Ubora wa Nabii Isa kwa Mtume wetu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ubora wa Nabii Isa kwa Mtume wetu Mohammad S.A.W.

Question

 Kuna Mkristo mmoja aliwahi kuwa Muislamu anafahamu Hadithi zote zilizomo kwenye Kitabu cha Hadithi cha Imamu Bukhary, anadai kuwa kuna Hadithi ndani ya Kitabu cha Sahihi Bukhary inasema kuwa Bibi Maryamu na Nabii Isa hawajawahi guswa na shetani kabisa, ama Mtume wetu Muhammad S.A.W aliwahi tawaliwa na shetani kama ilivyokuja katika Suratul-Haji Aya ya 52, kwa sababu hiyo Mtume Muhammad amekuwa si mwenye ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na vilevile alishawahi kurogwa huko nyuma, kwa sababu hiyo huyu Mkristo amekuwa na shaka na Qur’ani. Basi ni ipi kauli yenu kuhusu maneno haya?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ama Hadithi ni Hadithi sahihi imepokelewa na Imamu Bukhary na Muslim. Maana ya Hadithi iliyotajwa ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alijibu maombi ya Bibi wa Nabii Isa pale aliposema akimuombea dua binti yake Maryamu:
{Na mimi nimemuita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shetani aliye laniwa} [AALI IMRAAN: 36].
Haina maana kuwa hali hii maalum ya Bibi Maryamu ya kutoguswa na shetani haina nafasi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.W.A – Kwa mfano tuchukulie kuwa hivyo – shetani kumuendesha na kuwa na uwezo kwa Mtume S.A.W ni jambo lisilowezekana, kwani baadhi ya Wanachuoni Waislamu wamekubaliana kuwa hali za Manabii wote zinashirikiana, [Angalia kitabu cha Sherehe An-Nawawy 15/ 120].
Hadithi haina maana kuwa Nabii Isa ni mbora zaidi ya Muhammad S.A.W kwani kumekuwa na ubora mwingi wa Mtume Muhammad S.A.W na kuwepo pia ubora wa Nabii Isa A.S yaliyothibiti kwenye kauli ya Mtume Muhammad S.A.W hayaondoi kabisa ubora wa Mtume S.A.W uliothibiti.
Aya ambayo imechukuliwa ni ushahidi wa kurogwa kwa Mtume S.A.W ambayo ni Aya ya 52 ya Suratul-Haj, lau yatathibiti hayo anayotaka basi ingekuwa Manabii na Mitume wote waliobakia ni wenye kurogwa.
Ama yaliyokuja kwenye swali kuwa Mtume S.A.W alirogwa, madai haya si sahihi bali Jamhuri ya Wanachuoni wamekubaliana kuwa Mtume S.A.W amehifadhiwa na kulindwa kutokana na vitendo vya uchawi, isipokuwa Mtume S.A.W alikuwa anahisi maumivu ya kichwa kwa sababu ya aliyoyafanya Labid Ibn Al-Aaswam ambaye ni Myahudi ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu akamfunulia Mtume wake SAW asome Suratul-Nas na Suratul-Falaq ili kuondoa maumivu haya ya kichwa.
Jibu lingine:
Maneno haya hayana ukweli kabisa bali ni uwongo moja kwa moja, ambayo yamepokewa kwenye kitabu cha sahihi Bukhary ni kauli ya Mtume S.A.W:
“Hakuna mwanadamu yeyote aliyezaliwa isipokuwa anaguswa na shetani wakati anapozaliwa na kuanza kulia kutokana na kuguswa na shetani isipokuwa Bibi Maryamu na Mtoto wake” kisha akasema Abu Huraira – Mpokezi wa Hadithi – {Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shetani aliye laaniwa} kwa maana kama ilivyokuja Aya kwenye Suratu- Aal Imran kupitia kauli ya Mama wa Maryamu.
Hapa kuguswa na shetani maana yake ni kuchomwa mbavuni na kidole kama ilivyokuja tafasiri yake katika Hadithi nyingine imepokelewa na Imamu Bukhary pia kuwa Mtume S.A.W amesema: “Kila mwanadamu huchomwa na kidole cha shetani ubavuni kwake pale anapozaliwa tofauti na Isa Ibn Maryamu shetani alikwenda kuchoma kisha akachoma kidole chake kwenye hijabu”, kusudio la hijabu ni ile ngozi ambayo ndani yake kuna mtoto au nguo ambayo hufunikwa nayo mtoto baada tu ya kuzaliwa.
Ama Aya katika Suratul-Haj ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anapo soma, Shetani hutumbukiza katika masomo yake. Lakini Mwenyezi Mungu huyaondoa anayo yatia Shetani; kisha Mwenyezi Mungu huzithibitisha Aya zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima}.[AL HAJJ 52] Maana yake ni kuwa: Nabii katika Manabii alikuwa pindi anapotaka Uma wake unyenyekee na kumtii Mwenyezi Mungu na kufunganisha matumaini yake kwenye hilo, ndipo anapokuja shetani na kuingiza wasiwasi wake na udanganyifu ili kuzuia na kuziba yale anayoyataka Mtume au Nabii, na ikawa kwa kuingia kwake shetani ni kuzuia kukamilika kazi hiyo na umuhimu wa mambo hayo bila ya kuwepo vitimbi vyake, au shetani huingiza shari na uharibifu, kuambatanishwa kutamani kwa Manabii ni kuonesha kuwa ni kutamani uongofu na mema, na kuambatanishwa kuingia kwa shetani ni kuonesha kuwa ni uingiaji wa upotofu na ufisadi, hivyo maana inayochukuliwa ni kuwa: Shetani ameingiza kwenye nafsi za Uma upotofu unao haribu miongozo iliyosemwa na Manabii.
Na maana ya kuingia shetani kwenye matamanio ya Nabii na Mtume ni kuingiza kilicho kinyume chake, kama mwenye kufanya kitimbi akaingiza sumu kwenye maziwa, hivyo kuingia shetani na wasi wasi wake: Ni kuamrisha watu uwongo na mambo ya maasi, na anaingiza kwenye nyoyo za viongozi wa ukafiri maovu wanayopeleka kwa watu wao, na kueneza shaka shaka kwa kuingiza shaka ambazo zinapelekea akili kutokumbuka dalili, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anarudia tena kuleta miongozo na uongofu kupitia ulimi wa Nabii, na kuuweka wazi wasiwasi wa shetani na ubaya wa vitendo vyake, basi yapo wapi hayo wanayoyasema hao waongo wazushi kuhusu Aya.
Ama tukio la kurogwa Mtume S.A.W usahihi ni kuwa Labeed Ibn Al-Aaswam Myahudi alijaribu kumroga Mtume S.A.W kwani Madina kulikuwa na Wayahudi wengi wachawi ambapo Mwenyezi Mungu alimjuza Mtume wake S.A.W yale aliyoyafanya Labeed ili iwe ni muujiza kwake Mtume S.A.W katika kubatilisha uchawi wa Labeed na ili Wayahudi wapate kufahamu kuwa yeye ni Mtume hivyo hawezi kufikwa na madhara yao, na kama wachawi walivyoshindwa kwa Musa A.S vile vile uchawi wa Labeed haukuleta athari yeyote ya kutajwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.A.W bali Mtume S.A.W alitokewa na hali ya mabadiliko ya kimwili na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamponya, hivyo hali hiyo ikaendana na kulinganishwa na kile alichokifanya Labeed Ibn Al-Aswam ikiwa jaribio la kumroga Mtume S.A.W na Mtume hakuathirika na chochote, je hilo si ukafiri kwa Unabii kwa sababu Mtume S.A.W ni mwenye ulinzi ambapo shetani hana nafasi kwake, wala hakuna uhusiano wa jaribio hili lililofeli la kutaka kurogwa Mtume S.A.W na kazi ya ufikishaji wa ujumbe.
Maelezo yote yaliyotangulia yanafundisha vitimbi na ujinga wa huyo mtu anayejaribu kuwazuia Waislamu na dini yao kwa kuwajengea shaka zisizo kuwepo na uwongo pamoja na uzushi wa kutupwa.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas