Hukumu ya Kubadilisha Uraia na Kuch...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kubadilisha Uraia na Kuchanganya Zaidi ya Uraia Mmoja.

Question

Baadhi ya Waislamu wana uraia wa nchi isiyo ya Kiislamu, kama vile nchi za Ulaya na Marekani, na matokeo ya uraia huu ni kwamba wanatawaliwa na Rais, serikali, na sheria zisizo za Kiisilamu, kwa hivyo nini hukumu ya kuchukua hatua hii? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utngulizo huo:
“Uraia” ni sifa ambayo hushikamana na mtu kuhusu kufuata kwa watu au taifa maalumu. Katika sheria: uhusiano wa kisheria unaounganisha mtu na nchi fulani na inaweza kuwa asili au inayopatikana. [Al-Waseet, uk. 14, neno la J.n.s.i.a: Baraza la Kiarabu, na Mujam Maqayiis Al-Lugha na Ibn Faris 1/486, Ch. Darul Fikr].
Hukumu katika suala hili inategemea sababu za uhamiaji na kujipatia uraia, na pia inategemea hali halisi ya nchi ambayo imehamiwa, kwa hivyo inawezekana mtu akalazimishwa kufanya kitendo hiki kwani ni faradhi, kama vile kukimbia kwa ajili ya kuilinda dini yake na hali hii haiwezi kupatikana isipokuwa katika nchi hiyo tu au nchi nyingine kama hiito.
Pengine kusafiri na kufuatwa na hali ya kujipatia uraia kwa ajili ya kupata kitu kinachoruhusiwa, kama vile kutafuta riziki, au hali hii inaweza kuwa inapendekezwa au ni wajibu kifaya (yaani wakipatikana baadhi ya watu kuitekeleza, uwajibu wake unawaondokea waliobakia), kama vile kupata elimu za sayansi ambazo Waislamu wanazihitaji.
Kuna hali nyigine ambazo huchukua hukumu yao kutoka kwa mifano tuliyoitaja.
Kuhusu kujipatia uraia wa nchi fulani ambapo kuzuiliwa sana katika mambo yanayohusiana na itikadi, kama baadhi ya nchi ambazo zinakanusha dini kabisa, basi hairuhusiwi kujipatia uraia wake, isipokuwa kama atachukua uraia huu ili kupata pasipoti kutoka kwa nchi hii, halafu ahamie nchi nyingine.
Kuhusu kusafiri kwenda nchi ambamo uhuru wa dini uko huru na hauna athari kwa itikadi na dini yake, basi hakuna kibaya chochote kuhusu hali hii, na katika hali hii suala linazunguka juu ya kuruhusiwa, au kupendekezwa au kuwajibika, kulingana na hali kama ilivyotanguliwa hapo awali, na hukumu itaendelea isipokuwa hali zikibadilika.
Sio siri kuwa asili ya hali hiyo ni kukaa katika nchi ya Kiislamu kwa usalama wa dini, familia, na kizazi pia.
Na kwa kila hali zote zilizo hapo juu zina dalili yake, ikiwa ni faradhi ain (yaani ni lazima kila mwislamu atekeleza mwenyewe), kama vile kukimbia kwa dini wala haitekelezwi hivyo isipokuwa katika nchi hii au nyingine, kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AL BAQARAH:173] Aya hiyo ilionesha kuwa dharura inaruhusisha kinachoharimishwa.
Mwenyezi Mungu alisema pia: {Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa. * Isipokuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama * Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa maghfira} [AN NISAA : 97-99].
Aya hiyo ilionesha kwamba Mwislamu aliagizwa kuhamia Madina, ili aweze kusimamisha dini yake, na kumnusuru Mtume S.A.W. ikiwa hali ya kuhamia Madina haikuwa lazima tena, kwa mujibu wa kauli yake Mtume S.A.W. aliposema: "Hamna uhamiaji baada ya ushindi" [Al-Bukhari], kwa hivyo ilibaki hukumu ya asiyeweza kusimamisha dini yake isipokuwa tu kwa uhamiaji hiyo hiyo, ambayo ni wajibu. Al-Baydhawi alisema katika Tafsiri yake: “Na katika aya hiyo dalili ya uwajibu wa uhamiaji kutoka mahali ambapo mtu haweza kusimamisha dini yake” [Anwar At-Tanziil wa Asrar At-Tawiil: 2 / 92, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabi].
Miongoni mwa dalili za uhamiaji kwa mji ambao unatawaliwa na mtu ambaye sio Mwislamu ni agizo la Mtume S.A.W. kwa masahaba wake wahamie Uhabeshi na mtawala wake ni An-Najashi ambaye alikuwa Mkristo. Baadhi ya watu wa Yemen walihamia na meli ikawafikisha Uhabeshi, kwa hivyo Ja`far Bin Abi Talib aliwaamuru wakae nao. Ikiwa ukaji huo ulikuwa ukizuiliwa basi yeye na wenzake hawakukaa katika mji huo, vile vile hawakuwaamuru wengine kufanya hivyo, kwani Mtume S.A.W. alikuwa amehamia Madina, na Waislamu walikuwa salama katika dini yao, hata kama An-Najashi aliwatendea Waislamu vyema, isipokuwa kwamba watu wa nchi hiyo Hawakuwa kama yeye kuhusu jambo hilo, na hali hii inaonekana katika maneno ya Asma Bint Umais kama yatatajwa baadaye.
Inajulikana kuwa ujio wa Ja`far na wenzie wote kwa Mtume, S.A.W. ulikuwa katika mwaka wa Khaybar, yaani katika mwaka wa saba wa uhamiaji, kama inavyooneshwa katika Hadith hii ndefu iliyo katika Sahih mbili: imepokelewa kutoka kwa Umm Salamah, Binti Abi Umayya Bin Al-Mughaira, ambaye ni mke wa Mtume S.A.W. alisema: Tulipofika nchi ya Uhabeshi, tulikuwa jirani An-Najashi ambaye alikuwa jirani bora, alitupa amani katika dini yetu, tumeweza kumwabudu Allah pasipo na adha, na hatusikii chochote tunachochukia. Maquraysh walipojua hivyo, walishauriana kupeleka kwa An-Najashi watu wawili ambao walikuwa wenye nguvu, na kumpa zawadi kutoka mizigo ya Makka, na zawadi hizo ambazo ni ajabu zilikuwa ngozi, kwa hivyo wakakusanya ngozi nyingi, na hawakumwacha hata mmoja wa mapatriarki wake ila walimpa zawadi, kisha wakampeleka na Abdullah Bin Abi Rabiaa Bin Al-Mugheerah Al-Makhzoumi, na Amr Bin Al-Aas Bin Wael Al-Sahmi, na wakawafanya wao wawili ni watawala, na wakawaambia: mpeni kila patriarki zawadi yake, kabla kuzungumza na An-Najashi, kisha mtoeni kwake zawadi zake, kisha mwulizeni awakabidhi wao kwenu kabla kuzungumza nao, akasema: tukatoka tukaja kwa An-Najashi, na tulikuwepo nyumbani mwake amabyo ni nzuri, na jirani bora, kwa hivyo hatukumwacha patriarki yeyote ila tulimpa zawadi yake kabla ya kuongea na An-Najashi, kisha wakamwambia kila patriarki: kwamba wamekuja katika nchi ya mfalme kutoka kwetu wavulana wapumbavu, ambao waliacha dini ya watu wao na hawakuingia kwenye dini yenu, na walikuja na dini mpya ambayo hatuijui sisi wala nyinyi, waungwana wa watu wao wametutuma kwa mfalme ili kuwarudisha wavulana hao kwa watu wao, kwa hivyo kama tukizungumza na mfalme kuhusu wao, basi mshaurieni yeye awakabidhi wao kwetu na asiwaongee nao, kwani watu wao wanajua ni nini vyema kwao, na nini kibaya kwao, mapatriarki wakawaambia: Ndio, kisha wakamletea An-Najashi zawadi zao, akazikubali, kisha wakamwambia; Ewe mfalme, wavulana wapumbavu wamekuja kwa nchi yako kutoka kwetu, ambao waliacha dini ya watu wao na hawakuingia kwenye dini yenu, na walikuja na dini mpya ambayo hatuijui sisi wala nyinyi, waungwana wa watu wao kutoka kwa baba zao, wajomba wao na jamaa zao, wametutuma kwako ili kuwarudisha wavulana hao kwa watu wao, ili warudishe kwao. watu wao wanajua ni nini vyema kwao, na nini kibaya kwao.
Alisema: Na hakuna chochote walichochukia Abdullah Bin Abi Rabia, na Amr ibn Al-As zaidi kuliko kusikia An-Najashi maneno yao, kwa hivyo mapatriarki wake wakamwambia: Ee mfalme, watu hawa wanasema kweli, watu wao wanajua ni nini vyema kwao na nini kibaya kwao, kwa hivyo akawakabidhi kwao ili warudishwe kwao na kwa watu wao, alisema: An-Najashi alikasirika, kisha akasema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, sitawakabidhi kwao, na sitawakabidhi watu ambao walikuwa jirani yangu, na wameshuka kwenda katika nchi yangu, na wamenichagua juu ya mtu yeyote ambaye ni mpaka niwaite, na kuwauliza hao wawili wanasema nini juu ya jambo lao, wakiwa ni kama wanavyosema, nitawakabidhi kwao na wakiwa wao sio kama wanavyosema sitawakabidhi kwao, na nitawatendea vizuri kwao wakiwa majirani zangu. Alisema: Kisha akapeleka kwa masahaba wa Mtume wa Allah S.A.W. akawaita na wakati mjumbe wake alipowajia, walikusanyika, kisha baadhi yao wakaambiana: Je! mnasemaje kwa mtu huyo mkija kwake? Wakasema: Tutasema tunaapa kwa Mwenyezi Mungu hatujui chochote, na kile alichotuamuru Mtume wetu, S.A.W., kilitokea. Walipomwendea, na An-Najashi aliwaita maaskofu wake, kisha aliwauliza akisema: Ni dini gani hii ambayo mmewaacha watu wenu kwa ajili yake, na hamjaingia kwenye dini yangu au dini ya yoyote ya mataifa haya? Akasema: Jaafar Bin Abi Talib ndiye aliyezungumza naye, akamwambia: Ewe mfalme, tulikuwa watu wa jahilia, tunaabudu masanamu, tunakula wafu, tunafanya maovu, tunakata ukoo, na tunatedeana na jirani vibaya, mwenye nguvu hula mnyonge. Na tulikuwa hivyo mpaka Mwenyezi Mungu alitutumia Mtume miongoni mwenu tunafahamu nasaba yake, ukweli wake, uaminifu wake, na usafi wake. Alitulingania Allah, kumpwekesha, kumwabudu, na kuyaacha yale mawe na masanamu tuliyoyaabudu sisi na baba zetu badala yake, na alituamuru kusema kweli, kuzirudisha amana, Kuhifadhi ukoo, kutendeana na jirani mwema, kuzuia vitendo vya haramu, kutomwaga damu, ametukataza uzinzi, kusema uwongo, kula pesa za yatima, kumsingizia muumini mwema wa kike, na ametuamuru kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake wala tusimshirikishe na chochote, ametuamuru kusali, kutoa Zakat, na kufunga saumu, akasema: akamhisabia mambo ya Uislamu, tukamsadiki, tukamuamini na tukamfuata kulingana na kile alicholeta, kwa hivyo tukamwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na hatukushirikisha chochote naye, na tukaharimisha alivyotuharimisha, na tukahalilisha alivyotuhalilisha, watu wetu walitushambulia, Walitutesa na kututengana na dini yetu, ili kuturudisha kwa ibada ya masanamu kutoka ibada ya Mwenyezi Mungu, na kuhalilisha tulivyohalilisha kutoka maovu, wakati walipotushinda, walipotudhulumu, walipotukandamiza, wakajaribu kututengana na dini yetu, tukatoka kwenda nchi yenu, na tukakuchagua wewe tu siyo mwingine, na tukataka tuwe jirani yako, na tukatumai kwamba tusidhulumiwe katika nchi yako ewe mfalme. An-Najashi alisema: Je! Unacho chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambacho alileta nacho?: Ja`far alisema: Ndio, An-Najashi alisema: Basi unisomee, akamsomea kuanzia {kaf Ha ya Ayn Sad}. Alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu An-Najashi alilia hadi ndevu zake zikalowa na machozi, na maaskofu wake walilia hadi vitabu vyao vimelowa na machozi waliposikia Aya alizosoma Ja’far. Kisha An-Najashi alisema: maneno haya yanafanana sana na yale aliyotumiwa Musa yote yanatokana na taa moja, nendeni, naapa kwa Mwenyezi Mungu sitawakabidhini kwao, wala sitakaribia kufanya hivyo kabisa. Umm Salamah alisema: Wakati walipotoka, Amr Ibn Al-Aas alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kesho nitawaambia kasoro yao, kisha nitawapambana nao. Abdullah Bin Abi Rabia – aliyekuwa mcha mungu zaidi - akasema: usifanye hivyo kwa sababu tuna udugu nao, hata wakituhalifu. Akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, Nitamwambia An-Najashi kwamba wanadai kwamba Yesu mwana wa Mariamu, ni mja. Halafu kesho akamwambia: Ewe mfalme, wao wanasema neno kubwa juu ya Yesu mwana wa Mariamu. Basi akawatuma kwao na kuwauliza juu ya waliyoyasema kuhusu Yesu. Watu walikutana, wakaulizana: Je! Mnasemaje kuhusu Yesu akiwaulizeni juu yake? Wakasema: Tunasema: tunaapa kwa Mwenyezi Mungu, tutasema kama alivyosema Allah na kama alivyosema Mtume wetu. Walipokuja kwake, An-Najashi aliwauliza: Je! Mnasemaje kuhusu Yesu, mwana wa Mariamu? Ja`far Bin Abi Talib alimwambia: Tunasema alivyosema Allah na kama alivyosema Mtume wetu: yeye ni mja wa Allah, Mtume wake, roho yake, na neno lake alilotoa kwa bikira Mariamu. An-Najashi alipiga mkono wake chini, akakichukua kijiti, halafu akasema: Isipokuwa Yesu, mwana wa Mariamu nilisema hivi. An-Najashi aliposema hivyo maaskofu wake wakakasirika. Akawambia: hata mkikasirika nendeni enye Waislamu na ishini kwa amani katika nchi hii. Na mwenye kuwatukaneni atatoa gharama, kisha mwenye kuwatukaneni atatoa gharama. Sipendi kuwa na dhahabu nyingi kama mlima na mmoja mwenu anaudhika. Walirudishe zawadi zao, hatuna haja kwa zawadi hizo, naapa kwa Mwenyezi Mungu Allah hakuchukua rushwa kutoka kwangu wakati aliporudisha kwangu ufalme wangu, Je, nilichukue rushwa mimi? Na watu hawakunitii, je, nawatii mimi? Watu hawa wakatoka wakikebehika na wakarudishwa kwao zawadi wao wanazoleta, na tukikaa katika nchi yake nzuri pamoja na majirani wazuri. Alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, tulikuwa katika hali hii mpaka alikuja anayetaka kuchukua ufalme wa An-Najashi. Alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hatukuhuzunika zaidi ya huzuni hii wakati huo, kwa kuogopa kwamba adui huyo anamshinda An-Najashi, basi akaja mtu ambaye hajui haki yetu kama alivyoijua An-Najashi. Alisema: An-Najashi alitembea baina yao ni mto wa Nile. Akasema: masahaba wa Mtume S.A.W. walisema: Nani ambaye anaweza kutoka nje ili kuona watu hawa watafanyaje halafu anatuletea habari? Al-Zubayr Bin Al-Awam alisema: Mimi nitafanya hivyo, na alikuwa kijana wakati huo. Basi akavaa uBinda ili kuogelea mpaka aende upande wa Nile ambapo ndipo watu wanapokutana, kisha akatoka hadi akawajia. Alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu tulimwombea An-Najashi dua ili amshinda adui yake, na kumwezesha katika nchi yake, na alitiwa kiti cha enzi ya uhabeshi, wakati huu tulikuwa katika nchi bora, hadi tukarudi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. naye alikuwa yuko Makka. [Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad katika Musnad yake].
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Hisham: Kisha tukakaa naye hadi akatoka aliyetoka miongoni mwenu akienda Makka, na akakaa aliyekaa huko.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Barda, kutoka kwa Abu Musa R.A. akasema: "Tulikuwa kwenye Yemen tulijua kwamba Mtume S.A.W. alihamia, tukaenda kuhamia kwake, mimi na ndugu zangu wawili, mimi ndiye wa mdogo wao, mmoja wao ni Abu Bardah, na mwingine ni Abu Rahm, alisema: Katika watu hamsini na tatu, au hamsini na mbili kutoka watu wangu, tukapanda meli, tukaelekea An-Najashi kule Uhabeshi, Ja’far Bin Abi Twalib alitukubali, tukakaa naye mpaka sote tukakutana pamoja, na tukakutana na Mtume S.A.W. wakati alipofungua Khyber, na walikuwa Baadhi ya watu wanatuambia, yaani watu wa meli: Tuliwatangulieni kwa Hijra (uhamiaji), na Asmaa Binti 'Umais, aliyekuja nasi, alifikia Hafsa mume wa Mtume S.A.W. kama mgeni, na alikuwa amehamia kwa An-Najashi pamoja na waliohamia. Omar akaingia Hafsa, na Asmaa alikuwa naye, Omar alisema alipomwona Asmaa: Ni nani huyu? Alisema: Asmaa Bint ‘Umais, Omar alisema: Je, huyu mhabeshi? Asmaa alisema: Ndio, alisema: Tumewatangulieni kwa uhamiaji. Tunastahili zaidi Mtume Mwenyezi Mungu S.A.W. ziadi kuliko nyinyi, akakasirika na kusema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, mlikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. analisha mwenye njaa miongoni mwenu, kuhubiri mjinga wako, na tulikuwa katika nyumba - au katika nchi – ya chuki kule Uhabeshi, na hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Na kwa ajili ya Mtume wake S.A.W. naapa kwa Mwenyezi Mungu sitakula wala sitakunywa chochote, mpaka nimwambie Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. uliyoyasema na tulikuwa tumeudhika na kuogopa, na nitamwambia Mtume S.A.W. hivyo, nitamuuliza, naapa kwa Mwenyezi Mungu sitasema uwongo wala sitaongeza chochote katika hayo, basi wakati Mtume S.A.W. alipokuja, Asmaa akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Hakika Omar alisema hivi na vile? Akasema: Ulimwambia nini? Akasema: Nilimwambia: hivi na vile, alisema: hastahili yeyote kati yenu, na yeye na wenzake wana uhamiaji mara moja tu, na nyinyi; watu wa meli, mna uhamiaji mara mbili. Alisema: Nimemuona Abu Musa na watu wa meli wananikujia ili kuniuliza juu ya hadith hii, hakuna chochote katika ulimwengu huu ambacho wanafurahi zaidi na kubwa zaidi kuliko yale aliyoyasema Mtume S.A.W. kwao, Abu Bardah alisema: Asmaa alisema: Nimemwona Abu Musa anarrudiarudia Hadithi hii".
Pia kati ya dalili iliyopokelewa kutoka kwa Hudhayfah ambaye alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: ((Hairuhusiwi kwa Muumini kujidhalilisha). Wakasema: Je! Namna gani anajidhalilisha? Akasema: "Anajipatia shida ambayo hana uwezo wa kuisubiria". [Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy, na akasema: Hii ni hadithi nzuri, na mgeni.] Hadithi hii inamhimiza aliyekalifishwa asijipatie shida; kwa sababu mtu anaweza kuwa dhaifu na hawezi kuvumilia shida hii, basi dini yake inaweza kuangamizwa, na hiyo ndio hali yake ndogo kuhukumiwa kuwa inachukizwa.
Kundi la wanavyuoni wa zama hizi walisema kama tulivyotaja hapo juu, wakiwemo: Sheikh Yusuf Al-Qaradhawiy, Mustafa Al-Zarqa, Abdel Fattah Abu Ghadah na Manna’ Al-Qatwan.
Kundi lengine walisema kuwa hairuhusiwi kabisa, na miongoni mwa dalili zao ambazo ni muhimu sana: kauli yake Mwenyezi Mungu: {Wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamedhulumu nafsi zao, (kwa kutohajiri; Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani (katika jambo la dini yenu?) watasema: tulikwa madhaifu katika ardhi hiyo (kwa hivyo hatukuweza kufanya ibada yetu, (Malaika) watasema: Ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa na nyinyi kuhamia humo? Basi hao makazi yao ni Jahannam; nayo ni marejeo mabaya kabisa} [AN NISAA: 97 ].
Aya hii inatueleza kwamba hairuhusiwi kukaa katika nchi ambazo ndani zao watu hawawezi kufanya ibada zao za kidini na kuwazuiliwa kwa udhaifu wao.
Imepokelewa kutoka kwa Jarir Bin Abdullah, kutoka kwa Mtume, S.A.W., alisema: “Sina jukumu lolote kwa kila Mwislamu anayeishi kati ya washirikina.” [Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud na wengine].
Imepokelewa kutoka kwa Samarah Ibn Jandub, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: “(Yeyote mwenye kukaa pamoja na mshirikina anajifananisha naye).” [Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud].
Walitoa dalili kupitia matini za jumla zinazokataza kuwanusuru washirikina.
jibu la dalili hizi ni kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: {Wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamedhulumu nafsi zao, (kwa kutohajiri; Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani (katika jambo la dini yenu?) watasema: tulikwa madhaifu katika ardhi hiyo (kwa hivyo hatukuweza kufanya ibada yetu, (Malaika) watasema: Ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa na nyinyi kuhamia humo? Basi hao makazi yao ni Jahannam; nayo ni marejeo mabaya kabisa} [AN NISAA: 97], si hoja kwa aliyosema, kwa sababu hali ya kuwa dhaifu inaweza kuwa katika nchi za Kiislamu zenyewe, na wakati mwingine jambo hilo linaweza kuwa na faraja zaidi nje ya nchi za Kiislamu! Basi jambo la muhimu zaidi ni nchi ambapo ndani yake mtu anaweza kuitekeleza dini yake.
Al-Baidhawiy alisema: “Na katika aya hiyo ni dalili inayolazimisha kuhamishwa kutoka mahali ambapo mtu anashindwa kusimamisha dini yake.” [Tafsiri ya Al-Baidhawiy: 2/92].
Imam At-Twaher Bin Ashour alifafanua katika tafsiri yake aya hii akisema: “Wanavyuoni walikubaliana kwamba hukumu ya aya hii ilipitishwa siku ya ushindi wa Makka, kwa sababu uhamiaji ulikuwa wajibu ili kutengana na washirikina na maadui wa dini, na ili kuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kizuizi cha kuizuia. Wakati Makka ilipokuwa nchi ya Uislam, ilikuwa sawa na nchi nyingine, na inathibitishwa na hadithi: “Hakuna uhamiaji baada ya ushindi, lakini kuna jihad na nia tu.” Basi waumini walikaa katika nchi zao isipokuwa wahamiaji, ni marufuku kwao kurudi Makka. Na katika Hadithi nyingine Mtume S.A.W. alisema: "Ewe Mola upitishe kwa masahaba wangu uhamiaji wao wala wasirudishe nyuma)) alisema hivyo baada ya ushindi wa Makka, lakini kipimo cha hukumu ya aya hii kinawezesha weneye jitihada kufikiria hukumu za uwajibu wa kuondoka nchini ambapo ndani yake mwamini hufitiniwa katika dini yake, na hukumu hizi zinajumuishwa na hali sita:
Hali ya kwanza: Kuwa Muumini yuko kwenye nchi ambayo anavutiwa na imani yake, na analazimishwa kukufuru wakati anaweza kutoka nje. Hali hii hukumu yake ni hukumu ile ile ya wale ambao aya hiyo iliwateremkia. Na kundi la Waislamu walihamia kutoka Andalus walipolazimishwa na Manasara kuingia dini ya ukresto, wakahama kwa nafsi zao, imani zao, wakaacha pesa zao na nyumba zao, kundi lao waliangamia njiani mwaka wa 902 na baada ya tarehe hii, hadi uokoaji wa mwisho mnamo mwaka wa 1016.
Hali ya pili: ni kwamba muumini katika nchi ya kikafiri hafitinishwi katika imani yake, lakini ana hatari ya kupata shida katika nafsi yake au pesa zake kwa kufungwa au kuuawa au kudhulumiwa mali zake, katika hali hii Muumini atakuwa amedhurika kwa madhara hayo na hilo limekatazwa bila utata wowote, na huku kunazingatiwa ni kukaa katika nchi ya vita na ardhi ya adui kama ilivyoelezwa.
Hali ya tatu: kuwa kwenye nchi ambayo wasio Waislamu ni wengi, lakini hawakuwafitinisha watu katika imani yao, wala katika ibada zao, wala katika nafsi zao, wala pesa zao, na heshima yao, lakini kwa kukaa kwake, hukumu za wasio Waislamu zitatekelezwa kwake akiwa na ajali pamoja na mmoja wa watu wa nchi hiyo ambao sio Waislamu, na hali hii ni kama aliyekaa leo katika nchi za Ukristo wa Ulaya, nayo ni dhahiri ya kauli yake Imama Malik kwamba inachukiza sana kukaa katika nchi kama hiyo kwa sababu Muumini atahukumiwa kwa hukumu za wasio Waislamu, na hivyo ndivyo vilivyoandikwa katika kitabu cha Biashara kwenye Ardhi ya Vita, na vile vile Imam Malik alifasiri kauli ya wanavyuoni wa Kairouan, na hivyo ndivyo ilivyo kauli yake Al-Lakhmi mwanzoni mwa kitabu cha biashara kwenye ardhi ya vita. Al-Barazali alisema kutoka kwa Ibn Arafa: Ikiwa amiri wa Tunisia ni mwenye nguvu dhidi ya Wakristo, inaruhusiwa kusafiri, vinginevyo hairuhusiwi, kwa sababu wanawadharau Waislamu.
Hali ya nne: Kuwa makafiri wengi katika nchi ambayo watu wake ni Waislamu na hawafitinishwi katika dini yao, wala katika ibada yao au pesa zao, lakini makafiri wana utawala wa nguvu juu yao tu, na hukumu baina yao zinafanywa kulingana na sheria ya Kiisilamu, kama ilivyotokea huko Siqilyia wakati ilipotawaliwa na Roger Al-Narmandi. Vile vile kama ilivyotokea huko Ghiranada wakati wa utawala wa dikteta wa Jalaliqah alipoichukua kwa masharti yakiwemo ni kuheshimu dini yao, basi watu wake walikaa kwa muda huko na wanavyuoni wao pia walikaa na wakahama baadhi yao, basi mwenye kuhama hakumfedhehe mwenye kukaa, wala mwenye kukaa hakumfedhehe mwenye kuhama.
Hali ya tano: Kuwa wasio Waislamu wana ushawishi na mamlaka juu ya baadhi ya nchi za Kiislamu, na wafalme wa Uislam wanabaki ndani huko, na tabia zao zinaendelea pamoja na watu wao, mamlaka ya utawala wao kutoka kwao, kuheshimu dini zao na ibada zingine, lakini kutendea kwa wakuu wao chini ya macho ya wasio Waislamu na kwa idhini yao, hali hii inaitwa ulinzi, ukoloni, na udhamini. Kama ilivyotokea katika Misri wakati wa ukoloni wa jeshi la Ufaransa, kisha wakati wa ukoloni wa Waingereza. Vile vile kama ilivyotokea huko Tunisia na Magharibi ya mbali kutoka kwa ulinzi wa Ufaransa, na kama ilivyotokea huko Syria na Iraqi wakati wa siku za udhamini na kuhusu hali hii hakuna shaka lolote katika uwajibu wa kuhamia nchi kama hii.
Hali ya Sita: Nchi ambayo kuna maovu mengi na uzushi, na hukumu nyingi zinatekelezwa kinyume na Uislamu ulio wazi, ambapo inachanganywa kazi nzuri na mbaya na halazimishi Mwislamu ndani yake kufanya tendo kinyume na Sheria, lakini hawezi kuibadilisha isipokuwa kwa kusema tu, au haweza kufanya hivyo hata kidogo, na nchi hii imepokelewa kutoka kwa Imama Malik kuwa ni wajibu kuihamia. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Al-Qasim, lakini hali hii ilitokea katika Qairouan wakati wa Bani Ubayd, lakini haikukumbuka kwamba yeyote wa wanavyuoni wao wa fiqhi aliwaita watu kuhamia. Inatosha kwamba Sheikh Abi Muhammad Bin Abi Zaid na wengine kama wao wamekaa huko wakati huo. Na ilitokea huko Misiri katika zama za Al-Fatimiin pia, na hakuna hata mmoja wa wanavyuoni wao waadilifu aliyehamia.
Kuna hali nyingine nyingi zinazoruhusisha kukaa, nazo ni viwango vingi, na kwamba kama Waislamu wakibaki katika nchi zao bila ya kufitinishwa katika dini yao itakuwa hamu kubwa kwa jamii za Kiisilamu.” [Tafsir At-Tahriir wa At-Tanwiir: 5 / 178-180, Ch. Ad-Dar At-Tunisia lilNashr].
Kuhusu Hadithi ambazo walizotaja, basi kuna shaka katika mapokezi yao na matini zao. Kuhusu mapokezi ya Hadithi ya kwanza, Abu Dawud alisema: imepokelewa kutoka kwa Hanad Bin As-Suri kutoka kwa Abu Muawiya kutoka kwa Ismail, kutoka kwa Qais, kutoka kwa Jarir Bin Abdullah, alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alituma kampani kwa Khatham, baadhi ya watu wakagomea kusujudu, basi waliuwa haraka. Akasema: Kisha Mtume S.A.W. akajua hivyo, na aliwaamuru kwa nusu ya akili na akasema: Sina jukumu lolote kwa kila Mwislamu anayeishi kati ya washirikina, walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa nini? Alisema: kwa sababu Mwislamu atafananishwa na mshirikina", Abu Dawud alisema: Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Hashim, Muammar, Khaled Al-Wasiti, na wengine ambao hawakumtaja Jarir.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi katika njia hiyo hiyo, kisha akasema: imepokelewa kutoka kwa Hanad, kutoka kwa Abdah, kutoka kwa Ismail Bin Abi Khalid, kutoka kwa Qais Bin Abi Hazim, kama Hadithi ya Abu Muawiya, na hakumtaja Jarir, na Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Hammad Bin Salamah, kutoka kwa Al-Hajjaj Bin Arta, kutoka kwa Ismail Bin Abi Khalid, kutoka kwa Qais, kutoka kwa Jarir, kama Hadith ya Abu Muawiya. Na nikamsikia Muhammad akisema: Hadithi ambaye ni sahih zaidi ni iliyopokelewa kutoka kwa Qais kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W..
Muhammad ni Muhammad Bin Ismail Al-Bukhari, na Al-Tirmidhi alitaja Hadith hiyo katika Al-Ilal [uk. 483] kutoka kwa Hadithi ya Hanad kutoka kwa Abu Muawiyah, kisha akasema: Nilimuuliza Muhammad juu ya hadith hii, akasema: Hadithi ambayo ni sahih zaidi ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Qais Bin Abi Hazim. Nilimwambia: Hammad Bin Salamah alipokelea hadithi hii kutoka kwa Al-Hajjaj Bin Arta, kutoka kwa Ismail Bin Abi Khalid, kutoka kwa Qais Bin Abi Hazim, kutoka kwa Jarir! Lakini haikuhifadhiwa.
Sahihi katika hadithi hii ni kwamba mapokezi yake yanafikia Mtume S.A.W., na kwamba mapokezi mengine ambayo sahaba ametajwa hayajahifadhiwa.
Na kwa dhana ya usahihi wake, basi kukataza kuishi pamoja na washirikina katika Hadithi hii kulifungamana na kuogopa kufitinisha na sio kwa maana yake ya ujumla, kwani masahaba walihamia Uhabeshi na wakati huo hakukuwa nyumba ya Uislam kama ilivyopita, na hii ni madhehebu ya Imam Ash-Shafi. Imam al-Nawawi anasema katika [Al-Rawda: 10/28: 10/28 Ch. Al-Maktab A-Islami]: “Ikiwa Mwislamu ni dhaifu katika nchi za makafiri, na hana uwezo wa kuonyesha dini yake, amekatazwa kuishi huko, na lazima ahamie kwa nchi za Kiisilamu, ikiwa hana uwezo wa kuhamia, basi anasamehewa hadi atakapoweza, ikiwa amefungua nchi kabla ya kuhamia, ameondolewa hukumu ya kuhamia. Ikiwa ana uwezo wa kuonyesha dini kwa sababu ni mtiifu kwa watu wake, au kwa sababu kuna ukoo huko kumlinda, na hakuogopa kufitinishwa katika dini yake, basi uhamiaji haukumlazimisha, lakini unapendekezwa tu, ili idadi yao isizidi, au ili mwislamu asiwapende, au ili wasimkaidi, na ikasemekana kuwa: Uhamiaji ni wajibu, kauli hii imepokelewa kutoka kwa Imamu, na mtazamo wa kwanza ni wa sahihi zaidi, nikasema: Sahib Al-Hawi alisema: Ikiwa mwislamu anatarajia kusimamisha kwa Uislamu huko, basi ni bora akae. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi”
Kuhusu Hadithi ya Samurah, Al-Tirmidhi aliiashiria, na Abu Dawud aliipokelea. Imepokelewa kutoka kwa Muhammad Bin Dawud Bin Sufyan, kutoka kwa Yahya Bin Hassan, kutoka kwa Suleiman Bin Musa Abu Dawud, kutoka kwa Jaafar Bin Saad Bin Samurah Bin Juandub, kutoka kwa Khubayb Bin Sulaiman, kutoka kwa baba yake Suleiman Bin Samurah, kutoka kwa Samurah Bin Jundub, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alisema: “Yeyote anayeishi pamoja na mshirikina na kukaa pamoja naye, basi yeye ni kama mshirikina).” Al-Dhahabi alisema katika tafsiri ya Ja`far Bin Saad Bin Samurah: Ana hadith nyingine kuhusu Zakat kutoka kwa Binamu yake. Ibn Hazm hakukubali Hadithi hii akisema: Ja`far Bin Saad Bin Samurah na Binamu yake hawajulikani. Nikasema: Binamu yake ni Khubaib Bin Sulaiman Bin Samurah, [Mizan Al-Iitidal: 1/407, Ch. Darul Maarifa].
Hadithi hii sio sahihi kwa mujibu wa mapokezi yake, na ikiwa tunafikiria kwamba imekuwa na nguvu kwa njia zake, basi hakuna chochote katika matini yake hiyo ambacho kinachukuliwa kutoka kwa uharimisho kabisa, lakini badala yake jambo hilo linafafanuliwa kama ilivyoelezwa na kikundi cha wanavyuoni, kwa sababu Hadith hiyo imewekwa na dalili nyingine zilizotajwa katika sehemu hiyo. Kauli yake: "basi yeye ni kama mshirikina" Hiyo ni, kutoka kwa njia nyingine, kwa sababu mawasiliano yanaweza kusababisha kudhoofika kwa imani yake, kwa hivyo Sheria imekaripia mawasiliano hayo kwa ukali huu mkubwa kwa ajili ya kuzuia ufisadi. [Aoun Al-Maabud kwa Al-Adhim Abadi: 7/337, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Al-Hafiz Ibn Hajar alisema: “Al-Khatwabiy na wengine walisema: Uhamiaji ulikuwa ni faradhi mwanzoni mwa Uislamu kwa wale ambao wamegeukia Uislamu kwa sababu ya ukosefu wa Waisilamu katika mji huo na hitaji lao la kukutana. Wakati Mwenyezi Mungu alipofungua Makka, watu waliingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi makundi, hukumu ya uhamiaji kwa Madinah iliondolewa na imebakia faradhi ya jihadi na nia kwa aliyeshambuliwa na adui. na hekima pia ilikuwa kwamba ni wajibu kuhamia kwa yule aliyeingia Uislamu, ili wale ambao walidhuru jamaa yake kutoka kwa makafiri wawe wasilimu, kwa sababu walikuwa wakiteswa na wale ambao walikuwa wasilimu kutoka kwao hadi atakaporudi kutoka kwa dini yake na kuhusu wao Mwenyezi Mungu alisema: {Wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamedhulumu nafsi zao, (kwa kutohajiri; Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani (katika jambo la dini yenu?) watasema: tulikwa madhaifu katika ardhi hiyo (kwa hivyo hatukuweza kufanya ibada yetu, (Malaika) watasema: Ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa na nyinyi kuhamia humo? Basi hao makazi yao ni Jahannam; nayo ni marejeo mabaya kabisa} [AN NISAA: 97]. Na uhamiaji huu unabaki hukumu yake kwa yule aliyeingia Uislamu katika nchi za makafiri, na aliweza kuhamia. Imepokelewa kutoka kwa An-Nasai kutoka njia ya Bahz Bin Hakim Bin Muawiyah kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba: "Mwenyezi Mungu hakubali tendo lolote kutoka kwa mshirikina aliyekuwa msilimu ila baada ya kutengana na washirikina". Na imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud kutoka hadithi ya Samurah, kwamba "Sina jukumu lolote kwa kila Muislamu anayeishi kati ya washirikina)", na Hadithi hii inakusudia wale ambao wanaogopa dini yao [Fath Al-Bari: 6/38, Ch. Darul Maarifa].
Sheikh Zakaria Al-Ansari alisema: “(Sura: Inalazimika kuhamia) kutoka Nyumba ya ukafiri hadi Nyumba ya Uislamu (kwa anayeweza) (ikiwa hawezi kuidhihirisha dini yake), kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao} [AN NAHL: 28]. Vile vile kwa mujibu wa Hadithi ya Abu Dawud na wengine kwamba: "Sina jukumu lolote kwa kila Mwislamu anayeishi kati ya washirikina", ikiwa ni mwanamume au mwanamke, na ikiwa hakupata jambo la haramu, na vile vile kila mtu aliyeonesha haki katika nchi yake ambayo ni nchi ya Uisilamu na hakukubaliwa na hakuweza kuidhihirisha, basi analazimika kuihama nchi hiyo kama alivyosema Al-Awzai’y na wengine kutoka kwa Az-Zarkashiy kutoka kwa Al-Baghawiy pia. Lakini Al-Balqiniy alisema kuwa: ikiwa katika makazi yake kuna maslahi kwa Waislamu, basi inaruhusiwa kwake kukaa huko. Kama hakuweza kuhamia, anasameheka hadi atakapoweza, kwa sababu ikiwa nchi ingefunguliwa kabla ya kuhamia, uhamiaji wa yule uliondolewa. (Na ikiwa alikuwa na uwezo) wa kuonyesha dini yake, kwa sababu alikuwa mtiifu kwa watu wake, au kwa sababu alikuwa na ukoo uliomlinda (na hakuogopa kufitinishwa dini yake, inapendekezwa) kuhamia. Ili idadi yao isiongeze, au asiwapende, au wasimkaidi, na sio lazima kuhamia, kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alimtuma Othman Siku ya Hudaybiyah kwa Makkah, kwa sababu ukoo wake ulikuwa huko na ana uwezo wa kuonyesha dini yake huko (sio akitarajia wengine waingie Uislamu), kisha haifai kwake kuhamia lakini ni bora zaidi kukaa huko.” [Asna Al-Mutwalib: 4/204, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islami].
Yote yaliyotajwa katika suala la kukaa katika nchi zisizo za Kiislamu yanakuja katika suala la kujipatia uraia wa nchi hizi, kwani tofauti ni utaratibu tu, na Muislamu anaweza kufaidika kutokana na hilo kama inavyojulikana na kuonekana - kama ilivyotangulia hapo mwanzoni mwa fatwa hii.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, ni wazi kwamba hukumu ya kisheria kuhusu suala la kujipatia uraia na uhamiaji kwenda nchi zingine hutofautiana kulingana na nia ya hali hiyo na hali ya nchi hiyo, na kutawaliwa na hukumu yake na sheria yake, kwa hivyo ikiwa hilo ndilo linalomsumbua Mwislamu katika dini yake na ibada zake, kama vile baadhi ya nchi zingine ambazo zinaikana dini kabisa, basi hairuhusiwi kabisa. Vinginevyo, ikiwa nchi hiyo inaruhusu uhuru wa kidini na haina chochote chenye madhara kwa Mwislamu katika dini yake au maisha yake ya kidunia, basi hakuna ubaya wowote wa kujipatia uraia wa nchi hiyo na kuihamia kama hakuna mambo ya haramu.
Na Mungu Mwenyezi Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas