Urithi wa Kiislamu – Njia za Kimfum...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu – Njia za Kimfumo na Majaribio ya Kimatumizi.

Question

Msomaji wa Kisasa anasumbuliwa na Ugumu katika kuamiliana na Urithi wa Kiislamu. Je, kuna uwezekano wowote wa kuleta Njia za Kimfumo zitakazotusaidia kusogelea Urithi huo wa Kiislamu, pamoja na mfano wa kiutekelezaji ili jambo hili liwe wazi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika Uzuri wa kuuelewa Urithi wetu wa Kiislamu unazingatiwa kuwa ni hatua muhimu na ya kimsingi ya kuelekea katika Suala la jinsi ya kuamiliana nao, vikiwemo kukubali baadhi ya pande zake na kuzikataa pande zingine. Na kinachopatikana ni kwamba mbele yetu tuna vitabu, na tuna maandiko mengi yanayokusanya zalisho kubwa la kifikra; kubwa kwa upande wa uhusiano wake na zama pamoja na sehemu, na katika kina cha Kifalsafa na Kimfumo kilicholetwa, na katika yaliyomo ndani yake kwa wingi (mamilioni ya Masuala katika kila Elimu moja) iliyoyashughulikia, na yote hayo yanajulikana kwa jina la Urithi wa Kiislamu.
Na uhalisia ni kwamba maana ya Urithi wa Kiislamu ni kwamba neno hili hutumika kwa kila kilichozalishwa kabla ya miaka mia iliyopita katika zama zetu hizi. Pamoja na hivyo, hakika ya mwisho kuandika kwa njia ya Urithi wa kale (tunaoukuta Katika Vitabu Mama vya Fiqhi) na Mijeledi yake ikasambaa, ni Mwanachuoni Baijuuri katika Sherehe ya ziada na Sherehe nyingi nyingine kwenye vitabu mbalimbali. Na tunapokiangalia kipindi kilichovitangulia vitabu vya Baijuuri, tutajikuta mbele ya Urithi mwingi wa zama hizo unaokusanywa zaidi ya karne kumi (tangu kipindi cha uandishi wa Sayansi mbalimbali mwishoni mwa karne ya kwanza Hijiriya, na kipindi hiki kinaendelea mpaka katika zama zisizo mbali), na upeo wake wa kisehemu, unatosha kwa kiasi kikubwa; ambapo vyanzo vyake ni vingi kuanzia Andalusia mpaka Eneo la Indiasia, na kutoka Kaskazini mwa Afrika mpaka Kusini mwake. Vilevile tunaukuta Urithi huu ukiwa na pande zake mbalimbali: ambapo Maandiko yake yalielekea katika Maeneo, Fani na Sayansi mbalimbali, bali hakika ya Urithi huu unagawanyika na kuelekea katika Shule na Madhehebu mbalimbali, kwa kuhusisha aina tofauti tofauti za fikra za Watu; kwani kuna Eneo Kubwa mno la uzalishaji wa Kifikra ambao ulizalishwa na Uthubutu wa kimaumbile wa Waislamu. Na sisi hapa tuko katika kujaribu kuzitumia funguo za uzalishaji huo wa Fikra ambao kupitia kwake tunaweza kusoma na kuelewa Maandiko ya Urithi huu.
Hakika ya mzingatiaji wa tatizo la jinsi ya kushughulikia Maandiko ya Urithi hupelekea kwa Kiwango kikubwa matokeo ambayo kwayo: Msomaji wa Kisasa amepoteza Sura Jumla iliyokuwa imeenea kwa waandishi wa Urithi kupitia zama na sehemu mbalimbali. Na juu ya hivyo, kuna uwezekano tukasema kwamba Ufahamu zingativu wa Urithi Wetu ambao unatuwezesha kukamilisha na kugundua au kukubali na kukataa au kutofauyisha na kuchagua mbele ya Urithi huu; Uelewa huu unahitaji kutambua Mitazamo Mikuu ambayo ilikuwapo katika akili zao na iliziongoza akili hizo, mpaka Mitazamo Mikuu hiyo ikaenea na kuwa kama vitu vinavyokubalika bila upinzani wa aina yoyote. Na kisha baada ya hapo hakika kukosa Mitazamo hii au kutoelewa Watu wa zama zake na kuwahudhirisha katika Urithi huu wakati wa kuusoma kunasababisha sisi kupitwa na kheri nyingi sana na Ufahamu wa kina unatupotea.
Kuna nukta nyingine inayofungamana na Mitazamo hii Mikuu, nayo ni Suala la Nadharia zinazotawala na ambazo ziliitawala akili ya Muislamu wakati wa kuasisi elimu hizo au kushirikiana na akili ya kiurithi pale elimu hizi zilipoandikwa. Nadharia hizi zinazotawala kwa kawaida hatuzikuti zikiwa zimeandikwa wazi wazi katika vitabu tulivyo navyo, bali huzikuta elementi zake katika vitabu vilivyogawika katika zama zake, zikiwa zimegawanywa pia baina ya madhehebu na Watu na Wanachuoni kwa ujumla na Wanachuoni wa Fiqhi ambao waliyaandika yote hayo.
Tangu zaidi ya miaka hamsini, Wanachuoni wa Hadithi wa Kiislamu wanajaribu katika baadhi ya elimu- na hasa hasa zikiwemo elimu za Fiqhi na za Lugha ya Kiarabu – kugundua nadharia kama hizi za Kiujumla zinazotawala na ili waandae tafiti zao za kisayansi ndani ya elimu hizi, iwe ni katika Kiwango cha Uzamili au Uzamifu, na wengi wao wamepiga hatua kubwa sana katika hilo. Hakika wameandika katika nadharia ya Umiliki na nadharia ya Mali na nadharia ya Haki na nadharia ya kufunga Mikataba na nadharia ya Dhamana, na katika nadharia ya Kubeba Majukumu, na kuendelea…, wameandika mengi katika hayo lakini haikuwa rahisi katika kila elimu ambazo Mwelekeo wake ni wa Fiqhi. Kama ambavyo pia, hayakuenda yakiwa yamenyooka au kwa Kiwango kinachofanana kiufanisi na katika kina chake. Tukawa leo tuna nadharia zilizowezesha kuudiriki undani wa kufikiri Kiurithi, na nadharia nyingine zikiwa bado ziko mwanzoni mwake. Na kwa mfano Nadharia ya Fiqhi ya Kiislamu, hii imekomaa kiasi cha kutosha, na kwa namna inayowezesha tuitumie kama ufunguo tunaoweza kufungulia utambuzi wa elementi nyingi za mikataba katika Fiqhi ya Kiislamu, bali na katika mifumo mingine ya Kikanuni.
Na kwa kuongezea mapungufu ya Kisasa katika kuelewa vizuri Masuala mawili ya Mitazamo Mikuu jumuishi na Nadharia Kuu Jumuishi Zinazotawala – jambo ambalo linamfanya mtu asiwe na uwezo wa kuwasiliana na urithi wa Kiislamu kwa namna inayotarajiwa – Suala la msamiati linajitokeza; Kwa hivyo katika kila Elimu au Madhehebu kuna Istilahi au Misamiati yake ya kina, ambayo pindi Msomaji wa Kisasa anapoikosa au mwanafunzi mwenye Utafiti wake; basi hakika yeye hataweza kuyafikia mengi katika yaliyomo mikononi mwake. Na jambo hili litasimama kama kikwazo mbele ya Ufahamu wa kina na tulivu kwa ajili ya Urithi wetu wa Kiislamu.
Jambo la nne ambalo Mtafiti wa Urithi anatakiwa kulielewa ni: Suala la Elimu Tumishi. Kila elimu miongoni mwa Elimu ilikuwa ikitegemea Mjengeko wa Kifikra, nao ni ibarara ya kile alichokipata Mtaalamu kutokana na somo katika elimu mbalimbali. Kwa hiyo yule aliyeandika katika Fiqhi alisoma Mantiki hapo zamani, na aliisoma Elimu ya Maneno, na akajua hapo kabla hiyo inayoitwa Kumjua Mtunzi wa Elimu, na akazisoma Elimu mbalimbali za lugha ya Kiarabu ukiongeza na Chimbuko au Asili. Na hivi ndivyo tunavyokuta ya kwamba Elimu nyingi zimejiundia Mfumo wa Kifikra na Mjengeko wa Kiakili –akawa Wakati anaizungumzia Elimu ya Fiqhi– anazungumza kwa kutumia chombo hicho kilichozalikana ndani yake kutokana na kutendeana kwake na Elimu hizi tofauti katika akili yake.
Na sisi –kwa mfano leo– tunapotaka kulinganisha Shahada za Vyuo Vikuu, tunalazimika kujua uwingi wa maarifa aliyoyasema mwanafunzi, Idadi ya masaa ya masomo yake na kiwango cha mambo aliyoyapata ndani ya masaa hayo; mpaka tuweze kujua vilivyo iwapo Kiwango hicho kinalingana na kile cha mwanafunzi mwingine alichokitumia katika Chuo ambacho mwanafunzi huyu anaomba masomo. Kwa hiyo Idadi ya masaa aliyoyatumia mwanachuoni hapo zamani inakusanya Elimu nyingi, jambo ambalo linaweza kuwapotea wengi wanaowasoma. Na jambo hili ndilo lililosababisha kuasisiwa kwa Ibara na Muundo wa maneno na Uandishi wa Elimu kwa njia ambazo tunazitumia kuuona Urithi. Na Elimu ya Fiqhi ilipoandikwa tukaiona kama vile ni yenye kuingia katika Mantiki, au inaingiliana na mieleweko waliyonayo Wanachuoni wa Elimu ya Maneno, na ni yenye kuingiliana na kile walionacho Wanachuoni wa Busara ya Juu, na ni yenye kuingiliana na walichonacho Wanachuoni wa Elimu ya Mashina. Na hivyo ndivyo ilivyo katika kila fani na katika kila Elimu, kwani Mwandishi wake alipokuwa anaiandaa elimu hiyo hakika mambo yalivyo yeye anafanya hivyo akiwa ameathirika na somo alilolipata katika Maisha yake ya Kielimu. Kwa hiyo Elimu zote zikawa zinatumikiana, na kuwa mfumo mmoja na Mjengeko mmoja wa fikra. Jambo hili lazima liwe la msingi na la mwanzo kwa Mtafiti yoyote na Msomaji wa Mashina ili tuweze kukamilisha Mwelekeo Wetu.
Kuna pointi ya Tano inayoambatana na usomaji Wetu wa Urithi wetu, nayo ni: Muundo wa Kilugha na wa Mantiki, ambao unatulazimisha tuidiriki Falsafa ya Lugha na mahusiano yake na Akili na vilivyomo ndani ya Wataalamu. Miundo hii inatulazimu sisi tuisimamie kwa wingi na tuizingatie kwa njia ya kimsingi; mpaka iwe ni ufunguo Kwetu wa kuusoma Urithi wote kwa matawi yake yote na aina zake zote.
Haya ndiyo matakwa matano ya kuusoma Urithi Wetu, ambayo tutatenga kila moja kwa maudhi yake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na tunatarajia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atatusaidia kuangazia baadhi yake kwa undani zaidi. Na wala sidai kuwa mihimili hii ndio tu tunayoihitaji kwa ajili ya kugundulia Siri za Urithi Wetu, lakini mihimili hii – kwa vyovyote iwavyo – ni katika mihimili iliyo muhimu zaidi na ni funguo kuu za kuujua Urithi Wetu. Vilevile inafaa kuashiria ya kwamba Urithi Wetu huu unakuja kwa daraja na viwango mbali mbali, na Sisi hivi sasa tuko katika kuamiliana na ngazi yake ya kwanza. Lakini Sisi iwapo tutataka kusonga mbele hatua moja zaidi, basi tunalazimika kutafuta suluhisho la Maudhui hizi kwa ngazi nyingine. Na ngazi hizo zipo za Awali, zipo za Kati na zipo za kumalizia kwa ujumla wake, lakini ni nyingi kwa kweli na haziishii, kama vile ni kutoka katika Uwingi ulioungana na wala sio Uwingi uliotengana.
Kwa hali yoyote iwayo, chaguo limeangukia kwa kipande cha Mtunzi wa Vitabu vya Urithi ambapo aliandika katika karne ya saba Hijiriya, si mwingine bali ni Imamu Nawawiy. Na Imamu Nawawiy alikuwa Mtaalamu wa Fiqhi, Hadithi, Tafsiri pamoja na Elimu ya Machimbuko. Naye ndiye Kigogo wa Madhehebu ya Shafiyy na ana Kitabu muhimu ambacho ni cha Madhehebu ya Shafiyy baada yake, amefanya ndani ya kitabu hiki yale aliyoyaona kuwa ni Wajibu kwake kuyafanya kwa wakati wake, au ni Wajibu wa Wakati huo, na akaandika Fiqhi ya Shafiyy kwa ufupi, na akafupisha pia mwenendo mzima wa Fiqhi katika uandishi wake wa kitabu kinachoitwa Minhaaju Twaalibiina wa Umdatul Muftiina, na kwa kawaida kitabu hiki kwa kifupi kinaitwa Minhaaju. Na ili tuweze kupata kitu kwa wepesi zaidi, kwa jinsi kilivyo Kitabu hiki, kwanza kabisa tunalazimika kuangalia mwenendo wa Madhehebu ya Shafiyy kuanzia mwanzo wake mpaka kujitokeza kwa Imamu Nawawiy.
Mwanzo kabisa, tunajua kwamba Imamu Shafiyy – baada ya safari yake ya kuelekea Hijazi (Eneo la Kusini Magharibi kuanzia Tabuuk kwa juu hadi Makkah kwa chini) Yemeni pamoja na Iraki – na akatulizana kimaisha Nchini Misri ambako ndiko alikofia huko. Nchini Misri kuna Kaburi la Imamu Shafiy ndani ya Mtaa mashuhuri unaobeba jina lake Mjini Cairo. Na Imamu Shafiy alipoingia Misri alikuwa na wanafunzi wake, ambao miongoni mwao ni Buwaitwiyu, Rabiiu Muraadiy, na Rabiiu l Jiiziy, ambapo wote hao walipokea elimu kutoka kwa Imamu Shafiy na kuandika alichowasomea. Na baada ya hapo, vitabu vya Imamu Shafiy vikawa ni hoja katika Madhehebu yake. Na baada ya hao, walikuja Wanachuoni wengine wengi waliyoyatumikia Madhehebu ya Imamu Shafiy na wakavitumikia vitabu vyake hivyo. Na hivi ndivyo ulivyo ujumla wa Madhehebu yote ya Wanachuoni, waliojitahidi, madhehebu ambayo yapo na yamefikia mia moja isipokuwa Manne tu kati ya hayo ndiyo yaliyojipatia umaarufu mkubwa na Kutumikiwa zaidi kuliko Madhehebu mengine yote, na Madhehebu hayo manne ni ya Imamu Hanafi, imamu Maliki, Imamu Shafiy na Imamu Ahmad Bin Hanbali.
Na Imamu Shafiy alipoandika vitabu vyake na vikaenea kwa Watu, Wafuasi na Wanafunzi wake wakayatumikia Madhehebu haya na kuyasambaza pamoja na kuyatolea dalili mbalimbali kwa Kiwango ambacho kwamba Imamu Mazniy alikusanya kila kilichosemwa na Imamu Shafiy na akakifupisha katika sura ya Masuala yanayofuatana, na akakiita Kitabu chake kwa jina la Mukhtaswarul Mazniy.
Kisha baada ya hapo, akaja Imamu Baihaqiy alifanya kila Suala miongoni mwa Masuala ya Kitabu cha Muzniy kuwa ni Anuani kubwa ya Mlango miongoni mwa Milango ya Kitabu chake Kikubwa alichokiandika na kukiita Sunanul Kubraa. Ndani yake anakuja na Anuani [Inayokusanya Hukumu] kisha anakuja na Hadithi ambazo zinazingatiwa kuwa ni dalili kwake juu Hukumu aliyoifuata Imamu; mpaka ikasemwa kuwa Imamu Shafiy ana fahari kwa kila Mfuasi wa Madhehebu yake mpaka Siku ya Kiama isipokuwa Baihaqiy kwani yeye anajifaharisha kwa kumfuata Imamu Shafiy; ambapo yeye amedhihirisha dalili za Shafiy juu ya Masuala yote katika Kitabu hiki kikubwa kiitwacho Sunanul Kubraa.
Utoaji huu wa Elimu uliofanywa na Wanachuoni wa Madhehebu ya Shafiy umeendelea kizazi kwa kizazi na karne kwa karne mpaka ukatufikia sisi katika Karne ya Tano tukamkuta Imamu Abu Maali Jauniy ambaye aliandika kitabu muhimu katika Fiqhi ya Shafiy alichokiita Nihaayatul Matlabi Fii Maarifatil Madhhabi, kisha mwanafunzi wake Imamu Abuu Haamid Ghazaaliy akaja kuandika Kitabu alichopangilia ndani yake Kitabu cha Mwalimu wake na akakiita Al Basiitu, na akafupisha Al Basiitu katika kitabu cha [Alwasiitu], na akafupisha Alwasiitu katika kitabu cha [Alwajiizu], na hiki cha mwisho akakifupisha katika kitabu chake cha [Al Khulaaswah]. Vitabu hivi vya Juwainiy na wanafunzi wake vikawa ndivyo vilivyo tegemewa kuyahamisha haya Madhehebu, kutoka kizazi hadi kingine mpaka alipokuja Imamu Raafiiyu na Imamu Nawawiy na wote wawili hawa ni wa karne ya saba Hijiriya. Imamu Raafiiyu akaandika Kitabu kizuri mno na akakiita Fat-hul Aziizi fii Sharhi Kitaabil Wajiiz lil-Ghazaaliy, na baada ya hapo, akatunga Kitabu kingine alichokiita Almuharriru.
Akaja Imamu Nawawiy na kukielekea Kitabu cha Almuharriru ambacho kinazingatiwa kuwa ni ufupisho wa Madhehebu ya Shafiy, na akakifupisha katika kitabu chake tulichonacho cha Alminhaaju. Kisha baada ya hapo, akaja Jalaalul Muhalliy (Jalaalul Diinil Muhalliy) akasherehesha kitabu cha Minhaaju. Hapo ikajitokeza tofauti kubwa mno baina ya Kitabu kinachosomeshwa na Kitabu kinachozingatiwa kuwacni katika Vitabu Mama vya Madhehebu ya Shafiy. Na kuna vitabu vingi vizuri na vyenye elimu nyingi ndani yake kwa kadri ya Utashi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mjuzi wa Kila kitu, lakini ingawa viko hivyo, havifai kufundishia. Masomo yanahitaji jambo maalumu ambalo mwalimu anaweza kuliendesha kielimu na kivitendo akiwa na wanafunzi wake; kitabu kilicho Wazi kina mwanzo na mwisho, kina Istilahi yake Maalumu bila ya kuwa na matawi, kwani kuwa na matawi mengi kunaweza kukamfanya mwanafunzi na Mwalimu wake watumie muda mwingi bila ya kufikia kitu chochote.
Kwa hiyo, Kitabu cha Minhaaju kikawa ni cha kufundishia; na kwa ajili hiyo, kimekuwa na Sharhu nyingi mpaka zikafikia zaidi ya Sharhu sitini, na Sharhu iliyoenea zaidi ni Sharhul Jalaalil Muhallaa. Kila mwalimu alikuwa – anasherehesha Sharhul Jalaalil Muhallaa – anaweka andiko dogo linalomsaidia mwanafunzi kufahamu; kwa hivyo, Minhaaju tunaiita Almatnu, na Kitabu cha Jalaalu tunakiita Sharhu, ama yale maelezo ya ziada tunayaita Haashiyah. Na kwa ajili hiyo, Ushereheshaji wa Sharhu uliongezeka sana tukawa na kile kinachoitwa Hawaashi (Sharhu ya Sharhu) kubwa. Kama vile: Haashiyatul Qalyuubiy, Haashiyatul Sheikh Umairah, na hawa walikuwa Wanazuoni wa Azhar wa Madhehebu ya Shafiy ambao walisomesha Kitabu hiki.
Na tuelekee – katika jaribio letu la kutaka kubainisha njia ya kuelekea kwenye Urithi Wetu – kutokana na Ibara iliyotajwa katika Maandiko ambayo tunayasoma Kwanza, kisha tunaangalia upeo wa kuelewa moja kwa moja Ibara hiyo, kisha hali ya ufahamu huo ikiwa sisi tumezinduka na kuelewa Mitazamo Mikuu na nadharia Dhibiti zinazotawala, na Istilahi pamoja na Nadharia zake, na vilevile Elimu Tumishi na Miundo na Kilugha ya Kimantiki; ambapo uhakika wa kuudiriki hii hali yake tangulizi unatuwezesha sisi kufahamu Siri ya Andiko hili la Urithi (na ukisie vivyo hivyo Maandiko mengine) kwa namna ambayo inatufanya tuamiliane nayo kwa sura nzuri na bora zaidi.
Na imesemekana kwamba Ibara hii inatupasa sisi tulizindukie Suala la Usomaji; ambapo hali hutofautiana wakati wa usomaji ulio sahihi na usomaji usio sahihi.
Na tuone anayoyasema:
Kitabu cha Kuuza, amekichelewesha kikawa nyuma ya Ibada; kwakuwa Ibada ni Matendo yaliyo bora zaidi; na kwa kuwa kuhitajika kwake ni zaidi; na pia kwa uchache wa watendaji wake. Na Tamko lake katika Shina ni Chimbuko; na kwa ajili hiyo ameliweka peke yake, ingawa chini yake kuna aina mbalimbali, kisha likawa Jina kutokana na kuwa ndani yake kuna mkabala wa yatakayokuja. Kisha ikiwa itatakiwa kwayo moja ya pande mbili za mkataba ambao anayekuja nao huitwa Mchuuzi, na inaeleweka kwamba ni kumiliki kwa malipo mbadala kwa sifa maalumu, na hukabiliana na Ununuzi ambao ni upande mwingine ambao anayekuja kwayo huitwa Mnunuzi, na hujulikana kama ni Umiliki kwa malipo mbadala vilevile. Na inajuzu kuliita jina la Mchuuzi kwa Mnunuzi na kinyume chake kwa zingatio, na kueleza kwa tamko la Kumiliki na kutamalaki kwa kuiangalia maana ya kisheria kama itakavyokuja:
Na hata kama itakusudiwa kwayo mseto wa pande mbili kwa pamoja; kwa maana ya Muambatanisho unaopatikana kutokana na pande mbili ambazo zinarejeshewa Tamko la Kujuzisha na Kuvunja, na pakasemwa kwalo kilugha: ni Mkabiliano wa kitu kwa kitu kingine kwa namna ya kubadilishana, na kinaingia ndani yake kisichosihi kukimiliki kama vile kitu maalumu cha mwingine, na katika kile ambacho ikiwa hakuna Tamko kama vile la Kupeana, na pakatoka kwa namna ya kukabidhiana kwa amani. Na kisheria: ni kufunga mkataba wa makabidhiano ya kifedha yanayomaanisha umiliki wa kitu au manufa kwa sifa ya kudumu na sio kwa muda mfupi. Na nguzo zake ni Tatu: mtia Mkataba, kinachotiwa Mkataba na Tamko. Nazo kiuhalisia ni nguzo sita kama itakavyokuja hapo baadaye.
Na Mkataba – katika dhana yake – ni umbo na uhusika wake ni kuingiza. Lakini pakiwapo baina yake na kitengo chake kuna ujumla wa mwelekeo patatoka katika kila moja wapo kati ya pande mbili kile kilichoingia katika ujumla mwingine. Na kwa ajili hiyo, wamesema: kwa kufungwa Mkataba Mapeano yametoka, na kwa Kupeana mbadala kuelekea katika zawadi na kifedha kuelekea katika Ndoa, na kwa kufidisha Umiliki wa Kitu kwa kukodisha, na kwa kutokuwa na mwelekeo wa ukaribu Mkopo. Na maana ya manufaa hapa ni kuuza mfano wa Njia. Na kufungamanisha kwa kuunga mkono ndani yake kwa ajili ya kutoa Ukodishaji pia. Na kukitoa kitu kimoja kwa vifungamanisho viwili hakutii kasoro.
Na dhana hii ni bora zaidi katika dhana kwa kuwa kwake ni mkabala wa fedha kwa fedha kwa upande maalumu kwa yasiyofichika ndani yake [Ni kama vile Wote wanatambua utambuzi wa kina wa yaliyosiyofichika kwa mtu yoyote ]
Kisha, kuuza kunaishia katika pande tano:
Ya Kwanza: ni kusihi kwake na kuharibika kwake.
Na Pili ni: Kujuzi na Kulazimika kwake.
Tatu: ni katika Hukumu yake kabla ya kupokea na baada ya kupokea.
Na Nne: Ni katika Matamshi huru.
Na Tano: ni katika Kuungana na jinsi ya kumtendea mtumwa, na machumo yaliyo bora zaidi ni katika kilimo, kisha viwanda, kisha biashara, kwa usahihi wake.
Maandiko haya tuliyokuleteeni ndiyo tutakayojaribu kuyafahamu. Na huwenda mijengeko ya kifikra juu yake umetofautiana kutoka kwa msomaji hadi kwa mwingine, bali pia umetofautiana jinsi ya kuidiriki na kuzizindukia maana zake baina ya wasomaji wawili. Tofauti hii inarejea katika Asili na Zaidi – katika utofauti wa kujipatia Miono Mikuu, na Sayansi mbalimbali zinazoitumikia na Istilahi, na Nadharia Zinazotawala. Na tunaleta Ubainifu wa upande huo, kabla hatujasimamia mambo Manne kwa ufafanuzi zaidi.
Na Mtunzi wa Maandiko ya Kiurithi anasema hapa: Kitabu cha Kuuza. Katika lugha ya Kiarabu neno Baiu (Kuuza) ni Mzizi kwani Wataalamu wa Lugha ya Kiarabu wameleta picha ya Mzizi wa neno na maada yake na wakaona ya kuwa kuna miundo tofauti ya neno hilo na wakajiuliza: Ni lipi chimbuko la miundo hii yote: Kuuza, Uza, anauza, muuzaji, kinachouzwa, mauzo, Mauziano, kununua… na kuendelea. Wamekuta kuwa kila moja kati ya maneno haya linarejea katika neno ameuza, au mauzo: kuna herufu tatu katika neno (Baa-aa) ameuza kwa kiarabu, ambazo ni baau, alifun na ainun. Au baaun, yaaun na ainun. Na hivyo ndivyo tulivyojifunza katika madarasa ya Awali wakati wa kulifichua neno katika Kamusi, ambapo tunautafuta Mzizi au Shina. Wabusraa (ambao wanawakilisha Chuo cha Lugha) wameona ya kwamba chimbuko baiun (kuuza) ni Mzizi au Shina la Mnyumbuliko wa neno, na kutokana na Shina hilo yanazalika maneno yote yaliyobakia: ameuza, muuzaji na kuendelea.
Na wakauita huu kuwa ni Mzizi, na Mzizi kwa Wanachuoni wa Nahau unamaanisha tukio, na wala haumaanishi kitu chenyewe. Na tukio hapo kilugha ni Kitendo, kama vile kusogea kwa kitu kutoka hapa mpaka pale. Tukio hili tunaliita kusogea, nalo ni Mzizi usio na wakati Maalumu. Na ikiwa tukio litafungamana na muda maalumu basi litabadilika na kuwa Kitendo; kama vile “ameuza” kitendo cha muda uliopita, “anauza” kitendo cha muda uliopo na kuendelea. Na kuna Mzizi ambao unamaanisha Tukio.
Na linazuka swali iwapo mwanadamu ni mzushi wa Kitendo au Vitu vilivyozuka vinakuwa vina Idadi kubwa, na je tukio hilo linaweza kuwa na idadi kubwa? Na hapo, Wanachuoni wa Nahau wamekuta kwamba tukio haliwezi kuwa na Wingi; kwani Suala la kuhama ni Suala moja, an Suala la kupiga linaelezea pigo moja tu, haliwi na wingi kwa kuwa kwake ni mgongano wa kitu na kingine. Na Mgongano katika akili ya Mtu ni mmoja tu. Na kuanzia hapo, Wanachuoni wa lugha waliweka Msingi katika Nahau unaoielezea hali hii ya kiakili, ambayo kwamba “Mizizi haiwekewi wingi”. Kwa hiyo, Msingi hauna wingi wake, na hii ni katika Shina lake.
Lakini Wanachuoni wa Nahau waliibua swali lingine ambalo ni: je Uwingi huo kwa jinsi ulivyo hauna aina nyingi? Na je, kuna aina miongoni mwa aina za wingi ambayo tunaweza sisi kuipata katika Mzizi, kama vile kuwepo kwa kipido cha nguvu na kipigo kidogo na pia kipigo cha kati? Kwa hiyo Mgongano ndio unaosababisha kipigo kikubwa au cha nguvu na kidogo; kwa hiyo, wameona wao kwamba kuna uwezekano wa kukusanya Mzizi kwa upande mmoja, iwapo sisi tutaleta picha ya uwepo wa Watu tofauti tofauti. Kwa hiyo Mzizi ni jinsi wenyewe ulivyo, na kinyume chake ni jinsi watu wanavyoujengea taswira zao wenyewe. Kwa hiyo, Kipigo – kwa jinsi kilivyo – hakiwi na wingi kwa kuwa kwake kikali au kikubwa, lakini – kwa upande wa kuwa kwake kikali – kinyume chake ni jinsi ya kuwa kwake chepesi au kidogo; na kwa hivyo, inafaa kukipa wingi iwapo pataangaliwa kwa mtazamo huu.
Na kama ingelisomwa kimakosa kwa kuongeza herufi ya kuvuta – kama inavyotokea kwa baadhi ya wasioitambua lugha – basi maana ingelitofautiana na ile aliyoikusudia Mwandishi wa Urithi Wetu.
Ama kuhusu kauli yake ya kwamba: “ Kwa kuwa hilo ni katika Matendo bora mno” ina maana ya kwamba Mtunzi ameanza na Ibada zilizo bora zaidi. Kwani daima Mtu anapaswa kuyaanza maneno yake kwa vitu vilivyo vizuri zaidi. Na kwa kuwa Kulazimika kufanya hivyo ni zaidi, na hili ni jambo la kawaida tu, kwani Waislamu wote wanalazimika kutekeleza Ibada mbalimbali na kusimamisha Ibada za kuonekana kama vile Kusimamisha Sala, na kutekeleza ibada ya Saumu, na nyingine nyingi isipokuwa kwa wenye Udhuru unaokubalika kisheria, lakini sio lazima kwao Kuuza na Kununua. Kuuza na Kununua sio jambo la dharura katika maisha ya Mtu; na kwa ajili hiyo mwanzo wake ulikuwa kwa Mwandishi wake ni kuhusu kile Waislamu walichokuwa na haja nacho ya kutaka kukijua zaidi na kukifikia katika Maisha yao, nacho ni Ibada zao na matendo yake wayafanyayo kila siku maishani mwao.
Na kwa uchache wa watu wanaofanya hivyo; kwa maana ya Kuuza na Kununua, wanaofanya hivyo ni wachache kuliko wanaofanya Ibada mbalimbali. Na hapo ndipo miundo mbalimbali ya kilugha inapoingilia kati katika yale tunayotakiwa tuyasimamie katika Ibara hii na kuichunguza vilivyo. Na kwa hivyo tunasema: “Na asili ya Tamko lake ni Mzizi wa neno”. Neno lililopo hapa linarejea katika Kuuza, nako mzizi wa neno ameuza, anauza, ambapo Mzizi wake ni Kuuza, na anaendelea kusema: na kwa ajili hiyo ndipo alipolipwekesha neno hilo; kwa maana kwamba neno hili ni Mzizi na kwa hivyo amelifanya likawa moja, na akasema: Kuuza na wala hajasema Mauzo. Amefanya hivyo kwa sababu Mzizi wa neno unamaanisha Tukio, na Tukio moja haliwi na wingi kiasili kama tulivyokwisha ashiria; na kwa ajili hiyo ndipo alipolifanya likawa moja.
Na huwenda ikawasukuma baadhi ya Watu kwamba katika baadhi ya vitabu hukusanywa rejea zake kisha pakasemwa: Mlango au Kitabu cha Kuuza. Na hapo ndipo Mwandishi wa Urithi Wetu anapojibu: “na ikiwa chini yake kuna aina nyingi”: kwa maana ya kwamba kuna uwezekano mkubwa tukasema kwamba: “Mauzo” sio kwa kuzingatia kwamba ni tukio, bali ni kwa kuzingatia kwamba chini yake kuna aina nyingi; kwa maana ya aina za Kuuza. Ama kulizungumzia suala hili hapa ni kulizungumzia Tukio lenyewe kama lilivyo; na kwa hivyo ilikuwa ni kulijongelea Suala hili kwa kupitia njia ya kwamba hili ni Tukio.
Na anaendelea kusema kwamba: “kisha likawa Jina”. Na Kiwakilishi Jina cha Kitenzi kikabadilika na kikawa kinarejea kwa neno “Kuuzaa”. Na anaendelea kusema: “kwa kuwa kwake na maonano”; kwa maana ya kwamba neno Kuuza limekuwa jina la kila Tukio ambalo ndani yake kuna maonano, na vilevile neno Kununua.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Aya ya 111, Suratu Tauba.
Na hivyo ndivyo ilivyo katika kila Maonano yanayoitwa kuuza na Kununua.
Na anakamilisha kwa kusema: kisha ikiwa itakusudiwa kwayo moja ya pande mbili za Mkataba huo, hapa sisi tutalazimika kutambua Suala la “Zingatio” au Suala la “Lango”; ambapo Mwandishi amekuja na Milango mitatu hapa: Wa kwanza – iwapo tutaingia katika Kuuza kwa kukuzingatia kuwa ni Sifa miongoni mwa sifa za Muuzaji au Mchuuzi. Mlango wa pili – tunapoingia katika Uuzaji kwa kuizingatia kuwa ni Sifa miongoni mwa sifa za Mnunuzi. Na Mlango wa tatu – Kuuza ni kama uhusiano wa baina ya Mchuuzi na Mnunuzi. Milango mitatu na Sisi tunaweza kuuchagua wowote.
Na akaanza kwa kusema: “Kisha ikikusudiwa kwayo mmoja kati ya pande mbili ambapo anayekuja kutoka huko anaitwa Mchuuzi, basi itajulikana kuwa ni umilikishaji kwa kupokea malipo mbadala kwa sura ya Umiliki wa kudumu”. Angalia tofauti iliyopo baina ya Kumiliki kwa Malipo mbadala na katika hali ya kudumu ambayo imo katika Mlango wa kwanza (kwa upande wa Mchuuzi), na kujimilikisha kwa malipo mbadala pia, katika Mlango wa pili (upande wa Mnunuzi).
Kumiliki kwa malipo mbadala hapa kunawakilisha Maonano; kwa maana ya kwamba kuna bidhaa na kwa mkabala wake kuna fedha, na Kuuza ni kumiliki Bidhaa kwa kuilipia fedha, na anasema Mchuuzi: Hakika mimi nimeimilikisha bidhaa yangu kwa Mtu huyu na nikachukua kutoka kwake malipo. Na kwa sifa ya kudumu, kwa maana ya kuhusika na jinsi ya kuleta Mauziano; kama vile atasema Mchuuzi kwa Mnunuzi: nimekuuzia bidhaa hii kwa senti kumi, na Mnunuzi akajibu: na mimi nimeinunua bidhaa hii kutoka kwako kwa thamani ya senti kumi. Hili ndilo linaloashiria Mpatano wa lazima kwa ajili ya kusimamisha Uhusiano wa kuuziana.
Kisha tunakuta kwamba inaingia katika Suala hili kwa Mlango wa Kununua, na kwa hivyo tunasema: Na inaelekeana na Ununuzi ambao ndio upande mwingine ambao anaekuja kupitia huko huitwa Mnunuzi na unajulikana kama ni Umiliki. Liangalie neno Umiliki katika Kununua, na tofauti baina yake na umilikishaji katika Mauzo. Kwa mbadala kama ilivyo maana iliyotangulia kutolewa. Na neno “vilevile” hapa linaashiria Ibara iliyotangulia: “kwa sifa maalumu” katika Dhana ya kwanza.
Na anakamilisha kwa kusema: Inajuzu kumpa Mnunuzi jina la Mchuuzi, au kumpa Mchuuzi jina la Mnunuzi, kwa mazingatio; kwa maana mimi – kupitia mlango wa tatu – nitampa jina Mchuuzi au Mnunuzi yoyote kati ya pande mhuizo kwa zingatio lolote ninalolizingatia mimi. Na ikiwa nitasema kwamba mwenye cha kutoa kama mbadala ni Mchuuzi kwa kumzingatia kuwa yeye ndiye mwenye fedha, Mtu wa upande wa pili atakuwa mtoaji wa mbadala, kwa maana ya mwenye bidhaa ndiye Mnunuzi, na kwa hivyo mwenye Mali anakuwa anakuwa yeye ndiye anayeuza fedha kwa mali kwa kumzingatia kuwa ndiye mtoaji wa mbadala.
Baadhi ya Wanachuoni wanaokataa njia hii, na wanaona ya kwamba mtu mwenye pesa anaainika kama Mnunuzi na Mtu mwenye bidhaa ni Mchuuzi. Lakini inakuwaje kama hakuna fedha na bidhaa ikawa ikatolewa kwa bidhaa nyingine, kama vile Kitabu kwa Kitabu; kwa maana ya makabidhiano.Huku ni Kuuza na Kununua kwa makubaliano ya Wanachuoni. Basi ni nani hapo Mnunuzi na ni nani Mchuuzi? Hapa haiwezekani kuainisha wahusika isipokuwa kwa mazingatio. Kwani meno neno “kuzingatia” lina maana ya: kwa upande wa kuwa nimetaka kuingia katika Suala hili na kuzingatia.
Na anaendelea kwa kusema: Na Inajuzu kutumia jina la Mnunuzi kwa Mchuuzi na Mchuuzi kwa Mnunuzi ckwa kuzingatia. Na ibara hapa…: na hapa ametumia maneno mawili yanayoshabihiana kwa kuzingatia kinachokusudiwa kwa maana ya kila moja lina Mwelekeo wake wa maana. Na anaendelea akisema: na Ibara ya Kumiliki au Kumilikisha kwa kuangalia maana ya kisheria l. Na hapa jumla imekamilika na maana ikadhihirika jambo ambalo linatujulisha umuhimu wa kuelewa Kiwango Kamili cha Sentensi yenye Maana katika miundo ya lugha: Inaanzia wapi? Na inaishia wapi? Na kauli yake: “Maana ya Kisheria” kwa ajili ya kupambanua Maana inayolengwa mbali na zisizotakiwa za kienyeji au za kilugha au nyinginezo. Na kinachokusudiwa ni kwamba maana za Kumiliki na kumilikisha zitakuwa katika Mjengeko huu wa maana ya sentensi, kwa kuangalia Nadharia ya Kisheria, ambayo itadhihirika kwa upambanuzi wa nadharia mbalimbali zinazotawala.
Na anaendelea kusema: “na iwapo patakusudiwa kwa neno – Kuuza – kama ni muungano wa pande mbili kwa pamoja ambao ni Kuuza na Kununua kwa maana ya fungamanisho na Uhusiano unaopatikana kutokana na pande mbili ambazo zina upatikanaji wa Kujuzu na Kutenguka. Uhusiano huu au kukubaliana huku kunakotokea baina ya pande mbili na ambao kinapatikana ndani yake tuweza: kujuzisha na kupitisha au kuvunja na kuzuia, Mfungamano huu ndio tunaoutaka uwe sehemu ya Dhana yetu ya Kuuza kwa kupitia sehemu hii. Nao kwa hivyo ni mkabala wa Kitu kwa kingine kwa namna ya kupeana.
Kama Mtunzi wa Urithi angelinyamaza, basi Dhana hiyo ingelitumika kwa kila Mkabala hata wa Ndoa kwa Mfano, kwani ndani yake kuna Mkabala lakini ndani yake hakuna kupeana mbadala. Ingawa mume anatoa mahari, lakini sio kwa mbadala wa Kitu kingine, isipokuwa hufanyika hivyo kwa njia ya mapenzi na Zawadi iliyofaradhishwa.
Na anasema Mtunzi: “ndani yake inaingia..,” kisha mwisho wa mstari huo huo anasema: “na ametoka kwa njia ya kupeana mbadala”, ni Suala ambalo linaingia kwenye mweleweko wake na kutoka kwenye Dhana yake, Jambo ambalo hatuwezi kulifahamu isipokuwa tutakapotambua taswira Kuu ya maswali ya Dhana katika Mantiki; ambapo Watu wa Mantiki wana taswira kamili na kisa kikubwa katika Dhana, hapana budi kufahamu ili tuyadiriki maandiko mengi ya Urithi wetu.
Na wanasema – katika dhana ya mwanadamu kwa mfano:- Kwamba yeye ni mnyama anayezungumza. Mnyama maana yake ni kiumbe kinachoenda kwa Utashi wake chenyewe; kwa maana ya kwamba ni kiumbe na pindipo kinapotaka kujipatia kitu basi hukihangaikia kitu hicho na kukiendea.
Kwa hiyo, tuliposema: kwamba mwanadamu ni mnyama, hakika tumemtoa kwenye kundi la vitu vigumu vigumu kama mawe na mfano wake, ambavyo havitikisiki, na tukamtoa katika kundi la mimea ambayo hutikisika kwa mantiki ya kuathirika na kitu kingine kilicho nje yake kama vile upepo, na sio kwa utashi wake. Lakini Mifugo yote inaingia kwenye kundi la Wanyama, kama wanyama wanaotikisika kwa kutaka na kwa hivyo tuliposema: “anaezungumza”, tuliwatoa Wanyama ambao ni Mifugo katika kundi hili; kwa kuwa nao hawazungumzi, na uzungumzaji unakuwapo kwa kufikiri ambako huuathiri ulimi na kuufanya utamke maneno.
Kwa hiyo, maneno yanayotamkwa na mwanadamu ni alama Miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni moja kati ya Sifa Maalumu alizomuumbia nazo Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwanadamu.
Na katika Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. Aya ya 23, Suratu Dhaariyaat. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameijaalia kuwa Alama miongoni mwa Alama zake yeye aliyetukuka kwa waja wake, na Alama hii ni Muujiza wa kipekee, iwapo utazingatia jinsi herufi zinavyotamkika na jinsi zinavyojenga neno kwa neno na kuhamia akilini, na Mwanadamu akaweka hayo katika sehemu ya maana zinazomtukia akilini mwake. Hili ni jambo gumu, kubwa, na la kushangaza linafanyika kwa kasi kubwa na kwa wepesi.
Na kwa hivyo, nyanja za viapo na muongozo kwetu Sisi ni neema miongoni mwa neema nyingi. Na hivyo, Dhana hii iliwaingiza Watu wengi mno wenye akili katika mweleweko wa neno “Mwanadamu”, na kuwatoa Mifugo na Wanyama wengine. Kwa hiyo neno “anaingia” na neno “anatoka” ni miongoni mwa maneno ya kimantiki yanayokusudiwa kwayo kuwaza sura maalumu tutakayoiona tutakapozungumzia Mitazamo Mikuu.
Na Mtunzi anakamilisha kwa kusema “na inaingia ndani yake” kwa maana ya ndani ya Dhana hiyo – kila kile kisichofaa kumilikika kama vile Mali za Watu, na hii haiwezi kufahamika maana yake isipokuwa baada ya kuzijadili Nadharia tawala; kwa upande wa Nadharia ya Mali inavigawa vitu kwa mchango wa vitu hivyo na kuelekea katika vinavyofaa kuwa na thamani na vile visivyofaa kuwa na thamani. Na huwenda ikawa kwa vile visivyokuwa na thamani vikawa na manufaa fulani, na je, sisi tutafanya nini iwapo Umiliki hauwi isipokuwa kwa kitu kinachofaa kuwa na thamani? Hapo, Wanachuoni wanaona ya kwamba ikiwa hali itakuwa hivyo hakika jambo hili litahitaji kile kisichofaa kuwa na thamani na ambacho hakimilikiwi na Mtu yoyote – kipewe jina jingine litakalokusanya maumbo ya aina zake zote: Katika vyenye manufaa na visivyokuwa na manufaa; na jina hilo ni “Ikhtiswaasu” kwa maana ya kitu chochote kinachomuhusu mtu au kitu kingine).
Na Ikhtiswaasu; ni neno linalomaanisha kuwa kitu fulani kinamuhusu mtu au kinahusu kitu kingine; kwa maana ya kwamba kitu hicho ni maalumu kwangu mimi kwa mfano.
Wanachuoni wa Madhehebu ya Shafiy, Wao kwao kinyesi cha Mifugo ni najisi, na najisi haimilikiwi, isipokuwa mkulima katika shamba lake anakihitaji kwa kazi mbalimbali, na je, inajuzu kukiuza kinyesi hicho na kukizungusha katika soko la kibiashara baina ya Watu? Na hapa – kwa Mujibu wa Kanuni ya”Najisi haimilikiwi” – haijuzu, isipokuwa kwa Mujibu wa Kanuni ya Ikhtiswaasu – hakika kinyesi cha mifugo ni mali ya mmoja katika Watu; kwa maana ya kuwa yeye ndiye anayehusika nacho; na hakika mambo yalivyo, kutokan na Watu kuhitaji mno muamala huu,; na kwaku umekuwa muamala huu kama dharura ili kurahisisha maisha ya Watu katika Jamii Maalumu, kwa hiyo inajuzu kukihamisha kinyesi kutoka nyumba moja hadi nyingine ya jirani yangu na kuondosha umiliki wangu binafsi wa kinyesi hicho.
Na kujiepusha na kinachomilikiwa – kwa Mujibu wa Maneno yao – kuna maanisha kuachia kitu kwa mtu mwingine, na kwa malipo ya kitu chenye thamani au fedha taslimu. Jambo hili liko karibu mno na linashabihiana na Kuuza.

“Kujiepusha na Bobezi” – kwa mujibu wa ibada zao – kuna maanisha kuachana na Bobezi za jambo hili na kuepukana nalo kabisa, na hiyo ni kwa mkabala wa mali au fedha. Jambo ambalo linakaribiana na kuuziana, lakini wanazuoni wa Madhehebu ya Shafiy wanapinga kupewa jina hilo la Mauzo ingawa wao wanatoa jina la mabadilishano au makabidhiano kwa njia ya kujiepusha na Ubobezi. Na kwa hivyo wao hapa wanaashiria ya kwamba kama Maana ya Kuuza itakuwa katika lugha inaikusanya hali hii isipokuwa maana yake kisheria haikusanyi hali hii. Wanafanya hivyo ili wazilinde hukumu walizozipitisha juu ya suala la Kuuza na Kununua na wakajuzisha hapa jinsi ya kulishughulikia kwa kuendana na uelewa wao mpaka wasije wakawawekea Watu uzito.
Na turejee sasa kwa mwandishi: inaingia ndani yake – kwa maana ya Kuuza kilugha, na wala sio kisheria – kile ambacho hakisihi kukimiliki kama kitu cha mtu: kwa maana ya kuingia katika Kuuza hali ya kujiengua umiliki wa kitu. Na iwapo tamko halitakuwa kama la Kupeana kusiko na Tamko Maalumu. Kupeana ni Istilahi ya Wanazuoni wa Fiqhi inayotumika katika baadhi ya makubaliano ya kuuza na kununua wanayoipitisha Watu bila ya kuwapo Tamko Maalumu. Kwa mfano: Unapompa Muuzaji kiasi kadhaa cha fedha ili akupe kiasi kadhaa cha bidhaa bila ya Tamko Maalumu linalokadiria thamani au kiasi cha bidhaa husika iliyotolewa, basi hapo ndipo kunatuka Mapeano. Na katika njia hiyo hiyo kunakuja Chombo chochote cha Kisasa tunachokitumia kutia fedha kisha kujichukulia bidhaa.
Na hapa, ili tuweze kukifahamu ipasavyo kipengele hiki tunalazimika kuijua maana ya Kupeana (Muaatwaatu),
Hakika Tamko linazingatiwa kuwa ni nguzo katika Mauziano na hakika makabidhiano yanayofanywa na Watu, iwe ni katika suala la Miliki au Miamala inayofanana na Mapeano, basi makabidhiano yanayotokea hapo huitwa kilugha Kuuziana, lakini hayaitwi hivyo Kisheria.
Kwa hiyo, tunakuta anakamilisha akisema: na imetoka kwa sura ya Kupeana, kumetolewa katika Dhana ya Kuuza, kwa sura nyingi sana za makabidhiano na Maonano, na kwa hivyo kumeshibitiwa wigo wa Dhana ya Kuuza.
Na anakamilisha: Kisheria – ni makubaliano ya kupeana kifedha kunakomaanisha Umiliki kamili wa kinachotolewa au kunufaika nacho kwa Muda wote na wala sio kwa muda mfupi. Na hivyo ndivyo tuunavyoikuta Dhana inajumuisha sehemu kadhaa; nayo inajengeka kwanza kabisa kwa Makubaliano na pili Makabidhiano, na tatu mali, na nne – ni kumaanisha Umiliki wa Kitu au Manufaa yake, na tano ni kwa muda wote na sita sio kwa Muda mfupi. Sehemu zote hizo zinaashiria madhumuni na maana zinazoainisha kikamilifu Maana halisi ya Kuuza.
Na anakamilisha kwa kusema: Na nguzo zake ni tatu: Mtia Mkataba, kinachotiliwa Mkataba na Tamko. Na hivyo ndivyo ilivyo.
Ufupisho wa Mwisho:
Yaliyotangulia yanaashiria juu ya umuhimu wa tunachokihangaikia katika uchambuzi wa Maandishi ya Urithi na Misingi na Yanayotakikana ambayo lazima tuyafikie na kuyazingatia ipasavyo, mpaka iwe rahisi kuelewa alichokikusudia mwandishi wa maandishi hayo na kukifikisha hadi kwa msomaji kwa wakati huo, na ikiwemo katika hayo kufahamu mitazamo Mikuu au baadhi yake ambayo inasaidia katika kugundua usiri wa Urithi huo, na vilevile kufahamu baadhi ya mitazamo ya hekima na busara na Istilahi na dhana mbalimbali na miundo ya kilugha na elimu maalumu zinazoyatumikia mambo haya, na Kisha tukarejea kwenye maandiko mara nyingine na tukaangalia; Je kuna hitilafu katika kuyaelewa maandiko haya ambayo tunayo baada ya kupitia njia zote za kuyaelewa kutokana na jinsi tulivyokuwa tukielewa hapo kabla ya kuzipitia elimu hizo?
Chanzo:
Atwariiq ilaa fahmi Turaathi, (Njia ya kuujua Urithi Wetu) kitabu cha Samaha Mufti wa Misri Dkt: Ali Juma.

 

 

Share this:

Related Fatwas