Siasa ya Ndani na ya Nje katika Uis...

Egypt's Dar Al-Ifta

Siasa ya Ndani na ya Nje katika Uislamu – Somo linalotokana na Ufunguzi wa Makkah.

Question

Ufunguzi wa Mji wa Makkah unazingatiwa ni katika matukio makubwa ndani ya historia ya Uislamu. Ni mafunzo gani muhimu ya kunufaika nayo? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mtume S.A.W. ametufundisha namna ya kufanya mazungumzo kufikiri kwa ajili ya baadaye pamoja na busara, na kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu ndio msingi na asili ya matendo yote mema, kwani Mtume S.A.W. alikubali kwenye tukio la suluhu ya Hudaibiyah yote yaliyokuwemo kwenye makubaliano hayo, ambapo washirikina wa pande za kusini na Wayahudi wa kaskazini mwa Kheibar walikubaliana kuuingia Mji wa Madinah kwenye kona zake zote, ikaja hatua ya suluhu ya Hudaibiyah ili kuwaondoa washirikina na kubatilisha makubaliano yao na Wayahudi, kisha ikaja vita ya Khaibar ili kuondoa mzingiro eneo la Kaskazini mwa Mji wa Madinah, ikaja hatua ya ufunguzi wa Mji wa Makkah baada ya Makoreshi kuvunja makubaliano ambayo yalifikiwa kwenye kikao cha mazungumzo cha Hudaibiyah ili kuondoa kabisa mzingiro eneo la kaskazini, hivyo Mtume S.A.W. alikataa yale yaliyopendekezwa na Abu Sufyani Ibn Harbu akitaka kusainiwa tena makubaliano na kuongeza muda ndipo Mtume S.A.W. akakataa hilo na Abu Sufyani akaondoka na kuelekea Makkah, Mtume S.A.W. bila ya kutangaza alimwandaa mtu kwa ajili ya ufunguzi huo mkubwa ambao Mwenyezi Mungu aliipa nguvu Dini yake Mtume wake askari wake na kukomboa Msikiti wake wa Makkah kutoka mikonnoi mwa makafiri na washirikina.
Katika swala zima la ufunguzi wa Mji wa Makkah kuna mafunzo na hukumu zenye faida katika siasa za ndani na nje, na ndani yake kuna mazingatio na mawaidha tunayakumbuka kila kipindi cha Ramadhani ambapo ufunguzi wa Makkah ulifanyika ndani ya kipindi hicho.
1- Kabla ya Mtume S.A.W. na Waislamu kuchukua hatua kwa kutumia jeshi lao ili waweze kuifungua Makkah Hatibu aliandika kitabu na kukituma Makkah akiwapa habari ya hilo Mwenyezi Mungu akamjulisha Mtume wake kuhusu kitabu hicho na Mtume S.A.W. moja kwa moja akamwambia Ally, Zubeir na Mikidad: ”Nendeni mpaka eneo la Rawdhat Khakh, kwani mahala hapo kuna mwanamke ana kitabu basi kichukuweni”, anasema: Tulikwenda mpaka tukafika eneo la Rawdhat tahamaki tukajikuta tupo kwa huyo mwanamke, tukamwambia: Toa kitabu, akasema: Sina kitabu, tukamwambia: Utatoa kitabu au tukitoe kwenye nguo – walikuwa wanakusudia kumtisha – yule mwanamke akakitoa kwenye nywele zake alizosuka kisha wakakileta kwa Mtume S.A.W. na kukuta ndani ya kitabu kuna maelezo ya Hatib Ibn Aby Baltaat akiwaambia washirikina wa Makkah na kuwapa habari kuhusu mambo ya Mtume S.A.W., Mtume akauliza: ”Ewe Hatib ni nini hii? ” Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, usifanye haraka kwani mimi nilikuwa mtu mwenye mafungamano na Makuraish – sio muungano nao – na wala sikuwa katika hilo, na walikuwa miongoni mwa ulionao katika Waislamu waliohamia Madinah ”Muhajireen” na ukaribu nao wakiwalindia familia zao na mali zao basi na mimi nikapenda kwa sababu nina ndugu miongoni mwao ili nipate na mimi ulinzi wa familia yangu na wala sikufanya hivyo kwa lengo la kuritadi kwa maana ya kuacha Dini yangu wala kuridhia ukafiri baada ya Uislamu. Mtume S.A.W. akasema:”Ama hakika amewaambia ukweli” ndipo Omar akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ebu niachie mimi huyu nimkate shingo huyu ni mnafiki. Mtume S.A.W. akasema:”Hakika ni mtu aliyeshiriki vita vya Badri, ni kitu gani kitakujulisha huenda Mwenyezi Mungu amewatambua watu walioshiriki vita vya Badri!! Akasema: Fanyeni mnachotaka kwani mmesamehewa dhambi zenu” Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha Aya: {Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwishaikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi zangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayodhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi ameipotea njia ya S.A.W.} ( ).
2- Angalia namna gani Mtume S.A.W. alivyoshughulikia makosa ya ndani, pamoja na kuwa kitendo alichofanya Hatibu ni katika makosa makubwa lakini hata hivyo Mtume alichunga haiba ya mtu na kuangalia hali iliyopo pamoja na sehemu, na ametufundisha kuwa kuhukumu moja kwa moja haiji na kheri na siasa ni kuchunga mambo ya umma ndani na nje, tunapaswa kuwa na nia safi kwa Mwenyezi Mungu na kufahamu hali halisi pamoja na kuyaendea masilahi na kufikia makusudio, jambo hili sio linahusika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu tu kwani Yeye ni mwalimu kwa wale waliokuja baada yake na kuendelea mpaka siku ya malipo, bali ni lenye kubakia kwa muda wote wa kuwepo kwa dunia.
3- Mtume S.A.W. alipeleka wajumbe kwa watu wanaomzunguka miongoni mwa watu wa makabila ya Waarabu, miongoni mwao wapo aliokutana nao Madinah na wengine alikutana nao njiani na kutangulia Madinah akiwemo Ibn Ummu Maktoum, siku ya jumatano alitoka kwa siku mbili ndani ya mwezi wa Ramadhani, na inasemwa kuwa ni siku kumi wengine wanasema ni zaidi ya siku kumi alitoka baada ya Swala ya Al-Asri ndani ya mwaka wa nane wa Hijria, Waislamu wakati huo walikuwa kiasi cha elfu kumi na ikasemwa walikuwa elfu kumi na mbili, Abbasi alikuwa ametoka nyumbani kwake kwa watu wake na familia akiwa ni Muislamu mwenye kuhama ndipo alipokutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu katika eneo la Juhfah kabla ya hapo alikuwa anaishi Makkah akifanya kazi zake za kutoa huduma za ugawaji maji hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa amemridhia.
Miongoni mwa aliokutana nao njiani akiwa ni pamoja na Abu Sufian Ibn Harith mtoto wa baba yake mdogo Mtume S.W.A na ndugu yake wa kunyonya kwa Mama Halima Saadiyah akiwa na mtoto wake Jafar, Abu Sufiani alikuwa ameishi na kumzoea Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. lakini baada ya kupewa Utume alikuwa adui kwake na kutokuwa na uhusiano naye mwema, na kukutana kwao na Mtume S.A.W. kulikuwa eneo la Abwaa na walisilimu kabla ya Mtume S.A.W. kuingia Makkah kisha alikwenda mpaka alipofika eneo la Qudaid alifunga bendera na kwenda nayo kwa watu wa makabila la Kiarabu kisha akafika Dhaharani nyakati za usiku, akawataka maswahaba zake wawashe vizinga vya moto elfu kumi hivyo Makuraishi hawakukaribia msafara na Waislamu wakitumia nafasi kwa yale waliyokuwa Makuraishi wanaogopa ikiwa ni pamoja na kuwapiga vita Waislamu.
Wakamtuma Aba Sufian Ibn Harbi na wakamwambia: Ikiwa utakutana na Muhammad basi tufanyie makubaliano naye, ndipo alipotoka Abu Sufiani na Hakim Ibn Hizaam pamoja na Badil Ibn Warqaa mpaka wakafika Dhaharan, pindi walipoona kambi ya Waislamu ikawafadhaisha kwani waliwaona walinzi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakafahamika na kuchukuliwa mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. Abu Sufiani ndipo aliposilimu, pindi alipotoka Mtume alimwambia Abbas: Mzuie Abu Sufiani kule juu ya mlima ili apate kuwaona Waislamu Abbas akafanya hivyo, ikawa watu wa makabila ya Waarabu wanapita na Mtume vikundi vikundi mbele ya Abi Sufiani, ndipo Abu Sufiani akamuuliza Abbas ni nani hawa? Akamwambia hawa ni watu wa kabila la Ghaffar, kisha wakapita watu wa kabila la Juhainah akauliza kama alivyouliza mara ya kwanza mpaka likapita kundi kubwa zaidi ya yaliyopita akauliza ni nani hawa? Akaambiwa hawa ni Ansaar watu wa Madinah akiwemo Saad Ibn Ibaadah akiwa amebeba bendera, Saad akaita: Ewe Abu Sufian, leo ni siku ya vita vikali leo inakombolewa Kaabah, na katika maelezo mengine ni ukombozi wa Msikiti wa Makkah maneno haya yalisikiwa na mmoja wa wahamiaji waliotoka Makkah akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Makuraishi hawatokuwa na amani ikiwa Saad atakuwa na ushawishi. Mtume S.A.W. akamwambia Ali: Mfuate Saad na chukuwa bendera na wewe ongoza kundi. Imepokelewa kuwa Abu Sufiani alimuuliza Mtume S.A.W. pindi alipomfuata: Je umeamrisha kuuliwa watu wako? Mtume akamwambia: Hapana, akamuelezea yale aliyoyasema Saad Ibn Ibaadah, na kumwambia: “Ewe Abu Sufian leo ni siku ya mapigano makali ni siku Mwenyezi Mungu anawashinda nguvu Makuraish”. Akamtuma kwenda kwa Saad na kuchukua bendera na kumpa mtoto wake Qaid ( ).
Katika kisa hiki kuna masomo katika medani za siasa ambayo hayana idadi kutokana na siri ya nguvu ya kutishia ambayo inapelekea kutomwagika damu na kuwa malipo kwa mwenye kutaka kumwagika damu hata kwa nia njema na kukabidhi bendera kwa mtoto wa Abu Sufian Qais, jambo hili sio wivu au chuki isipokuwa ni kuheshimu mabalozi na busara ya mazungumzo na kuridhia mpango wa uongovu kutokana na adui.
1- Amesema Musa Ibn Aqabah: Mtume S.A.W. alimpeleka Zubeir Ibn al-Awwaam kwa wahamiaji na kumuamrisha kuingia maeneo ya juu ya Makkah na kumuamrisha pia kuisimika bendera kwenye mti wake na wala asiondoke mpaka Mtume afike. Na alimtuma Khalid Ibn Walid kwenye kwa watu wa makabila ya Qadhaat Salim na mengine, na kumuamrisha kuingia Makkaha kwa maeneo ya chini ya Mji na kuisimika bendera kwenye nyumba ya chini kabisa, akamtuma Saad Ibn Ibaadah kwenda kwa watu wa Ansaar watu wa Madina wakiongozwa na Mtume S.A.W. na kuwataka kukunja mikono yao bila kumpiga yeyote isipokuwa yule atakaye wapiga, Khalid Ibn Walid aliingia eneo la chini la Makkah na kukutawamekusanyika huko watu wa kabila la Banu Bakri na watu wa kabila Banu Haarith Ibn Abdulmanaaf na watu wa Huzail na Wahabeshi ambao Maquraish walishinda dhidi yao walimpiga Khalid wakashambuliwa na kushindwa vita, na waliuwawa watu wa kabila la Bani Bakri kiasi cha wapiganaji ishirini na wa kabila la Huzeil walikufa watatu au wanne mpaka ikamalizika kwao vita ndipo Mtume S.A.W. alipouangalia mkusanyiko wa Waislamu na akasema: “Ni nini hii na nimekataza kupigana vita” wakasema: Hakika Khalid alipigwa na kuanza mapigano na ilikuwa ni lazima kwa Khalid kupigana nao, Mtume S.A.W. akasema baada ya kumjulia hali Khalid: “Kwa nini umepigana hali ya kuwa nimekukataza kupigana?” akasema Khalid: Wao ndio walianza mapigano na nilizuia mkono wangu kadri nilivyoweza. Akasema Mtume S.A.W.: “Maamuzi ya Mwenyezi Mungu kheri” ( ).
Akasema Abbas baada ya kusilimu kwa Abu Sufiani na kutoa shahada ya kweli: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Abu Sufiani ni mtu anayependa fahari basi mfanyie kitu. Akasema: “Ndio” akaamrisha na kuita mwenye kuita: Mwenye kuingia Msikitini huyo atakuwa ameamini, mwenye kuingia nyumba ya Abi Sufiani naye atakuwa ameami na mwenye kuufunga mlango wake basi na yeye atakuwa ameamini ( ).
Katika yote hayo unaona ulinzi wa kisharia, na ujinga kwa mjinga na uadui kutoka kwa mwenye uadui ni sababu ya balaa, na ndani yake ni kuwaweka watu kwenye nafasi zao na kushauriana nao katika mambo.
2- Imepokelewa kuwa Mtume S.A.W. aliinamisha kichwa chake ikiwa ni unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kumkirimu ufunguzi wa Mji wa Makkah, mpaka kichwa chake kilikaribia kugusa mnyama wake ikiwa ni kumshukuru Mwenyezi Mungu na kunyenyekea ukubwa wake Mola kwa kumhalalishia mji wake na wala hajawahi kumhalalishia yeyote kabla yake wala yeyote baada yake, Hadithi inayotokana na Anas Mtume S.A.W. aliingia Mji wa Makkah siku ya ufunguzi kichwani kwake akiwa amevaa kitu kama kofia.
Kutoka kwa Jabir amesema kuwa Mtume kichwani kwake alikuwa amevaa kilemba cheusi, ilipofika siku ya pili ya siku ya ufunguzi wa Mji wa Makkah Mtume S.A.W. alisimama mbele ya watu na kutoa hotuba kwa kuanza na kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu pamoja na kumtukuza kwa sifa alizonazo kisha akasema: “Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameutukuza mji wa Makkah tokea pale alipoumba mbingu na ardhi, nao ni mji mtukufu kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu mpaka siku ya kiyama, hivyo si halali kwa mtu yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kuamini siku ya kiyama kumwaga damu au kuangusha mti, ikiwa kuna mtu amepewa ruhusa ya kupigana na Mtume ndani ya Makkah basi semeni: Hakika Mwenyezi Mungu amempa ruhusa Mtume wake lakini hamkuruhusiwa nyinyi, nimehalalishiwa wakati wa mchana na leo umerudi utukufu wake kama vile utukufu wa jana basi aliyopo amfikishiea asiyekuwepo”. Kisha akasema: “Enyi Makuraishi, mnaona ni kitu gani nitawafanya. Wakasema: Ni jambo zuri ndugu mwema na mtoto wa ndugu mwema. Akasema Mtume: Nendeni kwani mpo huru” ( ) kwa maana wameachwa huru na wala hawajafanywa watumwa wala mateka, pindi Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoifungua Makkah kwa Mtume wake S.A.W. watu wa Madinah waliongea wenyewe kwa wenyewe: “Je mnaona Mtume S.A.W. baada ya Mwenyezi Mungu kumfungulia ardhi ya mji wake na mji wake atauimarisha?” na Mtume S.A.W. alikuwa akiomba dua juu ya eneo la Safa akiwa ameinua mikono yake baada ya kumaliza maombi yake akauliza “Mmeongea nini?” wakasema hapana hakuna kitu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakuacha kuwauliza mpaka wakamwambia walichokuwa wanaongea, ndipo Mtume S.A.W. akasema: “Hapana maisha yangu ndio maisha yenu mwisho wangu ndio mwisho wenu” ( ).
Fadhalah Ibn Umeir Ibn Al-Mulawwih, aliamua kutaka kumuua Mtume S.A.W. akiwa Mtume anatufu Kaabah pindi alimposogelea Mtume akamwita: Fadhalah? Akajibu ndio ewe Mtume wa Mwenyzi Mungu. Mtume akamuuliza: Ulikuwa unaongea nini peke yako? Akajibu: Hapana hakuna kitu chochote bali nilikuwa namtaja Mwenyezi Mungu, Mtume S.A.W. akacheka, kisha akamwambia: Muombe msamaha Mwenyezi Mungu. Kisha Mtume akaweka mkono wake kwenye kifua cha Fadhalah na moyo wake ukatulia na Fadhalah akawa anasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu Mtume hakuweka mkono wake kwenye kifua changu mpaka Mwenyezi Mungu akatengeneza kitu ninachokipenda zaidi. ( ).
Angalia maana ya msamaha na uvumilivu kwa watu na muujiza wake kwa huyu Fadhalah kuna mazingatio na mawaidha.
3- Kutoka kwa Ibn Omar R.A amesema: Mtume aliupokea mwaka wa kufunguliwa kwa Mji wa Makkha akiwa kwenye ngamia wake akiwa na Osama mpaka walipofika kwenye Kaabah kisha Mtume akamwita Othman Ibn Twalhah na akamwambia: “Niletee ufunguo” akaenda kwa mama yake kuchukua funguo lakini mama akakataa kumpa. Akasema kumwambia mama yake: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu utanipa hiyo funguo au nikutolee huu upanga mgongoni kwangu” mama akatoa funguo na akaja nayo kwa Mtume kisha akafungua mlango ( ).
Katika kitabu cha “Twabakat” cha Ibn Saad kutoka kwa Othman Ibn Twalhah amesema: Tulikuwa tunafungua Kaabah katika zama za ujinga siku za jumatatu na alhamisi siku moja alikutana na Mtume S.A.W. akiwa anataka kuingia ndani ya Kaabah pamoja na watu wengine basi nikachukia na kumzuia basi Mtume akaniota kisha akasema: “Ewe Othmani, huenda siku moja utaona ufunguo huu upo mikononi mwangu ninauweka ninapotaka” nikasema: Makuraishi wakati huo watakuwa wameangamia na kudhalilika. Akasema: “Bali watakuwa wamejenga na kuwa na nguvu wakati huo” akaingia Kaaba na nikakutana na neno lake kwangu sehemu ambayo niliona siku hiyo kuwa mambo yatakuwa vile alivyosema, pindi ilipokuwa siku ya ufunguzi akasema: “Ewe Othman, niletee funguo”, nikamletea, na akauchukuwa kwangu kisha akanipa na kusema: “Uchukueni muwe nao siku zote hakuna wakuwavua hiyo funguo isipokuwa ni mtu dhalimu, Ewe Othman, hakika Mwenyezi Mungu amekupeni kazi ya ulinzi wa nyumba yake hivyo kuleni kwa uzuri vile vinavyowafikia kwenye nyumba hii”. Akasema: Pindi nilipompa mgongo kuondoka akaniita na nikaenda kisha akasema: “Je halijakuwa lile nililokwambia” anasema: Nikakumbuka kauli yake Makkah kabla ya kuhama aliyosema: “Huenda siku moja utaona ufunguo huu ukiwa mkononi mwangu ninauweka sehemu niitakayo” nikasema: Ndio, ninashuhudia kuwa Wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ( ) kwa Othmani huyu iliteremka Aya katika surat An-Nisaa: {Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu muhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayokuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona} ( ).
Imepokelewa kuwa aliingia Omar na Osama Ibn Zeyd pamoja na Bilali na Othman Ibn Twalhah ndani ya Kaaba na kufungiwa mlango, amesema Ibn Omar: Pindi walipofungiwa mimi nilikuwa wa kwanza nikakutana na Bilali nikamuuliza je Mtume S.A.W. aliswali, akasema: Ndio kati ya nguzo mbili za kulia nikaendelea kumuuliza aliswali swala ngapi ( ) katika moja ya mapokezi ya Imamu Bukhary: Nguzo moja ilikuwa kushoto kwake na nguzo ya pili ilikuwa kuliani kwake na nguzo tatu zilikuwa nyuma yake ( ) katika kitabu cha Makkah cha Azraqy na Faaqihy: Ni kuwa Muawiyah alimuuliza Ibn Omar: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliswali wapi? Akajibu: Umbali kiasi cha dhiraa mbili kabla ya ukuta au dhiraa tatu, kwa maelezo haya inapaswa kwa mwenye kutaka kufuata hili kuswali kwa umbali wa dhiraa tatu kati yake na ukuta kwani inawezekana nyayo zake zikakanyaga sehemu ambayo aliyokaja Mtume S.A.W. S.A.W.a ikiwa dhiraa tatu, au kukutana magoti yake au mikono yake au uso wake ikiwa chini ya dhiraa tatu. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua zaidi( ). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si muhitaji kwa walimwengu} ( ).
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: Kitabu cha Simaat al-Asri cha Fadhilatuh Mufti wa Misri Dr. Ally Juma.

 

Share this:

Related Fatwas