Akili ya Muislamu na Uwezo Wake wa Kuweka Nadharia - Nadharia za Usul Al-Fiqh Kama Mfano.
Question
Je! Akili ya Muislamu imejulikana katika historia yake na uwezo wa kuweka nadharia?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwamba akili ya Muislamu, wakati wa harakati zake za kiakili na kitamaduni katika historia yake ndefu, iliweza kuweka nadharia katika ngazi zote na nyanja ambazo akili ya mwanadamu huhamia, na tunaweza kuwasilisha mfano kwa hiyo kupitia taaluma ya Usul Al-Fiqh. Maswali yanayofuatia yametokea akilini mwa mwenye jitihada, majibu yake yaliwakilisha mada za taaluma hiyo, na tunawasilisha hapa majibu haya kwa mpangilio unaolingana na hitajio na nia ya kuuliza maswali haya akilini mwa mwanachuoni wa Usul Al-Fiqh, na tunaona kwamba jibu lao linawakilisha ile tunayoweza kuiita (Nadharia za Usul Al-Fiqh), ambazo mpaka kufikia sasa, tumeorodhesha nadharia saba ambazo zinaweza kufanyiwa kazi kwa kuzingatia kuziongezea, au kuziunga pamoja. Lakini, kushughulikia masuala ya Usul Al-Fiqh kupitia nadharia hizi huwezesha uelewa wa kina kwa masuala haya, inaonesha muundo wa mzozo na sababu yake, na inasaidia katika kuchagua na kupendelea rai moja juu ya nyingine, na pia inaonesha faida ya kuibua masuala ambayo faida yake inaweza kujulikana tu kwa kuziingiza kupitia nadharia hizi, na pia kuonesha umuhimu wa dalili fulani juu ya ubishani wa zamani ulioibuka, kama dalili ile ya Makubaliano.
Nadharia ya kwanza: Nadharia ya kihoja.
Je! Ni hoja gani ambayo tunaichukulia hukumu?
Swali hili la kwanza lilikuwa jibu lake ni: kwamba tunachukua hukumu kutoka katika Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia ni matini iliyoshushwa kwa Ufunuo, ambayo haina makosa kutokana na upotovu, ambayo ilifikishwa kwetu kwa utaratibu usio na shaka, na kwa kuizingatia kwamba ni neno la Mwenyezi Mungu ambaye tunamwamini kuwa ndiye Muumba, na kwamba tumejitolea katika maisha haya ya kidunia kwa kile alichoamuru na kukataza (fanya, usifanye), na kwamba hukumu hizi ni kipimo cha kuadhibiwa siku nyingine wakati watu wanaporudi kwa Muumba wao kwa ajili ya hisabu (adhabu na thawabu).
Kwa hivyo, inadhihirika kwetu kwamba misingi ya sheria imetokana na taaluma ya Usul Al-Fiqh, kwa hivyo ikiwa Qur'ani ndio chanzo cha kwanza cha msingi wa sheria, Sunna inakuja kwa ajili ya kufafanua na kuitimiza Qur'ani, kama ilivyothibitishwa kuwa Mtume, S.A.W., anafikisha maneno ya Mola wake na kwamba amri inaelekezwa kumtii Mtume na kuzingatia kwamba Mtume wake huyo ameepushwa na makosa yoyote.
Nadharia ya pili: Nadharia ya uthibitisho:
Ikiwa hali hii imethibitishwa katika Qur’ani na katika Sunna, basi nadharia ya uthibitisho inakuja, ambayo imeundwa na maono kamili ya suala la kupitisha matini kwa mdomo kupitia wasambazaji, na hali hii inalazimisha kupata taaluma nyingine kama vile Al-Jarhi Wal-Taadiil (Nayo ni taaluma inayotafuta hali ya wapokeaji wa Hadithi za Mtume kuhusu masharti ya kukubali mapokezi yao au la) na taaluma ya Qiraat inayosaidia kupitisha na kudhibiti matini za kisheria. kwa mujibu wa taaluma hizi, hali ya kupitisha imethibitishwa, baada ya hatua ya kuonesha hoja, inakuja hatua ya kuthibitisha kile kilichooneshwa kuwa ni hoja. Jukumu linaweza kuonekana katika taarifa hii, lakini jukumu hilo litafutwa kwa sababu ya kutenganishwa kwa hoja ya uthibitisho. Uthibitisho wa Qur’ani na Sunna umetokana na dalili za kiakili, kisha uthibitisho wa Qur’ani na Sunna kutokana na kwa ukweli wa hali ya kupitisha inayodhibitiwa na dalili kutoka katika Qur'ani na Sunna.
Nadharia ya tatu: nadharia ya ufahamu:
Baada ya hapo likaja jukumu la nadharia ya tatu, ambayo ni nadharia ya ufahamu: Je! Tunaelewaje Qur’ani (hoja kwetu), sasa hivi tuko mbele ya matini ambayo tuliizingatia hoja, halafu tuliithibitisha kwa njia ambazo wanachuoni walizihakikisha kulingana na mbinu ya kisayansi inayotimiza masharti yake, na wanachuoni wa Usul Al-Fiqh wameweka zana za uchambuzi na kuelewa kwa matini, wakichukua hili kutoka jumla ya lugha, sarufi zake, misamiati yake, na sifa zake kwa upande mmoja, na pia kutokana na jumla za hukumu za kifiqhi zinazosambazwa kwa upande mwingine. Hitimisho ni kwamba hatua hii katika ujenzi wa Usul Al-Fiqh ni hatua muhimu sana, na inawakilisha moja ya msingi wa taaluma ya Usul Al-Fiqh, bila kujali tofauti za wenye jitihada na pande za kifiqh katika ujenzi wa zana hizi.
Nadharia ya nne: nadharia ya uthibitisho na ya kidhana:
Kama chanzo kikiainishwa, hoja yake, uthibitisho wake na uelewa wake wanafiqhi walikabiliwa na shida ya uthibitisho na dhana, kwani kuridhika na zana hizi kunafanya nafasi ya uthibitisho kuwa chini kuliko inavyopaswa kuwa, jambo ambalo lilileta shida halisi ambayo ililazimisha kusema kuwa makubaliano ya wanachuoni ni dalili ambayo inapanua nafasi ya uthibitisho, na inabadilisha dhana kutoka hali yake hadi kwenye hali ya uthibitisho. Zana za lugha peke yake hazitoshi kwa kuelezea kauli yake Mwenyezi Mungu: {Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu.} (AL MAIDAH: 6) Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kutegemea makubaliano ambayo huondoa suala hilo kutoka kipindi cha dhana kwenda kwenye uthibitisho.
Kuelewa suala la makubaliano katika muktadha huu kunaondoa kutokubaliana sana juu ya suala hili, na hufanya maneno ya wafuasi kuwa na maana na manufaa.
Nadharia hii ya uthibitisho na dhana inakuwa na athari kubwa kwa masuala ya mzozo wa kifiqh, na suala la jitihada na kutoa Fatwa.
Nadharia ya tano: nadharia ya kiambatisho:
Kama ikiainishwa hoja, uthibitisho wake, na kuelewa kwake katika muktadha wa uthibitisho na dhana, basi matini zinazoainishwa katika maneno yake na mdundo wake kwa ukweli unaobadilika hazijumuishi hali zote, kwa hivyo iligunduliwa nadharia ya kiambatisho, ambayo ilichukua ndani yake aina mbalimbali kama kipimo, na kama utaratibu wa sehemu zote juu ya vipengele vyake, au matumizi ya kanuni ya jumla kwa washiriki wake (mmoja mmoja).
Kila mtu - hata Dhahriya - wanasema kile tunachoweza kukiita (kiambatisho), hata ikiwa wakikanusha aina yake, ambayo ni (kipimo).
Nadharia ya sita: nadharia ya udadisi:
Baada ya nadharia ya kiambatisho inakuja nadharia ya udadisi, ambayo mwanachuoni wa Usul Al-Fiqh aliona ndani yake aina za vigezo kama vile desturi, mila, na kauli ya Masahaba, na Sheria ya jamii iliyotutangulia, na kama vile inayoshawishi kwa maana moja au nyingine kufikia hukumu ya kisheria, ambapo wengine wao walidai kuwa kauli hizi ni dalili, na wengine walikanusha hiyo, kwa hivyo dalili hizi ziliitwa dalili ambazo zilitofautiana.
Nadharia ya saba: nadharia ya Fatwa:
Halafu inakuja nadharia ya Fatwa ambayo ni pamoja na kutaja malengo ya kisheria, kupingana na kupendelea maoni, pamoja na kuzingatia masharti ya jitihada na Fatwa, ambapo kila mwenye kutimiza masharti ya mtafiti atoe hukumu, kisha kulingana na malengo ya kisheria ili isikiuke, na kuipitia hukumu yake kama ikiikiuka ili iwe sawa na hukumu hizi ili zisipunguzwe hukumu kwa malengo kwa ubatili kwa sababu ya hali hii ni kinyume cha kile kinachohitajika.
Nadharia hizi saba na ufikiaji wa taaluma ya Usul Al-Fiqh kupitia nadharia hizo zinathibitisha masuala mengi ambayo mwanafunzi wa taaluma hiyo anafikiria hayatumiki mwanzoni mwa kuzingatia, pia nadharia hizi zinaunda mfumo wa utambuzi unaofaa kwa uchambuzi na utafiti, vile vile nadhari ni kigezo bora cha kupitisha maoni ya kimsingi, au kuyabadilisha na pia kuwawezesha kutekeleza na kuamilisha taaluma hiyo katika uhusiano wake kati ya taaluma ya kijamii na ya kibinadamu.
Na Mwenyzi Mngu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Chanzo ni: Usul Al-Fiqhi na Uhusiano wake na Falsafa ya Kiislamu.
Mufti Mstaafu wa Misri,
Profesa Ali Jumaa.