Machafuko na Machafuko ya Ubunifu

Egypt's Dar Al-Ifta

Machafuko na Machafuko ya Ubunifu

Question

 Kwa wakati huu wa sasa, ni kawaida kuzungumza juu ya machafuko na machafuko ya ubunifu, kwa hivyo, Waislamu wana maoni gani juu ya hilo?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Istilahi ya machafuko ya ubunifu ilianza kutumiwa katika nyanja ya kisiasa, istilahi hii ilitujia kutoka Magharibi kwa maneno ambayo hubeba dhana ambazo hatutambui kwa kina au mizizi yao au nadharia zilizoibuka kutokana nazo, na ni hali ambayo inawakilisha shida yetu ya kimawazo, nayo ni kinyume cha kile ambacho Abu Al-Hassan Al-Ash'ari alichoashiria aliyefariki mwaka (320 BH = 940 BK) katika kitabu chake kidogo “Istihsan Al-Khaudh Fi Elmil Kalam” (Kilichochapishwa katika Hyder abad Al-Dakn nchini India katika kurasa chache) ambamo anataja ndani yake jinsi mawazo yanayokuja – yaani ya kigiriki - yalivyoingizwa, kukita mizizi na kuweka kiwango cha kukubali na kujibu na kujua yanazofaa, na kwa hivyo walizidi kikomo cha fikra za kijinga, kwa fikra zilizoangaziwa, za kina, na hii inatukumbusha kile ambacho Waislamu wamekiita kwa uwiano wa duara ambalo tunafikia mzunguko wake na eneo lake, ambalo ni 7/22, ambapo waliiita “uwiano mzuri wa kimungu”. Kwa sababu Mungu ndiye aliyeumba uumbaji, aliumba uwiano huu wa ajabu na kuufanya uwe kila wakati katika miduara yote, kisha kuuelezea kuwa ni mzuri kunaongeza kiingilio cha kusoma usomaji wa ulimwengu, wakati istilahi ya kimagharibi ambayo ilitafsiriwa kwa Kiarabu cha kisasa wakati uigaji kamili ulikamilishwa ni “uwiano wa asili” na inaashiriwa na herufi ya (T).
Je! Vipi kuhusu istilahi ya kimagharibi ya machafuko na ile ambayo ina maana hiyo hiyo kwa Imam Al-Ash’ari (R.A) wakati alipoangalia mkusanyiko wa maarifa ambao mwanadamu aliupata kutokana na kuusoma Ulimwengu unaomzunguka.
1- Neno hilo linaashiria nadharia moja ya kisasa, ambayo inashughulika na uchunguzi wa sheria zilizofichwa ambazo zinatawala mazingira ya nasibu katika sura yake, ambayo imeenea katika ulimwengu. Ambapo nadharia hiyo ilipata umaarufu mkubwa kwa kuitumia katika riwaya nyingi na filamu kama vile Michael Crichton's "Bustani ya Dinosaur" mnamo 1990, iliyoongozwa na Steven Asplberg, na matukio ya filamu hii inaeleza jaribio la mwanasayansi mmoja kuiga kwa jeni ya dinosaurs ili kuwaonesha umma katika bustani ya umma. Na hadithi ya "Sauti ya Ngurumo", ambayo iligeuzwa sinema mnamo 2004 na inategemea nadharia ya machafuko, ambayo miongoni mwa misingi yake ni kwamba mabadiliko yoyote machache mwanzoni mwa jambo yatabadilika kuwa tofauti kubwa isiyotarajiwa mwishowe, Kwa kiwango ambacho hewa inayozalishwa na mabawa ya kipepeo katika Mashariki inaweza kusababisha kimbunga kikubwa katika Magharibi, nayo ni nadharia ambayo ilionekana na mtaalamu wa hesabu wa Ufaransa Henri Bonneker alipojaribu kutatua shida ya “Mwendo wa Miili Mitatu katika Fremu Moja ya Uvutano”, shida ya kimahesabu ambayo haikuwa na suluhisho kwa karne mbili, na hiyo ilikuwa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Licha ya hivyo, Wataalamu hawakufanikiwa kuelezea matukio mengi ingawa wamekusanya habari nyingi ambazo hawakuweza kuziunganisha kwa upande mmoja, na kutoweza kwao kutabiri mkondo wake wa baadaye na kwa sheria wazi kwa upande mwingine, hali ambayo iliwafanya kuliita neno bila mpangilio.
2- Hali iliendelea hadi nusu ya pili ya karne ya ishirini, wakati maono yalipoanza kutofautiana kati ya wasomi wengi, hakika ikawafikia ya kutokuwa na uwezo wa sheria ya kawaida kuelezea mambo mengi yanayowazunguka, na labda jambo muhimu zaidi ni ukuaji wa kibaolojia kwa idadi ya watu ambayo nadharia zote za kisasa zimeshindwa kutabiri kiwango cha ukuaji wake. Kompyuta ni zana ya ukuzaji na uenezaji wa madhehebu hii wakati wa nusu ya pili ya karne ya ishirini, haswa kupitia mfumo wake wa hesabu baada ya hali ya fizikia ilibaki kuwa kubwa katika nusu ya kwanza ya karne hii.
Mwanzo halisi wa mabadiliko haya ni ugunduzi wa "Edward Lorenz", mtaalamu wa hali ya hewa wa Marekani, ambaye aligundua, kwa bahati, kiwango cha ubadilikaji katika utabiri wa hali ya hewa, haswa kasi ya upepo. Mnamo 1961, "Lorenz" alitaka kuhakikishia data kadhaa juu ya utabiri wake wa hali ya hewa, na kwa kuhifadhi muda, alianza mchakato wa hesabu kutoka katikati, kwa kuingiza nambari sawa na hesabu anayohesabu, lakini aliingiza nambari hadi tarakimu tatu za desimali, na akakuta matokeo ni tofauti kabisa, na ingawa tofauti hii ilikuwa rahisi sana, kwani nambari aliyoingiza ilikuwa na nambari tatu za desimali, wakati kompyuta ilikuwa ikihesabu mchakato huu na nambari zenye sehemu tano za desimali. Lakini, "Lorenz "alikuja na nadharia inayosema: tofauti hizo rahisi zinaweza kusababisha matokeo tofauti sana ambayo yatazidisha tofauti zao wakati wowote kiwango cha uvumilivu wake kiliongezeka, na akatolea mfano wa hiyo: kwamba hewa iliyotengenezwa na mwendo wa mabawa ya seagull inaweza kubadilisha kabisa matarajio yetu ya zamani juu ya kasi ya upepo, na kisha akaendeleza mfano huu kwa mabawa ya kipepeo.
3- Madhehebu hii haikutumika katika riwaya tu, lakini pia iliongezwa hadi michezo ya video, ambapo michezo mingi ambayo inategemea yaliyomo kwenye nadharia hii, kama mchezo wa Tom Clancy Splinter Cell: The Chaos Theory na mchezo wa Sonic the Hedgehog. Mashine za umeme zilizo na jina la madhehebu kwa kufaidika na umaarufu wake mpana, kwa hivyo kampuni ya Marekani ya Goldstar iliyobobea katika utengenezaji wa vifaa vya umeme kwa kuzalisha mashine za kufua za machafuko mnamo 1993 AD, ambayo ni uzalishaji wa kwanza ulimwenguni uliotengenezwa kulingana na nadharia hiyo ya machafuko, ambayo inajulikana na uwepo wa kifaa kidogo husaidia kusonga maji ambayo huinuka na kuanguka bila mpangilio baada ya kuhamishwa na kifaa cha kimsingi, hali ambayo husaidia kutoa nguo safi, na ingawa ilipingwa kwamba inasababisha nguo kuchakaa haraka zaidi.
4- Kisha nadharia ya machafuko ikahama kutoka fizikia kwenda hali ya hewa kisha Hisa na kisha siasa, na kuathiri madhehebu ya sanaa, muziki na fasihi. Nadharia hii inarudia yale ambayo yametulia katika maarifa yao ya jadi kutoka umuhimu wa sababu, yaani uhusiano ambao ni kati ya sababu na anayesababisha, hali ambayo Al-Ash'ari na Wasunni walikataa na kusema: Kuna uhusiano kati ya sababu na anayesababisha, na kwamba Mwenyezi Mungu huumba anayesababisha pamoja na sababu yenyewe siyo kwake, na hii ilikuwa chini ya sheria kadhaa muhimu ambazo zinapaswa kutajwa wakati wa kulinganisha kati ya mfano wa kimaarifa wa kiislamu na mfano mwingine. Kwa Waislamu: {Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.} [YUSUF; 76]).
Mwenyezi Mungu anasema pia: {Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.} [AL-ISRAA: 85]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.} [AN-NUUR: 45]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.} [AR-RAHMAAN: 29]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo.} [HUUD: 107]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi (14) Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu (15) Atendaye ayatakayo.(16)} [AL-BURUJ: 14-16]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo.} [ALl-ANBYAA: 23]. Nadharia ya kudhalilisha kwa mkabala ya nadharia ya utawala kati ya kauli yake Mwenyezi Mungu: {Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.} [YUNUS: 24] Na Mwenyezi Mungu anasema pia: {Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi,na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili.} [AN-NAHL: 12].
5- Hali hii, ambayo kwanza waliielezea kuwa iko chini ya sheria za uamuzi ambazo hazirudi nyuma kabisa, zilipingana na mengi ya yale waliyoyaona baada ya hapo katika ulimwengu, na usemi wa uamuzi ulikuwa kinyume na imani ya Waislamu ambayo ilielezewa wakati huo kama ushirikina na kurudi nyuma, na sasa wanasema: Ikiwa tukipiga picha ulimwengu huu mkubwa; Sheria zilizopangwa zinatusaidia tu kuelewa ni nini kilicho katika sehemu ya mwisho ya mkia wake, wakati ambapo madhehebu ya machafuko inatusaidia kuelewa na kutambua mengine, hali ambayo inaweza kutafsirika kisayansi kwa ukweli muhimu ambayo ni: kwamba mazingira yaliyopangwa katika ulimwengu sio ya kawaida sana yakilinganishwa na mazingira ya kubahatisha, hali ambayo inapingana na nadharia za zamani za maarifa ambazo zinasisitiza kuwa ulimwengu katika asili yake ni mazingira yaliyopangwa na yanayosimamiwa na sheria kali zisizobadilika.
Hii ni kukubali kutokuamua, lakini katika wakati huo huo - kwa hamu isiyozuiliwa ya kutawala ulimwengu na sio kufaidika nayo tu na kuweka kando suala la uungu na uumbaji - unawaona wanaelezea kile wanachokiona kama ni hali ya kubahatisha.
Ama kuhusu sheria ambazo tumezitaja, zinaona vitu jinsi ilivyo, na zinaona hekima ya Mwenyezi Mungu nyuma ya kila kitu, kuna mfumo thabiti, na kuna utofauti uliowekwa mapema na Mwenyezi Mungu, na utofauti huu nyuma yake ni hekima, na huu ni mkanganyiko ambao tunauona katika maneno yao, mara wanapoielezea kama ni bahati, wakati mwingine wanayaelezea machafuko, na mara nyingine kuna Sheria inayosababisha bahati na machafuko. Ikiwa utafiti uliendelea chini ya sheria zilizopita na kuchagua maneno yake, utafikia zaidi ya maarifa ya siri za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wake uliodhalilishwa kwa wanadamu.
6- "Chuck Palahniuk", ambaye ni mwandishi wa riwaya wa Marekani, aliyezaliwa mnamo 1961, anasema: “Istilahi tunayoita machafuko ni kweli, mfumo mpya ambao hatuujui, na istilahi tunayoita jina la bahati pia ni mfumo mwingine ambao hatujafaulu kuufafanua.Tusichoelewa tunaita maneno matupu, na ile ambayo hatuwezi kuisoma tunaiita soga, na ukweli ni kwamba hakuna uwezo huru, hakuna utofauti, bali kuna tu jambo lisiloepukika”. Keri Thornley, mwanzilishi wa Dini ya Machafuko (1938-1998), anasema: "Tunachofikiria mfumo ni aina ya machafuko."
Sababu ya ukinzani huu ni ukosefu wa nia ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja na utambuzi kwamba ulimwengu umeumbwa, hali ambayo imekuwa ikitokea kwa mamia ya miaka, bali maelfu ya miaka. Je! Uwiano ni wa kimungu au wa kiasili? Je! Kile tunachokiona karibu na sisi ni machafuko au utofauti?
Kwa hali yoyote, neno la machafuko lina maana hasi kutoka maana ya upotezaji, kuchanganyikiwa, na mgongano. Kwa hivyo, tunaona baadhi yao wakijaribu kutofautisha kati ya neno machafuko, ambalo linamaanisha kwake kitu cha uhuru, na maana hizi, lakini istilahi na athari ya neno akilini mwa wale wanaolisikiliza - ina umuhimu mkubwa hata katika kupitisha maoni na madhehebu. Dhana hii ya kupoteza na kuchanganyikiwa haiwezi kutengwa na neno machafuko.
7. Padre Dave Fleming – ambaye ni kiongozi anayefanya kazi katika Kanisa la Jumuiya ya Kikristo huko mjini Pittsburgh, Pennsylvania, katika makala yake amegundua mawazo matano muhimu ya kuleta ufanisi na afya - anaona kinyume cha hii, akisema: "Hii ni mbaya kabisa; kuna tofauti kubwa kati ya machafuko na mkanganyiko." Padri Fleming alimtaka msomaji aondoe mawazo haya mabaya na afanye uhusiano mpya akiwa mtawala au mtawaliwa kwa neno la machafuko, na akaongeza: "Biblia inatuthibitishia sisi kwamba Ulimwengu uliumbwa kutokana na machafuko na kwamba Mola wetu alichagua machafuko kuunda Ulimwengu kutokana nayo, ingawa sisi tuna ukosefu wa kujua jinsi jambo hili lilivyo, hata hivyo, tuna hakika kuwa machafuko yalikuwa hatua muhimu katika mchakato wa uumbaji, na akaongeza kwamba: "Tatizo halisi haliko katika machafuko yenyewe, lakini kwa majibu ya watawala na serikali juu yake, ambayo yanasababisha kile tunachokiona cha matokeo mabaya”. Alisisitiza kwamba kuondoa machafuko hakutaleta utulivu kamwe, ambao unatokana tu na ubunifu, ambao pia huibuka kutokana na machafuko, na ikiwa tutatumia neno hili ili tushikamane na hofu zetu na kufeli kwetu, lazima tuwe na kiwango cha ujasiri ili kukabiliana na jambo hili.
Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa utawala na mpango ni adui wa kwanza wa ubunifu wa kibinadamu. Kwa hivyo, watawala wa enzi hii watagundua haraka kuwa machafuko ni silaha bora ya utulivu wa milele wa jamii zao.
8- Tunaona mkanganyiko huu ambao unachanganya ukweli na uwongo na ukweli na udanganyifu katika maneno ya Judi Neal (ambaye shahada yake ya uzamifu (Ph.D.) kutoka Chuo Kikuu cha Yale katika elimu ya Tabia ya Taasisi na sasa ni mkuu wa Kituo cha Kuhamasisha Kutenda katika Chuo Kikuu cha New Haven) vile vile Puran Perez katika Utangulizi wa kitabu chao “Jinsi ya Kukabiliana na Machafuko” ambapo imetajwa ndani yake: “Ushahidi wote unaashiria uwepo wa mfumo uliofichwa katika mazingira ya bahati ambayo yanategemea katika kiini chake juu ya sheria za maumbile. Waliongeza: “Hakika machafuko na bahati katika asili ni matukio ya kawaida na moja ya hatua za mchakato wa maendeleo katika historia ya mwanadamu. Mabadiliko ya mtu binafsi na ya taasisi yanaweza tu kutokea kupitia machafuko haya, ambayo kawaida hutoa mifumo mingi mipya na maana zenye ubunifu."
Ndio maana walisisitiza umuhimu wa kuelewa utaratibu uliofichwa wa mazingira haya na uwezekano wao tofauti, ambao utasababisha kupatikana kwetu kwa uwezo wa kupanda wimbi la maendeleo na ukuaji katika viwango vya mtu na vya taasisi. Kurasa zilizobaki katika kitabu hicho ni kuwasilisha kanuni za jumla za nadharia ya machafuko na jinsi ya kukabiliana nayo katika maisha halisi. Kitabu hicho kilitubainishia shida ya kifikra ambayo taifa la Kiislamu linapitia, kwa hivyo halikufikiria na halikutoa maoni yake kwa istilahi sahihi, wala halikusoma, kuchagua na kushiriki na watu katika kile kinachoendelea karibu nasi kwa maoni na mawazo, na hii inatukumbusha mwandishi wa Abu Al-Hasan An-Nadwi - RA- “Ulimwengu umepoteza nini? Pamoja na kushuka kwa Waislamu.”
9- Kama Martin Carruthers – ambaye ni mwanzilishi wa dhehebu jipya la tiba ya kisaikolojia anayejulikana kama Soulwork - alithibitisha kupitia tovuti yake ya mtandao wa Internet www.Soulwork.net, ambapo anasema chini ya kichwa "Machafuko, Mafunzo na Matibabu": “Hakika machafuko ni moja ya mambo ambayo ni muhimu katika mafunzo na matibabu ya kisaikolojia, nafsi inapofikia ukingoni mwa machafuko - halafu mtu hupoteza udhibiti na sheria zake zote - basi miujiza inaweza kutokea."
Lakini kusubiri miujiza bila kufanya chochote hakutatuongoza kwa chochote, kwani kuondoa sheria za zamani kunaweza kumpa mtu fursa ya kuona maisha kutokana na mtazamo mpya. Halafu, anaweza kuunda Utambulisho mipya, maadili ya ubunifu na dhana za kisasa ambazo zitamsaidia kukuza mazingira yanayomzunguka na kumrudisha kwenye mfumo.
10- Hii inatupeleka kwenye suala la ubaguzi, ambapo kila mtu anapendelea itikadi na maono yake kwa ujumla, na hii inatukumbusha juu ya hali ya kujuana kikabila ambayo tumetaja hapo awali, na juu ya suala la ubaguzi, Mkutano ulifanyika Cairo mnamo 1992 BK ulioandaliwa na Dk. Abdel-Wahab Al-Messiri na Taasisi ya Kimataifa ya Mawazo ya Kiislamu, na ulipelekea kuandikwa juzuu saba za utafiti juu ya ubaguzi katika nyanja mbalimbali, ambapo Juzuu hizo zilichapishwa na Dar Al-Shorouk, lakini kuna msomaji au mtu yoyote anayejibu?!
11- Tuna maono kamili ambayo yanaona kwamba Ulimwengu uliumbwa na Muumba mwenye busara. Kwa sababu ulidhalilishwa kwa wanadamu, na kwamba ujuzi wa mwanadamu ulikuwa mdogo, na aliamriwa ajitahidi katika Ulimwengu huu ili kuugundua. Kwa sababu anao uwezo huu {Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima (32) Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha?} (AL-BAQARAH: 32-33), na kwamba hakuna mwisho kwa kugundua, mapungufu ya kisayansi yanahimiza kuendelea, na kwamba Mwenyezi Mungu Atendaye ayatakayo, na ana uwezo wa kila kitu, hali ambayo ni mahojiano ya nadharia ya machafuko na utawala wa Ulimwengu, nafasi, bahati, kuepukika, na kuondolewa kwa Mungu, je, kuna anayefahamu hivyo?!
Kwa hivyo, inawezekana kufaidika na nadharia ya "machafuko ya ubunifu" ikiwa tunaichukulia kama utofauti wa ubunifu ambao unaficha mfumo ambao unaweza kufunuliwa, kwa hivyo haufanani na mashine ya kufua kwa fujo ambayo hufua nguo nyeupe zaidi mpaka kitambaa huchakaa, na kwa upande wetu kitambaa cha jamii, kitambulisho, uwepo na uhai, na wakati huo huo tunatafuta kugundua ubunifu ambao unawakilisha matumizi ya nguvu inayokuwepo na hauwakilishi ukosefu wa adabu kwa kisingizio kwamba machafuko ni mfumo wa ulimwengu, au kama Jim Morrison anavyosema: “Ninajali chochote kinachohusiana na mapinduzi, utaratibu na machafuko, haswa shughuli ambazo hazina maana yoyote. Hii, naamini, ndiyo njia ya moja kwa moja ya uhuru.” Yeye ni mmoja wa mwimbaji maarufu wa Rock wa Marekani na watu walimkuta ameuawa bafuni huko Paris. Njia hii ni ya chini sana na yenye sauti kidogo hadi sasa, lakini ni moja ya wito wa enzi mpya, ambao watu wenye busara bado wanakataa licha ya matamanio yaliyomo.
Rejea: Kitabu cha: [Simaat Al-Asr, cha Mufti Mkuu wa Misri, Dk Ali Jumaa].

Share this:

Related Fatwas