Nia Njema kwa Wachongaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Nia Njema kwa Wachongaji

Question

 

Katika hali ya utashi wa kuendeleza vyanzo vya mapato ya Jumuiya kumekuwa na pendekezo kutoka kwa wanasanaa wakubwa wa uchongaji: Ima wajitolee mapato ya kazi zao au watoe nusu ya mapato kwa kushirikiana na chama cha wanasanaa ya uchongaji, na shime yetu ni kutovuka kujitolea huku mipaka ya halali: Tumewataka kutojumuisha sanaa yao uchongaji wa vinyago vya watu walio hai, au michoro yenye kugusa maisha yao.
Swali:
Je! Sharti hili linatosha kuhalalisha mali hizi? Na je! utakapotufikia msaada huu unaweza kutumika kwenye kazi za ujenzi wa Msikiti wa Jumuiya au inatosha tu kuutumia kwa kuwasaidia wenye mahitaji?

 

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Sala na salamu zimwendee Mtume wa mwisho ambaye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Jamaa zake Masahaba zake na wale waliomfuata kwa wema mpaka siku ya malipo.

Hutumika neno kujitolea ni mjumuiko wa makubaliano katika Sharia ya Uislamu huitwa “Makubaliano ya kujitolea”, miongoni mwa makubaliano haya ni pamoja na: Makubaliano ya kutoa kitu kama zawadi, Waqfu, Nadhiri, Wasia, udhamini, kukopesha na mengine.
Kusudio hapa katika swali hili ni kuhusisha sadaka ya kujitolea, na sadaka ya kujitolea ni sehemu katika sehemu ya kutoa bure kama zawadi, nayo kumilikisha kitu bila malipo kipindi cha kuishi kinachotolewa, lakini kwa kusudio la kupata thawabu Siku ya Mwisho na kujiweka karibu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Sadaka ni jambo la Sunna, na imepokelewa kuhimizwa kwake katika Aya nyingi za Qur`ani Tukufu, mfano wa kauli ya Mola Mtukufu: {Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea} [AL BAQARAH, 245].
Amesema Imamu Abu Bakr Ibn Al-Araby: “Maelezo haya yamekuja katika kuhimiza na kuhusisha utoaji wa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa watu masikini na wenye kuhitaji na katika njia ya kutetea Dini” Kitabu cha [Hukumu za Qur`ani 1/306. 307 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Vilevile imepokelewa katika Sunna maelezo ya ubora wake, miongoni mwa mapokezi hayo ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kutoa sadaka ya kokwa ya tende - kwa maana thamani yake - inayotokana na kipato halali, na Mwenyezi Mungu hapokei isipokuwa kilicho halali, basi hakika Mwenyezi Mungu huipokea sadaka hiyo kwa mkono wake wa kulia kisha anaikuza kwa ajili ya mwenye sadaka yake kama vile mmoja wenu anavyokuza mtoto wa farasi mpaka mwisho inakuwa mfano wa mlima”.
Mali inayotolewa sadaka lazima iwe halali kwa mwenye kuitoa, kwani imepokelewa Hadithi kutoka kwa Imamu Muslim toka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakikubaliki kwake isipokuwa kitu kizuri, na hakika Mwenyezi Mungu Amewaamrisha Waumini yale Aliyoyaamrisha kwa Mitume, na Akasema: {Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayoyatenda} [AL MUMUNUUN, 51], na Akasema: {Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni} [AL BAQARAH, 172], kisha akataja mfano wa mtu aliyetoka safari ya mbali akiwa na nywele timtim huku akiinua mikono yake kuelekea mbinguni akisema: Ewe Mola Ewe Mola, lakini chakula chake ni cha haramu kinywaji chake cha haramu mavazi yake ya haramu basi vipi atajibiwa maombi yake katika hali hiyo”.
Na imepokelewa pia Hadithi na Imamu Muslim kutoka kwa Ibn Omar R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Hakuna Swala inayokubaliwa bila ya mtu kuwa na udhu, wala sadaka mbaya”.
Na imepokelewa pia na Imamu Ahmad katika upokezi wake kutoka kwa Ibn Masoud R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Hakuna mja anayechuma mali inayotokana na njia haramu kisha akaitoa na akabarikiwa kwa kutoa huko, wala kuitoa sadaka ikakubaliwa sadaka hiyo”.
Hadithi hizi pia zinaonesha kuwa mtu anapaswa kujipamba na uzuri ili sadaka yake iwe mbali na mambo ya shaka shaka, amesema Imamu An-Nawawy: Wamesema watu wetu: Inachukiza sadaka yenye kuleta shaka shaka, na inapendeza mtu kuteua mali iliyo halali na kuiweka mbali na haramu pamoja na mambo yenye kuleta shaka shaka” Kitabu cha: [Majmuu 6/ 238 chapa ya Al-Mimbaria].
Ama mwenye kupewa sadaka, naye ni yule anayechukuwa sadaka - ni mfano wa yule anayefanya kazi ya kugawa hii mali kwa niaba ya mtoa sadaka - hivyo hapaswi kuuliza au kutafuta chanzo cha hii mali, au kumwekea sharti mwenye kutoa sadaka kuwa hatochukua ila baada ya kufahamu chanzo chake, kwa sababu asili ni kuwa na dhana njema kwa kiumbe na kuwa mali zao zinatokana na njia halali, kwani Mwenyezi Mungu Amewakataza Waumini kumchimbua na kumchunguza aliyepewa majukumu ya mambo, na Akasema Mola Mtukufu: {Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni} [AL MAIDAH, 101], amesema Al-Hafidh Ibn Kathir katika tafasiri yake [3/203, 206 chapa ya Dar Tiba]: “Hii ni msingi ya adabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake Waumini, amewakataza na tabia ya kuulizia mambo yasiyo na faida kwao kuyaulizia na kuyachambua kwa sababu ikiwa watafahamu undani wa hayo mambo basi huenda ikawachukiza na kupasua usikivu wao ... uwazi wa Aya ni kuna katazo la kutoulizia vitu ambavyo ikiwa mtu atafahamu basi vitamchukiza, hivyo kilicho bora ni kupuuzia na kuacha”.
Imepokelewa kutoka kwa Masheikh wawili Bukhari na Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Tahadharini na dhana kwani dhana ni katika uongo mkubwa, wala msichunguze undani wa mambo ... Hadithi”. [Sherehe ya An-Nawawy ya Sahih Muslim 16/119 chapa ya Dar Ihayaa Turath Al-Arabiy].
Imepokelewa na Tabraniy kutoka kwa Harithat Ibn An-Nuuman R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Ikiwa utadhani basi usilihakiki”.
Bali ikiwa mwenye kutoa sadaka amechanganya mali yake kati ya ile halali na haramu na akafahamu hili kwa uhakika, basi Wanachuoni wengi wamesema kutozuiliwa kukubalika sadaka au kushirikiana na huyu mwenye kuwa na hali hii na jambo lake linaachwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu - isipokuwa akibaini mali haramu - na asili yake ni kauli sahihi kutoka kwa Ibn Masoud R.A. kuwa aliulizwa kwa yule mwenye jirani anayekula mali ya riba kwa wazi wala haoni ubaya wa mali chafu anaichukuwa na kuitumia kwenye kula yake, akasema: “Mwitikieni kwani yakupongeza yapo kwenu na uovu ni juu yake”.
Aliulizwa Al-Hassan kuhusu chakula cha mbadilisha fedha akasema: “Mwenyezi Mungu Amekupeni habari kuhusu Mayahudi na Wakristo kuwa wao wanakula riba lakini amekuhalalishieni chakula chao”. Na akasema Mansour: Nilimwambia Ibrahimu An-Nakhai: “Kiongozi wetu ni mwenye kudhulumu hivyo ananiita lakini si mwitikii” akasema Ibrahimu: “Shetani ana lengo kwenye hili la kuingiza uadui, wafanya kazi walikuwa wanadhulumiwa kisha wakiitwa na wakiitikia” Kitabu cha Al-Furuu cha Ibn Muslih Al-Hanbaly 2/659, 600 chapa ya Aalam Al-Kutub.
Amesema Shihab Qulyuuniyy katika kitabu chake katika kusherehesha kitabu cha [Minhaj 4/263 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: Si haramu kula chake wala kushirikiana wala kuchukua sadaka na zawadi kwa yule ambaye mali zake nyingi ni za haramu isipokuwa kwa ile itakayofahamika uharamu wake”
Kutoharamishwa kujenga mashirikiano na mtu ambaye mali zake nyingi zinatokana na haramu limeelezewa na Al-Hamawiyy mshereheshaji wa kitabu cha Al-Ashbah na kunukuu kwenye vitabu vyao kitabu cha [Fat-hu Al-Qadeer 1/193 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya], kinategemewa kwenye madhehebu ya Imamu Malik kitabu cha Hashiyat Ad-Dusuoqiy cha [sherehe Al-Kabeer 3/277 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah], na sahihi kabisa kwa upande wa Imamu Shaafi [Kitabu cha Al-Ashbah na Nadhaair cha Imamu Suyutiy ukurasa wa 107 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya], na kuhimiza Ibn Qudama katika watu wa Imamu Hanbal katika kitabu cha [Al-Mughniy 4/180 chapa ya Dar Ihyaau At-Turath Al-Arabiy] na mwisho wa kauli yake aliyoisema ni kuwa hilo linachukiza.
Vilevile mali ambayo inachukuliwa ni mali haramu ni ile iliyokuwa imekusanyikiwa na uharamu, miongoni mwa kanuni za Kifiqihi ni kuwa haichukizi mali yenye tofauti ndani yake bali inayochukiza ni yenye kukusanyikiwa na uharamu, kila Muislamu anamwabudu Mwenyezi Mungu sawa na jitihada yake akiwa ni mtu wa jitihada au kwa kufuata utaratibu sahihi ikiwa ni kwa Waislamu wote ambao si Wanachuoni, imepitishwa kwenye misingi ya Sharia kuwa mtu asiyesoma hana madhehebu, na madhehebu yake ni madhehebu ya Mufti wake, na kuwa ikitokea amefanya kitendo mtu asiyejua kusoma kinachofungamana na ibada au mashirikiano wala si kwa kumfuata Mwanachuoni maalumu basi kitendo chake hiki kinakutanishwa kwa kauli ya mmoja wa wanajitihada, ili kusahihisha ibada za watu na mashirikiano yao kadiri inavyowezekana.
Sehemu hii ambayo wametofautiana Wanachuoni kwenye hukumu yake inawezekana kuzingatiwa katika upande wa vyenye kuleta shaka na wala si upande wa haramu moja kwa moja, amesema Al-Hafidh Abu Faraj Zain Ad-Din Ibn Rajab Al-Hanbaly katika [sherehe Al- Arobaina] inayofahamika kama [Jaamii Al-Uluum wal Hikam, ukurasa wa 132 chapa ya Dar Ibn Al-Jawzy]: “Kilicho haramu moja kwa moja: Ni mfano wa kula mzoga, damu, nyama ya nguruwe, kunywa pombe, kumwoa ndugu wa karibu, kuvaa nguo ya matirio ya Hariri kwa upande wa wanaume. Na mfano wa kuchuma haramu: Ni kama vile riba, kamari, kuuza kisichokuwa halali kukiuza, kuchukua mali ya kupora kwa njia ya wizi, au uporaji, au kughushi na mfano wa hayo”.
Ama yanayoleta shaka: Ni mfano wa kula baadhi vyenye tofauti katika uhalali wake au uharamu wake. Ima katika wanyama ni kama vile kula farasi, nyumbu, punda na kenge. Na kunywa vyenye tofauti kwenye uharamu wake miongoni mwa mivinyo ambayo mingi yao inalewesha. Na kuvaa vyenye tofauti katika uhalali wa kuvaa kwake miongoni mwa ngozi za wanyama wakali na mfano wao. Ama katika mapato yenye tofauti ndani yake ni kama vile masuala ya uuzaji wa malipo ya hapo kwa hapo au kwa baadaye na mfano wa hayo. Mfano wa maana hii ndiyo iliyofasiriwa na Imamu Ahmad na Is-haq pamoja na wengine kwenye maana ya masuala yanayoleta shaka.
Masuala ya uchoraji pamoja na sanaa ya uchongaji si katika masuala yaliyotiliwa mkazo kwa kukubaliana juu ya uharamu wake, bali ndani yake yale yasiyokuwa na tofauti katika uhalali wake basi hakuna tatizo ndani yake, na ndani yake yapo yenye tofauti kati ya Wanachuoni hakuna kizuizi, machache ya hayo ni yale yaliyokubalika kuzuiliwa kwake na uharamu wake kati ya Wanachuoni.
Kwa maelezo hayo na uhalisia wa swali lenyewe: Hakuna ubaya wowote kwa Jumuiya iliyotajwa kupokea na kukubali pendekezo ambalo limewasilishwa na baadhi ya wanasanaa wa uchongaji, na sio lazima kuwawekea sharti lolote katika yaliyotajwa, wala si lazima pia kuuliza na kupembua ikiwa yanayopendekezwa kwenye kujitolea ni katika vinavyofaa au ni katika vinavyozuiwa.
Inafaa kutumika mali hii iliyotolewa katika yale yanayohusiana na ujenzi wa Msikiti wa Jumuiya au kwa kusaidia wenye mahitaji au tofauti na hayo, katika mambo ya kheri, wema na ihsani.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas