Hukumu ya Uuzaji kwa Kutazama Matan...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Uuzaji kwa Kutazama Matangazo Kwenye Mtandao.

Question

 Tumeona maswali mengi ambayo yalipokelewa kupitia vituo mbalimbali vya Fatwa kuuliza juu ya hukumu ya uuzaji kwa kupitia kutazama matangazo kwenye mtandao, na majibu yake yaliahirishwa hadi kukamilika kwa kufanya utafiti wake, yaliyomo kwenye maswali haya:
Baadhi ya kampuni hufanya kazi katika uwanja wa uuzaji kupitia mtandao wa habari wa kimataifa, na wazo la kazi yao linategemea matangazo na uuzaji kwa kutazama matangazo kwenye mtandao; Kampuni hizi zimetumia fursa kutokana tatizo linalozikabili kampuni zinazozalisha na kutangaza bidhaa; ambazo zimechwa kutazamwa na wanaolengwa kupitia matangazo ya runinga ingawa pesa nyingi hulipwa kwa utengenezaji na utangazaji wa matangazo haya, kwa hivyo kampuni hizi zilibuni wazo la uuzaji kupitia kampuni za biashara ambazo zinadhamini kiwango cha juu cha kutazamwa na kwa bei ya chini, ili watazamaji warudi na kutazama Matangazo, ambapo ilisababisha kupatikana kwa watazamaji wengi.
Matangazo hutazamwa kama ifuatavyo:
Kampuni hizi hukusanya pesa nyingi kufungua mkoba kwenye tovuti kwa mwaka, kwa mfano, na baada ya mwaka, mtazamaji lazima afanye upya, kwa hivyo kampuni inakodisha ofisi au tovuti kwa mtazamaji kwenye tovuti yake badala ya kiasi hiki, na mtazamaji hupewa nambari ya siri ili mtu mwingine yeyote asiweze kuingia kwenye tovuti yake. Kampuni inasambaza matangazo ambayo yameingizwa na wamiliki wao kutazama nambari maalumu na sawa kwa kila tovuti, na mtazamaji anapokea kiasi maalumu katika kurudi baada ya kudhibitisha utazamaji, na matangazo yanatumwa kwa siku maalumu kila wiki na lazima ayatazama mbele yake, na ikiwa hatayaangalia katika kipindi maalumu, hatapewa mshahara wowote, na anatakiwa kuingiza nambari baada ya kumalizika kwa tangazo ili kuhakikisha kuwa tangazo linaangaliwa ili kusudi linalotarajiwa lipatikane kwa kuhakikisha kiwango cha juu cha watazamaji, kwa kuzingatia kwamba matangazo haya ni yale yale yanayotangazwa kwenye vituo.
Pia, kila mtu anayejiandikisha na kutazama matangazo hupata mshahara maalumu kwa kila tangazo, na endapo mtu anayeshiriki ataleta watu wapya kushiriki, anastahili kamisheni juu yake kutoka kwa kampuni hiyo, na wakati mwingine kamisheni hii inajumuisha watu wengine ambao wameunganishwa naye juu yake katika mlolongo wa mtandao, mradi tu mizani ambayo inahitajika na Kampuni inatimizwa.
Baadhi ya kampuni hizi hazihitajiki kuleta watu kushiriki ili kuhakikisha kuwa atakuwa na mapato, na zingine zinahitaji hata kuleta angalau mshiriki mmoja.
Ni ipi hukumu ya Sheria katika shughuli hii?

Answer

 Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Imeamuliwa kuwa Fatwa hupitia hatua nne za kimsingi, ambazo ziko kwa mpangilio ufuatao: Sura ya asili, Hali ya tukio, na Dalili ya hukumu, kisha hatua ya kutoa Fatwa, na muhimu zaidi ya hatua hizi ni hatua ya Sura ya asili; Inajengwa juu yake kile kinachofuata, Hali ya tukio, Dalili ya hukumu, na Kutoa Fatwa; Sura sahihi ya uhalisia wa tukio linaloulizwa ni sharti la kutolewa kwa Fatwa, na wanazuoni walielezea hili kwa kusema: “Hukumu juu ya kitu ni sehemu ya asili”. Na sura ya asili kimsingi ni juu ya anayeuliza, lakini Mufti anachunguza kwa kuuliza juu ya njia nne ambazo uamuzi hutofautiana kulingana na tofauti zao, ambazo ni: Wakati, Mahali, Watu na hali, na pia anatakiwa kuhakikisha kwamba swali linahusiana na mtu binafsi, au kikundi au na Umma na Waislamu kwa jumla; Kwa kuwa umuhimu wa Fatwa unakwenda sambamba na ongezeko la janga la jumla.
Umuhimu wa sura ya tukio unakuwa muhimu zaidi ikiwa inahusiana na miamala mipya; Kama ilivyo katika uuzaji wa mtandaoni na uuzaji wa kihierarkia; Kwa sababu miamala hii ni migumu ambayo inahitaji kuzingatiwa zaidi.
Swali linalozungumziwa ni moja wapo ya miamala ya kisasa katika ulimwengu wa uuzaji, na hali halisi inatuonesha kuwa sio muamala wenye sura moja, bali una sura nyingi na maelezo tofauti. Ingawa imeunganishwa katika sifa zake kuu; Fatwa inaegemezwa juu ya hali halisi na maelezo maalumu.
Na sura ya suala kama ilivyoelezwa kwenye swali liliotajwa linaonesha kuwa muamala huu unajumuisha mahusiano matatu ya kimkataba: Uhusiano wa kwanza: kati ya mtazamaji wa kwanza na kampuni kuhusu kutazama matangazo.
Uhusiano wa pili: kati ya mtazamaji na kampuni hiyo kuhusu kuvutia wanachama wapya.
Na uhusiano wa tatu: ni kati ya wanachama wapya na kampuni ya uuzaji.
Ama uhusiano wa kwanza uliopo kati ya mtazamaji wa kwanza na kampuni kuhusu kutazama matangazo: ni muamala wenye mikataba miwili ya kukodisha;
Wa kwanza ni sharti kwa mwingine; Mkataba wa kwanza: kati ya kampuni na mtazamaji; Kampuni hiyo ni muajiri, na mtazamaji ndiye muajiriwa, na mahala pa mkataba kati yao ni utumiaji wa kuingia katika ofisi au tovuti ambayo utazamaji hufanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja; Halafu hufanywa upya na ushiriki maalumu.
Na mkataba wa Pili: kati ya kampuni na mtazamaji pia. Kampuni hiyo ni mmiliki wa biashara na mtazamaji ni muajiriwa, na mahala pa mkataba kati yao ni kutazama idadi fulani ya matangazo katika kipindi fulani, na mtazamaji anapokea malipo kutoka kwa kampuni.
Ya kwanza: ni sharti la pili; ambapo kukodisha kwa tovuti ni sharti la mteja kupata fursa ya kutazama kulingana na mkataba wa pili.
Na haiwezekani kuifanya kuwa tuzo; Kwa sababu wakati wa kutazama ni maalumu, na wakati wa tuzo haujulikani. Pia haiwezekani kuuza; Kwa maana haiwezekani humiliki.
Kwa uhusiano wa pili uliopo kati ya mtazamaji na kampuni hiyo kuhusu kuvutia wanachama wapya, ni kama udalali. Mtazamaji hufanya kama dalali kwa kampuni kuwashawishi watu wengine kujiunga na biashara ya kutazama matangazo.
Kuhusu uhusiano wa tatu ambao ni kati ya wanachama wapya na kampuni ya uuzaji, inasemwa juu yake kile kilichosemwa hapo mwanzo.
Kabla ya kuzungumza juu ya hukumu ya kisheria, tunaelezea maana kadhaa muhimu ambazo zinapaswa kuzingatiwa na kukumbushwa wakati wa kutoa Fatwa kuhusu maswala mapya ya uchumi kwa ujumla:
Kwanza: Inahitajika kujua hali ya uchumi wa soko ambalo muamala huu unafanywa. Kwa sababu baadhi ya miamala inaweza kuwa halali kufanywa kwenye soko kinyume na mingine;
Kwa kuzingatia hali ya uchumi wa soko hili, ambalo aina ya uchumi ambao soko hili linaingiliana sana, ni kwamba: baadhi ya miamala ambayo inafanywa katika masoko ambayo hufuata mfano wa uchumi huru, ni hatari kutekelezwa katika masoko yanayotegemea mfumo wa uchumi elekezi; Kama uchumi wa Misri, ambao unachanganya baadhi ya sifa za uchumi wa jadi na baadhi ya sifa za uchumi huru.
Ya pili: kwamba miamala ya kisasa mipya imekuwa migumu sana na inaingiliana; Ni nadra kuwepo ndani yake miamala ambayo inategemea mikataba rahisi ya Fiqh, bali imeundwa mara kwa mara, na mikataba tata inayohitaji kuzingatiwa kwa uangalifu katika uhusiano wa kimkataba unaotokea kati ya vyama vyake;
Kubainisha mikataba ambayo imewekwa kwa upande mmoja, na kuhakikisha kwa upande mwingine kwamba muundo huu haukusababisha kuibuka kwa maelezo katika shughuli hizi zinazoathiri usahihi wa mikataba ambayo ndio chanzo cha haki na majukumu ndani yake.
Ya tatu: kwamba soko la kisasa halizuii wachumi wanaofanya kazi ndani yake kubuni bidhaa za kiuchumi, ikiwa ni bidhaa au huduma, na hii inamaanisha kuwa bidhaa hizi zinabeba maoni mengi ambayo ni ya mawazo ya kisasa ya kiuchumi;
Kama vile uuzaji kupitia mtandao wa habari wa kimataifa (Internet), ambao unachanganya wazo la uuzaji wa moja kwa moja na matumizi ya mtandao yaliyotajwa kama chombo cha uuzaji kupitia matangazo.
Ya nne: Jaribio endelevu la ubunifu wa bidhaa za kiuchumi wakati wote - kupata faida kubwa zaidi - limesababisha uwepo wa bidhaa za kiuchumi ambazo hazina kifuniko cha kisheria, na hazizingatii kanuni thabiti zinazosimamia masoko ambayo shughuli za bidhaa hizi hufanywa. Ili wale wanaoshughulikia shughuli hizi wawe wazi kwa hatari kubwa inayotokana na ukosefu wa ulinzi wa kisheria kwao.
Ya tano: Kukosekana kwa utamaduni wa kiuchumi kutoka kwa wale wanaoshughulikia ubunifu katika uwanja wa uchumi mara nyingi husababisha unyonyaji wa kiuchumi wa mahitaji yao, uhitaji wao wa kazi unatumiwa, haswa kwa kuzingatia viwango vya juu vya ukosefu wa ajira.
Ya sita: Maadili ya jumla ya uchumi hufanya kanuni katika kushughulikia hitaji la kiuchumi ni kukidhi hitaji hilo bila unyonyaji kwa kumdanganya mmiliki wake, na kadhalika.
Baada ya hapo, tunachoona na kuchagua ni kwamba muamala unaohusika na swali ni marufuku na haramu. Hii ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
kwanza: Hatari zinazohusika ambazo zinasababisha madhara kwa umma, na Sheria inashughulikia zaidi katika sehemu hii ambayo ni miongoni mwa sehemu za miamala.
Miongoni mwa mfano wa hivyo katika Sheria ya Kiislamu ni marufuku dhidi ya ukiritimba; Mwanachuoni Al-Kasani alisema katika kitabu cha [Badai Al-Sana’i’ 5/129, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): [inachukiza ununuzi wa ukiritimba huko kwenye mji na kuacha kuuza; ni mahali pa kudhuru umma].
Ikiwa ni pamoja na: Marufuku kupokea watu wanaobeba bidhaa kwenda mjini, kwa ajili ya kuzinunua kutoka kwao kabla ya kuwasili kwao na ufahamu wao wa bei, wakitumia fursa ya ujinga wao.
Mwanachuoni Al-Kasaniy alisema katika kitabu cha [Badai Al-Sana’i’ 5/129, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): [Inachukiza kupokea kupokea watu wanaobeba bidhaa kwenda nchini, kwa ajili ya kuzinunua kutoka kwao kabla ya kuwasili kwao na kabala kufahamu bei, kama hali hii ikisababisha madhara kwa wananchi, kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kuhusu kukanusha jambo hilo kwa sababu ya madhara yanayopatikana kwa watu, kwa hivyo, inachukiza kama inavyochukiza ukiritimba].
Na imetajwa katika Jarida la hukumu za kiuadilifu katika Kifungu Na. (1254) kwamba: “Inaruhusiwa kwa kila mtu kufaidika na kile kinachoruhusiwa, lakini ni kwa masharti ya kutosababisha madhara kwa umma”.
Ama dalili ya kuwa muamala huu ni mojawapo ya miamala ambayo inaweza kusababisha madhara kwa watu na kupoteza maslahi yao: ni kwamba hakuna kifuniko cha kisheria kwake - Pamoja na kuenea kwake na shida zake kwa ujumla - na kwamba hakuna njia ya kushtaki wakati kutokea mzozo na taasisi inayoandaa muamala huu na kuienea katika nchi ya Misri, hali ambayo inaifanya miamala hii isiyodhibitiwa na viwango vya ubora wa kibiashara, na haina dhamana ya sheria zinazodhibiti mwendo wa soko, hali ambayo inasababisha kukosekana kwa kimbilio kwa wahusika wakati wa mizozo, na ukosefu wa ulinzi wa kisheria kwa wale wanaoshughulikia miamala hii, hali ambayo inafanya pesa zao kuathirika na hasara, na uhifadhi wa pesa ni moja wapo ya malengo halali ya jumla ambayo sheria ya Kiislamu iliagiza kwa kuyahifadhi, na vivyo hivyo sheria na dini zingine;
Kwa hivyo, Uislamu ulikusudia kutunga sheria itakayofanikisha uhafidhina huu, na ikafanya kazi kupunguza suala la mzozo na mafarakano kati ya watu na vinavyosababisha hivyo kwa kila njia.
pili: vitu vinavyoweza kutokana na muamala huu unapoondoka kutoka uwanja wa ubinafsi kwenda kwenye uwanja wa kawaida na kwamba ni jambo la kawaida la kuchezea usawa wa soko, kwani huondoa pesa na mtaji kutoka kwenye gurudumu la uzalishaji wa jamii na kuipenyeza ndani mifuko ya kikundi maalumu cha watu bila kuzunguka gurudumu la uzalishaji katika jamii, hali ambayo inasababisha madhara kwa wafanyikazi, kwa hivyo shughuli hii imekiuka moja ya masharti ya usahihi wa miamala mipya iliyoundwa, nao ni kwamba miamala hiyo inadumisha usawa wa soko na haiathiri vibaya. Basi shughuli hii itakatazwa kulingana na maana hiyo.
Tatu: Athari kubwa zinazotokana na miamala kama hiyo kwenye mfumo wa thamani katika jamii, kwa kuhamasisha matumizi yasiyo ya kawaida, na kupamba mwenendo wa kupata mapato haraka, ambayo unyonyaji hutumiwa kwa uwazi kwa mahitaji ya vijana kwa kuwafanya kazi inayofanikisha faida ya mtu binafsi kwao, lakini katika wakati huo huo hali hii haijumuishi kufanya juhudi kubwa zinazofaa, na haifikii kuboreshwa kwa kiwango cha uzalishaji katika kiwango cha kikundi.
Nne: Inajumuisha udanganifu. kwa sababu ya masharti ya mkataba wa kubadilisha katika mkataba mwingine wa kubadilisha, na hali hii ni marufuku kulingana na madhehebu ya wasomi wengi; Kutoka kwa Maimamu Abu Hanafa, Ash-Shafi na Ahmad Ibn Hanbal.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi na imethibitishwa kutoka kwa Abu Hurairah, R.A., kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., amekataza uzaji mbili katika uuzaji mmoja.
Baadhi ya Wasomi walibeba umarufuku wa uzaji mbili katika uuzaji mmoja kwa maana hiyo. Akasema: hali ya kuweka sharti la mkataba katika mkataba mwingine, hupelekea maana ya uzaji mbili katika uuzaji mmoja, na kuibatilisha, kwa ajili ya ujinga na udanganyifu..
Imamu Ibn Qudamah Al-Hanbali alisema katika kitabu cha [Al-Mughni 5/230, Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy]: [Na ikiwa atamwagilia bustani hii kwa theluthi, na kumwagilia bustani nyingine kwa sehemu inayojulikana, haisihi; kwa sababu ameweka sharti la mkataba katika mkataba mwingine, ikawa kwa maana ya uzaji mbili katika uuzaji mmoja; Kama usemi wake: (Nimekuuzia nguo yangu kwa sharti ninunue nguo yako).
Mkataba huu umeharibiwa kwa maana mbili:
Ya kwanza: kwamba ameweka sharti katika mkataba mkataba mwingine, na faida inayopatikana kwa hiyo haijulikani, kwa hivyo ni kana kwamba ameweka sharti la fidia badala ya inayojulikana na isiyojulikana.
Ya pili: kwamba mkataba mwingine haufungamani na sharti hilo, kwa hivyo sharti hilo limepotezwa, na ikiwa limepotezwa, sehemu ambayo aliacha lazima irudishwe kutokana na kuzingatia kwake, na hiyo haijulikani, kwa hivyo yote inakuwa haijulikani].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu jibu la swali limefahamika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Amanat Al-Fatwa

Share this:

Related Fatwas