Wakati wa Kumalizika Ulezi wa Yati...

Egypt's Dar Al-Ifta

Wakati wa Kumalizika Ulezi wa Yatima au Mtoto Asiyejulikana Ukoo wake.

Question

Ni upi wakati wa kumalizika muda wa Malezi ya yatima au Mtoto asiyejulikana ukoo wake? Na je, Wakati wa Malezi hayo unaishia kwa Mlezi kufariki dunia? Na kama kuna talaka kati ya mwenye jukumu la Malezi na mkewe, na kwa hivyo kafala ya mtoto huyu itakuwa kwa nani? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na watakaomfuata, na baada ya utangulizi huo:
Ulezi wa Mtoto ni aina ya mchango wa kujitolea, nao ni: pale mwenye kukalifishwa humpa mwingine mali au manufaa kwa sasa au baadaye, bila ya malipo ya thamani, na kuhusu kafala, Mlezi anampa Mtoto anayelelewa mali na manufaa kwa pamoja.
Kuhusu wakati wa kumalizika kwa muda wa Kulea, inajuzu kwa mwenye kulea kuvunja mkataba wa kulea mtoto katika wakati wowote; kwa sababu ni mkataba wa mchango wa kujitolea.
Kwa hiyo Jumuiya zenye Madaraka na zinazohusika na jukumu hili lazima zichukue hatua za kusimama mahali pa Mlezi anayejiengua Ulezi huo haraka iwezekanavyo, kwa ajili ya kumlinda mtoto anayelelewa.
Na kama Mlezi akishurutisha muda maalumu wa Malezi ya mtoto, basi sharti hilo litekelezwe kama ilivyoshurutishwa, kwa kuangalia sharti hili bila kuyadhuru masilahi ya mtoto, na huenda Mlezi akafilisika ambapo wakati huo hatakuwa na mali ya kuitumia kwa ajili ya mtoto huyo anayemlea, hapo mkataba utavunjika, pia huenda Mlezi akafariki dunia, hapo muda wa Ulezi unaisha, na mtoto atarudishwa kwenye nyumba ya mayatima; ambapo kwa kawaida Ulezi hauirithiwi; kwa sababu ni mkataba wa mchango wa kujitolea.
Na inajuzu kwa mwenye kuchangia avunje mkataba huu wakati wa maisha yake, kwa hiyo halazimiki mtu kuendeleza mkataba huu baada ya kifo cha Mlezi, kuelekea kwa warithi wake, na kwa sababu mkataba ni lazima kwa pande zake tu, lakini kama warithi wakichangia, wote au mmoja kati yao, kuitekeleza Malezi, hapo utakuwa mkataba mpya.
Na huenda Malezi ya mtoto yakawa yameandikwa kwa jina la baba na mama kwa pamoja, na katika hali ya talaka au kifo cha mmoja wao, itekelezwe na waliyoyakubali kati yao, na kwa upande mwingine nyumba ya mayatima yenye jukumu hili ibebe jukumu la kumlea mtoto huyo na hayo yote yazingatiwe kuwa ni kwa masilahi ya Mtoto anayelelewa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas