Uigizaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Uigizaji

Question

 Nini Rai ya Dini katika Uigizaji?

Answer

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Sala na salamu zimwendee Mtume wa mwisho ambaye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Jamaa zake Masahaba zake na wale waliomfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Asili ya Uigizaji: Ni kufananisha kitu kwa kitu kwa maana ya kukifananisha nacho na kukadiriwa sawa na makadirio yake, kwa mfano; husemwa huyu ni kama huyu kwa maana ya mwenzake, hivyo inakuwa kufanana kitu kwa kitu ni kulingana kwake, na husemwa amefanana na fulani ni pale anapofuata mwenendo wake na kupita njia yake.
Na Uigizaji ni mfumo wa kitamaduni unaoendana na ufuasi na simulizi za watu na matukio yaliyotokea hapo nyuma, au matukio yanayofikirika wakati uliopita au wakati uliopo au wakati ujao.
Na inaelezwa kuwa: “Ni kujenga taswira ya kitu akilini, nayo ni uwasilishaji wa vijenga matukio kwa wananchi” na inasemwa pia kuwa ni: “Ni uwasilishaji wa maelezo hai ya kisa na watu wake kilichotokea kweli au cha kufikirika”.
Asili ya Uigizaji kwa maana hii ni jambo lenye kufaa, kwani hakuna dalili inayoonesha kuzuia, bali zimekuja dalili za Kisharia zinazoonesha asili ya uhalali wa simulizi za maneno na matendo ambazo zenyewe ndio ukweli wa uigizaji, miongoni mwa hayo ni pamoja na yaliyokuja katika kisa cha watu watatu waliokimbia miongoni mwa watu wa Israili ambao ni: Mwenye ukoma, mwenye upara na mwenye upofu, na kujiliwa na Malaika katika umbile la mwanadamu ikiwa ni kupewa kwao mtihani na Mwenyezi Mungu, kwani imepokelewa Hadithi na Imamu Bukhari na Muslim katika sahihi zao kutoka kwa Abu Huraira R.A. kuwa alimsikia Mtume S.A.W. anasema: “Watu watatu katika wana wa Israil mmoja wao alikuwa: Mwenye ugonjwa wa ukoma, mwingine alikuwa ni mwenye upara, na mwingine alikuwa na maradhi ya upofu, ndipo Mwenyezi Mungu Alipoanza kuwapa mtihani kwa kuwapelekea Malaika, na akaja kwa huyu mgonjwa wa ukoma na kumuuliza: Ni kitu gani unapenda zaidi? Akajibu mgonjwa: Rangi nzuri na ngozi nzuri kwani watu wananinyanyapaa, anasema: Akampangusa na ugonjwa unaomsumbua ukaondoka na kisha kumpa rangi nzuri na ngozi safi, kisha akamuuliza ni mali ipi unapenda zaidi? Akajibu: Ngamia, basi akapewa ngamia mwenye ujauzito wa miezi kumi, na kuambiwa ubarikiwe naye, kisha Malaika akaja kwa yule mwenye upara na kumuuliza: Ni kitu gani unapenda zaidi? Akajibu: Napenda nywele nzuri, na kuondoka hizi zilizopo kwani watu wananinyanyapaa, anasema akamfuta nywele zile na kumpa nywele zingine nzuri, akamuuliza tena: Ni mali gani unapenda zaidi? Akajibu: Ng’ombe, basi akapewa ng’ombe mwenye mimba na kuambiwa ubarikiwe naye, mwisho akaja kwa yule kipofu na kumuuliza: Ni kitu gani ungependa zaidi? Akajibu: Mwenyezi Mungu Anirudishie macho yangu, na kaweza kuona watu, anasema: Akamfuta, na Mwenyezi Mungu Akamrudishia macho yake, akamuuliza tena: Ni mali ipi unaipenda zaidi? Akajibu: Mbuzi, basi akapewa mbuzi mwenye uzazi na kuanza kuzaliana, basi ikawa huyu wa kwanza ana bonde kubwa la ngamia na mwingine ana bonde la ufugaji ng’ombe na mwingine akawa na bonde kubwa la ufugaji mbuzi, kisha yule Malaika akaja kwa yule aliyekuwa na ugonjwa wa ukoma katika sura yake na umbile lake na akasema: Mimi ni mtu masikini safari yangu imekatika siwezi kufika leo isipokuwa ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kisha kwa uwezo wako wewe, ninakuomba kwa jina la Aliyekupa rangi nzuri, ngozi nzuri na mali hii je utanifikisha safari yangu? Akajibu kwa kumwambia: Hakika haki zipo nyingi, akamwambia: Kama kwamba nakufahamu, hivi haukuwa mwenye ukoma na watu wakikunyanyapaa, ulikuwa masikini kisha Mwenyezi Mungu Akakupa? Akasema, hii mali nimeirithi kizazi kwa kizazi, akasema kumwambia: Ikiwa utasema uwongo basi Mwenyezi Mungu Akurudishe kule ulipokuwa.
Akaja kwayule mtu aliyekuwa na kipara akiwa katika sura yake na umbile lake, akamwambia kama vile alivyomwambia wa kwanza, naye akamjibu kama alivyojibu mwanzake wa kwanza, kisha akamwambia: Ikiwa ni muongo basi Mwenyezi Mungu Akurudishe kule ulipokuwa hapo mwanzo.
Akaja kwa yule aliyekuwa kipofu katika sura yake na umbile lake, na akamwambia: Mimi ni masikini na mpita njia na safari yangu imevunjika hivyo siwezi kufika leo isipokuwa ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kisha uwezo wako wewe, basi kwa jina la yule aliyekurudishia macho yako ninakuomba mbuzi mmoja ili niweze kufika safari yangu, akasema yule mtu: Nilikuwa kipofu Mwenyezi Mungu Akanirudishia macho yangu, nilikuwa masikini kisha Mwenyezi Mungu Akanitajirisha basi chukua unachotaka, kwani ninaapa kwa Mwenyezi Mungu sitakusumbua kwa kitu nilichopewa na Mwenyezi Mungu, akasema yule Malaika chukua mali zako kwani mumepewa mtihani na Mwenyezi Mungu Amekuridhia wewe na hasira za Mwenyezi Mungu zipo kwa marafiki zako.
Vilevile imekuja Hadithi katika sahihi ya Imamu Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Waliozungumza utotoni ni watatu ... Hadithi” mwishoni: “Tumeelezea mtoto mdogo alikuwa ananyonya ziwa la mama yake, akapita mtu akiwa amepanda mnyama - akiwa mchangamfu na mwenye nguvu - pia ana vazi zuri - mama wa mtoto wakasema: Ewe Mwenyezi Mungu mjaaliye mwanangu mfano wa huyu mtu, ndipo mtoto akaacha ziwa la mama yake na kumuangalia kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu usinijaaliye mfano wake kisha akarudia ziwa lake na kuendelea kunyonya”.
Amesema Abu Huraira: “Kama kwamba nikiwa namuangalia Mtume S.A.W. akiwa anahadithia kunyonya kwa mtoto kwa Yeye kunyonya kidole chake cha kati mdomoni mwake”. Katika Hadithi hii Mtume S.A.W. amehadithia hali ya mtoto na kufananisha kule kunyonya kwake.
Na katika yanayohadithiwa kwenye mwenendo wa Masahaba R.A. ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika sahihi yake kisa cha Bi. Asmaa Binti Abi Bakr pamoja na mtu mmoja masikini ambapo kinasema: “Nilijiwa na mtu mmoja akasema: Ewe Mama wa Abdillah, mimi ni mtu masikini, ninataka kuuza kwenye kivuli cha nyumba yako. Akasema Asmaa: Hakika yangu ikiwa nitakuruhusu Zubeir anaweza kataa, hivyo njoo na uniombe Zubeir akiwa shahidi, akaja na kusema: Ewe Mama Abdillah mimi ni mtu masikini nataka kuuza kwenye kivuli cha nyumba yako, akasema Asmaa: Una nini ni kwa nini nyumbani kwangu? Zubeiri akasema kumwambia Asmaa: Una nini mpaka unamzuia mtu masikini kuuza? Basi yule mtu akawa anafanya biashara yake sehemu hiyo mpaka akapata faida.
Uigizaji wa maneno na matendo si jambo jipya kwa sura zake bali jipya ni kufanya sanaa na elimu yenye misingi na kanuni kwa jina la “Uigizaji”, na kanuni ya Kisharia inasema kuwa mifumo ina hukumu zinazokusudiwa, ikiwa uigizaji ni njia au mfumo wenye kuweka wazi na kufanya kazi ya kusambaza misingi ya kimaadili mema na kimalezi pamoja na kujenga akili iliyonyooka basi inakuwa ni jambo la Kisharia na linapendeza, na ni jema kwa kiwango cha uzuri wa lengo lake, kwa sharti la udhibiti wa kanuni za kisharia na kuepukana na ukiukajji na yanayokatazwa kisharia, kama vile kuleta misisimko, kuangalia, kugusa na matamshi yaliyo haramu.
Ikiwa uigizaji huo utakutana na mambo yanayopingana na misingi hii na kwenda kinyume, basi uigizaji huo unakuwa haufai kwa kiwango cha kukiuka kwake, wakati mwengine huwa inachukiza na wakati mwengine inakuwa ni haramu kabisa, lakini wakati huo inapokuwa ni chanzo cha kuchukiza au haramu ni jambo lipo nje halina uhusiano na uigizaji kama uigizaji, na hii inaitwa na watu wa elimu ya misingi ya dini ni chenye kuchukiza kwa kufungamana na kitu chengine, na haramau kwa kuingia kitu chengine. Hivyo haramu zipo aina mbili: Haramu kitu chenyewe, na haramu kwa kuingia kitu kingine, hivyo haramu ya kitu chenyewe: Ni kile ambacho kinakuwa chanzo cha uharamu ni kitu chenyewe, kama vile unywaji wa pombe, uzinzi, kula mzoga na mfano wa hayo. Ama haramu kwa kitu kingine: Ni ile ambayo chanzo cha uharamu wake kinatokana na kitu kingine, kama vile kuingilia wakati wa hedhi, ambapo uharamu sio kuingilia kwenyewe, bali uharamu ni kufanyika kitendo hiki pamoja na kuwepo hali hii.
Ikiwa uigizaji utakutana na jambo haramu au kitendo haramu kama vile kulingania kwenye yanayokwenda kinyume na Dini na maadili, au kupendezesha maasi, au kuonesha tupu ambazo ni haramu kuonekana kwake, au kuunganisha yaliyo haramu kati ya wanaume na wanawake, kuleta vitendo vyenye kufananisha wanaume na wanawake, au ikapelekea kushuhurishwa nayo na kupitwa na jambo la wajibu, wakati huo linakuwa ni lenye kuzuiliwa kutokana na kilichokutana nacho na wala si jambo lenyewe, tofauti na yanapokosekana hayo yote.
Miongoni mwa matamshi ya Wanachuoni wa zamani ambayo yanafuatwa kwenye uharamu wa uigizaji pindi unapokutana na jambo haramu, ni pamoja na yale waliyoyataja katika sura ya wengi waliokutana, kisha mmoja wao anakaa sehemu ya juu ni kama mfano wa sehemu ya walinganiaji, wakawa wanamuuliza maswala mbalimbali hali ya kuwa wakiwa wanacheka kisha wanampiga, au wakijifananisha na waalimu akiwa ameshika fimbo na watu wanakaa pembezoni mwake kama vile watoto wadogo, wakiwa wanacheka na kucheza shere na wanasema: Bakuli la uji ni bora kuliko elimu. Mifano hii miwili ameitaja Imamu Raafii miongoni mwa Maimamu wa madhehebu ya Imamu Shaafy katika sherehe fupi 11/104 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, na Mwanachuoni Damad katika wafuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa kwenye kitabu cha Majmaa Al-Afraad 1/695, 696 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy, kuwa hayo ni katika mambo yanayokufurisha, kwa maana ikiwa inakusudiwa kwa hayo kucheza shere dini au elimu ya Sharia, hivyo amesema Imamu An-Nawawy katika kitabu cha Raudha 7/287 chapa ya Dar Aalam Al-Kutub: “Nimesema: Usahihi ni kuwa hakuna kukufurisha katika masuala hayo mawili ya ufananishaji”.
Ama kuigiza Mitume Sala na Salamu ziwe kwao wote, hukumu inaonesha ni kutofaa, ikiwa ni kuchunga ukubwa wao na nafasi yao, kwani wao ni katika viumbe bora kabisa bila ubishi, na mwenye kuwa kwenye nafasi hii basi huyo ni mtukufu zaidi kuliko kuigizwa na mwanadamu au hata na shetani, linaonekana hili kupitia Hadithi iliyopokelewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim katika sahihi yao kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Itaneni kwa jina langu wala msiitane kwa majina yangu ya kutungwa, na yeyote mwenye kuniona ndotoni, basi atakuwa ameniona kweli, kwani shetani hawezi kujiigiza kwa sura yangu, na mwenye kunisemea uongo kwa makusudi basi na ajiandae makazi yake motoni”. Hadithi hii kuna dalili ya wazi juu ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu katika nafasi ya Mtume S.A.W. shetani kutokuwa na uwezo wa kujiigiza sura ya Mtume S.A.W. si katika ukweli wake wala katika njozi, ikiwa ni kulinda nafasi ya Mtume na nafasi ya ujumbe, ikiwa imethibiti hii basi yenyewe na katika kulinda nafasi hii pia huzuiliwa kumuigiza moja ya haiba ya Mtume S.A.W. au kuchukua nafasi yake katika kazi za michezo ya drama.
Amesema Al-Haafidh Ibn Abdulbarr katika kitabu chake kinachoitwa “Al-Istiaabu fi maarifat al-Ashaab 1/359, 360 chapa ya Dar Al-Jiil” katika kumfasiri Al-hakamu Ibn Abi Al-Aas kuwa Mtume S.A.W. alimtoa Madina na kumfukuza mwishowe akaenda Taif na ikasemwa kuhusu sababu iliyolazimisha Mtume S.A.W. kumwondoa ni alikuwa akiigiza haiba ya Mtume katika tembea zake na harakati zake mbalimbali, amesema Ibn Abdulbarr: “Wamesema kuwa Mtume S.A.W. pindi anapotembea alikuwa ni mwenye uchangamfu na Al-Hakam Ibn Al-Aas alikuwa akiigiza, siku mmoja Mtume alipogeuka nyuma akamwona Hakam anamwigiza hivyo ndipo akasema Mtume S.A.W.: “Basi na iwe hivyo”Hakam akawa kuanzia siku hiyo ni mwenye woga”. Katika maelezo haya kuna dalili ya kuzuia kumuigiza Mtume S.A.W. katika matendo yake na kumuigiza si kwa njia ya kufuata mwenendo wake.
Kuzuia kuigizwa kunathibiti pia kwa Manabii wengine walio baki Sala na Salamu ziwe kwao wote, kwa sababu wote wapo sawa katika cheo kimoja kwa upande wa kuzuiliwa kwao kufanya makosa na kukirimiwa.
Kama vile kuigiza haiba za Mitume na Manabii kunaundika na mkusanyiko wa uharibifu: Kama vile kuwa kwake hakuendani na uhalisia wa kweli katika matendo yao ya Kisharia, na kuigiza kunategemea na mchezo wenyewe wa drama ambapo hupelekea kuingia kwenye uigizaji wao yale yasiyokuwepo, na kanuni ya Kisharia inasema: Kuondoa uovu ni jambo lenyewe kutangulizwa kuliko kuleta masilahi.
Kwa watu wa weledi wa kazi za uigizaji wanapaswa kutafuta kazi mpya za kisanaa zinazoruhusu kunufaika na tabia na mienendo ya Manabii kama uhalisia ulivyo, pamoja na kuchunga kutoonekana haiba za kuigizwa, na kuwajibika na mazingira ya nafasi zao na utukufu wao.
Ama kwa upande wa kuigiza Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwao wote, Fatwa iliyopitishwa ni kwamba inafaa, isipokuwa Mama wa Waumini kwa maana ya wake za Mtume S.A.W. pamoja na wale Masahaba kumi waliobashiriwa Pepo, hao haifai kuwaigiza, kwa sababu ya nafasi yao, kwani wao ni viongozi wa Masahaba na ni Masahaba wakubwa, kufaa huku kunaendana na vigezo vilivyotajwa katika hukumu ya kuigiza kwa ujumla wake pamoja na kulinda vigezo vingine maalumu ambavyo vitaelezwa.
Muelekeo wa hukumu hii ni kutokuwepo kizuizi cha kuwaigiza kwa kuwa tu lengo ni zuri, kama vile kuonesha sura nzuri kwa hadhira, na kuleta maana ambayo wameiishi, na kusimika uelewa wa kigezo chema kupitia wao.
Vigezo vya kuwaigiza Masahaba:
Cha Kwanza: Kuwajibika na imani za watu wa Sunna “Ahlu Sunna” kwao, ikiwa pamoja na kuwapenda wote bila kuzidisha kumpenda mmoja wao zaidi au kuzidisha mapenzi kwa baadhi ya wengine, kwani amesema At-Twahawy katika kitabu chake cha Akida yake yenye kuridhiwa: “Tunawapenda Masahaba wa Mtume S.A.W. wala hatuzidishi katika kumpenda mmoja wao zaidi ya wengine wala kumtetea zaidi yeyote miongoni mwao, na tunamchukia yule anayewachukia na kuwataja kinyume na uzuri, kwani hatuwataji isipokuwa kwa uzuri, kuwapenda kwao ni Dini, Imani na ni wema, ama kuwachukia ni ukafiri unafiki na upotovu”. Kitabu cha [Akida ya Twahaawiya ukurasa wa 133 ya sherehe ya kitabu cha Maidan - chapa ya 2 ya Dar Al-Fikr - Damascus 1412H. – 1992 AB].
Cha Pili: Kuusisitizia utukufu wa Masahaba wote, kwa ukaribu wao kwa Mtume S.A.W. pamoja na kuheshimu haiba zao na kutozionesha katika sura ya hovyo na kejeli pamoja kushusha nafasi yao.
Cha Tatu: Kuhamisha mwenendo wao kama ulivyo, na kutochezea mwenendo wao kwa lengo la kupata faida ya kifedha, wala asijinasibishe mwandishi wa drama yeye mwenyewe kuwa ni kiongozi wa Maswahaba wala kuwakosoa, bali anapaswa kuwa na shime ya kuonesha nafasi zao zilizotukuka katika kumtetea Mtume S.A.W. na kuilinda Dini, pamoja na kueneza Sharia na Uislamu.
Cha Nne: Kutegemea mapokezi ya kina na kujiepusha na mapokezi yaliyo dhaifu na ya kutengenezwa.
Cha Tano: Kujiepusha na fitina na tofauti kati ya Umma wa Kiislamu.
Vigezo hivi vimepitishwa na jopo la watafiti wa mambo ya Kiislamu la Al-Azhar Al-Sharif katika maamuzi yao nambari 100 ya kikao chao cha kumi na nne katika Mkutano wao wa kawaida wa thelathini na tano ambao ulifanyika mwezi 16 - Mfungo Sita - 1420H. sawa na tarehe 30 - 07 - 1999AB, walipitisha kuwa haifai kukusanya kazi ya uigizaji kwenye kumbi za maonesho ya cinema na drama au hata kwenye runinga - au kwenye chombo chochote chengine - juu ya haiba ya hawa wafuatao: Manabii, Mitume, Masahaba kumi waliobashiriwa Pepo na watu wa nyumbani kwa Mtume.
Kulitangulia maamuzi nambari 20 ya kikao cha dharura cha Nne kilichofanyika mwezi 07 Mfungo Nne 1392H. sawa na tarehe 22 Mwezi wa Pili 1972 yalisema: Haifai kuigiza haiba za viongozi wa Kiislamu wenye nafasi ya Heshima na kigezo chema.
Haya yote yanakubaliana na kuwa kwetu walinzi wa haiba za Kidini ambao wana utukufu na heshima ili tusiwe mateka wa sanaa kwa haiba ya mwandishi wa sanaa anayelazimisha uhalisia kwa hadhira, jambo linalobadilisha moja kwa moja taswira ya hadhira kwa haiba hizi na mtazamo wa kiakili uliopo kwa watu hawa, na kubadilishwa kwa picha ya kisanaa inayotolewa, jambo ambalo linapelekea kuwepo athari kubwa ya kubadilisha sura ya haiba hizi na kulazimisha mtazamo wa mwandishi wa drama.
Wakati ambapo wengi wanajaribu kuondoa utakatifu wa Manabii na watu wa Dini zingine wenye utukufu na nafasi kubwa, wakifuata mwenendo wa fikra za Kimagharibi ambazo zinauondoa utakatifu kwenye kila kitu - Kutokana na mfumo wa kimaarifa - na wanaona katika hilo kuto ondoa utakatifu kunapelekea kwa mwandishi kuonekana ni mpungufu wa mtazamo wa kisasa na anauweka mbali ukweli.
Hivyo sisi tunaona kwa mtazamo wa Uislamu - pasi na kuingia kwenye uchambuzi zaidi wa mjadala wa kifikra - kwamba kupinga moja kwa moja fikra ya kuondoa utakatifu ni sawa sawa kwa upande wa kifikra au katika ufanisi wake wa kivitendo, fikra hiyo ambayo imewapelekea kupinga tamko na andiko takatifu la Kidini, na kuishia kwao katika kuwakosoa Manabii na kuwachafua, pamoja na kuwazingatia ni mfano tu wa watu wanaoweza kukosolewa na kufanyiwa tathmini.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

Dr. Ally Jumaa
Mufti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri
29/06/2009.

Share this:

Related Fatwas