Ishara ya Yusuf
Question
Nataka kujua ni ishara gani aliyoiona bwana wetu Yusuf, A.S. katika Aya hii: “Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi.” Basi ni nini ishara hii? Asante sana
Answer
Wafasiri wamekhitalifiana juu ya nini ishara hii, baadhi yao wakasema kuwa ni maana ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka juu ya moyo wake, basi kitendo hiki kilikuwa ni cha kulaumiwa kwake, hivyo akajiepusha nacho