Kuishia kwa Wanazuoni Enzi Moja ni...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuishia kwa Wanazuoni Enzi Moja ni Kizuizi

Question

 Wanazuoni wengi walitaja ndani ya maneno yao usemi kama vile: (Kuishia kwa Wanazuoni enzi moja ni kizuizi). Je, nini kusudio lao wakati wanaposema usemi huu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya Waislamu ni kuwa wao walibuni (Elimu ya Uthibitishaji) bila kuwa mfano uliotangulia, nao hawakuichukua kutoka kwa watu wa zamani, na hawakuiiga kwa watu wowote, na elimu hiyo inayohusu Waislamu ilijengeka na kukamilika mno. Elimu ya (uthibitishaji) ni mfano wa elimu zingine, K.v. (Elimu ya Ufahamu) na (Elimu ya Misingi ya Fiqhi), ambayo ni elimu ya hali ya juu sana na imeanzishwa kutokana na Ustaarabu wa Waislamu.
Na Ulimwengu wa sasa wa sifa ya mfumo wa kitaaluma, unahitajia sana Elimu kama hizi ili uthibitishe machimbuko yake, na kuangalia habari zake, ili usije kuzielekea akili za Hadithi za uwongo na mpaka wa mawazo holela.
1- Miongoni mwa Elimu za Uthibitishaji za Waislamu ni: (Elimu ya Visomo vya Qur`ani) na (Elimu ya Mapokezi ya Hadithi) ambayo imezaa (Elimu ya Ukosoaji na Urekebishaji) ambayo inashughulikia kuangalia hali za Wapokezi wa Hadithi, udhibiti wao, kukubalika au tofauti zao kuhusu Misingi ya mapokezi yaliyopokelewa; kisha kanuni nyingi zikazalika, miongoni mwake ni kanuni hii ya pekee, ambayo inaonesha ufahamu wa kina, uzuri wa maono, kuomba msamaha kwa wengine, kutotoa haraka hukumu holela, na uadilifu kwa mpinzani, au ukitaka kusema: hasa kwa mpinzani; Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda}.
Na kanuni hii ndiyo ni: (kuishia kwa Wanazuoni wa enzi moja ni kizuizi).
2- Na maana ya kanuni hii kuwa: maisha ya watu wawili ndani ya enzi moja hayatoi fursa kwa kila mmoja amjue mwingine ilivyo, kwa sababu fikra ya kiakili iliyopo kwa kila mmoja na mwingine itakuwa na kasoro, na huenda mtu akakamilisha maneno yake baadaye, ambayo yalifahamika kinyume cha muradi wake hapo awali, na huenda akabadili maoni yake ambayo aliyaelekea hapo awali, na zaidi ya hayo, huenda akabadili chimbuko lake au madhehebu yake kabisa, na huenda mtu akabadilika awe mwenye kupenda au mwenye kuchukia.
Na hii inasadikishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake}. Na kauli yake Mtume S.A.W: “Nyoyo zipo kati ya vidole viwili vya Ar-Rahmaan, ambavyo anavigeuza kama anavyotaka”.
Na kwa mujibu wa hayo: Tofauti iliyopo kati ya watu wawili kutokana na maoni yao ni tofauti ya muda, na huenda ikabadilika. Na msimamo unaomfanya mtu amtuhumu mwenzake huenda ukabadilika na kwisha.
Na kanuni hii imepitishwa na wengi katika Wema Waliotangulia R.A, na Ibn Abbas anasema: “Chukueni Elimu mnapoikuta, na msikubali kauli ya wanazuoni wenyewe dhidi ya wenyewe; kwa sababu wao wanageukana mfano wa mabeberu wanapokuwemo zizini”.
Na Malik ibn Dinar, Mwenyezi Mungu Amrehemu, anasema: “Kauli za wanazuoni na wasomi zimekubalika katika kila kitu, isipokuwa kauli zao wenyewe dhidi ya wenyewe; kwa sababu wao wanahusudiana sana kuliko mabeberu”.
Na Ibn Hajar, Mwenyezi Mungu Amrehemu, anasema: “Maneno ya wanazuoni wa rika moja (dhidi yao kwa wao) hayazingatiwi, hasa ukiangalia kuwa sababu yake ni uadui, madhehebu, au husuda. Na hasalimiki na hali hii isipokuwa mwenye kumwogopa Mwenyezi Mungu. Na sizijui zama katika zama zote kama watu wake wamesalimika kwa hali hii isipokuwa Manabii na Watu Wema, na lau ukitaka nisimulie basi kuna kurasa nyingi za habari hizi”.
3- Na kutoka katika kanuni hii, pamezalika kanuni nyingine ambayo inaiainisha, kuipangilia, na kuielezea Kanuni hii, nayo ni: “Haikubaliki kauli ya watu wa rika moja dhidi yao wao wenyewe kwa wenyewe), na hii ndiyo maana ya: Kuishi kwa Wanachuoni enzi moja ni Kizuizi. Na kanuni hii haipingi kukuubali ukosoaji na usahihishaji kutoka kwa watu wake, lakini inamwelezea yule anayemtuhumu mwenzake, wa rika lake, akiwapinga watu wengine wanaomsifu, wanaomrekebisha, na kuutaja ubora wake. Na kama muungwana miongoni mwa watu bora akija kumtuhumu yule anayesifiwa na kurekebishiwa na wote, basi haikubaliki kauli yake; ambapo haikubaliki tuhuma ya mmoja dhidi ya mwenzake kwa sifa hii. Kwa hiyo wamesema kuwa sababu ni: kuishia kwa Wanachuoni enzi moja ni Kizuizi.
4- Hivyo basi, Inakubalika kuwa: makundi ya wanazuoni kumtuhumu mtu na kumkataa, lakini kuishia enzi moja ni kizuizi kati ya watu wa rika moja. Na hapa enzi kwa uwazi haiufichi ukweli wa vitu na watu, lakini enzi ni kizuizi kati ya mmoja na mwenzake kutokana na kuwa kwao kiwango kimoja, ambapo anaukana uadilifu kutoka kwa mwenzake, akipata fursa ya kumtuhumu, na kujidai kuwa yeye ana makosa ambayo lazima yakatazwe.
5- Kupitia historia ya Kiislamu yametokea matusi kati ya wakubwa; Miongoni mwao (Abu Nuaim Al-Asbahaniy) aliyekufa mwaka wa: 436 H, na (Ibn Mandah) aliyekufa: 511 H. Na Al-Hafidh Adh-Dhahabiy kuhusu yaliyotokea kati yao anasema: “Maneno ya Ibn Mandah dhidi ya Abu Nuaim ni makali, na sipendi kuyasimulia, na siyakubali maneno ya kila mmoja wao dhidi ya mwenzake… Na maneno ya Wanachuoni wa rika moja hayazingatiwi, hasa ukiangalia kuwa sababu yake ni uadui, madhehebu, au husuda”.
Na (Al-Mughirah) aliyekufa mwaka: 105 H., na (As-Sabii’iy) aliyekufa mwaka: 129 H., na (Al-Aa’mash) aliyekufa mwaka: 148 H. Imepokelewa na Jarir, kutoka kwa Mughirah kuwa alisema: “Hawakuiharibu Hadithi ya Watu wa Kufah isipokuwa Abu Is-haq na Al-Aa’mash”. Na Adh-Dhahabiy anasema: “Maneno ya watu wa rika moja wenyewe dhidi ya wenyewe hayasikiki”. Na (Ahmad) aliyekufa mwaka: 241 H., na (Hisham Ibn A’ammar) aliyekufa nwaka: 245 H. Abu Bakr Al-Maruziy anasema: “Ahmad Ibn Hanbal alipomtaja Hisham Ibn A’ammar, alisema: Mzembe na hafifu”.
Miongoni mwake pia: ni tukio lililotokea kati ya (Al-fallas) aliyekufa mwaka: 249 H, na (As-Samiin) aliyekufa mwaka: 235 H. Abu Hafs Al-Fallas alipomtaja Muhammad Ibn Hatim Al-Baghdadiy As-Samiin - Mpokezi wa Muslim na Abu Dawuud - alisema: “Si kitu), kisha Adh-dhahabiy alijibu kuwa: “haya ni maneno ya watu wa rika moja, kwa hiyo hayasikilizwi”.
Na miongoni mwake, ni tukio lililotokea kati ya (Abdul Mughith Ibn Zuhair) aliyekufa mwaka: 583 H, na (Abul Faraj Ibn Al-Jawziy) aliyekufa mwaka: 597 H. Ulitokea uadui na fitina kati yao, na wao ni Wahafidhina, wanazuoni wa madhehebu ya Ibn Hanbal. Na sababu ya uadui huo ilikuwa suala la kumlaani Yazid Ibn Mua’awiyah. Abdul Mughith alifuata mtazamo wa kumlaani, na akaandika kitabu na kuwasikiliza watu. Kisha Ibn Al-jawziy akaandika kitabu cha kumjibu, na akakiita: (Ar-Rad A’ala Al-Mutaa’asib Al-A’anid Al-Manii’ Min Dham Yazid), na kulikuwa na masuala mengine zaidi ya hayo, na Abdul Mughith alikufa na wao wakiwa wanagombana.
Na miongoni mwake, ni tukio lililotokea kati ya (Mutayan) aliyekufa mwaka: 297 H, na (Ibn Abi Shaybah) aliyekufa: 235 H. Na Al-Hafidh Ibn Hajar alitaja katika Historia ya Muhammad Ibn Abdillahi Ibn Suleiman Al-Hadhramiy, lakabu yake ni (Al-Mutayan) kuwa: Al-Hafidh Muhammad Ibn Uthman Ibn Abi Shaybah alimpinga, na Mutayan alimpinga Ibn Abi Shaybah, kisha mambo yao yaliendelea kuwa ugomvi.
Na Al-Hafidh Ibn Hajar amesema: “Hatuzingatii, Walhamdulillahi, maneno mengi ya watu wa rika moja dhidi ya wenyewe kwa wenyewe”.
Na Adh-Dhahabiy anasema: “Maneno ya watu wa rika moja dhidi ya wenyewe kwa wenyewe hayazingatiwi, na kuyaficha ni bora zaidi kuliko kuyafichua”. Na Ibn Abdul Bar alitunga mlango katika kitabu chake: (Jamii’ Bayan Al-Ilm) akielezea ilivyo; kwa hiyo wanazuoni wa Elimu ya Ukosoaji hawazingatii wale walioteswa kutokana na kuishi enzi moja - kama ilivyojulikanwa kupitia Vitabu vya Wapokeaji. Na lau wao wangelizingatia maneno hayo, basi wasingalikuta mpokeaji mwaminifu hata mmoja.
Na hali ya kuishi enzi moja inatupelekea tuwe na subira ya kukubali maoni, na hivyo kutufanya tupambane zaidi na nafsi zetu ili tusiwatuhumu watu wa rika moja na wengine.
Na Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka}. [AN NAHAL 90]

Share this:

Related Fatwas