Mageuzi na Njia zake.
Question
Tunapotaka kuleta mageuzi, je, inatutosha sisi kutegemea Njia moja? Au tunahitaji ya kuwa na Njia mbalimbali?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mageuzi lazima yawe katika pande nyingi mbalimbali. Na sisi tunahitaji kuwa na mageuzi ya ngazi zote, ngazi ya kila mtu, na ngazi ya makundi mbalimbali: Familia, Makundi ya Kikazi, Makundi ya Elimu na mengine mengi. Bali ngazi ya Jamii yote kwa ujumla wake. Na mageuzi yana mielekeo miliwi mikuu: Mwelekeo wa kukua na kuwa bora zaidi na Mwelekeo wa kuporomoka na kuwa katika hali mbaya. Na Sunna ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Ulimwengu wake ni kwamba hawabadilishii watu mambo yao mpaka wabadilishe wao yaliyomo, ndani ya nafsi zao. Na kuna ishara iliyokuja katika Sunna hii ya Ulimwengu mara mbili katika Qur`ani Tukufu, moja ikiwa katika kumea kwa Afya na nyingine ikiwa katika kuzorota kwa afya:
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratul Raad: {Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake.}. [AR RAAD 11]
Na katika Suratul Anfaal, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua}. [AL ANFAAL 53]
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, anatubainishia Njia ya wazi katika kuleta mageuzi, na anasema: "Anza na nafsi yako, kisha na wale unaowalea". Nalo ni jambo jepesi mno na ni la kina mno. Na wepesi na Ukina ni alama mbili zinazoonesha upekee wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hivyo akili ya kibinadamu inaelezwa katika ngazi zote kwa namna ambayo inaushangaza Ulimwengu na inamsaidia mjinga na kuwawezesha watu wote kutenda na kufanya kazi ipasavyo.
Ni kitu gani cha kubadilisha? Tunalazimika kubadilisha mfumo wa maisha yetu. Huu ni mpango wa kila siku, na tuufanye uwe wa kweli zaidi kuliko ulivyo, na tuufanye uwe na hekima zaidi, kisha tupange vipaumbele na tujue kwamba kutenda yaliyo hafifu zaidi baina ya madhara mawili ni jambo la lazima, na kuondosha ufisadi mkubwa zaidi ni lazima, basi hapana budi tuzilinde nyakati zetu na tufanye kazi zetu kwa ufanisi na tudumu katika yale tuliyoanza kuyafanya na tusiyadharau mambo madogo madogo tukaja kujikuta tunatumbukia katika makubwa, na tujaribu daima kuwa na busara, kwani mwenye kupewa busara na hekima atakuwa amepewa Kheri nyingi mno. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Yeye humpa hekima amtakaye; na aliye pewa hekima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili.
Na hii ni kabla ya kupitwa na kabla ya kufariki dunia, kwa hivyo, mtu anatakiwa kuwa na kidao cha wino mpaka anapofariki dunia, na maana yake ni kwamba Elimu haitambui “uwepo wa neno la mwisho”, na kwamba kuitafuta Elimu ni mfumo wa maisha ya kila siku na endelevu. Haiwezekani kusemwa: kwamba Mtu fulani amefanikiwa kuimaliza Elimu yote. Na Neno alilolisema Imamu Ahmad au analonasibishiwa “Elimu (inatafutwa) tangu Utotoni mpaka Kaburini” ni Kauli yenye thamani kubwa sana leo na kesho, na maana yake pamoja na mpangilio wake ni mzuri. Kwa upande wa maana yake, hakika mambo yalivyo ni kwamba Mwanadamu anaitafuta Elimu, na anawajibika kuitafuta pindi anapozaliwa mpaka anapoiaga Dunia, hachoki wala hawi mvivu. Anatumia njia zote halali katika juhudi za kuitafuta Elimu, kila elimu, inaweza kuwa ni Elimu ya Yakini au Elimu ya Dhana, Elimu katika Mfumo wake uliokamilika na Elimu katika Sura ya Maelezo; na katika Kauli mbiu hii, mwanadamu anawekwa katika nafasi yake sahihi ambapo anamuhitaji mwingine, na kwamba Maisha yake ni mafupi mno katika kuelewa vyema Maelezo yaliyopo na kwamba Mambo ya Wajibu ni mengi kuliko Wakati uliopo, na kwamba Juu ya kila Mwenye Elimu kuna aliye na Elimu zaidi yake.
Mashirika sita Makubwa ya maelezo ya maarifa, yanasambaza kiwango kikubwa cha maelekezo kila siku, karibu maelezo milioni 120, kati ya habari na chambuzi mbalimbali za magazeti na taarifa zake na kuendelea. Kwa hiyo mapinduzi ya maelezo haya na maarifa yake, yamepindukia mtazamo wowote ule unaofikirika, na benki za maelezo Duniani zinajaribu kufuatilia, hasa hasa Athari zilizojitokeza katika miaka iliyopita za kile kinachoitwa (mlipuko wa maelezo), ambapo wastani wa ukuaji wake kwa Mwaka mmoja wa uzalishaji wa fikra unakuwa kati ya asilimia 4 na 8. Na tukitaka kujaribu kupata picha ya kiwango cha Maelezo yanayozalishwa Duniani kote, tuchukue mfano wa chombo kimoja kinachohusika na Vitengo vya Kemikali, nacho huchapisha maelezo nchini Marekani, na huwa kinakusanya sehemu kubwa ya maelezo yanayochapishwa na vyombo mbalimbali muhimu vya Kisayansi vinavyohusika na nyanja za Kemikali tu.
Chombo hiki kiliongoza Mwaka wa 1907 na kukamilisha milioni moja ya utafiti wake wa kwanza baada ya miaka thelathini na moja. Kisha ikafikia milioni. Kisha kufikia milioni moja katika utafiti wa pili ndani ya miaka kumi na nane, na kulifuatiliwa milioni moja katika utafiti wa tatu ndani ya miaka saba. Na kwa upande wa milioni ya nne ilifuatiliwa ndani ya miaka minne tu. Na kwa Sura ya jumla hakika mambo yalivyo, kiwango cha maelezo kinaongezeka mara dufu kila baada ya miaka kumi na mbili, na kiwango cha uzalishaji wa fikra zinazochapishwa kimekuwa katika mashirika mbalimbali ya uchapishaji, nayo ni moja tu ya aina mbalimbali za uchapishaji kutoka katika vyombo mia moja kwa Mwaka 1800, hadi zaidi ya elfu sabini ndani ya miaka ya themanini, ya karne iliyopita.
Na miongoni mwa sababu za mlipuko wa maelezo ya maarifa kuwa mwingi ni kuongezeka kwa kiwango cha bobezi mbalimbali za kielimu, na watafiti wakayaelekea yale yanayoonekana kuwa wanayajua kwa bobezi za kina – kwa mfano ubobezi wa Uganga – unagawanyika katika uganga wa Moyo, Ubongo, na Mishipa ya fahamu na kuendelea. Na katika Uganga pia kuna ubobezi wa Mishipa mikuu ya damu na upasuaji wazi wa moyo na katika kila ubobezi kunafanyika utafiti wa masuala mbalimbali yenye ubobezi wa kina , jambo ambalo linapelekea matawi ya tafiti hizo na upanuzi wake wa kiwango cha uzalishaji wa kisayansi katika nyanja mbalimbali, jambo ambalo linafanya ule mchakato wa kufuatilia maendeleo na mafanikio ya kisayansi na ilipofikia elimu ya mwanadamu, kuwa haiwezekani kwa hali ya kawaida.
Na takwimu zinaonesha kwamba uzalishaji wa Mwaka wa maarifa katika nyanja za tafiti mbalimbali za kisayansi, na makadirio ya idadi ya nyaraka zinazochapishwa na yanakaribia baina ya nyaraka milioni 12 na 14, na kwamba idadi ya watu wanaochangia katika uzalishaji huo kwa njia moja au nyingine, inaelekea kuwa kati ya milioni 30 na 35. Na ufuatiliaji wa kawaida ngazi ya kimataifa umefikia kiwango kinachokaribia vyombo milioni moja, ambapo inaongezwa katika idadi hiyo kila mwaka kiasi cha vyombo elfu 15 vipya. Na kwa upande wa vitabu, Kiwango cha uzalishaji wake wa kila Mwaka kimefikia kiasi cha maudhui laki sita, kwa maana ya wastani wa vitabu elfu kumi na sita na hamsini kwa siku, au Vitabu sabini kwa saa moja.
Na kwa hivyo, yote hayo, ni wajibu wa kila mtu kujifunza yeye mwenyewe jinsi ya kusafisha nia yake kwa ajili ya kunufaika na kiwango hiki kikubwa cha maelekezo ya kielimu, na namna ya kuyashughulikia. Anasema Mtume S.A.W: "Mtu yoyote atakayepita njia ambayo anatafutia kwayo Elimu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Atamrahisishia njia yake ya kwenda Peponi".
Kinachofaa ni Muumini kujipamba na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Wahbu bin Munabbih katika Hekima za Jamaa wa Daudi: Mtu mwenye akili analazimika kuwa Mjuzi wa zama zake, mwenye kuuzuia ulimi wake na kuukinga na majanga yake
Na huu ni mwelekeo wa Juu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, S.A.W, na hiyo ni Ibara yenye maana kubwa kutoka kwa Wema waliotangulia, na hali hii tunayoiishi hivi sasa inatulazimu tuwe na changamoto – inatupeleka sisi sote katika bidii ya kujitafutia Elimu na kuishi sambamba na Zama zetu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: Kitabu cha Simaatul Aswri, cha Samaahat Sheikh, Dr Ali Juma, Mufti wa zamani wa Misri.