hakuna udhuru kabisa”, katika kanuni za [Al-Maqry Al-Maaliky 2/412 Ch. ya Chuo Kikuu cha Ummu Al-Quraa]: “Hakuna udhuru kwa kutokujua hukumu ikiwa kuna uwezekano wa kusoma”.
Jambo la Pili: Vigezo vinavyofungamana na ujinga:
Kusudio la kufungamana na ujinga ni kitu kisichofahamika, kigezo ambacho kinarudi katika hilo ni sifa ya suala lisilo julikana kwa upande wa kuonekana kufahamika na kutofahamika, asili katika hilo ni kuwa kilichokuwa kimeenea sana hakikubali madai ya ujinga, hivyo hakuna udhuru wa hilo, ufafanuzi wa hilo tunaangalia nukuu zifuatazo kisha tutazichambua:
Kadhi Abu Yusuf anaona kauli ya Abi Hanifa: “Hakuna udhuru kwa kiumbe yeyote katika ujinga wake kumfahamu Muumba wake, kwa sababu jambo la lazima kwa viumbe wote ni kumfahamu Mola Mtakafu na kumpwekesha, kutokana na anavyoona namna ya uwepo wa mbingu na ardhi na kuumbwa kwake yeye mwenyewe pamoja na vyengine vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, ama mambo ya faradhi kwa asiyeyajua na wala hakufikishiwa basi hili hakutakuwa na hoja ya hukumu juu yake”. kitabu cha: [Badai Swanai 7/132 Ch. ya Dar al-Kutubi Al-Elmiya].
Anaema Sheikh Ally Al-Qaary katika [sherehe yake ya Fiqhi kubwa ya Imam Hanifa Uk. 451 Ch. ya Dar Al-Bashair]: “Fahamu kuwa ikiwa mtu atazungumza neno la ukafiri hali ya kuwa anajua maana yake lakini wala haamini maana yake lakini limetoka kwake neno hilo pasina ya kutenzwa nguvu bali kwa hiyari yake katika kulisema kwake basi huyo anahukumiwa ukafiri...ama ikiwa atasema neno bila ya kufahamu kuwa ni ukafiri basi katika Fatwa za kadhi Khaan kuna tofauti pasina ya kuwa na neno lenye kupewa nguvu, ambapo amesema: Pamesemwa: Hatozingatiwa kafiri, kwa sababu ya udhuru wake wa kutojua. Na pakasemwa: Huzingatiwa kafiri na wala hakuna udhuru kwa ujinga. Ninasema: Kauli ya wazi ni ya kwanza, isipokuwa ikiwa ni kwa upande wa mambo muhimu katika dini, hayo wakati huo hukafirishwa na wala hakuna udhuru kwa ujinga”. Na anasema pia Uk. 329: “Kiwango cha juu cha msingi wa dini ni elimu inayotafiti yale yaliyo lazima kuamini, nayo yapo sehemu mbili: Sehemu inayotokana na ujinga katika Imani kama vile kumfahamu Mwenyezi Mungu na sifa zake zilizothibiti, kufahamu ujumbe na mambo ya akhera. Sehemu ya pili ujinga haudhuru kama vile kufahamu tofauti ya ubora wa Manabii kwa Malaika, amesema Sabaky katika utunzi wake: Ikiwa mwanadamu atakaa muda mrefu katika umri wake pasina kuzingatia tofauti ya ubora wa Manabii kwa Malaika basi Mwenyezi Mungu hatomuliza hilo”.
Anasema Imamu Shafi katika kitabu cha: [Risala uk. 357 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Aliniuliza muulizaji: Elimu ni nini? Na mambo gani ya lazima kwa watu katika elimu? Nikamjibu: Elimu ni aina mbili: Elimu ya jumla haitoweza kufikiwa isipokuwa kwa yule aliyeshindwa na akili yake kwa ujinga, akasema mfano wake ni vipi? Nikasema: Ni kama mfano wa swala tano, na ulazima wa Mwenyezi Mungu kwa watu ibada ya funga ya Ramadhani, kuhiji kwa wenye kuweza, kutoa zaka katika mali zao, na yeye Mwenyezi Mungu ameharamisha uzinifu, kuuwa, kuiba na kunywa ulevi, na yaliyokuwa katika maana hii miongoni mwa yale yaliyowekwa kwa waja na kuyaweka akilini na kuyafanyia kazi kwa nafsi zao na mali zao na kujizuia na yale aliyo haramisha Mwenyezi Mungu kwao, aina hii yote ya elimu ina maandiko ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na yapo kwa Waislamu wote wakifundishana watu kutoka kwa wale waliowatangulia wakinukuu toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu pasi ya kuvutana katika kuyaelezea wala kwenye ulazima wake kwao, na elimu hii jumla ambayo haiwezekani kukosea katika kuelezea wala kuifafanua lakini wala haifai kuvutana.
Akasema: Ni ipi sura ya pili? Nikasema kumwambia: Ni yale yanayowakilishwa kwa waja miongoni mwa matawi ya faradhi na baadhi ya hukumu maalumu na mengineyo miongoni mwa yale hayana andiko la Kitabu wala Sunna, na ikiwa kuna andiko lake katika Sunna basi inakuwa ni katika habari maalumu na wala sio habari za wote”.
Katika sherehe ya Imamu An-Nawawiy kwenye sahihi ya Imamu Muslim pale aliposema juu ya hukumu ya mzuiaji zaka [2/205 Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby]: “Ama leo Dini ya Kiislamu imeenea na kujaa kwa Waislamu elimu ya zaka mpaka kufahamika karibu na kila mtu na kushiriki kwenye uelewa huo msomi na mjinga basi hakuna udhuru kwa yeyote wa maelezo anayoyatoa katika kupinga kwake, vile vile kwa kila mwenye kupinga kitu ambacho kimekubalika na umma wa wanachuoni katika mambo ya Dini ikiwa elimu ya jambo hilo imeenea kama vile uelewa wa Swala tano ibada ya funga ya mwezi wa Ramadhani...isipokuwa kwa mtu ambaye mgeni katika Uislamu wala hafahamu mipaka yake, basi yeye ikiwa atapinga kitu kwa kutokujua hakufurishwi, na mfano wake ni sawa na wale watu waliobakia na jina la Dini kwao, ama kilichokuwa kinafahamika kwa wanachuoni kwa njia ya elimu kama vile uharamu wa kuolewa mwanamke kwa umama wake mdogo na ushangazi wake, na muuaji wa makusudi hana haki ya kuridhi, na bibi anafungu la sita na yanayofanana na hayo katika hukumu, basi mwenye kuyapinga hayo hakufurishwi, isipokuwa anapewa udhuru kwa kutokuwa na elimu nayo”.
Anasema Sheikh Ibn Taimiya katika [sherehe yake ya kitabu cha Al-Umdah katika mlango wa swala 2/51 – 52 Ch. ya Dar Al-Aswimah huko Riyadh]: “Mwenye kupinga ulazima wake kwa kutojua basi atafahamishwa, ikiwa atapinga kwa ubishi basi atakufurishwa” huu ni msingi katika mijengo mitano ya Uislamu na katika hukumu za wazi zilizokubalika kwa mwenye kupewa jukumu la kutekeleza ikiwa anapinga hilo na kupewa udhuru, mfano wa kuwa mgeni katika Uislamu, au amekulia maeneo ambayo yanaujinga mkubwa wa Uislamu, basi hatokufurishwa mpaka afahamishwa kuwa hii ni Dini ya Uislamu”.
Anasema Al-Qurafy katika kitabu cha Al-Furuuq chini ya kichwa cha habari, hitajio la mwenye kudai kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu uthibiti wa kile chenye dalili ya wazi ya kiakili kwa kukanusha kwake [4/447 Ch. ya Dar A-Kutub Al-Elmiyah]: “Fahamu kuwa ujinga unaopelekea madai haya sio udhuru kwa mwenye kudai uthibiti kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu kanuni ya kisharia inaonesha kuwa kila ujinga ambao mtu anaweza kuuondoa hauwi hoja kwa mjinga...ndio na ujinga ambao mtu hawezi kuuondoa kwa hali ya kawaida huo unakuwa ni udhuru...ama ujinga ambao unaweza kuondolewa hasa kwa muda mrefu na masiku kuendelea, kwani ambaye asiyefahamu leo atafahamu kesho na wala kuchelewa kufahamu hakuwi ni uharibifu na kutokuwa udhuru kwa mtu”.
Na katika kitabu cha: [Al-Ittifaaq cha Imamu Suyutwy 2/182 Ch. ya Maktabah At-Tujaariyah]: “Ama yasiyokuwa udhuru kwa mtu kwa kutojua kwake ni katika mambo ambayo yanatakiwa kufanya haraka kufahamu maana yake kutokana na maandiko ya hukumu za kisharia na dalili, kila tamko lenye kuleta maana moja ya wazi yenye faida na kujua kuwa ndio kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hakuna ufafanuzi wa maelezo ambapo kila mmoja anafahamu maana ya upwekeshaji katika kauli yake Mwenyezi Myngu Mtukufu: {Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu} [MUHAMMAD, 19], na Yeye hana mshirika katika Uungu, hata kama hajui kuwa herufi “Laa” katika lugha lina maana ya kukanusha na kinyume ni kuthibitisha, muktadha wa neno hili ni wajumla, linafahamika na kila mmoja kwa umuhimu kuwa muktadha wa kudumisha Swala kutoa zaka na mfano wake ni jambo zuri lililoamrishwa hata kama hafahamu muundo wa kitenzi ni lazima, katika sura hii hakuna udhuru kwa yeyote anayedai kuwa ni mjinga kwa maana ya matamko yake kwa sababu ni yenye kufahamika na kila mtu kwa uzito wake”.
Yanayofahamika katika jumla ya maandiko haya ni kuwa kujitokeza masuala ya kisharia na kuenea kwake hutengeneza vielelezo kadhaa ambapo pindi inapopatikana hukumu kwa hilo na kukosekana kwake kunakuwa ni katika masuala yaliyojificha ambayo hupewa udhuru kwa asiyeyajua pamoja na kuchunga masharti mengine yaliyobaki.
Na kusudio la vielelezo hivi ni mambo mengi: Miongoni mwake ni masuala kuwa ni yenye kufahamika kuwa ni muhimu katika dini, na maana ya kufahamika kwake ni muhimu ni elimu yake kuwa sawa kwa watu wote hakuna tofauti kwa msomi na mjinga, ni sawa sawa masuala hayo ni katika masuala ya msingi wa dini au matawi yake.
Na miongoni mwake: Ni kuwa masuala yaliyo andikwa ndani ya Kitabu na Sunna au kukubalika na wanachuoni na kunukuliwa vizazi kwa vizazi pasina ya kuchanganya wala kukosea, au kuwa ni masuala ya hekima yasiyokubali maelezo.
Na miongoni mwake: Ni kuwa masuala haya hayana udhuru kwa mtu kutoyajua kikawaida, ambapo hakuna uzito kwake katika hilo.
Ufupi: Ni kuwa udhuru wa kutokujua una tofauti ya pande nne, nazo ni upande wa muda, sehemu, watu na hali.
Kutokaba na maelezo yaliyotajwa jibu linafahamika kwa mujibu wa swali.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas