Watu Wenye Busara – Maana Yake
Question
Tunasikia mengi matumizi ya neno la (Watu wenye Busara), Je ni nini maana yake na sifa zake hasa katika fikra za Kiislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Maana halisi ya Wenye Busara tunaiona katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na katika Sunna na katika hekima za watu na uhalisia wao. Lakini hukumbwa na baadhi ya vumi zinazokuja baada ya Usasa katika zama hizi, kwa wengi kukataa, na kuwepo majaribio makubwa ya kuvunjavunja na kung'oa kabisa kutoka mawazo mwa watu na uhalisia wao.
Na mwelekeo huu hautegemei zoezi lolote la kibinadamu lililotulizana, na wanalingania kitu kipya amabacho hatuzijui sifa zake au njia itakayotupelekea, na matokeo yake au matatizo yapi yatakayotukuta ambayo yanafungamana nacho. Na hivyo ni kwa kuwa inakwenda kinyume na Utaratibu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Ulimwengu wake, kutokana na kwamba yeye amezifanya zama kuwa bora zaidi kuliko nyingine. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya mahali kuwa bora zaidi kuliko pengine, na amefanya watu kuwa baora zaidi kuliko wengine, na amezifanya hali kuwa bora zaidi kuliko nyingine, na akajaalia utofauti ni sababu ya kuwashinikiza watu, na kujuana kwao, na kuijenga ardhi, na , na harakati zao kupitia we historia.
Na kuliangamiza kundi la wasomi wenye busara na kulingania uwepo wa usawa usio na mipaka kunaweza kuwa na maangamizi ndani ya ulimwengu, na kuna matini nyingi ambazo zinaweza kuwa msingi wa maana hiyo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda}. [AL -MUJAADILA;11]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu yawengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisemanao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao waliokufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo}. [AL- BAQARAH - 253]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, namt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Namkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema}. [AN-NISAA - 59]
Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia watu wawe viongozi, na akajaalia hivyo kutokana na uwezo wao wa kufanya kazi na utashi wao wa kuleta marekebesho bila ya kuleta ufisadi, lakini tunasisitiza zaidi hatari ya mawazo hayo ambayo watu wote watakuwa sawasawa na kutolingana kamwe:
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayoendeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yoteni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake}. [AR-RA`D - 31]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia Yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu}. [AL- HAJJ- 40]
Na kutokuwa sawasawa hakumaanishi kamwe kutokuwa na usawa, Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni}. [AN- NISAA - 1]
Na Mtume S.A.W. amesema; "Watu wako kama meno ya kitana"
Na Mtume S.A.W. akasema: "Enyi watu, tambueni kwamba Mola wenu ni Mmoja, na hakika baba yenu ni mmoja, hakuna ubora wa mwarabu dhidi ya mwajemi, au mwajemi dhidi ya mwarabu, au mwekundu dhidi ya mweusi, wala mweusi dhidi ya mwekundu, isipokuwa kwa Uchamungu"
Na uwepo wa wasomi wenye busara unapelekea utatuzi wa matatizo mengi, na kuleta usalama na utulivu kwa watu wote, na fitina zinazotokea baina ya nyakati na nyingine zinahitaji wasomi kuingilia kati na kuzisitisha, na kupotoka kunakoendelea kupitia vyombo vya habari vya Satalaiti iwe katika nyanja za kutoa Fatwa au vipindi mbali mbali vya kidini kwa upande mwingine, au ufisadi ulikuwepo wa wazi kwa upande wa pili, uwezekano wa kutatulia jambo hili na baraza la wasomi wenye busara. Isipokuwa sisi tunaona mashambulizi makali mno yasiyomtenga yeyote miongoni mwa Wamisri na viongozi wao. Mweleko huo unaotaka kung'oa wasomi wa Misri na kuwafyeka wasiwepo, unafuata hali isiyoeleweka na kutojua kwamba wasomi wakitoweka basi usalama, utulivu na maendeleo yataondoka nao, na kupelekea mzubao na magongano.
Na tunatamani kwa wale wenye kuvunjavunja alama za Wamisri wangezungumza ukweli, au wazungumze kuhusu kutafuta ukweli, bali wao wanazungumza kwa njia ya kitoto, wanatengeneza matukio katika mazungumzo yao, na wanazua kutoka akilini mwao mawazo wanayojaribu kuyaamini, na Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Muslim katika utangulizi wa kitabu chake cha: [Sahihu Muslim] amesema: "Inamtosha mtu kuwa mwongo pale anapozungumzia kila anachokisikia".
Na hawa wanaongeza zaidi uongo mpaka wanayageuza yale wayawazayo bila ya kusikia habari zozote za kuaminika, na kuelekea katika mawazo ya kufikirika wanayoishi ndani yake wakidhani kuwa ndio ukweli wenyewe, watu hawa; maneno ya Mtume S.A.W. yanazungumzia ukweli wao ambapo amesema: "Mtu anaendelea kusema uongo na anaupenda uongo huo mpaka anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni Mwongo".
Na angalia neno la (anachunguza uongo) kwa maana ya kupendelea uongo, na kuufuatilia na kuuanzisha, kwa hiyo, sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi tutarejea kwake, ewe Mola wetu tuokoa na janga hili tulilonalo. Na Mtume S.A.W. amesema: "Hakika mmoja wenu atazungumza kwa neno la kuchukiza kwa Mwenyezi Mungu na hadhani kuwa litafikia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwandikia kumkasirikia kwake mpaka ya siku ya kukutana naye". Na katika tamko la Al Bukhari "Litakalompelekea motoni kwa umbali wa Mashariki na Magharibi. Na hali hiyo ni kutokana na uovo na madhara kwa mtu mmoja mmoja ndani yake na watu wote.
Na kuwepo kwa Viongozi hawa na kuwalinda – bali Kuwaondosha madarakani viongozi waliokiuka maadili ya kazi miongoni mwao, kwa ajili ya kutimiza kauli ya Mtume S.A.W: "waondosheni madarakani, viongozi waliokiuka maadili ya kazi," – Ndicho kinachosimuliwa na Al Afwah Aloodiy katika Kasida yake, anasema:
Watu hawawezi kuurekebisha mvurugiko kama hawatakuwa na watu wazuri, na hawawezi kuwa na watu wema iwapo wataongozwa na wajinga wao.
Na Vigogo wema wa watu wanapotawala mambo ya watu, kwa utawala wao mambo ya watu hao humea na kukua zaidi.
Na maelekezo ya Qur`ani na Sunna na Hekima za Mashairi vyote vinasimulia uhalisia wa maisha usiokimbilika na utiifu kwa mambo haya ni aina ya hekima. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Yeye humpa hekima amtakaye; na aliye pewa hekima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili}. [AL- BAQARAH 269]
Na bila ya hayo inasadikika kauli ya Al Afwah Al Audiy katika shairi lenyewe:
Inakuwaje kwa mwenye kufuata Njia sahihi utakapo kuwa miongoni mwa watu, wanaowabana wazuri na kuwafunga?
Kwa hiyo, Watu wenye busara ndio waonao mambo halisi, kwa mfano mtu ambaye anataka kuchochea fitna na wala hajasoma katika Dini yake anayoiamini, Kauli ya Isa Bin Maryam iliyomo ndani ya Injili ya Matayo, Sehemu ya tano, 34-84: "Mlisikilizia kuwa ilisemekana unampenda ndugu yako na unamchukia adui wako", Lakini mimi nawasemea muwapende maadui wenu, muwabariki wanaokulaanini, fanya uzuri kwa wanaokuchezeeni, na mswali kwa ajili ya ambao wanafanya ubaya kwenu na wanakufukuzeni.
Ili Muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni, Jua lake huchomoza kwa wabaya na wema, na mvua yake hunyeesha kwa wema na wadhalimu, kwa kuwa mambo yalivyo ikiwa mtawapenda wao wanaokupendeni basi je, ni ujira gani mlionao? Je, watoza ushuru pia wanafanya hivyo? Na mkisalimiana na ndugu zenu tu, basi nyinyi mna sifa gani nzuri? Je, watoza ushuru pia wanafanya hivyo? Basi kuweni nyinyi mmekamilika kama alivyo baba yenu aliye mbinguni ambaye amekamilika.
Na hayo ni unukulu muhimu, Uislamu umeyaunga mkono, aliposema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada yakuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani yanafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu (109). Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazojitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya}.[Al-Baqara 109/110]
Na Uislamu uliyaunga mkono ambapo umewaelezea watu hawa wasioutekelea, bali wanaobadilisha nasaha hizi na mafunzo haya kwa kukebehe, kudharau na kwa kuwachezea shere wengine.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.(29) Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. (30) Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. (31) Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. (32) Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. (33) Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri. (34) Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.(35) Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwawakiyatenda? (36) [AL-MUTWAFIFIN 29-36]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anajaalia kuhesabiwa na kuchukuliwa haki na kuzungumza kuwe Akhera, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka ndiye aliyeiteremsha Qur'ani Tukufu lazima iwe kwa walimwengu wote ni onyo, na hili lieleweke kwa wote, na lisiishie kwa baadhi ya watu maalumu au viongozi tu, bali liwe ni mfumo wa maisha, ili mambo haya ya kipuuzi yasikariri tena, na yanyamaziwe milele.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: ni Kitabu cha Sifa za Zama, cha Mheshemiwa Mufti wa Misri Dkt. Ali Juma.