Tofauti kati ya Mwanamume na Mwana...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti kati ya Mwanamume na Mwanamke

Question

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh.
Ni matumaini yangu kwenu waheshimiwa kupata jibu kuhusu swali langu na kulipa uzito stahiki, mimi naipenda Dini ya Kiislamu na ninajifaharisha nayo lakini katika hali ya kuingia kwangu katika kutafasiri Qur`ani nimekuta Mwenyezi Mungu Mtukufu Anampenda mwanamume na kumpa sifa ya kipekee kwa kumpa wanawake wa Peponi na wake wengi ambapo inazingatiwa ni katika dharau kubwa kwa mtazamo wangu kwa mwanamke, na katika hukumu za ndoa kuwa hatutaingia Peponi isipokuwa kwa kuridhia kwao kwa kiwango ambacho kimenifanya mimi kujizuia kabisa na kuoa ili nisije ingia kwenye huu utumwa, kwa sababu mimi naweza kuishi bila ya kuwa na mke ima hili ni kwa vile Adam pindi alipoumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuhisi isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kumuumbia Hawa, je Mwenyezi Mungu Anachukia mwanamke mpaka akahalalisha kwa mwanamume kumpiga mwanamke, kwa sura ya wanawake ni kuwa Uislamu haukumheshimu mwanamke bali umemgeuza kuwa mikononi mwa mwanamume na Siku ya Mwisho mwanamke anakuwa ndio malipo ya mwanamume Peponi kwa kupewa wanawake wa Peponi Huur Al-Ain, ama mwanamke anakuwa ni malipo ni tatizo lile lile la kidunia nalo ni uke wenza, huu si mtazamo wangu bali ni mtazamo wa wengi miongoni mwetu kuwa tunahisi ni dharau kwa mwanamke je tunamakosa katika hilo?
 

Answer

 Assalaam Alaikum Ewe dada yangu muulizaji, ni kuwa Mwenyezi Mungu Amewapa wanaume wote haki na wajibu kwao, vile vile wanawake amewapa haki na wajibu kwao, haki na wajibu kwa wanaume na wanawake vinakubaliana sawa na umaalumu wao na majukumu yao.
Mwenyezi Mungu Amempa amri mwanamume kufanya kazi na akampa amri mwanamke kusimamia familia kuzaa na malezi, pia kufanya kazi ni furaha ya wanaume nayo inakubaliana zaidi na maumbo yao kimwili na kinafsi, ama mwanamke ulezi ni jukumu muhimu zaidi kwake ambalo mwanamke hujikuta yeye mwenyewe kwenye jukumu hili ndio asili ya mwanamke.
Katika hilo hakuna dharau kwa wanaume wala kwa wanawake.
Sifa ya wake wengi kwa wanaume inaendana na faida kwa jamii, na wanaume wengi kwa wanawake kunapelekea uharibifu mkubwa ndani ya jamii na kunapingana na maumbile salama. Mwenyezi Mungu Amewaahidi wanaume wanawake Peponi kwa sababu ni ahadi njema kwa waja wake kuneemeka Peponi, na kuneemeshwa kwa wanaume kunakuwa kwa kile kinachopenda nafsi zao, na kuneemeshwa wanawake vilevile kunakuwa kwa kile kinachopenda nafsi zao, na mwanamke hapendi kuwa na mwanamume zaidi ya mmoja kwani hili la mwanamke kuwa na wanaume wengi ndio kejeli na dharau kubwa kwa mwanamke.
Uislamu umemtaka mwanamume kuwa mkarimu kwa mwanamke kama vile umemwamrisha mwanamke kuwa mtiifu kwa mwanamume, na ukafanya neema za mwanamke Peponi ni kuwa na mwanamume mwema ambaye yeye anampenda, na Peponi hakuna matendo machafu wala kuudhiana kwa wakazi wake.

 

Share this:

Related Fatwas