Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtum...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtume, S.A.W.

Question

 Inajulikana kuwa jambo la kwanza lililoteremshwa katika Qur’ani ni mwito wa kujifunza na elimu, basi kwa nini Mtume S.A.W. alibakia maisha yake yote bila ya kujifunza?
Kujua kwamba anatuhumiwa kwa uchawi na kusema uwongo kabla ya Qur’ani kuteremshwa kwake na kabla ya wito wa kujifunza.

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Mtume S.A.W. hakuwahi kutuhumiwa kabla ya utume wake kwa uchawi au uwongo, kinyume chake, yeye S.A.W. alikuwa mashuhuri katika mazingira yake ya mwanzo kuwa ni mkweli na mwaminifu, na alibaki katika hali hii kabla ya utume na baada ya utume.
Ni watu wachache tu waliomkufuru Mtume S.A.W. waliodai mwito huu ili kuikimbia dini ya Mwenyezi Mungu, na hivi ndivyo utakavyomkuta katika kila zama mtu anayejaribu kujiepusha na dini kwa hoja hafifu.
Kuhusiana na kumfundisha Mtume S.A.W. kusoma na kuandika, Mwenyezi Mungu ndiye aliyemtaka hayo ili kuwe na dalili ya unyoofu wake katika madai ya kuteremshiwa wahyi, na kwamba asiyejua kusoma na kuandika hawezi kuitoa hii Qur'ani Tukufu, ambayo wanazuoni na wanachuoni hawawezi kuitoa mfano wake, basi ni Uteremsho wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mjuzi.
Na elimu sio kwa kusoma na kuandika, na Mtume huyu mkubwa, S.A.W., amewafundisha wanadamu yote yale ambayo wanachuoni wengine hawakuyajua. Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Awaongoze waja wake kwenye njia iliyonyooka na awaoneshe haki, kwani Yeye, Utukufu ni Wake, ndiye bwana bora na msaidizi bora.

 

Share this:

Related Fatwas