Urithi wa Kiislamu na Mitazamo yake...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu na Mitazamo yake kwa Ujumla

Question

 Ni ipi mitazamo jumla ya urithi wa Kiislamu ambayo husaidia kwenye ufahamu sahihi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Katika muktadha wa uchambuzi wetu wa kanuni ya urithi, tutajaribu kuelezea kipengele cha Mitazamo Jumla ambayo inachukuwa nafasi kwenye mawazo ya waandishi wa urithi wa Kiisilamu kwa ujumla. Mitazamo hii Jumla kwao huanza na fikra ya uwepo. Uislamu unatambua ukweli wa kimsingi ambao ni mwanadamu, ulimwengu, na uhai vyenye kuumbwa na Muumba, na kutambua ukweli mwingine nao ni kuwa maisha haya na ulimwengu ni vyenye kwisha, na kiyama kitasimama na kumaliza wanadamu, kisha baada ya hapo kuna siku ya kiyama ambayo watu watahesabiwa, ima waadhibiwe au walipwe thawabu, fikra ya Kiislamu inatofautiana na fikra za watu wengine katika kutambua kimsingi kuwa mwanadamu ni mwenye kuumbwa, na kuwa ni mwenye kurudishwa kwa Mwenyezi Mungu baada ya hapo kwa ajili ya hesabu na adhabu au thawabu.
Falsafa za Magharibi hivi sasa zinakwepa upande huu, nao ni upande muhimu umekuwa unatengeneza muundo wa kifikra kwa waandishi wa urithi huu, misimamo yao katika kadhia za uwepo ina mitazamo yake na misamiati yake ambayo inapaswa kuiangazia.
Tumeelezea – katika maudhui zingne – alama kuu za mtazamo wa hawa watangulizi wa falsafa ya uwepo, uhai, na mwanadamu, na kubainika kuwa kwao mitazamo hii mitatu ndio muundo wa Kimungu kutoka kwa Mwingi wa hekima na uwezo, Mwenye uhai wa kudumu, wameleta mtazamo wa uwepo kwa hukumu za kiakili kati ya Ulazima wa Kuwepo “Kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, au mwigine kama athari za rehma zake ambazo zinawajibisha kutokana na sifa zake nzuri: Mwenye kurehemu” na Uwezekano wa kuwepo “Nao ni ule unaokusudiwa uwepo na kutokuwepo, kama vile sifa ya viumbe vyingine” na Kutowezekana kuwepo “Nayo ni hali ya uwepo wake kama vile kukutana kwa vinyume viwili au kama vile kumuingiza ngamia kwenye tundu la sindano” na Uwezekano wake upo “Kama vile ndege mwenye mbawa mbili” na Uwezekano wake haupo “Kama vile ndege mwenye mbawa tano”.
Na uwepo wake wenye Upendeleo na usio na Upendeleo: Aina ya kwanza ni kama vile jicho na kiini, au kitu ambacho kina upendeleo au umiliki, na Usio na upendeleo ni kuonesha nako kuna aina tisa na hukumu saba, na vyote hivyo vimeshaoneshwa kwa sura inayojitosheleza na kutorudia, lakini ni namna gani mtazamo wa kijumla umegusa elimu zote ambazo zimetangulizwa na wazalishaji wa urithi wa Kiislamu, na ni vipi imechimbuka kutokana na mtazamo huu wa kijumla baadhi ya mitazamo mingine ambayo inapaswa kueleweka na kufahamika?
Miongoni mwa mitazamo iliyozaliwa kutokana na mtazamo huu wa Jumla ikiwa ni pamoja na Kadhia ya Nguvu na Kitendo: Nguvu ni nini? Na nini Kitendo? Na kutolea mfano wa hilo “Kisu chenye Kukata”. Tulisema - hapo awali - kwamba miongoni mwa hukumu za kuonesha ni kuwa haikusanyi, je inaweza kuwa uwongo kusema kuwa kisu chenye kukata wakati ambao sikitumii? Nini tafauti kati ya kisu kikiwa juu ya meza na kati ya kisu kikiwa kinafanya kazi ya kukata? Hapa wakasema: Ikiwa kinachoitwa jina la “Nguvu” na kuna kile kinachoitwa kwa jina la “Kitendo” kwa maana ya wametenganisha katika wasifu wa kitu kati ya nguvu na kitendo.
Kisu wakati wa kukata ni chenye kukata "Kwa kitendo” kwa sababu hivi sasa kinafanya kitendo hicho cha kukata, ama kikiwa juu ya meza chenyewe ni chenye kukata kwa nguvu, kwa sababu kazi yake kwa maana ya umaalum wake – sasa hivi sio – kukata, ikiwa kama kitatumika kwenye kukata basi kitakata, tofauti hapa inaweza kufahamika kwa wepesi sana. Na jambo hili, kwa maana ya tofauti kati ya kilicho kitendo katika harakati ya kitu na kati ya nguvu, imetumiwa na akili za Wanachuoni kwenye pande mbalimbali za urithi, kuanzia wasomi wa elimu ya maneno Wanasarufi Wanafiqhi na wengine, lau tungelikuwa tumefahamu mfano wa kisu na kuuelewa basi kungekuwa katika akili zetu na mfano wa kupimia, na kuwa na uwezekano kufahamu yale tunayoyaona yakienea kwenye matini na maandiko ikiwa ni pamoja na maana ambazo zinaelezea huo mtazamo kama tutakavyoelezea.
Kadhia ya Pili kwao na inayotokana na mtazamo Jumla ni - Kadhia ya hatua za uwepo, kwao ni hatua Nne tulizozieleza hapo mwanzo: Uwepo machoni, Uwepo akilini, Uwepo kwenye ulimi na Uwepo kwenye muundo, hatua hizi Nne – pamoja na kutofautiana majina yake na namna zilivyoitwa na Wanachuoni na Wataalam wa urithi mbalimbali – ispokuwa yenyewe imekuwa ni sehemu ya jambo muhimu katika mitazamo yao rai zao na maandiko yao.
Kuna uwepo kwenye macho na wanaita kwa jina la “Nje” nalo ni neno maana yake ni vitu vilivyo nje ya mwanadamu, mfano kama kalamu kiti meza nyumba na vingine, kwa sababu mwanadamu ana uwezo wa kufunika jicho lake na kufikiria vyote hivi akilini mwake, hivyo kunakuwa na uwepo wa aina mbili wa kitu: Uwepo wa Nje unaitwa “Kilichomo machoni”: na uwepo wa Ndani unaitwa “Kilichomo akilini” na linakuwa neno Nje msamiati mkuu unaotumika kwa wepesi, na wanasema katika maneno yao kuhusu hiki kitu: “Na hiyo ni kwa vile hakimo akilini bali kipo Nje”.
Tofauti kwao imeendelea kati ya kipi kilicho machoni “Cha Nje” na kipi kilichomo akilini “Cha Ndani” mpaka wakaingiza muundo wa kilugha na falsafa ya kilugha katika kadhia, wakasema: Hakika mwanadamu miongoni mwa sifa zake kuu ni lugha.
Maneno haya ambayo hutoka kinywani yanaonesha picha zilizomo akilini zinazokubaliana na uhalisia wa nje, na katika hilo kuna uwepo wa tatu, nao ni Uwepo wa Ulimi.
Ikiwa ulimi unafanya kazi na kutamka neno kwa mfano “Peni” na kutoa sauti inayotikisa hewa na kufika mpaka sikioni mwa mwenye kuambiwa kwa tamko la “Peni” hata ikiwa hiyo “Peni” yenyewe haipo “Kutokuwepo machoni” lakini kufika neno sikioni na kusikika na mwenye kuambiwa kunazalisha akilini mwake sura ya hiyo peni.
Hili ndio jukumu la lugha, kwa sababu sisi badala ya kuleta kile tunachotaka kukielezea basi tunabadilisha na kuonesha kwa ishara, maneno yanayozalisha picha akilini. Hivyo Uhusiano kati ya neno "Peni" na kati ya peni yenyewe ni uhusiano wa “Mjulishaji” na “Kinachojulishwa” neno “Peni” lenye kujulisha, na hiki kitu Peni wakati huo huo chenye “kujulishwa”.
Kwa hiyo, miongoni mwa mitazamo yao Jumla inayotokana pia na tofauti kati ya Mjulishaji na Kinachojulishwa, kwa mfano neno “Peni” inawezekana kuandikwa kwa njia tofauti, kwa mfano nitaliandika neno qalam, yule anayefahamu herufi za kilatini huenda akasoma – Kisauti – kama lilivyo “Qalam” na yule asiyejua herufi za kilatini atajizuia hata kama anafahamu “Qalam” kiakili na kiuhalisia, kwa sababu hii ni ibara tu ya mjulishaji au mjulishaji wa kitu, kisha hati iliyoandikwa inafanya kazi ya mjulishaji, vile vile neno lenye kutamkwa.
Na mfano wa hivyo pia kwao kumekuwa na uwepo wa machoni, uwepo wa akilini, uwepo kwenye ulimi na uwepo kwenye muundo, na uwepo wa aina mbili za mwisho hufasiri uwepo wa aina mbili za mwanzo, na huenda usipate neno kuhusu uwepo huu katika urithi kwa sura ya moja kwa moja, ambapo elimu inagawanyika makundi na kuongezeka kutokana na urithi huu, kwani tunaweza kumkuta muandishi wa elimu ya urithi anaelezea kuhusu uwepo kwenye muundo kwa maana ya “Uandishi” na huenda akaelezea yaliyomo ulimini kwa maana ya “Tamko” na kuelezea yaliyomo akilini kwa maana ya “Kitendo” au “Fikra” au “Kilichomo ndani” au “Kilichopo kwa Mwanadamu” au akaelezea kilichopo machoni kwa maana ya “Nje” hivyo ibara zikatafautiana.
Lakini muundo huu wa mwisho ambao umetumiwa na Wanachuoni – baada ya mlimbikizano wa fikra zao kwa muda mrefu – walitaka kuongezea kitu kizuri kinakuwa ndani yake kina aina ya muziki, wakasema: Macho akili ulimi na muundo, wakati ambapo wote hawakuwajibika navyo, hivyo ni jukumu letu kuvuka hatua ya maneno na kwenda kwenye maana, na kufahamu kuwa sisi tupo kwenye uwepo wa madaraja tafauti.
Hivi sasa tunajaribu kuelezea andiko la urithi ambalo tumelielezea katika maudhui ya “Urithi wa Kiislamu – tangulizi za kimbinu na jaribio la utekelezaji wa vitendo” ili kufahamu ni namna gani huonekana mtazamo jumla kwa Waislamu ndani ya Kitabu chao, ili tufahamu ni vipi walikuwa wanaufahamu ulimwengu na mahusiano mbalimbali, na namna gani walikuwa wanashirikiana na ulimwengu, anasema mtunzi:
“Kitabu cha mambo ya mauzo mwisho wake kinahusu ibada kwa sababu ni katika kazi zilizobora, na kuelekea kwenye hayo ni kwingi na uchache wa watu wanaofanya hayo, na neno lake kwa asili ni kitenzi kisicho ukomo”
Hapa anazungumza kuhusu uwepo kwa kutumia ulimi na kuonekana kwa macho, na anaashiria uwepo akilini, kwa mfano neno “Kuuza” linazingatiwa ni neno ima litakuwa limehifadhiwa kwa muundo wa maandishi au kutamkwa kwa ulimi, lakini kwa upande wa tukio “Matendo” nayo ni uwepo wa machoni, na neno kuuza linatokana na “Kitenzi kisicho ukomo” nacho ni kuwepo akilini.
“Hivyo kimefanywa kwenye umoja” na hilo ni kwa vile akilini mwetu maana ni neno moja na ukweli mmoja, kwenye akili wanaita uelewa wakati ambapo machoni wanaita asili na kukubalika, kwa maana kilivyokuwa akilini ndivyo kilivyo machoni, ama neno kukubalika lina maanisha kuamini kilicho akilini, yote haya yalikuwa yanazingatiwa na Waislamu ni mambo ya awali katika ufahamu wao na ambayo hayahitaji mjadala.
Pamoja kuwa kuna aina nyingi. Hapa tunaelezea aina za “Mauzo” kwa nje, lakini mauzo limekuja kwenye umoja kwa upande wa kiakili ni kwa sababu ukweli wake katika akili ya mwanadamu hauna tofauti, nalo ni neno linalo maanisha “Makutano”, ama uhalisia au kuonekana machoni kuna “Aina nyingi” ikiwa tutaangalia nyingine “Hali ya uwingi” itawezekana kusema: Mauzo kwa maana ya uwingi, kwani kuuza ni kitu kimoja akilini pamoja na kutafautiana umoja wake.
Katika hali ya kwanza huitwa pia “Ujumla” ama katika umoja wa kuuza na aina zake huitwa “Sehemu”, ujumla ni jambo la kufikirika tu ambalo halipo kwa nje, nalo halizuii maana yake kuingia kwenye ushirika na ushirikiano, kama vile ilivyoelezewa, mbele ya neno “Mwanadamu” ikiwa nitafumba macho na kufikiri “mwanadamu” akilini mwangu basi nakuwa wala sifikirii mtu mmoja mmoja kama vile: Zaidi au Amru au….bali nafikiria kikundi cha pamoja chenye watu wote, na kwa hili nakuwa nimemaanisha Ujumla, kikundi hiki cha pamoja hakipo kwa sura ya nje, chenyewe kinakubalika akilini tu, ama kwa sura ya nje huyu mwanadamu anapatikana na kwa kumuongezea baadhi ya vitu ambavyo vinamfanya kuwa ni wa kimaalum na kihaiba, badala ya kuwa kwake mwanadamu tu akiwa ni Zaidi au Amru, na hilo ni baada ya kuongeza kwenye ujumla kinachomfanya awe sehemu na mwenye haiba, hivyo kuwa ni Sehemu ni kule kunakozuia kufikiri maana yake kuwa kuna ushirika, na anakuwa katika hali ya Jumla ni kule kuwa kwake mwanadamu, na anakuwa ni sehemu kama vile Zaidi au Amru.
Na kama hivi uelewa wetu wa neno au matini huongezeka zaidi baada ya kufahamu kwetu “Nadharia ya Jumla” kwao, jambo ambalo linatuwezesha kukubali kukataa na kukosoa, vile vile kujenga kwenye urithi huu.
Anakamilisha: “Kisha linakuwa jina kutokana na uwepo wa yatakayoelezwa, kisha ikakusudiwa moja ya pande mbili za makubaliano”.
Kusudio la maneno “Imekusudiwa moja ya pande za makubaliano” ndio mbinu za mazingatio, hivyo anasema: “Kuuza ni mwenye kuja na kitu akiwa muuzaji, kikitambulika kuwa kinamilikiwa kwa kubadilishana kwa mfumo maalum” kwa maana ya upande maalum, nao ni upande mwengine ambao mwenye kuja kutoka upande huo anaitwa mnunuzi, na hutambulika pia kumilikishwa kwa mabadilshano, inafaa kuitwa mnunuzi muuzaji na kinyume chake, kwa maana ya sura maalum.
Hapa tunakuta muunganiko wa tamko kati ya muuzaji na mnunuzi kutokana na msingi mmoja nao ni mabadilshano, na inafaa kumuita muuzaji mnunuzi na kinyume chake na kutafautisha kati ya pande mbili hizo: “Kumiliki na Kumilikishwa” kwa mfano “Kuuza kitu…… kuna kutana na kununua kitu…..” na kwa vile tumefahamu kuwa kuna kitu akilini, na kuna kitu machoni, imekuwa kwa uwezo wetu kufahamu yaliyofikiwa kwa mazingatio kuwa mwanadamu anaweza kutafautisha akilini mwake kipi kilichoungana kwa nje na kukiunganisha akilini mwake na kile kilichotengana kwa nje.
Mfano wa hali ya kwanza ni kuwa inawezekana kwa mwanadamu kutafautisha – akilini mwake – kati ya Muislamu na Muumini, wa kwanza ndiye ambaye huonesha alama na ishara za Uislamu wakati ambapo Muumini ndiye ambaye ana amini kwa uyakini amri za Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W lakini wote wawili kwa nje ni kitu kimoja, na hilo ni kwa vile hakuna – Kisharia – Muumini isipokuwa lazima awe Muislamu, na mwengine kwa kawaida nje ni Muumini hata kama hilo litakuwa kwa ulinganiaji, hivyo Muislamu na Muumini kwa ukweli ni wanatafautiana lakini wote wawili ni wenye kuungana, hapa wanatengeneza ibara inayoendana na hali hii nayo ni: “Ni mmoja kwa uhalisia ni tofauti kwenye mazingatio”.
Na neno mazingatio hapa lina maana ya upende au hutokana na kipimo ambacho akili inafikiri katika hii hali. Na kutokana na hilo uelewa wetu unajikita zaidi kwenye kauli ya mtunzi – kupitia neno ambalo lipo mbele yetu – “Na kinyume chake kunazingatiwa”.
Anakamilisha: “Mazingatio ya neno kumiliki na kumilikishwa kwa kuangalia maana ya Kisharia kama itakavyokuja, ikiwa inakusudiwa ni muundo wa pande mbili pamoja kwa maana ya pande mbili ambazo zinauwezo wa kukubaliana na kuvunja makubaliano, husemwa kwa upande wa lugha: Kubadilishana kitu kwa kitu…. Na kuendelea.
Ufupi:
Haya ni maelezo ya haraka hatuwezi kusema kuwa tumeelezea mitazamo yote ya Kijumla ambayo yamo kwenye akili ya warithi, lakini ni kiashirio tu kidogo kinachoonesha ulazima wa kuipa umuhimu mitazamo hii, na kuigundua pamoja na kuunda tena muundo wake, na kuelewa andiko kupitia maelezo hayo, hii kwa sababu huathiri katika kiwango cha ufahamu na uelewa, kama vile huathiri katika uwezo wa kuelewa maana za ibara za kiurithi kwa mtunzi yeyote wa mambo ya urithi, kwa kuzingatia ni ishara ya kwanza ya kufahamu urithi.
Kuwepo na kutokuwepo, hukumu za kiakili, na maudhui na maelezo, ndani na nje, na madaraja ya uwepo pamoja na nguvu na kitendo….. na mifano ya nadharia hizi zote inawezekana kuzikuta katika tangulizi za elimu ya maneno, vile vile tunazikuta zikiwa zimefafanuliwa vizuri na Al-Ghazaly katika kitabu cha “Arobaini katika misingi ya dini” vile vile ufafanuzi wa Imamu Razy katika kitabu cha “Arobaini katika misingi ya dini” pia, lakini katika sherehe ya kitabu cha Makaswid cha Tiftaziyy pamoja na ufafanuzi wake katika kadhia za elimu na namna gani walikuwa wanaifahamu au ramani ya elimu kwao, vile vile katika kadhia ya uwepo, katika tunzi hizi tunakuta eneo lisilo na ubaya wowote wa kufafanua mitazamo hii.
Katika uhalisia ni kuwa, mitazamo hii haijahusisha kwenye tangulizi hizo tu, bali imekuwa ni misingi iliyoenea katika mazingira ya kielimu zaidi kuliko kuwa maandiko ya kitafiti, hali iliyopelekea kuwa kwenye kiwango cha juu cha kielimu, kwa maana wanafunzi walikuwa wanaifanyia kazi kwa kuwa ni wasifu wa uhalisia unaohusiana na maana ya mwanadamu aliyopo kwenye ulimwengu ambapo anaishi, na kuna Mola aliyemuumba, na bado anaendelea kuumba, na kuwa ikiwa atakatikiwa mwanadamu mwendelezo hakutabakia maandalizi na upatikaji, kwa kifupi, mitazamo ya jumla imekuwa ni mfumo unaosimamia maisha ya mwanadamu Muislamu pamoja na matendo yake tabia zake na mashirikiano yake na hali za kijamii.
Mitazamo hii ilianza kusimamia maandiko ambayo yameandikwa na watengenezaji wa ustaarabu wa Kiislamu na wana fikra wake mwanzoni mwa karne ya kwanza na ya pili ya Hijra, na hiyo ni pale Waislamu walipokutana na maswali kutoka kwa wasiokuwa waislamu ndani ya nchi ambazo Waislamu walizifungua, ni maswali yanayotokana na tamaduni zenye mitazamo jumla yenye mabadiliko kama vile hali yetu hivi sasa na watu wa Magharibi. Waislamu walifikiri kwenye maswali haya kutokana na Kitabu na Sunna pamoja na Imani sahihi, na wakatoa majibu yao sawa na vyanzo hivi, na wakaendeleza harakati mpaka ilipotokea hali ya mgawanyiko ndani ya Umma kuhusu vyanzo hivi.
Na ilikuwa kilele cha mgawanyiko huu ni katika kadhia ya “Kuumbwa kwa Quran” kadhia ambayo ilimpelekea Imamu Ahmad Ibn Hambali akiwa na msimamo wa kutoelekea kwenye misamiati au majibu mapya, na akaendelea na msimamo wa kuhusisha kuwa Quran Kitabu cha Mwenyezi Mungu si zaidi wala si chini ya hapo, pindi fitina ilipoenea akalazimika kujibu kwa njia nyengine, akasema: Ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, hakina sifa ya kuumbwa, kusikia kwetu kumeumbwa na kinachosikika hakijaumbwa, kuandika kumeumbwa kilichoandikwa hakija umbwa, na kutamka kwa Quran – kwa maana ya hewa inayotoka kwenye kolomeo – ni imeumbwa, pindi ilipoenea kwa watu kuwa Imamu Ahmad Ibn Hambal anasema: “Utamkaji Kiquran kumeumbwa” watu wakasema: Kwa hali hiyo “Quran imeumbwa” Imamu Ahmad akarudi nyuma na akasema: Mwenye kusema kuwa, utamkaji wa Kiquran umeumbwa basi huyo ni kafiri, na sababu ni misamiati mipya, pindi misamiati hii ilipokuwa haipelekei kwenye kusudio Imamu alirudi kwenye asili, na akazingatia kinyume na hivyo ni ukafiri, kwa sababu sifa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu haiwezekani kuwa imeumbwa.
Pindi ilipoingia elimu kwa wote ndani ya ulimwengu wa Kiislamu ikifuata jaribio la Muhammad Ally nchini Misri, elimu ikiwa ni ya aina mbili: Aina ya kwanza – Inafundisha urithi na dini, na aina ya pili – Inafundisha elimu asilia na kimajaribio, jambo ambalo lilipelekea mchanganyiko katika elimu na maisha jumla kisha maisha maalum ya Waislamu, na kuzaliwa mwanya mkubwa kati ya watu na urithi, mwanya huu ndio ambao umepelekea kuondoa mitazamo na imani za mambo ya jumla kwenye akili ya Kiislamu, ispokuwa katika akili za hawa ambao walidhamiria maisha yao kusoma elimu za urithi na kuzifanyia kazi nao ni wachache.
Chanzo: Kitabu cha muelekeo wa kufahamu urithi, cha Mufti wa Misri Dr. Ally Jumaa.

Share this:

Related Fatwas