Hukumu ya Kisheria Juu ya Maandaman...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kisheria Juu ya Maandamano, Malalamiko na Migomo

Question

Je! Ni ipi hukumu ya kisheria juu ya maandamano, malalamiko na migomo? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salaamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba wake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Neno “Maandamano” ni wingi na umoja wake ni andamano, ambalo maana yake ni: kukusanyika kwa Kikundi cha watu mbele ya eneo la wazi ili kudai jambo moja au zaidi kutoka kwa mtawala mara nyingi, kusudi lao ni kuonesha kwamba mahitaji yao sio mahitaji ya mtu binafsi bali ni mahitaji ya pamoja. Maandamano ni ushirikiano kati ya waandamanaji, na kuimarisha kati ya washiriki wao, na maana hii ndiyo maana ya kilugha; Katika “Mukhtar Al-Sahah” [Kidahizo: (Maandamano) na Ushirikiano.
Maandamano yanaundwa na vitu viwili, kila kimoja kati ya viwili hivyo kinaruhusiwa kuwa peke yake;
Cha kwanza: ni mkutano tu wa watu; Kanuni ya msingi katika vitu hivi viwili ni kukataa kasoro yoyote, mpaka dalili ioneshe kinyume chake.
Cha pili: Ni kutaka jambo la Halali litekelezwe, au kuondosha jambo baya; Maandamano ni njia bora ya kufanya hivyo, na njia zinachukua hukumu ya nia. Kanuni ya msingi katika kuomba mahitaji kutoka kwa mtawala ni Uhalali; Kwa hivyo mwenye mamlaka yupo kwa ajili ya kutimiza matakwa ya raia, na kwa hivyo, Mtume S.A.W., alikemea kutoonekana kwa wenye mamlaka na kuwa mbali na wenye mahitaji. Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud kwamba Mtume S.A.W., amesema: “Mwenye kutawala mambo ya Waislamu kisha akajificha mbali nao ili asikidhi mahitaji yao, na kuondosha umaskini wao, Mwenyezi Mungu hatamkidhia mahitaji yake wala hatamwondolea umaskini wake”. Vile vile imepokelewa kutoka kwa Ahmad kwamba Mtume S.A.W., amesema: “Mwenye kutawala mambo ya Waislamu kisha akajiweka mbali na anaowatawala ili asikidhi mahitaji ya wanyonge na wenye umaskini, Mwenyezi Mungu atajiweka mbali naye, siku ya Kiyama”
Mtume S.A.W. amewahimiza masahaba wake katika kukidhi mahitaji ya watu. Imepokelewa kutoka kwa Abu Mussa R.A. katika Sahihi mbili kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alikuwa anapojiwa na mtu mwenye shida na kumwomba amsaidie haja yake, basi Mtume S.A.W. alikuwa akiwaambia masahaba wake: “Msaidieni ndugu yenu nanyi mtapata ujira, kisha Mwenyezi Mungu hukidhi haja zao kupitia ulimi wa Mtume wake anachotaka yeye Mwenyezi Mungu”.
Pia imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy kutoka kwa Anas bin Malik, R.A., alisema kuwa watu miongoni mwa Ansaar walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. wakati Mwenyezi Mungu alipompa ‘fay’i’ katika mali ya Hawaazin kama alivyompa, akawa anawapa watu katika Makureshi mamia ya ngamia, wakasema: Mwenyezi Mungu amsamehe Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., anawapa Makureshi na sisi anatuacha, na hali panga zetu zinadondoka damu zao (hapo watu wa Hawaazin walipokuwa makafiri). Anas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akahadithiwa hayo maneno yao. Akawapelekea ujumbe Ansaari akawakusanya katika Hema la ngozi na hakumwita mtu mwingine pamoja nao asiyekuwa miongoni mwao. Walipokwishakutani na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akawajia, akasema: “Ni maneno gani haya yaliyonifikia kutoka kwenu?” Wanachuoni katika wao wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa upande wa wenye fikira zenye busara kama zetu hawakusema kitu, ama watu kati yetu walio wadogo kiumri wamesema: Mwenyezi Mungu amsamehe Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anawapa Maqureshi na anawaacha Ansaari wakati ambapo panga zetu zinadondoka damu zao (Maqureshi kabla hawajasilimu) Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: “Hakika mimi huwapa watu ambao wametoka katika Ujahilia hivi karibuni. Kwani nyinyi hamko radhi kuwaona watu wanakwenda na mali, na nyinyi mnarejea kwenu huku mmefuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi naapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hicho mnachorejea nacho nyinyi ni bora zaidi kuliko wanachorejea nacho wao” Wakasema: Ndivyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi tumeridhia. Akawaambia: “Hakika nyinyi mtaona baada yangu watatangulizwa watu mbele kuliko nyinyi, basi subirini hata mkutane na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwenye Al-Hawdh” (jina la sehemu Peponi). Anas akasema: Na hawakusubiri.
Hadith hii ina dalili ya kuzungumzia suala linalohusiana na ombi la mtawala kwa kiwango cha kikundi; kufuatana na idhini ya Mtume, S.A.W. kwao.
Ikumbukwe kuwa idhini hii iko chini ya masharti kadhaa na inadhibitiwa na udhibiti wa aina kadhaa, pamoja na:
1- kutokuwa suala la ombi la kutekeleza jambo baya haliruhusiwi na Sharia.
2- kutojumuisha wito au maneno yaliyokatazwa na Sharia.
3- kutojumuisha vitu ambavyo ni marufuku, kama vile kudhuru watu, au kushambulia mali za watu, au mchanganyiko uliokatazwa kati ya wanaume na wanawake.
Na malalamiko ni kama maandamano katika hukumu na udhibiti, na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Haakim katika Kitabu chake cha Mustadrak, kutoka kwa Abu Hurairah, R.A., inaashiria uhalali wa kitendo chao, kwamba mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W., akimlalamika jirani yake, na akasema: Ewe, Mtume wa Mwenyezi Mungu, jirani yangu ananiudhi. Akasema: “Toa mizigo yako nje, iweke barabarani.” Basi akatoa mizigo yake nje na kuiweka barabarani, kwa hivyo kila mtu aliyepita alisema: Je! una nini? Akasema: Nilimlalamikia jirani yangu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., kwa hivyo akaniamuru nichukue mizigo yangu na kuiweka barabarani, wakasema: Ewe Mola, umlaani, Ewe Mola, umdhalilishe.. Akasema: hali hiyo ikamfikia huyo jirani yake, na akamwendea mtu yule akamwambia: Rudi, naapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kamwe sitakuudhi tena.
Kuhusu wale waliosema kwamba maandamano hayo ni marufuku kwa sababu ni uzushi wa kimagharibi, basi maoni hayo hayakubaliki, kwa sababu suala hilo sio miongoni mwa vitendo vya ibada ili isemwe kwamba ni uzushi, kwa hivyo ikisemwa: Kinachokusudiwa ni kwamba suala hilo ni miongoni mwa mambo ya uzushi wa mila inayokuja kwetu kutoka Magharibi, jibu ni: kwamba maoni hayo pia siyo ya kweli; Kwa sababu maandamano hayo yalikuwa yanajulikana kwa Waislamu katika nchi zao karibu zote na tangu kale, na yalitumiwa na watawala baadhi ya nyakati, na wakati mwingine kwa mwenyeji aliyetawaliwa; Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Abu Nuaim, kitabu cha Hilatul Awliyaai [4/324, As-Saadah] Imepokolewa kutoka kwa Ash-Shabi kuwa alisema: “Jambo lililo bora ni umati wa watu, wanaozuia mbubujiko, na kuzima moto, na wanaopinga watawala wabaya.
Sio yote tuliyoyapokea kutoka katika Nchi za Magharibi ni mabaya. Imepokelewa katika Sahihi mbili kutoka kwa Anas bin Malik, R.A., alisema: “Alipotaka Mtume S.A.W. kuwaandikia Warumi, aliambiwa: Wao hawasomi barua ila iwe na muhuri. Akatengeneza muhuri wa fedha, na ulinakishiwa kwa maneno haya:``Muhammad MtumewaMwenyezi Mungu kama kwamba nautizama weupe wa mkono wake. At-Twabariy Akasema kutoka kwa Omar: Ni wa kwanza aliyebeba kiboko, na kupiga nacho, naye ni wa kwanza aliyewafanya watu madiwani katika Uislamu, na waliandika watu kufuatana na makabila yao, na kuwalazimishia zawadi. Al-Harith aliniambia akasema: Tuliambiwa na Ibn Saad alisema: Tuliambiwa na Mohammed bin Omar, alisema: Niliambiwa na Aa'idh bin Yahya, kutoka kwa Abu Al-Huwayrith, kutoka kwa Jabir bin Al-Huwayrith bin Nuqaid, kwamba Omar Bin Al-Khatwab (R.A.) alishauriana na Waislamu katika kuandika madiwani, Ali bin Abi Talib akamwambia, Kila mwaka pesa hukusanywa kwako, kwa hivyo usichukue chochote kutoka katika pesa hiyo. Ibn Affan alisema: Naona pesa nyingi ambazo zinaweza kuwatosha watu, hata ikiwa hazikuhesabiwa ili ujue ni nani kachukua na nani hakuchukua, niliogopa kwamba itaenea. Al-Walid Bin Hisham bin Al-Mughiarah akamwambia: Ewe mkuu wa waumini nimekuja kutoka Sham, nimeona Wafalme wao wamefanya diwani, na wakakusanya majeshi, akafuata kauli yake. Tarikh Al-Tabari (4/209).
Hoja iko wazi, nayo ni kujifunza mambo kadhaa ya Ufalme kutoka kwa mataifa mengine, hali ambayo haipingani na sheria yetu.
Jambo la msingi ni kwamba: maandamano na malalamiko asili yake ni halali, na hukumu nyingine tano zinaweza kupotoshwa kulingana na madhumuni na njia zake. Kutokana na hayo, hali ya kushiriki katika maandamano hayo itakuwa ni kwa kulingana na hukumu yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Ofisi ya Fatwa.
 

Share this:

Related Fatwas