MLIMA WA MUSA.

Egypt's Dar Al-Ifta

MLIMA WA MUSA.

Question

Baada ya maamkizi kwa upande wa Walimu, mimi ni mwanafunzi wa taifa la Senegali miongoni mwa wanafunzi wa kigeni, nawashukuru sana kwa juhudi zenu kubwa za kutufundisha sisi ndani ya shule ya Kiislamu ya wanafunzi wa kigeni.
Baada ya maelezo hayo mafupi: Napenda kuwauliza kitu kidogo na nategemea kutoka kwenu jibu lenye kutosheleza kwa utashi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, swali langu ni kuwa tokea kufika kwangu Jijini Cairo nimekuwa nikisikia wanafunzi wanasema, ndani ya kipindi cha majira ya joto kwa maana ya kiangazi huwa wanaandaa safari za kuelekea maeneo mbali mbali nchini Misri ili kutembea na kufanya utalii, nimewasikia baadhi yao wanasema kuwa wanaelekea kwenye mlima wa Musa ambao Mwenyezi Mungu alizungumza na Nabii wake hapo.
Swali langu, je mlima huu bado upo mpaka leo nchini Misri, na ikiwa upo nataka kufahamu ni namna gani umekuwa mlima baada ya Mwenyezi Mungu kuzungumza na Nabii Musa sehemu hiyo? Na nimesoma katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinatuelezea kisa kwa uwazi zaidi ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Basi alipo jionesha Mola Mlezi wake kwenye mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Pindi alipo zinduka akasema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni katika Waumini wa kwanza}.
Kwa maana baada ya Mwenyezi Mungu kuzungumza na Nabii Musa mlima ukavurugika kwa Utukufu wa Mola na Uwezo wake na Ukubwa wake, hivyo ni namna gani mlima uwepo bado upo na Mwenyezi Mungu Anasema
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Ameuelezea mlima kuwa ulikuwa umevurugika ni kwa uzito lakini sio maana ya Aya kuwa mlima uliondoka na kuvurugika bali ulitikisika mtikisiko mkubwa na kupoteza fahamu Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa Amani iwe kwake au kwa wakati huo ni sehemu ya huo mlima, na mlima umeendelea kuwa kwa sura yake iliyopo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio Anajua zaidi.

Share this:

Related Fatwas