Wake wa Mtume S.A.W

Egypt's Dar Al-Ifta

Wake wa Mtume S.A.W

Question

  Kwanini Mtume S.A.W alioa wake 9 na nini sababu ya kuoa kwake wote hao, na je Mtume S.A.W alioa wake 9 kabla au baada ya Mwenyezi Mungu kuwa amepangilia mwisho wa wake wanne? Naomba maelezo.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Shaka ya muulizaji imejengeka katika hali ya kuchanganya kati ya asili ya mazingira tofauti, kwani kila zama zina asili yake ambayo huathirika nayo wale wenye kuishi kwenye mazingira hayo, na zama za Mtume S.A.W kulikuwa na ndoa nyingi za wake wengi pamoja na kuoa wajakazi, lakini pamoja na hayo yote Mtume S.A.W kuoa kwake hakukuwa ni kwa utashi wa kupenda wanawake wengi kama alivyoashiria muulizaji, bali kuoa kwake kulikuwa ni kwa sababu za kijamii Kisharia na kisiasa kwa ufafanuzi ufuatao:

Kwanza: Sababu za Kijamii.
Kumuoa kwake Bibi Khadija R.A ni kuimarika kijamii, ambapo mwanamme anaoa mwanamke mwenye akili nyingi na ubora, na Mtume S.A.W alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano na aliishi naye yeye peke yake mpaka alipofarikia Bibi Khadija Mtume S.A.W akiwa na umri wa miaka hamsini.
Baada ya kifo hicho ndio Mtume S.A.W alimuoa Bibi Sauda Binti Zam’ah na alikuwa ni mwanamke mjane, hii ni kutokana na binti zake wanne kuhitaji mama mwingine atakaye wasimamia na kuwaangalia kama wafanyavyo wakina mama.
Hafswa Binti Omar Ibn Khattab Mtume S.A.W alifunga naye ndoa baada ya kufariki kwa mume wake ikiwa ni kumkirimu baba yake ilikuwa ni mwaka wa 3 H,
Bibi Zainabu Binti Khuzaimah mume wake alifariki katika vita vya Uhdi akaolewa na Mtume S.A.W ulikuwa mwaka wa 4 H.
Bibi Ummu Salama Hindi Binti Umayyah mume wake alifariki na kumuachia watoto aliolewa na Mtume S.A.W ndani ya kipindi cha mwaka wa 4 H.
Imebainika wake wa Mtume S.A.W waliotangulia kutajwa kuwa Mtume S.A.W aliwaoa wakiwa wajane wa waume waliofariki katika jihadi ya Waislamu dhidi ya washirikina ili kuwaliwaza na kupendezesha miili yao pamoja na kulea watoto wao, hii ikawa ni kama Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwafidia.
Pili: Sababu za Kisharia.
Kumuoa kwake Bibi Aisha R.A kulikuwa ni kwa ufunuo, ambapo Mtume S.A.W aliona kwenye nyozi kuwa amemuoa Bibi Aisha, na ndoto za Mitume ni ufunuo.
Zainabu Binti Jahshi alikuwa mke wa Zaidi Ibn Harithah ambaye alikuwa anaitwa Zaidi Ibn Muhammad ki ubini, ndipo ikateremka Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu hasa} [AL AHZAAB: 04].
Na kauli nyingine: {Waiteni kwa majina ya baba zao, huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu} [AL AHZAAB: 05]. Baada ya kutokea tofauti na mume wake ndipo alipoachwa na Mtume S.A.W aliamrishwa kumuoa ili kusimamisha dalili kwa vitendo juu ya ubatili wa mtoto wa ubini, hayo yalitokea mwaka wa tano Hijria.
Tatu: Sababu za Kisiasa.
Mtume S.A.W, aliwaoa baadhi ya wakeze kwa sababu za kisiasa kwa upande wa kuunganisha nyoyo na kupinga uadui pamoja na kuwaachia huru mateka na mambo mengine, kwa sababu hiyo ya kisiasa ni pamoja na:
Mtume S.A.W, kumuoa Bibi Juwairiyah Binti Al-Harith, kiongozi wa ukoo wa Bani Al-Muswatwalaq, kabila la Khuza’a, alikuwa mateka kisha Mtume akamuoa ndani ya mwaka wa 6 H.
Bibi Ummu Habiba Binti Abi Sufyan, mume wake alikuwa Mkristo na yeye akabakia kwenye Uislamu wake, kumuoa kwake Mtume S.A.W kulikuwa na athari kubwa katika kuvunja nguvu ya Abi Sufyani ya kuendelea kuushambulia Uislamu mpaka mwishowe naye Mwenyezi Mungu akamuongoza.
Bibi Swafiyyah Binti Huyayy Ibn Akhtwab, alikuwa katika mateka wa vita vya Khaibar, Mtume S.A.W akamuacha huru na akamuoa mwaka wa 07 H.
Bibi Maimuna Binti Al-Harith alimuoa mwaka wa 07 H.
Katika wake hawa walifariki wawili wakati wa uhai wa Mtume S.A.W nao ni: Bibi Khadija na Zainabu Binti Khuzaimah, na alipofariki Mtume S.A.W aliacha wajane tisa.
Ama kwa upande wa vijakazi ni Maria Qibtwiyah ambaye alizaa naye mtoto Ibrahimu na alifariki mapema akiwa bado mdogo, na mjakazi mwingine ni Raihanah Binti Zaidi Qartwiyah.
Hivyo kuoa wake wengi alianza kipindi cha umri wa miaka hamsini na mitatu. Je, hii inatosha kusema kuwa ni dalili ya kwamba Mtume aliwatamani wanawake wengi? Na mwenye shauku ya kuoa wanawake wengi je anaweza kuoa wanawake wakubwa na wenye watoto na wajane? Ni vipi wakati Mtume S.A.W alipewa wanawake wazuri wa Kikuraishi aoe na akakataa?!
Uoaji wake S.A.W wa wake wengi kulikuwa na hukumu zake – Ukiacha zilizoelezewa – lakini hukumu zote zinazotokea nyumbani kwa Mtume S.A.W ni matokeo ya kufanyia kazi Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hekima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye habari} [AL AHZAAB: 34]. Na kuwajengea heshima makabila ya Kiarabu kwa sifa ya ukwe wake kwao na kuongeza hali ya mshikamano kwa ndoa hizo, lakini pia kuongeza ukoo wake kwa upande wa wake zake na kuzidisha wasaidizi wake dhidi ya wanaompiga vita.
Wake wengi ni mwenendo wa Manabii kwa Maandiko ya vitabu vitakatifu:
Vitabu Vitakatifu vimetaja idadi kadhaa ya Manabii na kutaja idadi ya wake zao, miongoni mwao:
Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahimu Amani ya Mungu iwe kwake, ametajwa kuwa na wake watatu ndani ya Kitabu Kitakatifu, akiwemo Bibi Sara, ametajwa kwenye Kitabu cha Mwanzo: (20: 12). Hajara Al-Masriyah, ametajwa kwenye Kitabu cha Mwanzo: (16: 3). Ketura ametajwa kwenye Kitabu cha Mwanzo: (25: 1), vile vile ametajwa kuwa alikuwa na wajakazi kwenye Kitabu cha Mwanzo: (25: 6).
Nabii wa Mungu Yaakub Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwake, alikuwa na wake wanne ndani ya wakati mmoja, yamekuja haya kwenye Kitabu cha Mwanzo: “Akaondoka usiku ule akawatwaa wekeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki” (32: 22).
Nabii wa Mwenyezi Mungu Daud Amani ya Mungu iwe kwake, ametajwa kwenye Agano la Kale ana wake tisa:
Ahinoamu Myezreeli.
Abigaili, mke wa Nabali, Mkarmeli.
Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
Hagithi.
Abitali.
Egla. Samueli 2 (3: 1-6)
Mikali. Samueli 2 (6: 23)
Bathsheba mwanamke wa Uria. Samueli 2 (11: 26)
Abishagi Mshunami. Kitabu cha Wafalme 1 (1: 1 - 5)
Nabii wa Mwenyezi Mungu Sulaiman Amani ya Mungu iwe kwake, ametajwa kwenye Agano la Kale kuwa alikuwa na wake Elfu moja na Mia saba wakiwa ni wanawake huru na masuria mia tatu.
“Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu. Kitabu cha Wafalme (11: 3).
Hawa Manabii: Ibrahim Isaka Yakobo Daud na Sulaiman Kitabu cha Agano la Kale kimetaja kuwa walikuwa na wake wengi, hivyo kuoa wake wengi ni Sunna na mwenendo wa Manabii miongoni mwao ni Mtume wetu Muhammad S.A.W.
http://www.dar-alifta.org/ViewDI.aspx?ID=191

 

 

Share this:

Related Fatwas