Je Inashurutishwa kwa Mwenye Kumlea...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Inashurutishwa kwa Mwenye Kumlea Mtoto wa Kike au wa Kiume Kwamba Mke Wake Amnyonyeshee .

Question

Je inashurutishwa kwa mwenye kumlea mtoto wa kike au wa kiume kwamba Mke wake amnyonyeshee au mmoja wa Ndugu wa mke wake? Na ni ipi idadi ya milo ya kunyonya ambayo humfanya mtoto wa kike au wa kiume awe ameharamika kwa Mlezi wake wa kike au wa kiume? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ulezi wa mtoto usiofungamana na unyonyeshaji, unaweza kuwepo bila ya kunyonyesha na huwenda pakawepo unyonyeshaji bila ya ulezi isipokuwa ulezi unapokuwa ni wa kuendelea mpaka mtoto abaleghe pamoja na uwepo wa tofauti ya jinsia baina ya mlezi na mtoto, na hapo panashurutishwa unyonyeshaji wa Kuharamisha kwa mtoto huyo wakati akiwa ananyonya, kwa mkewe au mmoja wa nduguze ili pasiwepo uzito wowote wakati mtoto anapobaleghe, kwa kuwepo wajibu wa kuvaa hijabu wanawake wa familia inayomlea mtoto huyo mbele yake, na uharamu wa kuwa faraghani na mmoja wa wanawake hao na mfano wa hayo miongoni mwa hukumu, na hiyo inakuwa kwa masharti yaliyopitishwa kisheria kwa unyonyeshaji unaopelekea undugu wa kunyonya pamoja.
Na Idadi ya milo ya kunyonya inayoharamisha ni mitano inayotofautiana – kwa kuchaguliwa katika Fatwa zinazofanyiwa kazi katika miji ya Misri:- kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Bi Aisha R.A, kwamba alisema: "milo ya kunyonya iliyoteremshwa katika Qur`ani Ilikuwa ni kumi inayotambulika kuharamisha kisha Aya ikafutwa kwa milo mitano ya kunyonya inayojulikana, na Mtume S.A.W, akafariki dunia na hiyo milo mitano ya kunyonya ikiwa ndiyo inayosomwa katika Qur`ani Tukufu. [Imetolewa na Muslim 1075/2, Ch. ya Dar Al Kutub Al Elmiyah, na aya tukufu hiyo katika Surat AN NISAA 23].
Na udhibiti wa kunyonya (mlo) unarejeshwa katika Desturi ya watu; kwani Sheria imekuja bila mipaka na haikuainisha Kiwango wala muda, na ikawa inamaanisha ya kwamba yeye ameirejesha hukumu yake kwenye desturi za watu, na kinachohukumika kidesturi kwa kuwa kwake ni mlo mmoja wa kunyonya au mingi basi huzingatiwa hivyo na kama sio hivyo basi hapana. Na wakati wowote unyonyaji unapochanganyika na kile kinachoweza kusemwa kuwa ni utenganishaji: ni kuhesabika kwa Idadi. Na lau mtoto alinyonya kisha akasita kunyonya na akajishughulisha na kitu kingine chochote kisha akarejea tena na kuanza kunyonya basi huko ni kunyonya mara mbili. Na kama mnyonyeshaji angelisitisha kisha akaja kunyonyesha tena basi huko kutahesabika kuwa ni kunyonya mara mbili kwa usahihi wake, kama ambavyo mtoto angelikatisha kunyonya kisha akarejea tena. Na wala haipatikani Idadi kwa kuacha ziwa kisha kulirejea tena hapo hapo, wala kwa kuhamia ziwa moja kwenda jingine hapo hapo, wala kwa kulichezea kwa kulinyonya nyonya huku ziwa likiwa mdomoni mwake, wala anapokata pumzi, au kuchanganyika na usingizi wa kusinzia, hayo yote ni kunyonya mara moja tu. [Kitabu cha: Mughniy Al Mohtaaj kwa kujua maneno ya Al Minhaaj 133-135/5].
Na wala haishurutishwi katika unyonyeshaji mmoja uwe ni wa kushibisha, na hivyo ndivyo walivyoeleza Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi katika vitabu vyao. Amesema Khatwibu Sharbiini katika kitabu cha Iqnaau: "wamesema: kama isingelipafikia kooni mwake isipokuwa matone matano ambayo katika kila mlo mmoja wa kunyonya tone moja basi yangeharamisha. [Hashiyat Al Bigermiy Ala Al Khatweeb 73/4, Ch. ya Dar Al Fikr].
Na Mwanachuoni Al Baijuriy amesema katika kitabu chake: [Hashiyat yake ya Kifiqhi 188/2, Ch. ya Muswtafa Al Babiy Al Halabiy]: "Na wala haishurutishwi katika unyonyeshaji kushibisha ".
Na kinachozingatiwa na madhehebu yanayofuatwa na yaliyopo katika umma ni kwamba kunyonyesha kunakoharamisha hakika mambo yalivyo huwa kunakuwa kwa kipindi cha miaka miwili; kwa Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha} [AL BAQARAH 233]. Na wanachuoni wa Kimaliki wanarahisisha katika kuongeza mwezi mmoja au miezi miwili juu ya miaka miwili, Na Imamu Abu Hanifah kajaalia miaka miwili na nusu, kwa kutoa dalili kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} [AL AHQAAF 15].
Na Imamu As Sarkhasiy akasema katika kitabu cha: [Al Mabsuotw]: "Na uwazi wa nyongeza hii, inahukumia kuwa kila kilichotajwa kuna muda wa kila kimoja kati ya viwili, isipokuwa ni kwamba dalili imesimamia kuwa muda wa mimba usipindukie zaidi ya miaka miwili, na ukabakia muda wa kunyonyesha kwa uwazi wake].
Na Mwenyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Ofisi ya kutoa Fatwa
 

Share this:

Related Fatwas