Yasemwayo katika sijida ya kushukur...

Egypt's Dar Al-Ifta

Yasemwayo katika sijida ya kushukuru

Question

Husemwa nini katika sijda ya kushukuru na sijda ya kusahau?

Answer

Mwanadamu atakaposujudu humshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni jambo la Sunna kwake aseme yale anayoyasema katika sijda ya kisomo, atasema kama ilivyokuja katika Hadithi ya Mama wa waumini Aisha R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W.: “Umesujudu uso wangu kwa aliyeuumba, na akawekea usikivu na uoni kwa uwezo wake na nguvu zake” ameipokea Abou Dawoud, na Al-Hakim akazidisha: “Utakaso ni wa Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji”.

Pia kunasuniwa kusema kama ilivyokuja katika Hadithi ya Ibn Abbas R.A. yeye na baba yake: “Ee Mweyezi Mungu niandikie malipo kwa hili, na niondoshee dhambi kwa hili, na nifanye kwako kuwa simulizi njema, nanikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Dawoud” ameipokea Al-Timidhy. Pia ni jambo la Sunna kusema kama asemavyo katika sijda za Swala pamoja na kumhimidi na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi.

Share this:

Related Fatwas