Mtu wa Kuzingatiwa.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtu wa Kuzingatiwa.

Question

Kwenye vitabu vya Fiqhi ya kisasa kumekuwa na msamiati “Mtu wa kuzingatiwa”, ni nini makusudio ya msamiati huu, na je kuna tofauti kati yake na msamiati wa “Mtu halisi?” 

Answer

Shukrani za Mwenyezi Mungu, sala na salamu zimwendee Mtume wa mwisho Muhammad S.A.W. pamoja na jamaa zake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho, na baada ya hayo:
Mifumo ya kisheria ya kisasa imekubali kile kinachoitwa “Mtu wa kuzingatiwa” na huelezewa pia kuwa ni “Mtu kihukumu” au “Mtu kimaana” au “Mtu wa kukadiriwa” mifumo hiyo imeweka hukumu inayobainisha kuhusu hukumu za mtu halisi, pamoja na msamiati huo kuwa mpya, “Mtu wa kuzingatiwa” kwa upande wa kuitwa jina hilo halizingatiwi kuwa ni geni kwenye urithi wa kifiqih na upande wa kinadharia, bali kuitwa huko kuna dalili zake zinatokana na Fiqhi ya Kiislamu kwa namna moja au nyingine kama itakavyoelezwa, kumeanza kuonekana umuhimu wa aina hii ya mtu mpaka imekuwa mtu wa kuzingatiwa ni ukweli halisi ndani ya sheria za nchi za Kiarabu na Kiislamu, sheria ya Misri imelichukua jina hilo na kuliainisha pamoja na kubainisha uhalali wake na haki zinazotokana katika kifungu nambari 52, 53 vya sheria ya kiraia nambari 131 ya mwaka 1948.
Nadharia ya msamiati wa “Mtu wa kuzingatiwa hatuzingatii maana ya kilugha ya tamko la mtu pamoja na kuwa mtu katika lugha inakuja kwa maana ya kuainisha na kudhihirika, huitwa haiba ya mwanadamu, kwa maana ya mtazamo wake unaoonekana kwa mtazamaji kwa mbali, au mtu kuelekea kwa fulani, maana yake kuonekana na kubainika uwepo wake, na huitwa: Jicho lililotulia, kwa maana: Limethibiti bila kucheza, angalia, [Lisaanu Al-Arab cha Ibn Mandhur, 7/45 chapa ya Dar Sadir], mtu wa kuzingatiwa: “Ni mjumuiko wa watu na mali zinaimarisha chombo huru kinalenga kufikia lengo maalumu na kuwa na haki ya sheria katika mipaka ya lengo hili”.
Kusudio la chombo huru ni kukadiriwa kwa mtu wa kuzingatiwa uwepo wake huru mbali na watu halisi wanaotengeneza mtu wa kuzingatiwa, na uwepo huu unakuwa na uhai wa kisheria ambapo anakuwa na uwezo wa kuingia makubaliano na watu wengine ambao ni watu halisi na wale wa kisheria, kwa maana: Uhalali wake wa kuwa na haki na wajibu.
Ama mtu halisi: Ni binadamu ambaye anakuwa na haki za kisheria kwa kuzaliwa kwake tu, na wakati mwingine huitwa mtu asili kuwa ni mtu wa kisheria, kwa sababu asili ni kuwa mtu wa kisheria hathibiti isipokuwa kwa mtu asili, isipokuwa mtu wa kisheria kwa nadharia yake ya kimsamiati anakusanya aina zote mbili kuanzia mtu wa kuzingatiwa na yule mtu halisi, imesemwa kwenye nadharia yake: Ni kila aliyopo anazingatiwa na sheria kuwa ni mwenye haki na wajibu, na kusudio la kila aliyopo linakusanya na kujumuisha mwanadamu na asiyekuwa mwanadamu katika vilivyopo, kila kilichopo hakizingatiwi na sheria kuwa ni chenye haki na wajibu hazingatiwi ni mtu hata kama atakuwa ni mwanadamu, na kubainisha mtu halisi na mtu wa sharia na watu kwa ujumla na watu maalumu, yanafaa maneno haya kuyaelezea tofauti iliyopo kati yake, vilevile msingi ambao unaomsimamisha mtu wa kuzingatiwa na ushahidi wake katika urithi wa kifiqih, lakini kabla ya hilo inapaswa kusema: Tofauti ya Fiqih ya kisasa kuhusu mtu kwa kuzingatiwa kwa upande wa kukubali au kukataa ni jambo lisilo na uzito mkubwa katika nchi zetu au zinginezo ambazo sheria zake zimemtambua huyu mtu kwa kuzingatiwa na kuweka mfumo wa kushirikiana naye, inafahamika kuwa pindi kunapokuwa na tofouti ya kitu kati ya uhalali wake na uharamu wake, na kufikishwa jambo kwa hakimu basi hakimu anapaswa kutoa Fatwa sawa na vile anavyoamini yeye, na hukumu yake inaondoa tofauti, mtunzi wa sheria wa Kimisri alionesha mtazamo wake kwa huyu mtu kwa kuzingitiwa kwa kufaa na kuondoa tofauti.
Uwiano kati ya mtu halisi na wa kuzingatiwa unazalisha tofauti nyingi za wazi:
Miongoni mwake: Sifa na jina, kwani mtu wa kuzingatiwa anao uwepo wa kisheria, kwa maana kimakadirio na kimazingatio na wala sio uwepo wa kuhisika, ama mtu halisi ni mwenye uwepo wa kuonekana na kuhisika, kama vile mtu wa kuzingatiwa anafahamika kwa pande mbalimbali ambapo inawezekana kuwepo kwa zaidi ya sehemu moja ndani ya wakati mmoja kwa pande zake tofauti, na kuthibiti kwake kwa zaidi ya sifa moja kama vile kuwa muuzaji na mnunuzi wakili na kaimu kwa mwingine na yasiyokuwa hayo miongoni mwa migawanyiko tofauti, na miongoni mwa anayosifika nayo mtu wa kuzingatiwa ni kuwa hana nafsi yenye kutamka, hivyo hawezi kubeba yale anayobeba mtu halisi ambaye kwa asili yake ya kibinadamu anakuwa na baadhi ya sifa za mwanadamu kama vile sifa ya ushujaa ukarimu na zisizokuwa hizo miongoni mwa tabia na maadili mema, na huenda miongoni mwa mifano ya wazi ya hilo ni masuala ya usimamizi na dhamana, ambapo wanachuoni wa Sharia wamekubaliana kutoka madhehebu manne ya kutofaa kuchukua malipo kwenye ulezi, kwa sababu ulezi ni miongoni mwa mambo ya kumuondolea tatizo mtu wa karibu, hivyo kuchukua malipo kwake ni jambo lisilokubaliana na kuwa kwake makubaliano ya kujitolea, ni kama kwamba maana ya hilo ni kuwa sheria inalea kwa mtu Muislamu maana ya kujitoa muhanga, na hilo linapaswa kutokuwa na malipo ya kifedha au kitu chochote, lakini hilo lipo tofauti ikiwa tunashirikiana mtu wa kuzingatiwa, kwa mfano benki – nayo ni moja ya mtu wa kuzingatiwa – wakati wa kusimamia kwake mmoja wa wateja wake kama inavyofahamika kwa jina la “waraka wa dhamana” wala hazingatii suala la kulea kujitoa muhanga isipokuwa inachukua malipo kwenye hilo, kwa sababu mtu wa kuzingatiwa anafanya kazi zake kwa malipo, kuchukulia mtu wa kuzingatiwa kutoa huduma zake pasi na malipo kwa kuitikia wito wa murua na ukaribu ikilinganishwa na mtu halisi kwanza kabisa hubebesha gharama na kumtia mtu kwenye gharama, na kanuni ya kifiqih inasema: Ngawira kwa gharama.
Tofauti nyngine: Kufuata, kwani mtu wa kuzingatiwa uwepo wake ni wa kufuata, kwa maana anakuwa siku zote ni mwenye kufuata kwa uwepo wa mkusanyiko wa watu halisi au mali, ama mtu halisi uwepo wake unajitegemea wenyewe katika uhalisia na kuzingatiwa.
Pia tofauti: Haki na wajibu, kwani si kila kilichothibiti kwa mtu halisi kinathibiti kwa mtu wa kuzingatiwa, kama vile hali ya kuoa kuacha hukumu za mirathi na mfano wa hayo miongoni mwa yanayozingatiwa ni katika sifa za lazima kwa mwanadamu kama ilivyoelezewa kwenye kifungu nambari 53 cha sheria ya kiraia, kama vile mtu wa kuzingatiwa hawajibiki kutekeleza huduma za kiaskari wala kuwa na haki za kisiasa, wala haitekelezwi kwake adhabu za kimwili, kama vile kuchapwa viboko kupigwa mawe na kukatwa mkono, isipokuwa hutekelezwa kwake adhabu za kiraia na kiidara, kutokana na matokeo hayo: Ni kuwa haiwezekani kutekelezwa hukumu ya kufungwa jela katika kuteleza yale anayostahiki kutekeleza kama vile madeni bali huzuiliwa tu.
Tofauti nyingine pia: Mtu wa kisheria huthibiti kwa mtu halisi kwa kule kuzaliwa kwake tu kama ilivyoelezewa hapo nyuma, tofauti na mtu wa kuzingatiwa ambaye inategemea kupewa kwake sifa ya mtu wa kisheria ni baada ya kutambulika na sheria.
Miongoni mwa tofauti hizo: Harakati, ambapo harakati za mtu halisi si harakati maalumu, bali ni mwenye uhuru kamili pindipo tu hatokwenda kinyume na mfumo mkuu au sheria, tofauti na mtu wa kuzingatiwa ambapo sheria ya Misri inasema kuwa harakati zake zimefungwa kutokana na sababu ya kuanzishwa kwake, kama vile miongoni mwa sifa kubwa za mtu wa kuzingatiwa, anazingatiwa ni katika sababu za kuanzishwa kwa utu wake: Ni endelevu, kwani kuendelea kwa mtu halisi kunaambatanishwa na kifo chake, kila mwanadamu ana muda wa kuishi, wakati ambapo mtu wa kuzingatiwa pamoja na kuwepo kwake kisheria kunaishia kwa kuharibika au kufungwa mwisho wa wakati, isipokuwa anasifa ya kudumu wala haathiriki vibaya kwa kifo cha mmoja wa wajumbe wake au kujitoa, bali inawezekana kuendelea kuishi kwa vizazi kadhaa bila ya kwisha, naye kwa sifa hiyo anatofautiana na watu walioanzisha na anaendelea kuwepo kwake hata kama watakufa hawa waanzilishi, bali sifa pia ya watu wa kuzingatiwa wanasifika – sawa na asili yao – kuunga mkono mfano wa nchi na asasi zake, na sifa hii ambayo anasifika nayo mtu wa kuzingatiwa miongoni mwa kazi zake ni kutoa ulinzi toshelezi kwa wale anaoshirikiana nao.
Tofauti kati ya watu hawa wawili – wa kuzingatiwa na kawaida – inaonekana wazi kwenye masilahi ambayo yanafikiwa na kila mmoja, kwa kuongezea na sifa ya kuendelea hivyo masilahi ya mtu halisi ni masilahi binafsi, tofauti na mtu wa kuzingatiwa ambapo masilahi ya kuanzishwa kwake yanarejea kwa waanzilishi wake au wale wenye kunufaika, kama vile mtu wa kuzingatiwa anafikia masilahi mengine ambayo mtu halisi anashindwa kuyafikia, miongoni mwa masilahi yasiyofikiwa na mtu binafsi ima kwa uhitaji wake wa mali nyingi au juhudi zaidi ya mtu binafsi, kwa kuongezea hayo: Ni kuwa fikra ya mtu wa kuzingatiwa ni yenye athari kwenye mabadiliko ya Fatwa, kwani mtu halisi ni moja ya pande nne za Fatwa ambazo hubadilika kwa kubadilika kwake, nayo ni: Muda sehemu na hali za watu, miongoni mwa mfano wa kubadilika kwa Fatwa kwa kutofautiana na mtu ni kuwa sehemu ya Fatwa kuwepo kwa mtu halisi au mtu wa kuzingatiwa, kwa mfano: Baadhi ya miamala ya kifedha wakati mwingine inakuwa haifai kufanyika na mtu asili au mtu halisi na inafaa kusema inafaa miamala hiyo kwa mtu wa kuzingatiwa kama vile uuzaji wa faida kwa mteja, ni kuuza kwa faida pamoja na kununua ambapo kunakamilika kwa mteja kuipelekea ombi benki kuitaka kununua bidhaa inayohitajika kwa sifa ambayo ameianisha mteja mwenyewe kwa mujibu wa makubaliano na benki kununua hiyo bidhaa ni faida ya asilimia ambayo wanakubaliana asilimia hiyo na mteja kufanya malipo kwa awamu, nayo ni katika makubaliano ya kibiashara mapya na pia huzingatiwa ni katika makubaliano ya kifedha, wanaosema inafaa miamala hii wameweka sharti la kutokuwa muwakilishi wa taasisi katika kununua ndiyo mteja wa kununua, sharti hili linaendana na kukubaliana na mtu halisi na wala sio mtu wa kuzingatiwa kutokana na kumiliki sifa zinazombadilisha na kuwa ni mteja mwenye kutoa amri ya kununua, na wakati huo huo anakuwa mjumbe kwa upande mwingine ambao ni taasisi, mfano mwingine: Zaka ya mashirika ya hisa, pamoja na kuwa masuala ndani yake kuna mitazamo minne lakini hakuna sababu ya kufafanua isipokuwa haikuangalia masuala ya mtu wa kuzingatiwa kwenye shirika, ambapo miongoni mwa masharti ya kuwajibika Zaka ni kukamilika kwa umiliki, na shirika – ni mtu wa kuzingatiwa – ni lenye kumilikiwa na wenye hisa, kila mmiliki wa hisa ni mmiliki mpungufu asiyekamilika, na hilo linapelekea kuwa hakuna zaka kwenye shirika.
Masuala haya kwa sifa yake yanahitaji jitihada za pamoja mpaka tufikie hukumu ya kisharia iliyosahihi hasa ikizingatiwa kumekuwa na mivutano ya pande mbalimbali, inaongezwa kwenye mifano hii miwili: Kuwa wanachuoni wamethibitisha baadhi ya hukumu za mtu wa kuzingatiwa isiyothibiti kwa mtu halisi, kama vile kutokuwepo zaka ya Misikiti au majumba ya elimu na mfano wake, na kama vile kutokatwa mkono mwizi anapoiba kwenye hazina ya taifa, anasema Sheikh Zakariya Al-Ansariy katika: [Sharhu ya kitabu cha Al-Bahja 2/158 chapa ya kituo cha uchapishaji cha Al-Maimaniya]: “Hakuna Zaka ya mali kwenye mali ya hazina ya taifa, na Zaka ya mali za Misikiti na vituo vya elimu”, na anasema Al-Khatwib Sharbiniy kwenye kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj, 2/82 chapa ya Dar Al-Fikr]: “Matunda ya kwenye bustani na mali ya kijiji iliyowekewa wakfu Misikitini hazipaswi kulipiwa Zaka kwa kauli sahihi kwa sababu mali hizo hazina mmiliki maalumu”, katika kitabu cha: [Al-Insaf cha Mardawy 3/15 chapa ya Dar Ihyaau turaath Al-Arabiy]: “Ikiwa inazalisha au kutozalisha ikiwa ni wakfu si kwa mtu maalumu au kwa Misikiti na shule pamoja na madrasa na mfano wake hakuna Zaka, na hii ni kauli ya madhehebu”, na amesema Ibn Al-Himam katika kitabu cha: [Fat-h Al-Qadeer, 5/376, chapa ya Dar Al-Fikr]: “Hakatwi mkono mwizi kwenye mali ya uma, pia amesema hayo Imamu Shafiy na Ahmad pamoja na Nakhiy na Shaabiy, kwa sababu ni mali ya uma na yeye ni miongoni mwao…pia amesema Omar na Aliy mfano wa hivyo”, amesema Ibn Qudamah katika kitabu cha: [Al-Mughniy, 9/101, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Ikiwa utaibwa mlango wa Msikiti au mlango wa Kaaba au kikaibwa kitu kwenye dali ya kaaba basi kuna mitazamo miwili…..mtazamo wa pili: Hakatwi mkono, nayo ni kauli ya watu wa mitazamo, kwa sababu hakuna mmiliki wake katika viumbe, hivyo hakatwi mkono, kama vile taa ya Msikitini, huwa hakatwi mkono kwa kuiba kama vile kuiba kwenye mali ya uma”. Kauli ya kutokuwepo Zaka kwenye upande huu wa uma ambao ni sifa ya mtu wa kuzingatiwa na kutokatwa mkono kwa mwizi kwenye mali hizo ina maana tofauti hukumu hii na ile kama ingekuwa ni watu halisi.
Miongoni mwa masuala ambayo yanatofauti ya hukumu ndani yake kwa mtu halisi na mtu wa kuzingatiwa ni pamoja na masharti yaliyowekwa na wanachuoni katika makubaliano ya mudharaba ikiwa ni pamoja na sharti za kufikiwa kwa kukinga upotevu wa mali na ujinga, miongoni mwa sharti hizi: Iwe kwa kutumia sarafu iliyochapwa, na faida igaiwe baada ya mali kubadilika kutoka kuwa bidhaa na kuwa fedha, anasema Ibn Rushdi katika kitabu cha: [Bidayat Al-Mujtahid, 2/240 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Wala hakuna tofauti kuwa mwenye mtaji anachukua sehemu yake ya faida baada ya kutoa mtaji” wala halifikiwi sharti hilo isipokuwa kwa mtu halisi, kwa sababu mtu wa kuzingatiwa hawezi kuchunga sharti hili kwenye ushirika wa mudharaba, inafahamika kuwa muundo wa mudharaba kwenye mabenki ya Kiislamu hayachukui kwa tamko, hilo haliwezekani, kwa sababu zao la uwekezaji ikiwa faida au hasara haviji ndani ya wakati mmoja – kwa kuwepo mchanganyiko wa mara kwa mara na wenye kuingiliana – lakini huanzishwa matokeo hayo ndani ya kipindi cha uwekezaji, pia ikiwa haijakamilika utekelezaji wa uelewa wa tamko la hukumu basi matokeo ya uwekezaji ikiwa faida na hasara inathibitishwa tu wakati ambao umekamilika hesabu za mwaka za uwekezaji, na hilo hupelekea kuzuia watu wa hesabu washiriki katika uwekezaji na ambao wamejitoa moja kwa moja au sehemu kabla ya tarehe ya kufungwa hesabau katika faida au kuwapa hasara ambayo imetokana kabla ya tarehe ya kufunga hesabu na kabla ya kuondoa hesabu hizi.
Miongoni mwa hukumu ambazo zinatofautiana kati ya mtu halisi na yule wa kuzingatiwa – na hii ni kwa mjibu wa marejeo ya sheria – ni muda wa kimahakama, kwani kusikiliza madai kuhusu mtu halisi muda wake ni miaka kumi na tano, na kwa upande wa mtu wa kuzingatiwa ni miaka tisini, kifungu nambari 172, 180, 374, 388 vya sheria ya kiraia.
Sheria ya kiraia ya Misri imeainisha kwenye kifungu cha 52 mtu wa kuzingatiwa kwa vipengele kadhaa, kama ilivyobainisha yanayotokana na uwepo wake kwenye kifungu nambari 53 na kubainisha kuwa mtu wa kuzingatiwa anakuwa kama ifuatavyo:
Kwanza: Nchi, halimashauri Miji na vijiji kwa masharti ambayo yameainishwa na sheria, idara za uma ambazo sheria inazipa sifa ya mtu wa kuzingatiwa.
Pili: Makundi ya Kidini na Taasisi ambazo nchi inatambua kuwa ni watu wa kuzingatiwa.
Tatu: Wakfu na mashirika ya kibiashara na kiraia, vilevile Jumuiya na Taasisi, na mijumuiko yote ya watu na mali inayothibiti mazingatio ya mtu wa kuzingatiwa kwa mujibu ya tamko la kisheria.
Maelezo kuhusu aina hizi ambazo zimeainishwa na kifungu hiki ni kuwa uwepo wa mtu wa kuzingatiwa na kuanzishwa kwake kunategemea na kutambulika na sheria, ni sawa sawa kwa kuanzishwa sheria inayounda au kukamilika masharti ya kutambulika kisheria, na hili limetajwa na kifungu nambari 506 katika sheria za kiraia za Misri ambapo imekuja “Shirika kwa kuanzishwa kwake tu huzingatiwa ni mtu wa kuzingatiwa, lakini hajengewi hoja isipokuwa ni baada ya kukamilika hatua za kutangazwa ambazo zinatambulika na sheria”. Na kwa kuwepo mtu wa kuzingatiwa na kutengenezwa kwake na mtu halisi anakuwa na haki zote na kuwajibika na wajibu wote isipokuwa zile zinazolazimika kwa mtu halisi kama ilivyoelezewa, na hilo katika mipaka ambayo imepitishwa na sheria nayo ni kama:
1- Sehemu huru ambapo hunasibishwa na sehemu hiyo na kupewa utaifa, sheria imefasiri sehemu huru kuwa ni sehemu ambayo kunapatikana ndani yake makao makuu ya idara ya mtu wa kuzingatiwa.
2- Haki ya kimahakama, kwa maana haki ya kuwa mlalamikaji au mlalamikiwa, wala haiwi hiyo isipokuwa kwa kuvaana na mwakilishi katika kufikisha malalamiko au kuondoa malalamiko.
3- Nayo ni muhimu: Ni jukumu huru la kifedha tofauti na jukumu la waasisi wake, na yanayofungamana na hayo ni pamoja na kumpa mtu wa kuzingatiwa uhuru kamili wa kufikia yale yaliyoanzishwa kwa ajili yake, na kutorudi wenye kudai kwenye mali binafsi za waasisi ili kufahamu kati ya jukumu la waasisi na lile la mtu wa kuzingatiwa, na jukumu hili la fedha ambalo linathibiti kwa mtu wa kuzingatiwa ni zao la kutambulika kisheria kwa kuwa na uhalali wa wajibu, na ina maanisha uhalali wa wajibu ni uhalali wa mwanadamu kwa kuthibiti kwake haki na wajibu, kwa sababu aina hii ya uhalali wa jukumu kwa mujibu wa sheria ni umethibiti kwa mtu wa kuzingatiwa, hivyo kuthibiti jukumu la kifedha kwa mtu wa kuzingatiwa kwa sura hii ni kuthibiti uhalali wa wajibu, na hii pamoja na hilo – kwa maana ya jukumu la kifedha na uhalali wa wajibu – ni misingi miwili katika kumjenga mtu wa kuzingatiwa, kwani jukumu la kifedha kama ilivyoelezewa na jopo la wanachuoni wa Sharia: Ni sifa inakisiwa na kumfanya mwanadamu kuwa na uhalali wa kukubali na wajibu kwake, angalia: Kitabu cha: [Kashf Al-Asrar cha Alaa Deen Al-Bukhari, 4/238 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Islamia], na kitabu cha: [Al-Furuq cha Qirafiy, 3/231 chapa ya Aalam Al-Kutub], na jukumu la kifedha linaanza na mtu tokea pale anapoanza kulibeba na kubakia nalo kwa muba wote wa maisha yake, na wanachuoni wanasema litabakia baada ya kifo mpaka pale itakapofungwa haki inayofungamana na urithi, na hali hiyo basi inafaa kwa mtu aliyefariki kupata haki mpya baada ya kifo chake ikawa ndiyo sababu ya hiyo haki, kama vile mtu kupora nyavu za kuwindia na akamnasa mnyama basi mnyama huyo anakuwa ni miliki yake marehemu, rejea kitabu cha: [Al-Mausua Al-Fiqihiya, 21/277 chapa ya Wizara ya Waqfu ya nchini Kuweit], na ushahidi wa hilo:
Ni kuwa kuthibiti jukumu baada ya mtu kufariki mpaka kumalizwa haki zinazofungamana na urithi, na uhalali wa kupata haki mpya kwenye jukumu la kifedha baada ya kufariki mtu inakuwa ni kanuni inayofaa ya kuangaliwa mtu wa kuzingatiwa ambapo inathibiti kwake dhima hii ya kifedha au jukumu hili, na kukamilika mtazamo huu kwa matamko ya wanachuoni ambayo wanafahamu kukubalika kwa jukumu kuthibiti kwa asiyekuwa mwanadamu ni sawa sawa liwe la vitu kama vile vitu vya waqfu mali za hazina ya uma mali za Misikiti maeneo ya elimu kwa maana ya maeneo ya uma, au mkusanyiko wa watu na mali kama vile shirika, katika kitabu cha: [Al-Uqudul Durriyah cha Ibn Aabideen uk. 203 chapa ya Dar Al-Maarifah]: “Msimamizi wa Msikiti na Msikiti una mali za waqfu, msimamizi akaidhinisha malipo kwa mtunza Msikiti kwa kazi za kupangilia misala na malipo hayo ya mtunza Msikiti yakatokana na mali ya waqfu ya Msikini na akafanya hivyo, msimamizi akaacha kazi ya usimamizi kisha akaja msimamizi wa pili ambaye mpaka hivi sasa ndiyo msimamizi, na msimamizi wa kwanza hakuchukua malipo yoyote kwenye mali za waqfu za Msikiti kwa yule mtunza Msikiti, je msimamizi wa pili analazimika kufanya malipo ya mtunza Msikiti kwa sababu haki yake ipo kwenye ile mali ya waqfu ya Msikiti? Au analazimika yule msimamizi wa kwanza?
Jibu: Misimamizi wa pili anapaswa kufanya malipo ya mtunza Msikiti na kumlipa haki yake kwenye mali ya waqfu ya Msikiti, na wala msimamizi wa kwanza hawajibiki kufanya malipo hayo kwa sababu yeye ameondolewa usimamizi” ambapo maelezo haya yanaonesha ulazima wa kulipwa mtunza Msikiti katika mali ya waqfu.
Wanachuoni wamesema kuwa Msikiti unakuwa ni mshirika na unapata shufaa kwa maana ya kugawa sehemu mbili, anasema Al-Harshiy katika sharhu ya kitabu cha: [Mukhtasar Khalil 6/163 chapa ya Dar Swadir]: “Mtawala atachukua shufaa kwenye mali ya hazina” na anasema Sheikh Zakariya Al-Ansariy katika kitabu cha: [Asnaa Al-Matwalib 2/363 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Islamiyah]:
“Ikiwa Msikiti una sehemu ya ardhi ya pamoja – kwa maana inamilikiwa na Msikiti kwa kununua au kupewa zawadi ili iweze kutumika katika kazi za ujenzi za Msikiti kisha mshirika mwenza akauza – sehemu yake – basi mfanya tathmini anapaswa kufanya shufaa, kwa maana anachukua kwa hesabu ya shufaa ikiwa ataona kuna masilahi, kama vile ikiwa kwenye hazina ina mshirika kwenye kipande cha ardhi mwenza wake akauza sehemu yake basi Kiongozi anatakiwa kuchukua kwa namba ya shufaa ikiwa ataona kuna masilahi”.
Kama vile wamethibitisha wanachuoni umiliki wa msikiti, na kwa umiliki huu wamethibitisha kuwa msikiti una dhima ya mali, ambapo hawezi kumiliki kwa asiyekuwa na dhima ya mali, na wamethibitisha katika hali hii sawa na yanayokuwa kwa mwanadamu huru, anapaswa kumiliki kile kilichotolewa zawadi na kunufaika nacho, katika kitabu cha: [Asnaa Al-Matalib 2/470]:
“Imefanywa sehemu ya Msikiti au makaburi maeneo yote hayo yanamilikiwa kama vile na mtu huru”, kama vile kumkomboa mtumwa na kumwacha huru na mtumwa anakuwa ni mtu mwenye uhuru kamili na kuwa na jukumu huru au dhima huru ya mali, vilevile kuitoa mali toka kwa mmiliki wake na kuifanya mali ya Msikiti na kuwa na jukumu la mali.
Anasema Shamsdiin Ramly alipozungumzia kazi za msimamizi wa mali za waqfu: “Kazi yake kuu ni kulinda mali na kusimamia kwenye shughuri zingine kama usimamizi wa watoto yatima kusimamia malipo ya kodi na malipo ya nyumba, vile kukopesha mali ya waqfu pale kunapokuwa na haja ya hilo” kitabu cha: [Nihaayatul muhtaaj 5/399, 400 chapa ya Dar Al-Fikr], na akasema pia katika kitabu cha wasia 6/47, 48: “Nyumba inakuwa ya Msikiti pamoja na shule au madrasa hata kama itakua imetolewa na kafiri au kufanya matengenezo, kwa sababu jambo hilo linapelekea ukaribu zaidi na maelewano, vilevile ikiwa atasema nimeusia iwe ni mali ya Msikiti, na akataka kumilikiwa na Msikiti hivyo wasia huo utafanyiwa kazi kwenye nyumba na masilahi yake na kutumia msimamizi kwa mambo muhimu na yenye masilahi kwa jitihada zake”, na katika kitabu cha: [Al-Furuu cha Ibn Muflih 4/600 chapa ya Aalam Al-Kutub]:
“Msimamizi anaweza kukopesha pasina ruhusa ya kiongozi kwa jambo lenye masilahi” na anasema Ibn Jaziy katika kitabu cha: [Kawanuun Al-Fiqhiya, uk. 273, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Ama kilichofungiwa: Kinaweza kuwa ni binadamu au sio binadamu, kama vile Msikiti na shule, maandiko haya yanaonesha juu ya kufaa kukopa mali ya waqfu, na wasia kwa ajili ya Msikiti na kutoa waqfu, wala haliwi hilo isipokuwa itakapokuwa mali ya waqfu Msikiti kuwa na dhima ya kifedha.
Kufaa kwa baadhi ya matumizi yanayofuangamana na tuliyotaja, kama vile usia ushirika na kukopa, pia kuthibiti kwa umiliki na shufaa, ni dalili ya wanachuoni ya kukopa kwa mali za waqfu, na unazidi uwazi wa dalili hii kwa kuhalalisha makubaliano ya ushirika, kwani ushirika ni mchanganyiko kati ya mali mbili au watu wawili unatokana na makutano katika haki na matumizi.
Baadhi ya hukumu za Sharia ya Kiislamu katika ushirika hazielezei kwa uwazi isipokuwa kwa kuzikubali tu na katika wigo wa fikra ya mtu wa kuzingatiwa, hasa kwa upande wa mudharaba, miongoni mwa hukumu za makubaliano ya ushirika katika Sharia ya Kiislamu ni pamoja na sharti zilizowekwa na wanachuoni katika dhamana ya shirika kutokana na kuchanganya kati ya mali za aina mbili, ambapo mmoja wa washirika anachukuliwa kupotea mali zake ikiwa kabla ya kuchanganywa, ama ikiwa baada ya kuchanganywa basi hupotea kwa uwingi wa mali ya shirika, anasema Ibn Al-Humam katika kitabu cha: [Fat-h Al-Qadeer 6/179]:
“Pindi zinapopotea mali zote za kampuni au shirika basi ushirika unakuwa umekufa” vilevile pindi mali ya mdau mmoja inapopotea kabla ya kuchanganywa na kabla ya kununua kitu hupotea mali ya mwenye mali peke yake, ni sawa sawa imepotea mikononi mwa mmiliki mwenyewe au mikononi mwa mshirika mwenzake kwa sababu hiyo mali ni amana mkononi mwake, tofauti na baada ya kuchanganywa ambapo hupotea mali zote kwa kutowezekana kubainika”, anasema Sheikh Aliish katika kitabu cha: [Manhul-Jalil 6/254 chapa ya Dar Al-Fikr]:
“Ikiwa watu wawili wameshirikiana au zaidi ya washirika wawili kisha ikaharibika mali ya mmoja wao au baadhi ya mali atadhaminiwa na mshirika wake pamoja naye ikiwa wameshachanganya kwa maana ya washirika wawili kile kinachotokana na ushirika wao kinyume na kuchanganya basi mali iliyoharibika ni ya mwenye mali yake”, ufafanuzi huu kati ya shirika kama chombo na kati ya watu wa shirika ni dalili ya kukubalika uwepo wa dhima au jukumu la kifedha lililojitenga la shirika, anasema Al-Khatwib Sharbiniy katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj 2/213, 214]:
“Inashurutishwa kuchanganya mali za pande mbili ambapo si za kutenganishwa, ni lazima kuchanganywa kuwe kabla ya mkataba, ikiwa itatokea baada ya mkataba ndani ya kikao inakuwa haitoshelezi kwa kauli sahihi, au baada ya kuachana inakuwa si jambo la lazima, ambapo hakuna ushirika wakati wa mkataba na mkataba unakuja baada ya ushirika, wala haitoshi kuchanganya mali pamoja na kutambulika kwa mfano tofauti ya jinsi ya mali kama vile sarafu na isiyokuwa sarafu, au jinsi ya sifa kama vile kitu sahihi na kilichovunjika, ikiwa itachanganywa na kuharibika mali ya mmoja wao itakuwa imeharibika na kuvunjwa ushirika kwa mali iliyobaki” ni lazima kuchanganya kati ya mali za wawili kwa maana ya kuziweka pamoja ili kutoka kwenye jukumu la ushirika na kuwa jukumu la shirika, na hii inaonesha kuwa shirika lina haiba tofauti na haiba ya ushirika.
Miongoni mwa hukumu zake ni kuwa asili katika shirika ni kuwa hubatilika na kumalizika kwa kufa mmoja wa washiriki, imekuja kwenye kitabu cha: [Al-Mudawana 4/45 chapa ya Dar Al-Fikr]: “Ikiwa mmoja wa washirika amefariki haitokuwa kwa aliyebakia kuendeleza mali iliyobaki wala kufunga hesabu ya bidhaa ziwe chache au nyingi isipokuwa kwa ridhaa ya warithi, kwa sababu ushirika pindi anapofariki mmoja wao hukatika ushirika kati yao na kuwa fungu la marehemu ni la warithi”, katika kitabu cha [Ibn Aabidiin 4/327 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]:
“Hubatilika ushirika wa makubaliano kwa kufariki mmoja wapo, ikiwa mwingine amefahamu kufariki kwa mwenzake au hakufahamu, kwa sababu kihukumu hayupo”, lakini wanachuoni wa Sharia wamehukumu kuendelea ushirika mpaka ikiwa atafariki mmoja wa washirika, kwa hali zifuatazo: Ikiwa wapo watatu au zaidi ya watatu ambapo huvunjika haki yake tu pasina haki za wale waliobaki, anasema Ibn Aabidee: “Lau wadau watakuwa watatu na akafariki mmoja wao basi itavunjika haki yake marehemu pasi na kuvunjika haki ya waliobaki” miongoni mwa hali hizo pia: Ruhusa ya warithi wa marehemu, anasema Al-Bahuuty katika kitabu cha: [Kas-shaaf Al-Qinaai 3/506 chapa ya Aalam Al-Kutub]:
“Ikiwa atafariki mmoja wa washiriki wawili na marehemu akawa na mrithi mwenye umri wa kujitambua basi ana haki” kwa maana ya mrithi kuendeleza ushirika, na kumruhusu mshirika mwenzake kuendesha, pia yeye atamruhusu mdau mwenzake kwenye ushirika kubakia kwenye ushirika kukamilisha shirika na wala sio kulianzisha upya”, hukumu ya kuendelea shirika baada ya kuvunjika kwake kwa kufariki mmoja wa washiriki ni dalili ya kuthibiti dhima huru kwake, na sifa hiyo ni katika sifa muhimu sana anayosifika nayo mtu wa kuzingatiwa.
Wanachuoni wamesema kuwa mshiriki aliyeruhusiwa ana haki ya kusimamia kuuza kununua na kumiliki shirika, na kumshirikisha na mwingine, na kufanya mudharaba na yeye akiwa wakili wa mshirika wake na ni mmiliki pia, yote haya yanafungamana na sifa kuu ya kuwa ni mwenye kufaa kusimamia wajibu na utekelezaji, na hivyo vinahamisha shirika kwa kuzingatiwa ni mtu wa kuzingatiwa kwenye wigo ambao inawezekana shirika kusimama, na katika hili shirika linaweza kumiliki na kutumia, na kumiliki pamoja na kutumia ni katika athari za kuthibiti kwa jukumu la mali.
Na huenda katika masuala yaliyo wazi ambayo yanabainisha uthibiti wa jukumu la mali kwa asiyekuwa mwanadamu baadhi ya hukumu zimepitishwa na wanachuoni katika mlango wa mudharaba, wamesema watu wa Hanafiy kuwa mshiriki kwenye mudharaba lau atanunua nyumba kwa mali ya mudharaba na akawa mwenye mali ni jirani wa yule aliyenunua toka kwake basi atastahiki mwenye mali shufaa, anasema Al-Kasaaniy katika kitabu cha: [Al-Badaiy 6/101 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]:
“Lau atanunua mshiriki wa mudharaba nyumba na mwenye mali mdau mwenzake akawa kwenye nyumba nyingine pembezoni mwake basi anapaswa kuchukua shufaa, kwa sababu mnunuzi hata kama atakuwa na mali katika uhalisia lakini katika hukumu ni kana kwamba hana, kwa dalili kuwa hamiliki kwa kujivua mikononi mwa mwenye mali”, anasema pia: “Lau mtu wa mbali amenunua nyumba pembezoni mwa nyumba ya ushirika wa mudharaba, ikiwa mikononi mdau wa mudharaba ana fedha za kulipia basi anapaswa kuchukua shufaa kwa ajili ya mudharaba, na wala sio mwenye mali kuchukua yeye mwenyewe tu, kwa sababu shufaa ni lazima kwenye mudharaba na umiliki wa kutumia katika mudharaba ni kwa mdau wa mudharaba”, tofauti hii kati ya jukumu la mali la mdau wa mudharaba na mwenye mali kwa upande mmoja na kati ya mudharaba wenyewe kama chombo kwa upande mwingine ni dalili ya dhima ya mali kwa chombo, na kauli yake: “Ni kwa vile shufaa imelazimishwa kwenye mudharaba” ni wazi katika hili, na kuungwa mkono tofauti hii kati ya dhima ya mali kwa mwenye mali na dhima ya mali kwa mdau wa mudharaba na mudharaba wenyewe:
Watu wa Imamu Abu Hanifa wamepitisha mwenye mali kununua katika mali ya mudharaba, na kununua pia mdau wa mudharaba kutoka kwenye mali ya mwenye mali ya mudharaba hata kama kwenye mudharaba hakuna faida, katika hali mbili, kwa kuchukulia mali ya mudharaba ni mali ya mtu wa mbali kwa upande wao wawili, anasema Al-Kasaniy 6/102: “Inafaa kununua mwenye mali katika mali ya mudharaba na kununua mdau wa mudharaba katika mali ya mwenye mali, hata kama hakuna faida kwenye biashara ya mudharaba kwa kauli za wenzetu watatu….kauli yetu: Ni kuwa mwenye mali katika mali ya mudharaba ni miliki ya utumwa na wala sio miliki ya kutumia, na miliki yake katika haki ya kutumia ni kama miliki ya mtu wa mbali, na kwa mdau wa mudharaba ana miliki ya matumizi na wala sio miliki ya utumwa, na imekuwa katika haki ya miliki ya utumwa ni kama miliki ya mtu mgeni, ili mmiliki wa mali asiwe na uwezo wa kumzuia mdau wake kutumia, na kuwa mali ya mudharaba katika haki ya kila mmoja kati ya wawili ni kama mali ya mtu baki, hivyo imejuzishwa kununua kati yao hao wawili.
Kutokana na maelezo hayo: Hakuna kizuizi cha kuthubutu jukumu la mali kwa mtu wa kuzingatiwa hasa kuzingatiwa kwa jukumu la mali hakuwi isipokuwa kwa hatua zilizopangiliwa ili kudhibiti hukumu, anasema Fadhilatuh Sheikh Ally Al-Khafif katika kitabu chake cha: [Ushirika katika Sharia ya Kiislamu uk. 26 chapa ya Dar An-Nashr ya Vyuo Vikuu vya Misri]:
“Jumla ya maneno katika hilo ni kuwa mtazamo wa dhima au jukumu la kifedha na yanayotokana na hilo miongoni mwa hukumu haikuwa isipokuwa ni mpangilio wa Sharia unaokusudia kudhibiti hukumu na kuziunganisha pamoja, inafaa kubadilika na kuboreshwa kutokana na miamala na kuboresha ikiwa masilahi yatahitaji kufanyika hivyo, sio katika yale yaliyokuja wazi ndani ya Kitabu wala katika athari za Sunna yanayozuia kuzingatia dhima au jukumu la mali kwa asiyekuwa mwanadamu, na kufasirika kwa tafasiri pana ya kuthibiti kwenye mashirika taasisi na mali za uma, ya kuwa yanayothibiti kwenye pande hizi miongoni mwa majukumu ya kifedha kinyume na yanayothibiti kwa mwanadamu kwa kiwango cha ukamilifu na kumfanya kuwa ni mwenye sifa ya kupewa jukumu ambalo ni ibada na kushughurikia kile kilichokuwa lazima kidini”, sababu iliyopita ambayo imetajwa na watu wa Abu Hanifa katika sura ya shufaa kwa maana ya kugawa sehemu mbili ya kuwa mwenye mali kwa upande wa kimaana sio mmiliki wa mali ya mudharaba bali yeye kwa mtazamo wa kisheria ambapo hazingatiwi kuwa ni miongoni mwa washiriki au wadau katika shirika wenye kumiliki vilivyomo kwenye shirika kwa upande wa maana na uwazi.
Lakini wao ni wamiliki kwa upande wa mali, kwa dalili kuwa wao hawana haki ya kutumia katika vilivyomo madamu mtu wa kuzingatiwa shirika lipo na kutambulika, kama vile yaliyotajwa na wanachuoni miongoni mwa majukumu ya mwenye mali katika mudharaba hayavuki kwenda kwenye mali yake binafsi katika hali ya kuchukua mkopo kwenye mali ya mudharaba au kununua kwa zaidi ya mali ya mudharaba ni katika yaliyopitishwa na sheria ya kutorejea wenye kudai kwenye mali binafsi za waasisi ili kubainisha kati ya dhima ya mali ya waasisi na dhima ya mali kwa mtu wa kuzingatiwa.
Wala haifai kugonganisha mitazamo kati ya shirika ndani ya Sharia ya Kiislamu na mtu wa kuzingatiwa katika sheria kuwa shirika halipo katika uhalisia isipokuwa kupitia washiriki au wadau wanaounda, kwani shirika kwa ujumla ambapo halifikiwi isipokuwa kwa hatua zake za awali, na hali hiyo kauli ya uwepo jumla inatokana hatua za awali na kuwa lina mamlaka huru katika mamlaka ya hatua za kuundwa au hatua za awali ni maneno ya kipuuzi yasiyokuwa na maana, jibu la hayo:
Ni kuwa masilahi ambayo yanafikiwa na shirika ni masilahi ya pamoja msingi wake ni mali na utashi wa pamoja ambao umepelekea kufikiwa masilahi haya, na utashi huu ni kuwa shirika ni lazima liwe na idadi ya watu wadau wakikubaliana kati yao haki ya matumizi na uwakilishi wa shirika sawa na mazingatio ya vitendo, na wala hili sio isipokuwa ni njia ya kurahisisha na kuendesha chombo hiki kwa maana ya shirika, kama vile utashi huu wa pamoja pindi unapothibiti umbali wake wa kufikiwa masilahi haya ya pamoja basi hapo hatofanyiwa ubaya mtu wa kuzingatiwa kwa maana ya shirika, na kuongezea hayo yale yaliyotangulia kuwa mazingatio ya jukumu la kifedha ni hatua ya kulinda na kudhibiti hukumu na kupangilia masuala.
Ufupi wa maelezo: Ni kuwa kuna tofauti kati ya mtu halisi na wa kuzingatiwa, na imekuwa tofauti hii kati ya watu wawili na athari zake kwenye hukumu zinazofungamana na watu hao, na mtu huyu wa pili kwa kueleweka kwake kisheria hakuwa mgeni kwenye Sharia za Kiislamu, bali wanachuoni wamemtazama pamoja na kutomzungumzia kwa jina lake, sheria ya kiraia ya Kimisri ni kama vile sheria zengine za nchi za Kiarabu imechukulia hivyo na kuweka muundo wa kushirikiana naye kwa mtu anayemuwakilisha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas