Mauaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Mauaji

Question

Je, inajuzu kushiriki katika mashambulio ya mauaji mfano wa wanavyofanya wafuasi wa makundi ya kigaidi?

Answer

Haijuzu kushiriki katika mashambulio haya kwani yanapinga makusudio ya Sharia likiwemo; kulinda nafsi iliyo haramu kuuawa isipokuwa kwa haki, kama vile kulipiza kisasi, au kupigana na wanaofanya uadui, na anayefanya jambo hilo basi hukumu yake katika Uislamu ni sawa na anayeua nafsi kimakusudi, kwani anakusudia kumaliza maisha ya mtu pasipo na haki na kumfanyia hiyana, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa" [An-Nisa'a: 93], na hakuna tofauti katika hukumu hii kati ya kumuua Muislamu na kumuua asiye Muislamu, naye Mtume (S.A.W.) amekataa kukubali udhuru wa Al-Harith bin Suweid alipomuua Al-Mugdher bin Ziad pasipo na haki.

Vile vile, uhalifu huu wa kumuua mwanadamu unajumuisha maovu na ufisadi mkubwa, kwani husababisha kumwaga damu, kutishia amani na utulivu kwa hiyo hatia hii ni aina ya hatia ya mauaji yaliyokatazwa na Sharia ya Kiislamu, kijumla mauaji yanayofanywa na makundi ya kigaidi ni hatia inayokataliwa na dini na Sharia, hivyo inamwajibisha mtendaji wake adhabu kubwa mno.

Share this:

Related Fatwas