Kuua Kisiasa
Question
Tumepitia ombi lililowasilishwa na ndugu/ Abdulsalaam Abdulmunsif Ally la tarehe 27/03/2013, limepewa nambari: 137 la mwaka 2013 lililokusanya:
Hivi karibuni kumeonekana video iliyotolewa na moja ya makundi ya kidini ya watu wenye siasa kali, ndani yake kunatolewa tangazo kuwa kundi hili litatoa fedha taslimu kwa atakayefanikiwa kuuwa wanadiplomasia na askari waliomo nchini Yemen, hivyo tunahitaji kufahamu hukumu ya Kisharia katika yafuatayo:
Kwanza: Fikra ya kuuwa kwa kulipia fedha.
Pili: Kuuwa watu ambao wanaingia kupitia mwanvuli wa makubaliano ya amani na ulinzi mfano wa wanadiplomasia au watalii au wageni wanaoishi ndani ya nchi za Kiislamu kwa lango la kufanya kazi ndani ya nchi hizo.
Answer
Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na aliyemfuata kwa wema mpaka Siku ya Kiyama.
Asili katika nafsi ya mwanadamu – kwa upanda huo zaidi kuliko ule wa Mwislamu – ni kulindwa na kutofaa kuthubutu kumaliza uhai wake isipokuwa kwa sababu za Kisharia,na hakika Maandiko ya Qurani Tukufu yanaelezea juu ya uharamu wa kuuwa nafsi kwa ujumla wake kinyume na haki, ndipo Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala musiiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuiuwa isipokuwa kwa sababu za Kisharia} An-Aam: 151, Imamu Ar-Razy amesema katika tafasiri yake 13/179 chapa ya Dar Ihyaau At-Turaathi Al-Araby: “Asili katika kuuwa nafsi ni jambo lililoharamu, na uhalali wake hauthibiti isipokuwa kwa dalili ya wazi”.
Bali Mwenyezi Mungu amefanya kuuwa nafsi – ya Mwislamu au si mwislamu – kinyume na haki ni sawa na kuuwa watu wote. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa sababu hiyo tumeandika kwa Wana wa Israel kuwa mwenye kuuwa nafsi pasi ya muuliwa kuuwa au kuleta uharibifu duniani basi ni sawa na kuuwa watu wote, na mwenye kumwacha hai mtu mmoja ni sawa na kuacha hai watu wote} Maidah: 32.
Amesema Imamu Ar-Razy pia katika tafasiri yake 11/344: “Makusudio ya kufananishwa kuuwa nafsi moja ni sawa na kuuwa nafsi nyingi: Ni kufikia kiwango kikubwa cha kupewa uzito jambo la kuuwa kwa makusudi na kiuadui kwa maana: Kama vile kuuwa viumbe wote ni jambo kubwa kwa mtu yeyote yule, vilevile ni lazima kuwe kuuwa nafsi ya mwanadamu mmoja ni jambo kubwa”.
Hadithi imepokelewa na Imamu Bukhari katika sahihi yake kutoka kwa Ibn Umar R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Muumini hatoacha kuwa na nafasi kwenye dini yake wakati wote ambao hajafikwa na damu haramu”.
Katika kuhusishwa asiyekuwa mwislamu – Ambaye hazingatiwi mpiganaji vita – amepokea Imamu Bukhari kutoka kwa Abdillah Ibn Amru R.A. kuwa Mtume S.A.W.
Amesema: “Mwenye kuuwa mtu mwenye makubaliano basi hatonusa harufu ya Peponi, na harufu yake inapatikana umbali wa mwendo wa miaka arobaini”.
Na kwa maelezo hayo watu wageni waliomo ndani ya nchi za Kiislamu kama vile Wanadiplomasi au watalii au wageni wanaoishi ndani ya nchi ya Kiislamu kwa lengo la kufanya kazi, asili katika nafsi zao ni kuzuiliwa kufanyia uadui wa aina yeyote, kwani uwepo wao ndani ya nchi ya Kiislamu kunatokana na kupewa kwao visa ya kuingia, na visa hii ni sehemu ya makubaliano ya amani na usalama: Ni makubaliano ya Kisharia na makubaliano yanayolazimisha kwa mwenye kuthibiti kwake uharamu wa nafsi yake na mali zake.
Kwani Sharia Tukufu imeamrisha kutekeleza ahadi au makubaliano, na zimekuja dalili za Kisharia za ulazima wa utekelezaji kwa ujumla kwenye makubaliano yote, kwani Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi watu tekelezani makubaliano} Maidah: 01. Amesema Mwanachuoni Abu Suud katika tafasiri yake 3/2 chapa ya Dar Ihayaai turathu Al-Araby: “Kusudio la makubaliano: Yanayokusanya ni yote yaliyolazimishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake na kuwapa amri na hukumu za kidini, na yale wanayokubaliana wao kwa wao miongoni mwa makubaliano na mikataba ya mashirikiano na mfano wake katika yanayo lazimisha kutekelezwa.
Imepokelewa na Hakimu pamoja na Baihaqy na wengine kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Waislamu huthibiti kwenye sharti zao pale zinapokubaliana na Sharia”.
Imamu Bukhari pamoja na Imamu Muslim wamepokea kutoka kwa Amiri wa Waumini Ally Ibn Aby Talib R.A. kuwa amesema: Hatuna kitabu tunachokisoma isipokuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sio hili gazeti, anasema akalitoa likiwa limeandikwa: “….amani ya Waislamu ni mmoja, hutekelezwa mpaka na wa mwisho wao, mwenye kuvunja amani ya Mwislamu basi laana ya Mwenyezi Mungu ipo juu yake na ya Malaika pamoja na watu wote, na Siku ya Kiyama hatokubaliwa matendo yake”.
Haafidh Ibn Hajar Al-Askalany amesema katika kitabu cha Fat’hul-Bary 4/86 chapa ya Salafiah: “Maana ya jukumu la Amani ya Waislamu ni sawa sawa amani hiyo imefikiwa na Mwislamu mmoja au wengi awe mwenye utukufu au wa hali ya kati na kati, pindi Mwislamu mmoja anapoingia kwenye makubaliano ya amani na kafiri basi hapaswi Mwislamu yeyote kuvunja na kukiuka makubalianao hayo, inakuwa sawa katika hilo mwanamume mwanamke mtu huru na mtumwa, kwa sababu Waislamu ni sawa na nafsi moja”.
Na kwa maelezo hayo hukumu ya mtu mwenye makubaliano ya amani: Ni kuthibiti amani kwake, na ulazima wa kulindwa yeye mali yake na heshima yake katika hilo ni sawa sawa na wazawa na wananchi kwa ujumla, ikiwa patafikiwa makubaliano ya amani na asiyekuwa mwislamu kupitia Imamu au kupitia kwa Mwislamu mwengine basi ni lazima kwa Waislamu wote kutekeleza makubaliano hayo hivyo haifai kumuuwa yeye mwenyewe wala kufanywa mateka wala kuchukua chochote katika mali yake wala kufanyiwa kero na maudhi.
Visa ya kuingia nchini inazingatiwa ni aina katika aina za makubaliano ya amani yanayozingatiwa na Fiqhi ya Kiislamu – kwa kuongezea yenyewe ndio inayotumika na kukubalika na makubaliano ya kimataifa – ambapo imepitishwa kuwa usalama unafikiwa makubaliano Kisharia kwa kila chenye faida, yawe makubaliano hayo ni kwa kauli au maandishi au ishara au hata mazoea, na kila chenye kutimiza lengo kiwe kwa lugha ya wazi au kwa maandishi, na kwa lugha yeyote ile itakayotumika bali usalama Kisharia hupewa pia hata yule mwenye kudhani yupo kwenye makubaliano ya usalama hata kwa kukosea, wala haifai kwa Waislamu kuyavunja na mali zake na amani yake ni vyenye kuzuiliwa kufanyiwa madhara yeyote.
Katika hayo ni pamoja na yaliyokuja kwenye vitabu vya madhehebu manne yenye kufuatwa kuhusu katika hali ya kivita – nayo ni hali mbaya zaidi kitendo tu cha asiyekuwa mwislamu kuingia ndani ya nchi ya Kiislamu akiwa si mpiganaji vita – anasema Imamu As-Sarkhasy katika Maimamu wa Abu Hanifa ndani ya kitabu sherhu sairi al-kabiiir 1/289, 290 chapa ya shirika la matangazo la Kimashariki: “Hata ikiwa askari Mwislamu akaashiria ishara ya amani kwa mshirikina akiwa ngome au akaashiria kwa watu wa ngomeni kwa kufungua mlango, au akaashiria maana ya amani kwa kuashiria mbinguni kisha washirikina wakadhania kuwa ishara hiyo ina maana ya amani kwao basi na wafanye walichoamrishwa, kwani inaweza kuwa hiki alichofanya kinafahamika kati ya Waislamu na watu wa vita kuwa pindi wao wanapofanya kitu kama hiko inakuwa ni ishara ya amani, na likawa hilo si lenye kufahamika basi hiyo inafaa kuwa ndio amani kwa nafasi ya kauli yake: Nimewapa amani, kwa sababu jambo la amani limejengwa kwa upana na kuhifadhiwa na kile kinachofanana na uvunjaji wa makubaliano ya lazima ya amani ikiwa inafahamika kati yao, kilichothibiti kwa mazoea ni sawa na kilichothibiti kimaandiko, na ikiwa haitofanywa ni amani basi inakuwa ni uvunjaji wa amani, na kama haitokuwa inafahamika na kukutana na dalili ya hali inayokuwa mfano wa mazoea au ikawa na nguvu zaidi ya mazoea nayo ni kufuata kwao hali hiyo na zile ishara zinazotumika kwao, hiyo inakuwa ni dalili ya wazi zaidi ya amani na usalama, hivi haoni kuwa wao ikiwa watasema kuwaambia: Tokea ili tuvunje hii ngome kisha wakatoka kuwa hawatokuwa salama?
Hafidhi Abu Umar Ibn Abdulbarr mfuasi wa madhehebu ya Imamu Malik amesema katika kitabu cha Istidhkaar 5/35: Kila anachozingatia mtu wa vita kuwa ni amani kuanzia maneno au ishara basi hicho ni amani, inapaswa Waislamu wote kutelekeza amani hiyo.
Sheikh Khatibu Sharbiny amesema katika kitabu cha Al-Mughny Al-Muhtaj miongoni mwa vitabu vya Mashaikh wa madhehebu ya Imamu Shafii 6/52 chapa ya Al-Halaby: Inafaa kuwa jibu la amani kila tamko linalomaanisha makusudio yake kwa uwazi, kama vile nimekuajiri na nimekupa amani au neno usichanganyikiwe, kama vile kuwa upendavyo au kuwa utakavyo na inafaa kuandikwa.
Na amesema katika kitabu cha Iqnaai cha Imamu Al-Hajawy na sherehe yake kitabu Kashaafu Al-Qinaai cha mwanachuoni Al-Bahuuty 3/106, 107 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Ilmiya: “Inafaa kuwa ni amani kwa kila chenye kumaanisha miongoni mwa kauli na ishara yenye kufahamika hata kama upo uwezo wa kutamka, kwa kauli ya Umar, naapa kwa Mwenyezi Mungu lau mmoja wenu ameashiria kwa kidole chake mbinguni mbele ya mshirikina kisha akakiteremsha ikiwa ni ishara ya amani kwake basi atakayemuuwa nami nitamuuwa yeye kwa kumuuwa kwake”, tafauti na mambo ya kuuza na talaka pamoja na kulinda damu pamoja na jambo linahitaji ishara, kwa sababu wengi wao hawafahamu maneno ya Waislamu, hivyo pindi Mwislamu anapomwambia kafiri wewe upo kwenye amani basi ameshampa amani, kwa kuali yake Mtume S.A.W. siku ya ufunguzi wa Makka: “Mwenye kuingia kwenye nyumba ya Abi Sufyan basi yupo kwenye amani” au Mwislamu akasema kumwabia kafiri: Hakuna ubaya wowote kwako atakuwa amempa amani, kwa sababu Umar pindi alipomwambia Harmazan: Zungumza hakuna ubaya wowote kwako, kisha akataka kumuuwa, akaambiwa na Anas pamoja na Zubeir: Umempa amani hauna njia wala sababu nyengine yeyote kwake, au akamwambia kafiri Nimekupa kazi au nimekuajiri; kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Kwa hakika tumempa kazi uliyempa kazi ewe Mama Hany”, au akasema kumwambia kafiri au mshirikina: Simama au inuka au usihofu au usiogope au hakuna hofu yeyote kwako au weka chini silaha yako basi atakuwa amempa amani, kwa dalili ya hilo kwake.
Imethibiti kwa hayo kuwa kutoa visa ya kuingia nchini ni amani, na inakuwa katika yanayopelekea hii visa ikiwa ni makubaliano ambayo lazima yatekelezwe, na makubaliano hufanywa kwa sura ianyomaanisha hivyo, ikiwa asiyekuwa mwislamu ameingia kwenye nchi ya Kiislamu kwa malengo yeyote katika malengo kama vile – utalii au mambo mengine – basi anakuwa ni mtu wa amani wala haifai kudhuriwa yeye mwenyewe wala katika mali yake, na kudhuriwa kwa kuuwawa au kero zengine ni dhambi kubwa kwa kudhuriwa pamoja na kuwa chini ya usalama wetu ambao tumemdhaminia kwa kumruhusu kuingia nchini kwetu kwa njia halali.
Imamu Bukhari amepokea katika sahihi yake kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mambo manne mwenye kuwa katika mambo hayo ni mnafiki moja kwa moja, na mwenye kuwa na jambo moja kati hayo anakuwa na sehemu ya unafiki mpaka aache, pindi anapoaminiwa hukosa uaminifu, anapozungumza huongopa, anapofanya makubaliano hukiuka, na pindi anapoingia kwenye ugonvi hongopa zaidi”.
Sharia imetoa ahadi kwa watu wa mfano huu ambao huvunja na hukiuka makubaliano ya amani kuwafehesha kukubwa Siku ya Kiyama, imepokelewa na Ibn Maja kutoka kwa Amru Ibn Al-Hamiq Al-Khazaai R.A. amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.: “Mwenye kumhakikishia mtu amani kwenye damu yake kisha akamuuwa basi mtu huyo Siku ya Kiyama ataongoza bendera ya wakiukaji wa makubaliano”.
Vilevile Sharia imekataza kuuwa watu waliojisaha, kwani imepokelewa na Abudardai pamoja na Hakim kutoka kwa Abi Hurairah R.A. amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Muumini hauwi, Imani imezuia kuuwa”, maana ya Hadithi ni kuwa: Imani huzuia mauaji.
Katika uharibifu mkubwa ni kuwa vitendo hivi viko nje ya hukumu ya Uislamu kwani vinazidisha kuenezwa kwa tuhuma batili ambazo wanaziambatanisha na maadui wa Waislamu kwenye dini ya Uislamu, na wakiwa wataka kuchafua sura ya Uislamu kuwa ni dini ya kijinga na umwagaji damu, lengo lake ni kutenza nguvu watu na kuleta uharibifu duniani, haya yote ni kuzuia kwa Mwenyezi Mungu na kwenye dini yake.
Miongoni mwa uharibifu mkubwa pia: Ni pamoja na yanayofungamana na hayo miongoni mwa mateso kwa Waislamu waliopo baadhi ya nchi za kigeni wakifanyiwa na watu wenye sera za ubaguzi, wanafikwa na kero nyingi kwao wenyewe na kwa familia zao mali zao na heshima zao, baadhi yao wakilazimika kuendelea na misimamo yao na kubakia kwenye dini yao na wengine wakiachana na dini yao.
Wanachuoni wameelezea kuwa ikiwa kutakuwa na mgongano kati ya masilahi na uharibifu, basi kuondoa uharibifu ndio hutangulizwa kwanza kuliko kuleta masilahi, na maneno yao haya ni kwenye masilahi yaliyofikiwa basi ni namna gani ikiwa masilahi yanadhaniwa au hayapo?
Ama kutumia mali kwa mtu mwengine ili kufanya kazi ya hiyo ya mauaji, inazingatiwa ni katika kazi chafu ambazo hazikubaliki makubaliano, kutumia mali hizi kwenye hili ni katika uchochezi na kuzikubali ni katika uchochezi ambao yote hayo mawili ni haramu Kisharia.
Ama ni kazi hofu na chafu haikubaliki makubaliano, ni kwa sababu zinamanufaa yaliyo haramu – nayo ni uuaji – na manufaa yaliyo haramu yanahitajika kuondolewa, na kutoa kazi kwenye hilo kunafanya kazi ya kurejesha na kuwa kinyume na makusudio ya Sharia.
Amesema Mwanachuoni Al-Bahuty katika kitabu cha Rawdha Al-Murabba ukurasa wa 410 chapa ya Dar Al-Muayyidu – Taasisi ya Risalah: “Haifai kutoa kazi kwenye masilahi haramu….” Kwa sababu manufaa haramu yanahitajika kuondolewa na kutoa kazi hizo kunapingana”.
Ama kuwa haifai kutumia mali katika uchochezi wala kuikubali mali kwenye kazi za uchochezi kwa sababu kufanya hivyo ni kusaidia maasi, na Mwenyezi Mungu Amesema: {Na saidianeni kwenye wema na ucha-Mungu na wala msisaidiane kwenye dhambi na uadui} Maidah: 02.
Al-Hafidh Ibn Kathiir amesema katika tafasiri yake ya Aya 2/106 chapa ya Dar Tiba: “Mwenyezi Mungu Mtukufu Anaamrisha waja wake Waumini kusaidiana kwenye kufanya matendo ya kheri, nayo ni wema na kuacha makatazo, nayo ni ucha-Mungu, na anawakataza kusaidiana kwenye mambo batili, na kushirikiana kwenye madhambi na yaliyo haramu”.
Amesema Imamu Al-Qurafy katika kitabu cha Dhakhiirah 5/422 chapa ya Dar Al-Gharbi Al-Islaamy: “Ikiwa atampa kazi ya kuuwa mtu kwa njia za dhuluma na akamuuwa basi hana malipo kwa sababu kilichoharamu hakina nafasi yeyote Kisharia”.
Amesema Imamu Al-Umrany katika kitabu cha Al-Baan 7/288, 289 chapa ya Dar Al-Minhaaj: “Wala haifai kuajiri mtu kwenye manufaa yaliyo haramu….” Dalili yetu ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenyezi Mungu ameilaani pombe na mbebaji wake”. Ikiwa kubeba pombe ni haramu, tukasema: Manufaa yake ni haramu, wala haifai kuchukua thamani yake kama vile kwenye mzoga na damu.
Na Sheikh Al-Islaam Zakaria Al-Ansary amesema kwenye kitabu cha Asnaa Matalib 1/569 chapa ya Dar Al-Kitabu Al-Islaamy: “Kama ilivyo haramu kuchukua malipo kwenye jambo la haramu ni haramu pia kutoa hayo malipo” kwa sababu katika hilo ni kusaidia maasi.
Na kwa maelezo hayo kupitia swali halisi: Vitendo vya mauaji pamoja na kutumia mali na kuchukua mali kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, yote hayo ni katika mambo yanayozuiwa na ni haramu ambayo Sharia ya Kiislamu hairuhusu wala kuyakubali.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.