Kumwamini Mwenyezi Mungu na athari ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwamini Mwenyezi Mungu na athari yake katika Mwenendo wa Mtu na Jamii

Question

Nini athari ya Kumwamini Mwenyezi Mungu katika Mwenendo wa Mtu na Jamii? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1-Tunajua kwamba kuamini Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutomshirikisha ndio mhimili wa Dini ya Kiislamu. Mwaenyezi Mungu Mtukufu amesema; {Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja} [Suratul Al Ikhlas]. Na hii hapa Sura fupi ya Qur’ani Tukufu inaelezea alama ya Upweke huo kwani inaelezea Upweke huu wa Mwenyezi Mungu na hukanusha ushirika wowote baina yake Mwenyezi Mungu aliyetukuka na mwanadamu, na Imani ya Mtu juu ya Upweke wa Mwenyezi Mungu inamzuia asitumbukie katika kumtukuza mwanadamu mfano wake kwa kiwango cha kumwabudu kwa sababu tu ya Cheo chake, madaraka yake au kwa ukaribu wake jambo ambalo hufungua mlango wa changamfu za kibinadamu bila ya kufungamanishwa na kutishika, woga, au kujidhalilisha.
2-Hakika Suala hili la Imani kwa Mwenyezi Mungu linaathiri moja kwa moja uhalisia wa kibinadamu katika suala la kunyoosha starehe za maisha ya kimali, na kunyoosha utashi wa (shahawa za) Nafsi ya mtu na matamanio yake. Kwa hiyo Imani inazinyoosha pande mbili unyooshaji unaozifanya zijiepushe na kujikweza, na kuufuata ukati na kati kila kinachotakiwa na msimamo kuyahusu mawili haya ni kwamba mtu asipindukie katika kuyapima kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufua amesema: {Enyi mlio amini! Yasikusahau lisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri}. [AL MUNAFQUUN 9] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini}. [AL KAHF 46] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na Akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu}. [AL HADID 20]
3 - Qur’ani Tukufu imekataza Mali na Watoto kuwahadaa watu kwa kuwatumbukiza katika kustarehe navyo, na hiyo inafuatia kuanza kudanganyika na kufuata matamanio na utashi, na Uislamu haukukataza kunufaika navyo, na kutumia vizuri kwa Ukati na kati wa manufaa.
4- Na kwa ajili hiyo, Kuuamini Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu hupelekea kuamini Utu wa mwanadamu na hadhi aliyonayo na heshima mbalimbali na nyenzo, kwa hiyo Kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee huonekana moja kwa moja katika nafsi ya Muumini na Mfanya ibada, ambapo Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu unaichota nafsi ya kibinadamu kuelekea katika Umoja, na kuyatibu yaliyomo ndani yake miongoni mwa uwili na mseto baina ya Akili na Tabia, baina ya Nafsi na Moyo, baina ya Undani na Mwenendo wa kiutendaji. Kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kunambeba Mwanadamu na kumwelekeza katika mwelekeo sahihi uliopangika usio na mvutano ndani yake wala mgongano baina ya Uwili uliotajwa, na kinachopelekea mtu katika mwelekeo huu sahihi uliopangika katika Maisha yake ni Kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, na sio Imani yoyote, na ikiwa Muumini Mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na Kumpwekesha, haufikii uratibu huu wa kamili wa Uwili unaokinzana maana yake hamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Imani yenye Mzinduko, Komavu na ya Kina.
5- Katika Umoja wa mwanadamu kama ulivyo na kutojigawa baina ya nguvu zinazotofautiana nayo kwa nguvu na mvutano (vuta na kuvuta) ni moja ya matunda ya msingi ya kuamini Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu – ambaye Mwanadamu analazimika Kuuamini Upweke wake na kwa hivyo analazimika kumwelekea Yeye pekee kwa Ibada – Yeye anazikusanya sifa zote za Uzuri, Utukufu na Ukamilifu. Sifa hizo ambazo kwazo, kama zinakuwa ndani ya Nafsi ya Mtu wakati akihangaikia kujisogeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu zitasaidia kuepukana na Uwili Uwili uliotajwa na kusukumia msukumo wa kuelekea katika Umoja wa kinafsi (Saikolojia) na kimwenendo nyoofu, unakaribia kutokuwa na Idadi kama Idadi ilivyotoweka katika Njia ya Ukweli katika Dhati yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hivyo, Kuamini Upweke wake Mwenyezi Mungu Mtukufu kumsaidiana mwanadamu kuepukana na mapambano makali ya ndani ya nafsi ya asiyeamini.
6- Na Mwanadamu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu sio kuwa karibu kwa Sehemu au muda, bali hakika mambo yalivyo ni kwa kuwa na Maadili mema na Kuambatana na Majina yake Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na Sifa zake, na Mwanadamu kila anapozama zaidi katika hali hiyo basi anakuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tunalazimika kupata sura ya upeo wa athari juu ya mwenendo wa mwanadamu ikiwa mwanadamu huyu ataamua kuambatana na Jina lake Mwenyezi Mungu la Amani, au kwa Jina lake Mwenyezi Mungu la Mwingi wa Rehma au Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa, au jina lake la Mwadilifu…, Na kwa haraka, Uislamu utaningiza rehma na Uadilifu katika mwenendo wa mwanadamu na kutoka katika jali hiyo kuelekea katika Jamii na kuenea kwa watu wote, nasi tunapaswa kuleta sura ya namna gani iwapo mja atatundika Imani yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa majina hayo yenye hadhi kubwa ambayo mwanadamu hanayo, kama vile Mwenye Nguvu, Mwenye kutenza Nguvu, Mwenye Kiburi, kwa hiyo Muumini mwenye yakini anatambua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mmoja, basi hakitoki kwa mwanadamu kitu kama hicho kuwaelekea wengine, kwani anatambua fika kwa yakini na anamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kikamilifu kwamba hali ilivyo Mwenyezi Mungu ni mmoja.
7- Na muumini aliyemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, na akajua ya kwamba miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mfano: Ni Elimu, atajikuta yeye akiihangaikia Elimu, kwa kuamini kwake kwamba kila anapokuwa na Elimu zaidi ndivyo anavyomkurubia zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Muumini aliyemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, kwamba Yeye ni Mtukufu aliyetakasika na upunbufu na kila kibaya, basi mtu huyu daima atahangaikia kujiepusha na mambo mabaya na yenye kuchukiza na aina zote za mabaya.
8- Na kupitia mifano hii, inatupambanukia ya kwamba Imani ya Maana yake ya Uislamu ni Imani chanya na ina athari yake ya kiutendaji na ya kudumu kwa mwenendo wa Mwanadamu Muumini, na kwa ajili hiyo, imepokelewa kwa mlolongo wa mapokezi kutoka kwa Wema waliotangulia ya kwamba Imani ni kauli na kitendo.
9- Na kuanzia hapo, Muislamu Muumini analazimika kuwa mtu chanya katika maisha yake, na anaanzia katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa kwake na maadili mema na kujiambatanisha na majina mazuri ya Mwenyezi Mungu na Sifa zake zenye Hadhi kubwa katika kila anayoyafanya na kuyatengenezea, na kama hakufanya hivyo basi atapatwa na hali ya kujitenganisha na ataishi maisha mseto ambayo hayaendani na mmoja wa nyuso mbili na Uso mwingine
10) - Na kwa ajili hiyo, Mwislamu aliyeamini na mfanya ibada – na kutokana na ufunuo wa Imani yake na Uislamu wake na Ibada yake – hapana budi awe na mahusiano mazuri na wengine katika Jamii yake, na uhusiano huo uwe katika wigo wa kubeba jukumu la kuleana na wengine, iwe ni katika kuwaletea matumaini kwa misaada ya kifedha wanapohitaji kwa njia ya Zaka na Sadaka, na kwa maana ya kiroho daima kama vile upendo, kuhurumia na kuonesha upole, na kuleta uadilifu wa kudumu katika mwenendo wake hata katika nafsi yake kuwaelekea wengine.
11) - Na katika wigo huu, tunapaswa kusoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa}. [AAL IMRAAN 104] Yanayotakiwa na Qur’ani Tukufu hapa katika Ulinganiaji wa Kheri na kuamrisha mema na kukataza mabaya inatuonesha athari za Uongofu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Mwenendo wa binadamu kwa kufanya mazuri, na uchanya katika mahusiano pamoja na wengine na mwenendo nyoofu ambao unamfanya mtu ajiepushe na kuwaudhi au kuwadhuru wengine.
12) - Ama kuhusu athari za Kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa Jamii: na pia lazima Ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, lazima ionekane kati nafsi yake mtu na huko kuna mwelekeo uliojipangilia vyema mmoja kati ya tabua na akili ndani yake, na vilevile lazima ionekane katika mwelekeo Jamii ya Kiislamu kwa ujumla wake baina ya watu, na hivyo wao wanakuwa na mwelekeo wa pamoja uliopangika, na huo upili uliopo kwa mtu baina ya akili na kwa mfano, upo pia baina ya mtu na mwingine katika jamii rkutokana na tofauti za kimaumbile walizonazo kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kunamfanya mtu aweze kuyakwepa na kuyaondosha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi} [AL ANBIYAA'I 92]. Kwa hiyo Aya hii imefungamanisha baina ya Umoja wa Umma na Umoja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Mola anayeabudiwa, Aya imewaashiria Waumini katika mkusanyiko wao, na kuwaambia kwamba mkusanyiko wao huo ndio ujengao Umma wa Waislamu, kisha ikauelezea Umma huo kuwa ni Umma mmoja, na ili Umoja wake kudumu katika umoja wake, inawalingania katika kuendelea kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye peke yake.
13) - Na kama ilivyo katika Jambo la kila mtu, kama kumwabudu kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutaonekana katika nafsi yake, katika umoja wa mwelekeo wake katika Maisha, vivyo hivyo Jamii isiyoonesha Waumini kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee ndani yake, kwa vitendo vyake kwa ujumla na kama Umma mmoja na Jamii, basi hakika mambo yalivyo ni kuwa hali hiyo inarejea katika kutoelewa vyema Imani sahihi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani Jamii ni mkusanyiko wa watu katika lengo moja, kama lengo hilo ni kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, na halipo katika nyoyo zao basi hilo halikustawi katika Jamii inayojengwa na watu hao, na inakuwa sababu ya kutokuwepo kwake katika Jamii ndio sababu ya kutoathiri kwake nafsi zao, mmoja mmoja.
14) - Na kuanzia hapo, Qur'ani Tukufu inapowasemesha Waumini kwa njia ya pamoja ikiwaamrisha kufanya bidii ya kuleta Umoja baina yao na kushikamana nao, Hakika Qur'ani inmwamrisha kila mtu, mmoja mmoja katika hilo pia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyikwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka}. [AAL IMRAAN 103]
15) - Na Jamii ya Kiislamu katika kumwamini kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Mola wake Mlezi, na Uislamu kuwa ndio Dini yake na Muhammad S.A.W, kuwa ndiye Mtume na Mjumbe wake maana yake hii ni Jamii isiyoufuata matamanio yake katika Mwenendo wa kila mmoja na vitendo vyake, na hawi chini ya hukumu yake kwa kuathirika na matamanio na udanganyifu wa starehe za maisha ya Duniani, naye katika Juhudi zake hataki isipokuwa Unyoofu na Uadilifu katika vitendo vyake, na hilo ndilo linalomsaidia kabisa katika kukifanyia kazi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
16) - Na kwa hivyo, Jamii ya Kiislamu kamwe haielemei upande wa yeyote dhidi mwingine, kwa sababu mtu anayeelemea upande wowote ni yule mwenye masilahi maalumu anayapenda na kuyatanguliza, na Waumini wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu hawana wao masilahi binafsi wanayoyapata kwa kukifanyika kazi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali masilahi yao ni masilahi ya wote na ambayo yanasimamiwa na Sheria ya Kiislamu, na masilahi ya wote katika Jamii yoyote yanaendeshwa kwa Uadilifu, na kile kilicho juu ya daraja mbalimbali za Uadilifu ambacho ni Wema katika mtangamano na Kunyoosha Mwenendo. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wala usiyafuate matamanio yao. Nasema: Naamini aliyo teremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake. [AS SHURA 15]
17) - Wakati ambapo Jamii isiyoufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Jamii choyo, kimsingi inategemea ukabila au kasumba yake, au ubepari na unyanyasaji wake, au ubaguzi wa rangi na ubaya wake, kwani choyo ikiwa nyuma ya mmoja, inakuwa katika fungu moja ikifungamana kwa sababu ya kasumba ya damu, au kasumba ya mali, au kasumba ya watu, au kasumba ya jinsia ya ubinadamu, au kasumba ya ubepari.
18) - Na kitu kinachobakia kwa Utu katika Jamii ya Kibinadamu iwapo mabaya yataongoza katika mwenendo na matendo na dhulma ikaenea katika mahusiano, na pakashamiri udanganyifu mwelekeo wa kutunga, na kumchukia Mtu na kumdhalilisha na kumfedhehesha kwa kumwabudu kwake mwanadamu mwingine, au kukiabudu kilicho chini ya mwanadamu katika viumbe, na Mwislamu anayejihimiza kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee ni mtu anayejielewa na kumwelewa vyema Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yeyote anayeyaelewa mambo haya mawili hawi mwovu katika matendo na mwenendo wake, na sio mwenye kuporomoka kiitikadi, na sio mnyonge anayechukiwa au mtumwa anayetengwa
19) - Na Jamii ya Kiislamu inayofuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Jamii inayoulenga Umoja wa Kibinadamu na inaufikia kwa msingi usawa wa kuzingatia katika Jamii, na Thamani ya Kibinadamu kwa watu wote, na kwa hivyo, mazingira yake ni mazingira ya kibinadamu, na kuanzia hapo, tunaweza kuielezea kama Jamii ya Kiungwana na ya Kibinadamu.
20) - Na wala haimaanishi hivyo kwa vyovyote vile kwamba hiyo ni Jamii ya Kidini na Kiungu kwamba ni Jamii iliyokingwa na makosa ya kibinadamu au uongozi wenye utukufu wa Kinga ndani yake, na kwamba unaongoza kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Duniani, bali ni Jamii ya Kiislamu inayohukumu kwa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni jamii inayokosea na kupatia, nayo kwa hali hiyo, ni jamii ya kibinadamu kwa maana yake hasa ya jina lake isipokuwa wasifu wake wote wa kipekee – ni jamii ya Kiislamu:- Hakika hiyo ni Jamii inamwamini Mwenyezi Mungu na Ujumbe wake na Kitabu chake Kitukufu na inashughulikia kwa ajili ya kuyafanikisha yote yanayolengwa na Ujumbe wake huu wenye hadhi kubwa, Ujumbe huo ambao umeulinda Utu wa mwanadamu, ukawa haufikii utukufu wa kiungu na ukawa haujaporomoka hadi ngazi ya mnyama, bali daima umemweka mwanadamu katika ngazi yake ya kibinadamu pale anapotoa maamuzi au kuchukua hatua, kutenda, kufikiri, au kufanya changamfu yoyote ile, kwa hiyo Jamii ya Kiislamu ni Jamii ya Kibinadamu inayojitahidi kuyafikia maadili ya juu ya Kiislamu yanayopupia juu ya utu wa mwanadamu katika jamii yake.
21) - Na kama hivyo ndivyo, basi hakika Umoja wa Fikra ya Kiislamu ndilo lengo la kudumu la mwanadamu, kwani Umoja ni lengo la mwanadamu katika ibada zake, katika nafsi na Jamii yake, na kwa njia kuufikia Umoja huo katika nyanja hizo tatu, changamfu za mtu zinaishia katika Ujenzi na ujenzi miji, Usafi wa moyo, na kuziwezesha njia za kupendana na kushirikiana baina ya watu katika Umma na katika Jamii, badala ya kusambaratika, kutengana, kugombana na kuuwana.
22) - Na kwa ajili ya matokeo mazuri ya kuuamini Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umoja wa Jamii na mshikamano wake na kuendelea kuwa na nguvu, na heshima dhidi ya Udhalili wowote au Unyonge, Qur'ani Tukufu katika Aya nyingi, inawataka Waumini wajiepushe na Migawanyiko iliyozitokea Jamii zilizopita. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini -ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui (30). Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Sala, na wala msiwe katika washirikina (31). Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, nawakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahiakilicho nacho}. [AR RUUM 30-32] Aya Tukufu katika sehemu hii, pamoja na kulingania kwake katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee, hakika zinathibitisha kwamba Dini inayolingania Umoja huu inaelezea Uasili wa mwanadamu na maumbile yake halisi yasiyobadilika au kugeuza, na kuanzia hapo, hii ni Dini iliyonyooka ambayo mtu anastahiki kuipupia. Umoja huo pia unathibitisha kutoka katika Imani ya kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee na kuelekea katika kumshirikisha ni sababu tosha ya mgawanyiko katika Jamii zilizotangulia na daima itaendelea kuwa kwamba kutoielewa vizuri kunapelekea Nafsi kuwa na matokeo yafuatayo: Mgawanyiko, ukabila, makundi, kasumba, ugomvi, Uadui na kuanguka.
23) - Na Umoja wa Jamii katika mielekeo inayoibuliwa na kumwamini Mwenyezi Mungu peke yake, haukanushi kuzidiana baina ya watu ukaribu wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pia hakuzuii kutofautiana katika riziki na katika kuwa na njia mbalimbali za maisha kwa watu bila ya kuwapo kwa wengine, kwa hiyo kuzidiana kwa Watu katika kuwa kwao karibu zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu na katika Maisha yao hakupaswi kuwa kisingizio cha kuwa dhidi ya kuwa pamoja katika mwelekeo unaoitaka Jamii ya Kiislamu iwe kama Jamii inayomwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee. Kwa hiyo kuwa na mwelekeo mmoja au Umoja ndani yake, unajengeka juu ya lengo la pamoja, na mwenendo ulionyooka, wakati ambapo kuzidiana katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni kuzidiana upeo wa kulifikia lengo ndani ya nyoyo za watu, ama kwa upande wa kuzidiana katika riziki na njia za maisha kunarejea katika utashi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwanza, na kwa kile alichomjaalia Mwenyezi Mungu kila mtu katika nguvu na maandalizi ya kimaumbile ya aina mbalimbali yanayomwezesha kila mtu kuelekea katika changamfu za kibinadamu anazonasibiana nazo na kwa namna inayomfanikishia haja zake mbalimbali za kijamii.
24) - Vilevile Umoja huo katika kuielekea Jamii ambao unatokana na kumwamini Mwenyezi Mungu na Upweke wake hakuzuii kutofautiana maoni, kwani kutofautiana maoni ni kawaida ya binadamu kutokana na kutofautiana tabia zao na mazingira yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na Mola wako Mlezi angelipenda angewafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachiku khitalifiana (118). Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kwelikweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja} [HUUD 118-119]. Na hakika kinachokatazwa ni kukombana. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri}. [AL NFAAL 46]
25) - Hakika Umoja wa Jamii unapokutana katika maalumu huwa ni dalili ya Ustaarabu wa Jamii hiyo na kusonga mbele kwa wanajamii katika kiwango cha kibinadamu, kwani huo ni uchache wa wasifika wa hiyo Jamii Hakika mzinduko wa kila mtu umepevuka zaidi na kuwa juu ya umimi wa mtu mmoja mmoja kwa kiasi cha pamoja baina ya watu inakuwa katika Maadili ya Juu yaliyoletwa na Risala ya Uislamu. Mzinduko huo wa Wote ambao Umimi wa mtu mmoja mmoja hutoweka, na hutoweka pia kasumba za kikabila na utaifa wa kibaguzi, na kwa upande mwingine, tunaziona nadharia mbalimbali za kimagharibi zinashindwa kufikia hivyo. Uliberari unaposhikilia Uhuru wa kila mtu kwa mfano, unakuwa na sifa ya Ustaarabu bila shaka, lakini unapoangukia katika Ubaguzi na kuufufua upya, na kupelekea Ukoloni dhidi ya mnyonge na kumtumia kidhalimu, hakika yake kwa wakati huo, hurejea nyuma kutoka katika hali ya Ustaarabu na kuufichua uso wake wa kweli. Na mfano ulikuwepo pia katika Ujamaa wa Kimaksi ambapo katika ulinganiaji wake, lilikuwepo suala la kuondosha ubaguzi kuelekea Amani ya Kimataifa na unabeba alama ya Ustaarabu, lakini unaposimama kwa udikteta wa tabaka la wafanyakazi na kulingania mapambano ya umwagaji damu dhidi ya Ubepari nao pia unakosa sifa yake ya Kistaarabu na kuufichua uongo wake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Rejeo: Profesa Mohammad Al Bahiy; Al Mojtama' Al Hadhariy wa Tahadiyatahu Min Tawjih Qur'aani Tukufu, Maktabta Wahbah, Ch. 1 Kairo (1397 Hijra- 1977) Uk.

 

 

Share this:

Related Fatwas