Ibrahim ni Nabii au Mtume

Egypt's Dar Al-Ifta

Ibrahim ni Nabii au Mtume

Question

 Sisi tunasema kuwa Nabii Ibrahim alikuwa ni Mtume lakini katika Surat Maryam Mwenyezi Mungu Anasema: {Na kumbuka ndani ya kitabu Ibrahim alikuwa ni Nabii mkweli} hii inamaanisha nini?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe kwa Mtume S.A.W. pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake.
Kusudio la Nabii katika sehemu hii ni kuwa yeye alikuwa amepata habari zitokazo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa njia ya Ufunuo, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Amempa uwakala wa kufikisha Ujumbe wake kwa waja wake, na Wanachuoni wengi wanaona kuwa hakuna tofauti kati ya Nabii na Mtume, wapo wenye kuona tofauti kati ya wawili hao Mwenyezi Mungu pale Aliposema kuwa Ibrahim A.S. Nabii hilo halipingani kuwa kwake pia Mtume kwa sababu Unabii ni mpana zaidi ya Utume, na kutajwa Unabii hakukanushi Utume.

 

Share this:

Related Fatwas