Yenye ukomo na Isiyo na ukomo Nisbi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Yenye ukomo na Isiyo na ukomo Nisbiyu na Mutwlaqu

Question

Tunasoma katika maandiko mengi na tunasikia kutoka kwa wasomi wengi maneno mengi kuhusu: Nisbiyu na Mutwlaqu. Basi ni nini dhana ya istilahi hizi na sifa zake kuu kutokana na mtazamo wa Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mzingatiaji wa fikra ya kiislamu ataona kuwa Waislamu wameiamini fikra ya: Nisbiyyu na Mutw-laqu na wameikubali fikra ya: Yenye ukomo. Na imani yao kwa Isiyo na ukomo imedhihirika katika imani yao kwa Mwenyezi Mungu. Na hakika Mwenyezi Mungu alikuwepo kabla ya zama, mahali, watu, na hali. Na hizi ni pande nne zinazodhibiti uhalisia wa maisha, ambao unahusishwa.
Kwa hiyo tunayaita haya ni mabadiliko: yenye kiwango maalumu katika zama, mahali, watu, na hali. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mpweke na Asiye na kiwango maalumu, na hazungukwi na kitu chochote katika vitu hivi.
Pia Waislamu wameshaamini ujumla wa maadili, kwa mfano; uadilifu ni uadilifu katika pande hizi nne, na rehema ni rehema, na dhulma ni dhulma, na ujeuri ni ujeuri, kama tunavyoona katika Qur`ani Tukufu, kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda}. [AL MAIDAH 8]
Na Mola wetu Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka}. [AL AN'AAM 152]
Kutokana na maana hii imani kwa Isiyo na ukomo ni mojawapo ya nguzo za Uislamu, na kipengele asili cha akili ya kiislamu, nayo ni mfano wa kimaarifa ambao Muislamu anaweza kwa njia yake kuukabili uhalisia wake, kuufafanua, na kuuthamini.
Huenda tunaweza kufafanua Usekyula kuwa: unaamini sehemu ya ujumla, na kuwa imani kwa sehemu ya jumla hakika inaashiria kama alivyoita Dkt. Abdul Wahab Al-Misiriy kuwa ni (Usekyula kamili) na hapo hakuna ugumu kwa mwenye itikadi hii kumkana Mwenyezi Mungu, na hakuna ugumu kwake pia amtenge na kupokea kutoka kwake Mwenyezi Mungu, au kumtenga na maisha yake, na kubadilisha suala la imani liwe suala la binafsi na la kando, ambalo linaashiria aina ya imani maalumu wala haliashirii suala la kuwepo.
Na sehemu hii ya ujumla huathiri sana katika maelezo ya kilugha ambapo hujaalia Ulimwengu usio na hakika ndani yake, bali ni kutokana na maoni ya mchunguzi, na kama anavyoona kila mwanadamu peke yake, na vitu visivyo na hakika thabiti.
Basi maoni haya yanatupelekea kwenye Madhehebu ya Sophistic ya zamani, na baadhi ya Madhehebu mengine ambayo kutokana nayo mwanadamu anafikiri kuwa Mwenyezi Mungu ni sehemu ya ndani ya Ulimwengu na sio nje yake.
Nao ni mwelekeo ulioenea kati ya harakati iliyokuwepo kabla ya zama za sasa, na kupelekea kudhibiti mwelekeo mkuu wa fikra ya kimagharibi kupitia wakati wa zama za sasa. Na kwa mujibu wa hayo tunaweza kuutumia utangulizi huo katika ufafanuzi unaozidisha uwazi wake kuhusu namna ya kuutumia katika matini ya kisheria na uhalisia wa maisha:
1- Kuna tofauti kati ya maana ya ujumla wa Qur`ani, na tafsiri yake kwa njia ya kweli, na tafsiri yake kupitia mfumo wa sehemu ya ujumla. Hivyo ujumla wa Qur`ani ulifahamisha historia ya fikra ya kiislamu kwa kauli ya kuwa: Qur`ani haijaumbwa, na sisi sote tunakumbuka utahiniwa wa Imamu Ahmad Ibn Hanbal- Imamu wa Watu wa Sunna na Jamaa, na mmojawapo wa Maimamu wanne wanaofuatwa mpaka sasa - aliposimama msimamo wa nguvu dhidi ya wito wa uumbaji wa Qur`ani.
Wito ambao hupelekea moja kwa moja kuwa: Qur`ani inaainishwa ndani ya zama yake, mahali pake, watu walioambiwa kwayo, na hali iliyoteremshwa ndani yake.
Na jambo hili ndio limekanushwa na Waislamu wote; kwa sababu wanajua madhumuni ya madhehebu hii; iliyosemwa kuwa: Uhistoria wa Qur`ani, yaani imeteremshwa kwa ajili ya enzi maalumu, na enzi hii imeshapita pamoja na hali yake, watu wake, na masilahi yake, na haijabaki katika Qur`ani ila baadhi ya mambo ambayo tunaweza kuyaamini, au kuyatumia katika enzi yetu ya sasa.
Na kwa mujibu wa hayo Qur`ani itatengwa na maisha ya watu, na kuitenga kama ni kitabu cha uongozi, na kuutenga uislamu mbali na kazi yake ya ulimwengu, na mfumo wake wazi ambayo imekuja kwa ajili yake, na hali haikutofautisha kati ya Mwarabu na Mwajemi, mweupe wala mweusi, na mwanamume wala mwanamke. Na pia madhehebu hii hupelekea usemi wa sehemu ya ujumla ambayo tunaona umepelekea kukanusha hakika ya vitu.
2- Kuhusu tafsiri ya ukweli ndiyo inaamini Ujumla wa Qur`ani, ambapo inavuka mipaka ya pande nne zilizotajwa, na kuwa haijaumbwa, bali ni Maneno ya Mwenyezi Mungu ambaye bado anazungumza, na kama kwamba Qur`ani imeteremshwa kwa sasa, na kama kwamba inamwambia msomaji wake, na siku zote ni kitabu cha uongozi, na haipingani na uhalisia wa maisha.
Lakini inaainisha tabia kiujumla, maadili kiujumla, na ndani yake alivyojaalia Mwenyezi Mungu Mtukufu iwe mifumo thabiti, kwa mfano: nidhamu ya ushahidi; na ndani yake pia jumlisho ambalo Mwenyezi Mungu alijaalia kufaa kwa kila zama na mahali.
Kwa hiyo tunaona Qur`ani ni yenye maoni mbali mbali, kama alivyoielezea Bwana wetu Ali Ibn Abi Twalib RA, alipomwambia Abdullahi Ibn Abbas RA, wakati wa mashauriano yake na Al-Khawarij: “Usiwahasimu kwa Qur`ani, hakika Qur`ani ni yenye maoni mbali mbali, na wewe utasema, na wao watasema”.
Na kama alivyoielezea Mtume S.A.W, alivyopokea Ali Ibn Abi Twalib R.A., kuwa alisema: “Hakika itakuwa fitna”. Nilisema: “Nini mahali pa kutokea?” Alisema: “Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndani yake habari za waliotangulia, na habari za waliofuata, na ni hukumu kati yenu, na ni kauli ya kupambanua wala si mzaha, na aliyeiacha kutokana na ujeuri humkosea Mwenyezi Mungu, na mwenye kutaka uongofu – au kasema: elimu- iliyokinyume na hii, humpotosha, na ni kamba ya Mwenyezi Mungu iliyothabiti, na ni mawaidha yenye hekima, na ni njia iliyonyooka, na ambayo haibadilishwi na matamanio, na ndimi hazibabaiki kwayo, na maulamaa hawashibi kwayo, na haiwi kale kutokana na kukariri kwake, na maajabu yake hayaishi, na ambayo majini walipoisikia walisema: {Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu! Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi}. [AJ JIN 1-2]
Na aliyesema usemi wake, basi aseme kweli, na aliyefanya kwa mujibu wake, basi atapata ujira, na aliyehukumu kwa mujibu wake basi ni mwadilifu, na aliyelingania njia yake ataongozwa kwa njia iliyonyooka”.
Na sisi tunaona ndani ya Qur`ani desturi nyingi ambazo zinapanga maisha ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa kwa njia ya kuweka kanuni na misingi ya mambo haya ya maisha, lakini haiingii katika ufafanuzi wa sehemu ya kiwango maalumu kutokana na unyumbuliko wake.
Katika muktadha huu tunaweza kuita hali hii iwe (sehemu ya kiwango maalumu) yaani siyo sehemu ya ujumla ambayo hufikia hadi hitilafu ya kupingana, bali ni sehemu ya kiwango maalumu ambayo inakusanya hitilafu ya aina fulani, ambapo kwa njia yake tunaweza kupata unyambuliko huu.
Na hayo yote yalikuwa utangulizi muhimu kwa ajili ya kujadili suala hili, ambapo tunataraji kufikia misingi inayotofautisha kati ya sawa na kosa, kuhusu suala la Tafsiri ya Qur`ani katika wakati wa sasa.
3- Qur`ani Tukufu imeteremshwa Kwa Lugha ya Waarabu, na hali ya kuwa ni matini, hivyo uelewa wake unaambatana na uelewa wa lugha, basi huwa na maana ya asili na maana ya kufuata. Na maana ya asili ni ile inayoweza kufasiriwa kutoka lugha moja hadi nyingine, ambapo hufahamika maana ya maneno katika sura yake kwa kamusi, na kutokana na miundo ya muktadha, na ilivyofahamika katika akili za wazungumzaji wa lugha hiyo, na kwa kujali uendelezaji wa maana ya maneno, ambapo inaonekana tofauti yake katika Lugha Takatifu yaani Lugha zenye Matini Matakatifu zinazoambatana na Dini, kama vile: Kiibrania, Kiaramia, Kisinsikritia, na kiarabu.
Na jambo hili ni ya tofauti na utukufu wa lugha, kama tulivyoelezea kwa kina hapo mwanzo..
Na idadi ya maana ya asili kuhesabiwa, lakini maana ya kufuata ni yenye idadi zaidi, na inahitajia sana vigezo ambavyo hukataza maana iwe ya Uishara, au kuelekea iwe ya ajabu. Na miongoni mwa masharti yake muhimu isibatilishe maana ya asili, lakini huongeza maana mpya ambayo inajiunga nayo wala huitengui.
Na huenda suala hili ni tofauti muhimu kati ya Usufi wa Sunna- ambao umeelewa maana nyingi za matini ya kisheria hasa Qur`ani Tukufu na hujiunga na maana ya asili ya marejeo- na Ubatini ambao umejaalia maana ya kufuata kama hakimu ya maana ya asili, na maana yakufuata ikawa ya asili, na ya asili ikawa kizuizi cha kuelewa.
Kwa hiyo Imamu Al-Ghazaliy aliandika kitabu chake cha(Fadhaihul Batiniyah) kwa ajili ya kubaisha maana hii, na kuwajibia, na kubainisha ubaya wa madhehebu yao; na kwa sababu fadhila ya Qur`ani ndiyo imeteremshwa kama ujumbe kwa walimwengu, basi haiwezekani kukubali nadharia ya Tafsiri ya Ishara au Esoteriki (Kuwahusu watu maalumu), ambayo husababisha uelewa wake kwa baadhi ya watu, na kutoelewaka na wengi wao.
4- Lugha yoyote inakusanya, kutokana na maoni ya wataalamu wa lugha, inayojulikana kwa Ukweli na Sitiari. Ukweli ni: kutumia neno katika maana yake iliyowekwa na mtungaji wa lugha mwanzo mwanzo, na mtungaji wa lugha, kwa maoni ya wengi wa Wanazuoni wa kiislamu, ni Mwenyezi Mungu.
Na wanatoa dalili ya hii kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote}. [AL BAQARAH 31] Na majina hapa ni maneno yaliyowekwa mbele ya maana ya vitu na mambo maalumu, na huu ni ukweli wa nidhamu ya lugha, yaani kuweka neno mbele ya maana pekee.
Na Sitiari ni: kutumia neno katika maana isiyowekwa nayo, kwa hiyo inahitaji dalili, na ni lazima kuwepo uhusiano kati ya neno na maana hiyo.
Na wakahesabia mahusiano haya yanayokuwepo kati ya neno na maana yake nyingine isipokuwa maana ya asili, wakayakuta zaidi ya mahusiano ishirini na matano; miongoni mwake: kuonesha sehemu ya maana, kuonesha maana zaidi, kuonesha maudhui, kuonesha hali, kuonesha itakayokuwa, na kuonesha iliyokuwa… n.k., miongoni mwa mahusiano haya ambayo Wataalamu wa wa Elimu ya Balagha wakishughulikia. Kadhalika Wataalamu wa Misingi ya Fiqhi wakishughulikia, kwa ajili ya uelewa sahihi uliojengeka kwa mfumo wa kweli na wa kitaaluma kwa matini ya kisheria, iwapo ni Kitabu au Sunna.
Na Wafasiri wa Qur`ani kwa jumla hawakukanusha Sitiari isipokuwa Ustadh Abu Is-haaq Al-Isfrainiy, kisha akamfuata baadaye Sheikh Ibn Taimiya, kutokana na mielekeo ya imani inayohusu maoni yake, lakini wengi wa Maulamaa na Wafasiri hawakukubali maoni yake.
Na kwa mujibu wa hayo Maulamaa walitoa kanuni muhimu , nayo ni: “Sitiari ni kinyume cha asili, kwa sababu asili ya maneno ni ukweli, na maana ya hayo kuwa: jumla ya maneno ni yenye maana ya ukweli, na msikilizaji huchukua maneno yaliyosikilizwa mwanzo mwanzo yawe kweli, na ukweli hufikia akilini kwa kwanza.
Na Wataalamu wa Usuuli waliweka kanuni nzuri zaidi katika suala hili, ambayo hukusanya kazi ya lugha, na alivyotuneemesha Mwenyezi Mungu yanayohusu faida ya uzungumzaji, wakasema: Utumiaji ni sifa ya msemaji, na uelewa ni sifa ya msikilizaji, na maana ni kabla ya hayo yote.
Katika ibara hii fupi kuna taarifa ya uthabiti wa lugha ambayo matini yaliandikwa kwayo, na kuna pia taarifa ya uhuru wa msemaji atumie maneno yake katika lile analolitaka kusema, na kulifikisha kwa wengine. Na kuna pia ishara ya kazi ya upokeaji ambao anautekeleza msikilizaji, ambapo anaweza kuchukua maneno kwa kadiri ya maana yake.
Na maelezo ya ibara hii yanaambatana sana na suala la (yenye ukomo na isiyo na ukomo), pia inaambatana na kufaa Qur`ani kwa kila zama na mahali, na umuhimu mkubwa kwa mbinu za njia ya tafsiri ya Qur`ani ambazo hazipelekei kwenye kukanusha sehemu ya kiwango ya uhalisia na kuzama katika ujumla; wala hupelekea pia kupoteza Tafsiri, ambapo Dini haijakuwa na utambulishao, na kila mtu anaweza kusema allivyotaka kuhusu Dini, kwa sababu hiyo ni kinyume cha asili ya itikadi na asli ya uhalisia, nayo ni umuhimu wa kuwepo kwa isiyo na ukomo na yenye ukomo wakati wa kutambua matini na kutambua uhalisia na kuungana kwa hizi mbili.
5- Tumekwisha amua mara nyingi kuwa: Kuna maana ya kufaa kuhusu kauli yao: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichoandikwa yaani Qur`ani, na kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichoonwa yaani Ulimwenguni, na tukaonesha ulingano kati ya maana hizi mbili, inayomaanisha kuwa vitu hivyo viwili vimetolewa na Mwenyezi Mungu; Qur`ani imetolewa kwa mujibu wa Amri, na Ulimwengu umetolewa kwa mujibu wa Uumbaji.
Na Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu chake: {Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote}. [AL A'ARAF 54]
Na katika muktadha huu kuna suala la visomo viwili; Kisomo cha Qur`ani, na Kisomo cha Ulimwengu, ambapo Aya za Suratul A’alaq huonesha hivyo, ni Aya zilizoteremshwa mwanzo mwanzo, ambapo Mwe nyezi Mungu Mtukufu alikaririsha ndani yake Amri ya kusoma, na ambapo kisomo cha kwanza kinaambatana na Uumbaji, na cha pili kinaambatana na Ufunuo, akisema: {Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu}. [AL ALAQ 1-4]
Hapa kalamu ni ishara ya Ufunuo, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mutukufu: {Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo}. [AL QALAM 1]
Hapa tunaona Yeye Mwenyezi alitaja kwanza Uumbaji, kisha akataja Ufunuo, hivyo kama kwamba mwanadamu analazimika kujua Ulimwengu na yaliyozunguka ili aweze kuelewa Ufunuo, pia analazimika kutambua Ufunuo kwa njia sahihi ili aweze kubadilisha uhalisia wake kwa njia sahihi.
Kwa hiyo tunaona kuwa: Uumbaji na Amri zinazunguka ndani ya duara moja, na tukianza kutoka kwa nukta moja ya duara hii tutafikia mwishoni mwake. Na kama tulivyoona kauli yake Mwenyezi Mungu: {Arrah’man, Mwingi wa Rehama. Amefundisha Qur`ani. Amemuumba mwanadamu}. [AR RAHMAAN 1-3] Ina ishara ya duara hiyo.
Kwa hiyo tunaona kuwa kulaumu ulingano wa matini ya Qur`ani kuhusu ukweli, na kukataa hivyo kwa uwazi siyo rai nzuri; kwa sababu inaziba mlango wa visomo viwili kwa upande mmoja, na kukanusha ukweli kwa upande mwingine. Hakika Qur`ani Tukufu imeteremshwa kwa kuambatanisha, nayo kwa kuchora wavu wa mahusiano, ambapo mzingatiaji wake anaweza kutoa kanuni na hakika nyingi kutoka katika pande za wavu huu. Kadhalika ukweli kuhusu maendeleo yake au kuanguka kwake huwa ni wavu, na siyo sura ya mstari kama wanavyoeleza Wataalamu wa Hesabati.
6- Mfumo wa Maadili ni miongoni mwa (Mutw-laqu) isiyo na ukomo, na dhana ya Uadilifu ni thabiti siku zote, na pia ni thabiti pia katika nyanja zote, a uadilifu wa jamii haitofautiani na uadilifu wa mahakama, wa siasa, au wa fikra. Na kuacha uadilifu katika zama zozote, mahali popote, au nyanja yoyote kunazingatiwa ni dhuluma na uwongo. Hakika hii kwa wepesi wake imezingatiwa kupitia itikadi zenye ukomo ambazo wamezishikilia wamiliki wake, ambao tumewaona wakiacha uadilifu kwa ajili ya kupata nguvu, masilahi, au misimamo binafsi, na wao hawaizingatii hiyo kama ni dhulma, bali waliuita uhalisia, siasa ya uhalisia, na masilahi ya juu… n.k., miongoni mwa maneno ambayo yalikuwa yanamaanisha kitu, na uhakika wake yalimaanisha udanganyifu na uzushi.
Na jumla ya matini yanayothibitisha uadilifu na kuukiri yana nguvu zaidi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka}. [AN NAHL 90]
Na kauli Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka}. [AL AN'AAM 152]
Na kauli Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona}. [AN NISAA 58]
Na kauli yake: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda}. [AL MAIDAH 8]
Na katika Sunna Kauli yake Mtume S.A.W: “Umma huu utaendelea kuwa mwema, ukisema utasema kweli, na ukihukumu utafanya uadilifu,, na ukiombwa kusamehe utahurumia”. Na kauli yake: “Dhulma ni giza katika Siku ya Kiyama”. Pia imepokelewa na Mtume S.A.W, kutoka kwa Mola Muweza, ambapo alisema: “Enyi waja wangu! Mimi Nimejiharamishia dhuluma, na Nimeijaalia kuwa haramu miongoni mwenu”. Na Mtume S.A.W, aliulizwa: Ukabaila ni nini? , akasema: “Kuwasaidia watu wako wawadhulumu wengine”.
Na Mwadilifu ni miongoni mwa Majina ya Mwenyezi Mungu.
7- Mara nyingi kutotambua maana ya Nisbiyyu (Yenye ukomo) na (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo huwa ni kizuizi cha kuzuia kutambua misimamo isiyo na mantiki ambayo hutokea kila siku ndani ya Siasa ya Kimataifa, au ndani ya misimamo ya Madola, na Uhusiano wa Kimataifa; kutokana na sisi kuamini (Mutw-laq) isiyo na ukomo, na tukaijaalia kama kipimo cha haki.
Na kwamba hatufikirii kuwa mmoja miongoni mwa wenye akili anaweza kubadilisha msimamo wake kiajabu kinyume na kinyume zaidi, bila ya kulaumu dhamiri, au kuyarudi matendo yake, bali yeye ameshawishika anavyofanya na kuendelea hivyo.
Katika Semina na Taasisi moja ya Kijerumani kuhusu suala la Uadilifu, Mheshimiwa Mufti alitaja kuwa: Uadilifu katika Uislamu ni Miongoni mwa Majina ya Mwenyezi Mungu, na mmoja wa waliohudhuria alielezea kuwa: kuna katika itikadi ya Wagiriki wa zamani yule aitwaye: Mungu wa Uadilifu.
Na Mheshimiwa Mufti akajibu kuwa: hapo inadhihirika tofauti kati ya: (Nisbiyyu) Yenye ukomo na (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo, na vipi Mungu wa Uadilifu huu asie na sifa ya kuwepo kamwe, na aliyekuwa kama sura tu katika akili ya aliyemwanzisha, hakika amebadilishwa kutokana na kubadilishwa kwa sura yake, pia amebadilishwa wakati watu walipoelewa kuwa: hakuna Miungu mingi.
Na kuhusu Uadilifu ambao ni Sifa miongoni mwa Sifa za Mwenye kutengeneza, hakika unatulazimisha tuwe waadilifu, Kwa sababu Mwenyezi Mungu alitulazimisha kupata tabia zake, na kutekeleza maamrisho yake kwa kutii, na kwa sababu Mwenyezi ni Mwenye kubakia milele. Na hapo tunajua vipi akili hii ambayo ilikuwa kikiiamini miungi mingi, ikajiandaa kuikubali sehemu hii ya kiwango isiyo na mfano.
Kisha tumeendelea kujadiliana kuhusu Suala la Palestina, mara mmoja wa waelezaji akasema: hakika kushikamana kwenu na uadilifu ndiyo huahirisha suala hili, na ni lazima mketi kwa ajili ya majadiliano, na mkubali kilichowezekana na kilichopatikana, na hayo ni yote ambayo mnaweza kuyaomba, na hamuwezi kuuomba uadilifi, kwa sababu uadilifu hauwezekani, bali ni kikwazo na kizuizi cha kufikia amani.
Lakini Mheshimiwa Mufti akajibu akisema: Kuketi kwenye majadiliano ni kitu, na dhana ya uadilifu ni kitu kingine; Kuketi kwenye majadiliano ni lazima kwa ajili ya kufikia amani, na kufanya madogo ya maovu mawili, na kufikia amani ya watu na kuhifadhi mahitaji yao makuu: kuhifadhi nafsi, akili, haki za bianadamu, na heshima yake, n.k.
Lakini matokeo ya majadiliano haya yanaambatana na kanuni nyingine inayojulikana katika siasa, nayo ni (Chukua na uombe), na kama siasa ni sanaa ya uwezekano, basi haitoshi kupata sehemu ya haki, bali itaomba upya kinachowezekana, na hapo maombi yataendelea mpaka uadilifu upatikane.
Kuhusu kukanusha dhana ya uadilifu wenyewe na kuuelezea kuwa hauna faida, hakika ni jambo la hatari na kulijitokeza kutokana na uzito wa hali ya Kiisraili katika akili ya Kimagharibi, ambao unaiharibu kwa upande mmoja, na umeijaalia nje ya mpaka wa mantiki kwa upande mwingine, na sababu ya hayo ni kutanguliza (Nisbiyyu) Yenye ukomo mbele ya (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo, kwa ajili ya kuleta masilahi.
8- Kupitia maana hii tunaweza kueleza misimamo ya Mataifa ya Kaskazini na Mataifa ya Kusini kuhusu Mkataba wa GAT, Hakimiliki na matumizi ya Maliasili, na pia kuhusu dhana ya Ustaarabu pekee, na dhana za Mwisho wa vitu mbali mbali, kama vile: Mwisho wa Historia, Mwisho wa Mwanadamu, na Mwisho wa Ustaarabu… n.k., miongoni mwa walioiita (Ends).
Na uwazi huu wa kutofautisha kati ya (Nisbiyyu na Mutw-laqu) Yenye ukomo na Isiyo na ukomo sio kuenewa kwa kila mtu katika Ulimwengu wa kimagharibi, au Ulimwengu wa sasa, lakini ni hivyo katika akili za Viongozi na Watoaji maamuzi katika nyanja za Siasa na Fikri, na pia kwa wengi wa Maprofesa, na Wafanyakazi wa vyombo vya habari.
Kwa hiyo tunaona pia watu wengi wanahisi upinzani kati ya itikadi yao ya maadili Jumla na maamuzi ya serikali zao, viongozi wao, na mienendo yao, kwa hiyo tunaona Taasisi nyingi za jamii ya kiraia zinapinga Vita dhidi ya Iraqi, na kupinga Utandawazi na Uzayuni, n.k.
Na wao hawafikirii kuwa: hivyo ni kwa ajili ya kutanguliza (Nisbiyyu) Yenye ukomo mbele ya (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo au kwa ajili ya kukanusha (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo yenyewe. Na Nadhria ya Uwiano ni kukataliwa kwa ndani yake, ambapo imani yenyewe ya uwiano jumla hukusanya (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo, kwa hiyo mtu yeyote -hata wale- hawezi kuondoa imani ya (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo, na kama kwamba yeye amelazimishwa kwa imani hiyo.
9- Waislamu wameathiriwa kwa dhana ya (Nisbiyyu) Yenye ukomo na (Mutw-laqu) Isiyo na ukomo katika maandishi yao. Tumewaona wakianza kukiri kwa Imani jumla, na kwa kinachopelekea kwenye imani hiyo, kama vile: Imani ya Mwenyezi Mungu, Mitume wake, Maadili Mema ya Juu ambayo tumeyaelezea hapo juu.
Na hii inadhihirika mwanzoni mwa vitabu, ambapo wanaanza kwa kauli: (Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu) ambayo huitwa kwa lugha ya Kiarabu: (Al-Basmalah), na matumizi yake ni mengi katika mwanzo hasa, kisha wanataja baada yake: (Sifa Njema ni za Mwenyezi Mungu), ambapo wamechangia mno sura za usemi huu, kisha wakataja Sala ya Mtume SAW.
Na wanatoa sababu ya kufanya hivyo wakieleza maneno yao kuwa: kuanza maneno kwa usemi wa: (Kwa Jina la Mwenyezi Mungu) na (Sifa Njema ni za Mwenyezi Mungu) kuwa huu ni Ufuasi wa Kitabu Kitukufu (Qur`ani) ambapo kilianza kwa Fatha yake na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote}. [AL FATIHA 1-2]
Na kauli yake Mtume SAW: “Jambo lolote muhimu lisiloanzwa kwa Jina la Mwenyezi ni lenye kukataliwa sana”. Na katika mapokezi mengine: “Kwa Sifa zote za Mwenyezi”. Na katika mapokezi mengine: “Kwa kumbukumbu Mwenyezi Mungu”.
Na kutaja Sala ya Mtume SAW, ni kufauatana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu}, [AL AHZAAB 56]
Na kuomba thawabu nyingi iliyopokelewa katika kauli yake S.A.W: “Mwenye kunisalia Mimi Sala moja, Allah Atamsalia, kwa Sala hiyo, mara kumi”. Na kuutekeleza wajibu wa Mtume S.A.W, ndani ya nafsi zetu, kumuadhimisha, kumheshimu, na kumpenda.
Na kupitia tangulizi za vitabu hivi ambazo ni afadhali kufanywa ndani yake uchunguzi muhimu kwa kuanzia kukiri huku yaani kukiri wa Mutw-laq (Isiyo na ukomo) ambapo wanataja Suala la Uumbaji, na ulimwengu kuzunguka kwetu, na wakataja neema ya Mwenyezi Mungu ya kutuelimisha, maamrisho, makatazo, na ukalifishaji, na wakataja kitu cha kutia wasiwasi wa maisha, matatizo, kazi na shughuli zake, wakakiri ukomo wa mwanadamu na udhaifu wake, na kuwa mwanadamu anahitajia kuongeza maombi ya msamaha wa Mwenyezi Mungu, pamoja na kuomba msaada na kuongoza kwa shukrani hii ambapo alianza nayo. Na huenda wakakiri Shahada Mbili kama utangulizi wa kimaarifa ambao unaunganisha kati ya wanavyosema kuhusu (Nisbiyyu) Yenye Ukomo, na wanachokiamini kuhusu (Mutw-laq) Isiyio na ukomo.
10- Utawaona wakisema mwishoni mwa jitihada yao au utafiti wao: (Mwenyezi Mungu ni Juu kabisa na Mjuzi kabisa) au (Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kabisa). Na neno hili ni lenye hekima, na huonesha mambo, miongoni mwake ni: kutangaza kuwa elimu ya mwanadamu ina ukomo, na hisia zake za kutambua mambo ya maisha yanayomzunguka nazo pia zina ukomo, na akili ambayo ni mahali pa kufikiri na chombo chake pia ina ukomo.
Hayo huonesha kuwa: ingawa mwanadamu ana jitihada na kutendeana na maisha na kuchunguza, lakini anakiri kuwa ana ukomo. Na hayo huzuia nafsi yake isije kushawishika au kujiona kwa kile alichokifikia. Na kutoa fursa kubwa kwa masuala ya ukweli, yakini, na lazima, mbele ya masuala ya dhana.
Na katika hekima ya neno hili pia kuwa: mwanazuoni huyo yuko tayari kubadilisha aliyoyakosea, na kuyaacha haraka pale anapopata dalili ya haki, na kutangaza kuwa: elimu haijui neno la mwisho; kwa hiyo hawezi kamwe kupata ujinga, kama walivyoelekea baadhi yao. Na katika hekima ya usemi huu pia kuwa: mwanazuoni anarejesha elimu kwa watu wake, na Mwenyezi Mungu ndiyo aliyemfundisha mtu aliyokuwa hayajui, kama alivyotaja katika kauli yake: {Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui}. [AL ALAQ 5]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu}. [AT TAWBAH 114]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakuilimisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu}. [AL BAQARAH 282]
Na katika asili ya uumbaji, ambapo anasema: {Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote}. [AL BAQARAH 31]
Na kurejesha elimu kwa Mwenyezi Mungu kuna leta faida mbili kubwa. Kwanza: kiwango cha kufikiri vizuri kwa ubora kinachounga nyanja za maisha na hakika zake, na kuwa dunia imeumbwa na Muumbaji, na Mwenyezi Mungu hakutuacha bure baada ya kutuumba, kwa ajili hiyo anasema Mwenyezi Mungu: {Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa}? [AL MUMINUN 115]
Faida ya Pili: ni ya kinafsi ambayo huambatana na mwanazuoni mwenyewe, ambapo unyenyekevu wake kwa Mwenyezi Mungu unazidi kila ilipozidi elimu yake, na yeye anajua kwa yakini maana ya kauli yake Mwenyezi: {Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi}, [YUSUF 76] na maana ya kauli yake Mwenyezi: {Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu}, [AL ISRAA 85]
Na miongoni mwa hekima za usemi huu mkubwa ni kuwa: mwanazuoni anaacha eneo kwa ajili ya uchunguzi wa wanazuoni wengine wanaomfuata.
11- Maana hizi za juu zilizozunguka kauli ya wanazuoni (Mwenyezi ni Mjuzi zaidi) ndiyo zimekosolewa na wale wanaojiingiza kwenye kazi zisizo zao bila elimu, wale ambao Mtume SAW, amewanasihi akisema: “Katika uzuri wa Uislamu wa mtu, ni kuliacha lisilomhusu”.
Utawaona wale wakijadili kila aina ya maarifa bila elimu, na wakadhani kuwa: wakimaliza maneno yao kwa usemi wao: (Mwenyezi ni Mjuzi zaidi) basi watasalimika na jukumu, na malipo mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini si hivyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu ametuongoza kwenye jukumu la neno na umuhimu wake, hivyo Mtume S.A.W, anasema: “Mshauri anaaminiwa”, na pia anasema: “Mwenye kutolewa Fatwa bila ya elimu, hakika dhambi yake itamhusu mwenye kutoa Fatwa hii”.
12- Unaona wanazuoni hawa katika vitabu vyao – hata katika masuala muhimu zaidi – wakiangalia suala la Almutw-laqu na Nisbiyyu kwa njia madhubuti sana, hasa kupitia lugha, kuhusu uhusiano kati ya Muumbaji na Muumbwa.
Utawaona wakiamua kuwa: lazima tuitoe Dhati ya Juu, yaani Mwenyezi Mungu nje ya muktadha wa Malimwengu, na Mwenyezi lazima ahusishe nje ya matumizi na maana ya maneno ya lugha.
Na lililotegemeza hilo ni kauli ya Sheikh Al-Amiir: “Jina Karima ni hakika, na katika Al-Itqaan anasema: Majina Pekee kwa ujumla ni ukati kati wa ukweli na sitiari, kama kwamba yeye aliangalia kuwa: hayo siyo miongoni mwa lugha asili, na haifichiki kuwa: hayapungui yakawa ya istilahi ya mazungumzo.
Ni dhahiri ni: kutokuwa na sitiari hata kidogo, na kama tukisema: nayo ni jumuishi kutokana na asili yake, na kwa upande wa sehemu ya kiwango- kwa kuzingatia hali yake hasa- ni sitiari; ambapo hakuna kizuizi cha kuyahusisha Majina yake Mwenyezi yawe Pekee, na kuyaainisha kwa sifa za juu, kama walivyojaalia Uainishaji wa Upekee wake ni juu kuliko Kiwakilishi… n.k.”.
Na ilivyotajwa katika Hashiyat Sheikh Hassan Al-A’attaar, anasema msemaji: “Kuhusu kuzingatia maana ya Tamko la Utukufu ni Dhati ya Mola Mlezi Mwenyezi, na mfano wake: Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu; hayo yote ni lazima yauzuie ulimi usiyaseme hayo na mifamo yake; kwa sababu semi ni aina juu za vitu kama vile: (Jauhar) yaani kitu asili kamili hakihitaji kingine kwa ajili ya kubaki, na (A’aradh) yaani kinachohitaji kingine kwa ajili ya kubaki. Lakini Wajibu Aliyetakasika na Aliye juu , hawezi kuelezwa kwa semi hizi mbili”. [Mwisho}.
Laiti tungeyasoma maandishi yetu ya zamani kwa njia mpya, ambayo yanatuwezesha kuzitoa tunu zake, na kufaidika nazo, pamoja na kutambua ukamilifu wa uhalisia wa maisha, na mahitaji ya maisha ya sasa; na laiti tungefanya hivyo ili kuturejeshea kitu katika ubinadamu wetu, na laiti pia kama tungefanya hivyo ili kuturejeshea kitu katika fikra iliyonyooka.

Marejeo: Kitabu cha Simaatul A’asr, cha Mheshimiwa Mufti wa Misri Dakirai Ali Juma.

 

 

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas