Muda Mrefu zaidi wa Ujauzito kwa W...

Egypt's Dar Al-Ifta

Muda Mrefu zaidi wa Ujauzito kwa Wanachuoni

Question

Ni muda upi mrefu zaidi wa ujauzito kutokana na maoni ya wanavyuoni?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanachuoni wa Fiqhi wakiwemo Wanachuoni wanne wamepitisha muda wa ujauzito wa zaidi ya miezi tisa, kukiwa na tofauti kati yao kwa upande wa muda wa mwisho kabisa na ambao tumeuteua katika Fatwa ni ule waliousema Wanachuoni wafuasi wa Imamu Shafi na Imamu Hanbal nayo ni moja ya kauli mbili iliyopokelewa na Imamu Malik( ) muda wa mwisho wa ujauzito ni miaka minne.
Na dalili ya hili ni ufuatiliaji, na ufuatiliaji unakuwa ni dalili katika masuala kama haya, kwa sababu hakuna andiko linaloainisha na kuwa kuainisha kwake kumeegemezewa uwepo ambao unafahamika kwa ufuatiliaji( ).
Amesema Ibn Khuweiz Min’dad: Muda mdogo wa hedhi na nifasi na muda wa ziada, na muda mdogo wa ujauzito na muda wa ziada ni wenye kuchukuliwa kwa njia ya jitihada, kwa sababu elimu ya hilo Mwenyezi Mungu Ameifanya ni maalumu kwake, hivyo wala haifai kuhukumu kitu kinachohusu kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa kiwango kile alichotuonesha, wala hatujapata kusikia mwanamke ameshika ujauzito wa miaka minne miaka mitano tukahukumu kwa kigezo hiko, na nifasi pamoja na hedhi hatujapata mwanamke wa kigezo katika hali ya mara chache kutokea miongoni mwao( ).
Imewahi kutokea katika historia uwepo wa ujauzito uliodumu kwa kipindi cha miaka minne, kutokana na hilo imepokelewa na Baihaqy kuwa Walid Ibn Musallam amesema: Nilimwambia Malik Ibn Anas kuwa: Mimi nimezungumza na Bi. Aisha R.A na amesema: “Hauzidi muda wa ujauzito wa mwanamke zaidi ya miaka miwili, akasema: Ametakasika Mwenyezi Mungu mwenye kusema haya!! Huyu jirani yetu mke wa Muhammad Ibn Ajlaan ni mwanamke mkweli na mume wake ni mtu mkweli ni mwanamke aliyeshika ujauzito mara tatu ndani ya kipindi cha miaka kumi na mbili na kila ujauzito ulichukuwa miaka minne( ).
Amesema Mubarak Ibn Mujahid: Ni mtu maarufu kwetu, mke wa Muhammad Ibn Ajlaan alishika ujauzito wa miaka minne na kujifungua, na alikuwa akiitwa mbeba tembo( ).
Amesema Ally Ibn Zaidi Al-Qurashiy alinionesha Saidi Ibn Al-Musayyib mtu mmoja na akasema: “Baba wa huyu alipotea kwa mama yake huyu kwa muda wa miaka minne, kisha akawa amejifungua huyu mtoto akiwa na meno manne mawili juu na mawili chini”( ).
Kuna mtu mmoja alimwambia Malik Ibn Dinar: “Ewe baba Yahya mwombee dua mwanamke mjamzito tokea miaka minne akiwa kwenye mateso makali, akamwombea, akaja mtu na kusema: Muwahi mke wako, yule mtu akaenda haraka kisha akaja akiwa na mtoto wa aliyekaa miaka minne ya ujauzito akiwa na meno yake kamili”( ).
Na Muhammad Ibn Abdillah Ibn Al-Hassan Ibn Al-Hassan Ibn Ally alibakia tumboni mwa mama yake miaka minne, vilevile Ibrahim Ibn Najih Al-Uqaily, amehadithia hilo Abul-Khattab Al-Kaludhany katika watu wa Imamu Hanbal( ). Na Harima Ibn Hayyan alishika ujauzito wa miaka minne kwa sababu hiyo ndio maana ameitwa Harima( ).
Imepokelewa pia hali zilizozidia muda wa ujauzito kwa zaidi ya miezi tisa na chini ya miaka minne, kwani amenukuu Fatiyyah kuwa Dhihhak Ibn Muzahim alizaliwa akiwa ni mtoto wa miezi kumi na sita na akasema: “Amenizaa mama yangu akiwa amenibeba kwenye tumbo lake miaka miwili, kisha akanizaa nikiwa nimeota meno”, na Shuuba Ibn Hajjaj alizaliwa kwa ujauzito wa miaka miwili.
Amesema Al-Waqidy: Nimewasikia wanawake wa watu wa Jihaaf wakisema: Hakuna mwanamke miongoni mwetu aliyebeba ujauzito chini ya miezi thelathini( ).
Hili likithibiti uwepo wake basi lazima lichukuliwe hukumu bila ya kuzidisha kwani haujapatikana muda zaidi ya huo, Omari amepigiwa mfano wa kuwa mbali na mkewe kwa muda wa miaka minne, mwanamke mmoja alipeleka malalamiko kwa Omar kuhusu mume wake ameondoka miaka miwili aliporudi mume alimkuta mkewe ana ujauzito, Omar akafahamu anastahiki kupigwa mawe huyu mwanamke kwa uzinifu, ndipo aliposema Muadh Ibn Jabal: “Ewe Amiri wa Waumini kuna njia yoyote kwako juu yake kwani hakuna njia kwako kuhusu kilichopo tumboni, Omar akamwacha mpaka alipojifungua mtoto wa kiume - akiwa ameota meno - ndipo alipofahamu mume wake kwa kufanana naye, akasema Umar: “Wanawake wameshindwa kuzaa mfano wa alivyoshindwa Muadh, bila ya Muadh basi Omar angeangamia”( ). Imepokelewa kwa Uthman na Ali pamoja na wengine. Ikiwa litathibiti hili basi mwanamke pindi anapojifungua kwa ujauzito wa miaka minne au chini kidogo ya muda huo kuanzia siku aliyofariki mume au kuachika na wala hakuolewa wala kuingiliwa wala eda yake kwisha wala kuzaa basi mtoto anakuwa ni wa mume, na eda yake inakuwa imekwisha kwa kuzaa kwake.
Ikiwa patasemwa kuwa utaalamu wa tiba ya kisasa haujazungumzia chochote kuhusu kufikia ujauzito muda huu, tunasema: Jambo ambalo linalazimisha tiba ya sasa ni ujauzito unaovuka miezi kumi basi daktari huufanyia upasuaji hivyo hukuna la kushangaza kukosekana uwepo wa mifano ya ujauzito kama hii ya muda mrefu.
Katika maelezo muhimu kwenye Fatwa yetu tunatoa wito wa kutenganisha hukumu, na kutenganisha hukumu ni fikra katika fikra ambazo zimebuniwa na akili ya Mwanafiqhi wa Kiislamu, na fikra hii inautekelezaji mwingi katika milango mingine ya Kifiqhi.
Sisi tunatoa wito kutekeleza fikra hii katika masuala haya, hivyo tunasema kumwambia daktari ambaye amefikiwa na hali ya mwanamke kuchelewa kujifungua: Fanya yaliyofikiwa na elimu ya majaribio, wala usimuingize mwanamke kwenye maangamizi kwa kuchelewa kujifungua, na ikiwa mwanamke atadai unasaba wa mtoto baada ya muda ambao umezingatiwa na sheria kuthibiti kwa nasaba hajauthibitisha Hakimu kwa sababu mwenye kazi ya kuhukumu ni kuwa muda mrefu zaidi wa ujauzito ni mwaka mmoja.
Hii ni kwa upande mmoja, ama upande mwingine ni kuwa huyu mwanamke ambaye amejifungua baada ya kuachwa na mume wake kwa chini ya muda wa miaka minne wala hatuhumiwi uzinifu, na hilo ni kutokana na hali hii ambayo imeelezewa na Imamu Shafiy na wengine,na ambayo imepelekea Wanachuoni wanaipa nguvu kuwa kipindi hiki ndio kipindi kirefu zaidi cha ujauzito, kwani kunakuwepo hali ya shaka uwezekano wa kuwa huyu mwanamke ni wa hali ya pekee sana au mara chache kutokea hivyo anaondokewa na tuhuma pamoja na dhabu, kwa sababu adhabu ya uzinifu huondoka kwa kuwepo shaka na tahadhari ni lazima katika mambo ya uzinzi na umwagaji damu, hii ndio fikra safi na bora ambayo bado haijafikiwa na watu wengi.
Ameashiria Imam Ezz Ad-Din Ibn Abdulsalaam sehemu ya hiyo katika kanuni zake na akasema: “Ikiwa mke atakuja na mtoto wa ujauzito wa chini ya miaka minne tokea kuachika kwake na kumalizika kwa eda yake, basi huyo mtoto ana nasibishwa na mume pamoja na kuwa mara nyingi mtoto huwa hachelewi kwenye muda huu, ikiwa itasemwa: Amenasibishwa na huyo baba kwa sababu asili ni kukosekana kwa uzinifu na kutoingiliwa kwa kutenzwa nguvu, tunasema: Kutokea uzinifu ndio zaidi kuliko kuchelewa kwa ujauzito kwa miaka minne, vilevile kutenzwa nguvu na kuingiliwa kwenye kuleta shaka, wala hali hiyo hailazimu kutendewa adhabu kali ya uzinifu, kwani adhabu za uzinifu huondoka kwa uwepo wa hali ya shaka, tofauti na uwepo wa nasaba kwani ndani yake kuna uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kupitisha haki za mirathi, pia wajibu wa huduma za chakula mavazi makazi na malezi kwa ujumla( ).
Ama yaliyoletwa na wapingaji wa Fatwa hii kuwa, Fatwa imebainisha misingi dhaifu, nayo ni Jitihada za Wanachuoni wa zamani wala hakuna ushahidi unaozingatiwa, kwa sababu Fatwa inabainisha dalili si ya Qur`ani wala Hadithi, bali ni hali tu zilizopatikana na kufasiriwa, huenda tafasiri hii kielimu na kisayansi ikawa ni yenye makosa, kwani hali hizo ni za zama ambazo hapakuwa na vyombo na njia za vipimo zilizo sahihi, yenyewe ni dalili ya kidhana inayopingwa na uhalisia au uyakini, watu waliopokea kisa cha mke wa Muhammad Ibn Ajlaan na ujauzito wake ulioishi miaka minne hawakuwa na njia za vipimo vinavyofahamika hivi sasa kama vyombo na vifaa vilivyoendelea vimekuwa na uwezo wa kufahamu jinsi ya mtoto aliye tumboni, umbile lake hali yake kiafya na tiba yake ya upasuaji hali ya kuwa akiwa bado yumo kwenye mfuko wa uzazi wa mama yake, na inawezekana kuwa maelezo yao haya ni makosa matupu kutokana na udhaifu wa uwezo wa kugundua ndani ya wakati wao huo.
Vilevile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliyosema: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} [AL AHQAAF: 15], inaonesha kuwa muda wa ujauzito pamoja na kumwachisha kunyonya ni miaka miwili na nusu, jambo ambalo haliwezekani pamoja nalo kuwa mimba ya miaka minne, na Wanachuoni wamekusanya Aya hii Tukufu na Aya nyingine ambayo inasema: {Na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili} [LUQMAAN: 14], wakachukua dalili kuwa muda mchache wa ujauzito ni miezi sita, kwa maana ya Aya imetoa hukumu ya Kisharia katika kadhia yenyewe ambayo ni kuainisha muda mchache wa ujauzito, ni katika mantiki pia kuifanya dalili ya muda wa mwisho pia.
Jibu la upingaji wa kwanza ni kuwa, hailazimishi uthibiti wa hukumu kuegemeshewa na Aya maalumu au Hadithi bali huenda chanzo chake kikawa ni hali halisi au uwepo wa kweli kama tulivyoelezea, na Fatwa hii haikujengea kwenye msingi dhaifu bali imejengewa juu ya ufuatiliaji halisi kama tulivyotaja, na maelezo ya Wanafiqhi kuhusu muda zaidi wa ujauzito unathibiti hata kwa hali moja, imeshatajwa mifano hai mingi na athari nyingi juu ya hilo, na kuzingatiwa hali hizi zilizopokelewa ni makosa yatokanayo na udhaifu wa vifaa vya kisayansi ni ujinga usio na dalili.
Ama Aya za Qur`ani zilizotajwa zenyewe hazioneshi isipokuwa muda mchache wa ujauzito, wala si dalili ya muda wa mwisho wa ujauzito, na kuwa Aya imetaja kwa uchache muda wa ujauzito basi hii sio dalili ya ulazima wa kutaja muda wa ziada ambapo hakuna mahusiano kati ya hili na hilo, inawezekana kufahamu Aya Tukufu kuwa ni kanuni ya wakati mwingi, kwa maana ujauzito mwingi wenye kuongezewa na unyonyeshaji unakuwa ni miezi thelathini kwa dalili kuwa mimba nyingi na kujifungua wakati mwingine unazidia hapo kwani mwenye kubeba ujauzito wa miezi tisa kisha akanyonyesha miaka miwili kama Alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, basi ujauzito wake na kuacha kunyonyesha kwake kunakuwa ni kipindi cha miezi thelathini na tatu na wala si miezi thelathini, hivyo Aya Tukufu kama lilivyokujia andiko inahusu muda mdogo wa ujauzito, hivi ndivyo ufahamu wake ulivyopokelewa na waja wema waliotangulia, wala hakuna uhusiano kabisa wa muda wa mwisho wa ujauzito.
Na Sharia Tukufu inapingamizi la mbali zaidi katika mambo ya tupu na umwagaji damu, ambapo imethibiti kuwa kuna hali moja hata kukiwa na hali milioni mia moja ya mwanamke kujifungua baada ya miaka minne, kwa sababu hali hii inaweza kuwa ndio ambayo ameielezea mfano wake Imamu Shafi na Imamu Malik na wengine miongoni mwa Wanachuoni Waislamu, miongoni mwa kanuni za dini hii ni kuwa inaondoa utekelezaji wa hukumu kwa uwepo wa shaka au kutokamilika ushahidi, ikiwa kutaonekana uwepo wa shaka au kutokamilika ushahidi hata kama ni kwa udhaifu kuwa huyu mwanamke hakufanya jambo la haramu basi sisi tunakuwa nyuma ya shaka hii ili kuepusha adhabu kwa huyu mwanamke.
Miongoni mwa ziada ya Sharia katika mambo ya tupu na umwagaji damu ni kuwa imetoa hukumu ya adhabu kwa mwenye kumsingizia Muislamu bila ya kuja na ubainifu wa usingiziaji huo, kwa sababu hiyo pia kumewekwa masharti ikiwa hakujakamilika ushahidi wa mtu juu ya uzinifu basi huyu mtu ataadhibiwa adhabu ya kusingizia kwa kushapwa viboko themanini.
Kisha Fatwa hii haimlazimishi mtu ambaye anashaka na tabia za mke wake na akawa amemuacha na mwanamke anataka kumnasibisha mtoto kwa huyu aliyekuwa mume wake kwa tamaa ya kitu chochote kile, kwa sababu huyu mwanamume ana uwezo wa kumkana huyu mwanamke mbele ya hakimu kwa njia inayofahamika, kama vile kuapa viapo vinne na mwanamke naye kuapa viapo vinne na anaapa kiapo cha tano kisha hakimu anaachanisha na kutenganisha kati ya wawili hao. Ikiwa msemaji atasema kuwa: Fatwa hii inafungua mlango kwa mwanamke ambaye hana maadili kumpa mwanamme unasaba kwa watoto wasiokuwa wake kwa utashi wake tu mwanamke?
Jibu kama tulivyosema: Fatwa imetenganisha kati ya uthibiti wa nasaba na uthibiti wa uzinifu, sheria ndio ambayo inahukumu nasaba ndani ya mwaka mmoja tu, lakini Fatwa haihalalishi kutuhumiwa huyu mwanamke na uzinifu, kwa sababu Sharia ni yenye kuchunga kuepusha adhabu kama tulivyotaja, na imethibiti kuwa kuna wanawake waliotokewa na hali hiyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi


Share this:

Related Fatwas