Neno Kwa Mtazamo wa Kiisilamu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Neno Kwa Mtazamo wa Kiisilamu.

Question

Ni lipi Jukumu la kutamka neno “kutokana na mtazamo wa Kiisilamu”?

Answer

 

3- Neno Kwa Mtazamo wa Kiisilamu.
Swali:
Ni lipi Jukumu la kutamka neno “kutokana na mtazamo wa Kiisilamu”?
Jibu:
Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo
Neno ni njia ya kwanza ya kukutana mtu mmoja mmoja na jamii, na neno ni njia ya kuhamisha urithi wa kitamaduni kutoka kizazi hadi kizazi, vile vile neno ni sehemu muhimu ya ustaarabu, na ni kiungo muhimu miongoni mwa viungo vyake, na neno ni lenye kueleza ujumbe wote na dini, na kwamba mawazo ya mwanadamu husimama kwa mshamgao yanapojaribu kutafakari kumbukumbu ya kukamilika kwa neno Kupitia Qur'ani Tukufu na vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu, na mabadiliko ya kihistoria yaliyoletwa na vitabu hivi katika mawazo ya kibinadamu kwa upande mmoja, na katika maendeleo ya ustaarabu kwa upande mwingine.
Neno peke yake lilibeba Maneno ya Mungu kwa wanadamu, na ni peke yake ndilo lenye kubeba mafanikio yote ya ustaarabu wa wanadamu, na hivyo kusababisha mapinduzi makubwa katika historia ya maandamano ya wanadamu hadi sasa.
Labda kwa kutazama kutajwa kwa (neno) ndani ya Qur'ani Tukufu, likiwa ni matini au maana yake, na tukitafakari asili ya kutajwa kwake, tunaweza kuweka chini ya macho yetu katika sifa za neno kama ni ukweli wa malengo kutokana na mtazamo wa Kiislamu, kama ambavyo Mtume S.A.W., katika harakati zake za neno ameweka kwetu pia masharti ya neno linalolifanya liwe chombo chenye lengo linalolipuka kwa nguvu, harakati na usafi, na kukumbatia ulimwengu wote, na kuliweka neno hilo mbali na kuwa fomu tupu bila maudhui au kauli mbiu tofauti na ukweli katika harakati za uwepo.
Neno, kama lilivyooneshwa katika Qur'ani Tukufu, lilikuja katika siku za mwanzo za kuishi kumwokoa Baba wa mwanadamu Adam A.S. {Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.} [AL BAQARAH: 37].
Neno hili ni muhtasari wa falsafa ya Uislamu kama dini kamili, ambayo vipindi vyake vilikamilishwa na kukamilika. {Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.}. [AL ANA'AM: 115]
Neno ni ishara ya kuwa chini ya uelewa halisi kwa ukweli mkubwa, nalo ni kushiriki na wengine {Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.} [AAL IMRAAN: 64].
Neno ni upanga wenye pande mbili, {Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. (24) Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. (25) Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng'olewa juu ya ardhi. Hauna imara (26)} [IBRAHIIM 24:26).
Na neno ni mwanzo ambao hauishi, na wino ambao haukauki; {Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea.} [AL KAHF: 109].
Neno ni mizani ya ukweli na upanga wa haki {na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliomo vifuani} [ASH SHURAH:24].
Neno huwa linaweza kuinuka kama ndege anayepenya kwenye upeo wa macho na mbingu {Kwake Yeye hupanda neno zuri, na a'mali njema Yeye huitukuza} [FATIR: 10]
Mbali na nafasi nyingine ambapo neno linaonekana katika Qur'ani Tukufu, na kwa kiasi kwamba neno linaonekana katika Qur'ani Tukufu, ambayo ni chombo cha kweli cha mtazamo wa Kiislamu.
Kwa upande mwingine, Qur'ani Tukufu ilibeba kampeni kali dhidi ya tabia mbaya ya neno, ikisisitiza vipimo vikali ambavyo mtazamo wa Kiislamu unaweka juu ya neno ambalo halipaswi kuwa na vipimo vibaya kwa neno. Mwenyezi Mungu amesema: {Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa (10) Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie (11)} [AL QALAM: 10 11], na Mwenyezi Mungu amesema pia {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.} [AL HJURAAT:12]. Vile vile Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.} [AL HUJURAAT: 6]. Hakika neno hapa linakaribia kuwa kama mwanadamu ambaye anasema, ikiwa linakuwa la uwongo, basi mwanadamu wake ni mwongo, na ikiwa linakuwa la kusengenya, basi mtu wake anakula mizoga na ni katili, na yuko mbali na silika ya kawaida, na ikiwa ataendelea na hali hiyo, basi kwa ujinga wake atauma vidole kwa majuto.
Ama neno katika mtazamo usio wa Kiislamu, au kwa wasiokuwa Waislamu linaweza kutumiwa kwa maana ya mapenzi na mfano wake hadi kufikia maana ya uasherati, na hutumika kwa maana ya urithi wa kitamaduni kwa maana yake, na pia linatumiwa na wale wanauopinga urithi huu kwa imani zao zenye shaka, na linatumiwa na dini za mbinguni, na linatumiwa kuzitukuza dini za kupangwa na mawazo yasiyo ya kawaida, na linatumiwa kwa maana ya uhuru kwa vipengele vyake vyote mpaka kufikia machafuko yanayotokea kwa jina la uhuru wa maoni.
Ama neno kutokana na mtazamo wa Kiislamu, mtazamo wa Kiislamu unafahamu jinsi ya kuweka vitu katika mahala pake pa uhakika, kwani urithi ni ustaarabu wa uelewa, na sio ustaarabu wa holela, dini ni ufunuo wa Mungu, na sio upotovu wa kibinadamu, na uhuru ni wajibu, sio kusahau sheria.
Kwa hivyo, uelekezaji wa Mtume S.A.W. kwa neno ulikuwa endelevu na usio na kikomo, na kampeni yake pia ilikuwa juu ya kila kitu kwa kinacholiweka neno katika sehemu isiyo kuwa ya kawaida, kwa hivyo Mtume S.A.W., alisema: “Hakika Mja anaweza kuzungumza neno katika yanayoridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu bila kukusudia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamnyanyua hadhi ya juu. Na hakika Mja anaweza kuzungumza neno katika yanayomchukiza Mwenyezi Mungu Mtukufu bila kukusudia na likampeleka neno hilo Motoni.” [Imepokelewa kwa Al-Bukhariy (6113) na kwa Abu Hurairah].
Na Mtume S.A.W., amesema: “Hakika kipenzi zaidi miongoni mwenu kwangu mimi na wa karibu zaidi kwangu mimi siku ya kiyama ni mzuri wenu wa tabia na anayechukiza zaidi miongoni mwenu kwangu na wa mbali zaidi kwangu mimi siku ya kiyama ni wenye maneno mengi wanaojisifu walio na kiburi. [Imepokelewa kutoka kwa At-Termithi (2018) na kwa Jabir R.A.].
Neno katika mtazamo wa Kiislamu lazima liwe katika kiwango ambacho limekuwa katika mfumo wa malengo ya Qur'ani Tukufu, na kwa sababu hii, neno katika mtazamo wa Kiislamu lina jukumu, linalohusiana na kuelezea yote yaliyomo katika kina cha wanadamu, na linalohusika na matumizi ya urithi wa kiustaarabu katika kuendelea kwa maisha na vitongoji, sio katika uharibifu wao. Neno linahusika na kuhifadhi ujumbe na dini za Mungu, na ndani ya mfumo wao wa Kiungu ili cha duniani kisichanganywe na kile kinachotokana na ufunuo wa mbinguni.
Neno linahusika na mawasiliano ya milele kati ya mwanadamu na Muumba wake. Kwa neno tunamwabudu Mungu Mwenyezi, na kwa neno hilo tunaelewa kitabu Chake Kitakatifu.
Jukumu la neno katika Uislamu linaonesha falsafa ya msimamo wake wa kipekee, kwa sababu linabeba jukumu la mzigo wa dhamira ya mafundisho ambayo huweka Ulimwengu mbele ya macho yake, kwani hali hii inaelezea harakati za mtu binafsi, msukumo wa kikundi, maadili ya ustaarabu, na zana za mawasiliano.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Marejeo: Fi Al-Fikr Al-Islami Min Al-Wijahtil Adabiyah, na Dkt. Muhammad Ahmad Al-Azab, Cairo: Baraza Kuu la Utamaduni, 1983 BK, (uk. 103-113).

Share this:

Related Fatwas