Msimamo wa Qur’an juu ya Taurati

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa Qur’an juu ya Taurati

Question

 Vipi tunajibu madai ya Mayahudi kuhusu Qur`ani?
Nimesoma katika moja ya mitandao ya Kiyahudi maelezo yanayomaanisha ya kwamba kila Mtu wa Kitabu ni Muislamu. Na madai mengine mengi... lakini lililo kubwa zaidi ni dai lifuatalo: Haikupokelewa katika Qur'ani kinachowalingania Wayahudi wakiache Kitabu chao cha Taurati kwa ajili ya kuifuata Qur'ani, bali kinyume ni sahihi. Qur'ani imekariri kauli ya kwamba Qur'ani imekuja kwa ajili ya kuthibitisha ukweli wa Vitabu vilivyotangulia na wala sio kuviondosha, na Hakika ni kwamba Qur'ani (imewakosoa Wayahudi wa Madina kwa kuja kwao kwa Muhammad ili awatolee maamuzi baina yao wakati wao wana Taurati. {Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini.} [AL MAIDAH 43].
Na Aya ifuatayo inaongeza kukazia umuhimu wa Taurati, na hakika ya kwamba wafuasi wake ni Waislamu: {Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasiohukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.} [AL MAIDAH 44]
Ninaomba majibu ya Shubuhati hizi (huwenda Mwenyezi Mungu Akaimarisha Haki kwangu na kwenu)

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Qur'ani Tukufu imerudiarudia kwamba anayetafuta (anayechukuwa) dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:{Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.} [AALI IMRAAN 19] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema pia: {Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.} [AALI IMRAAN 85]
Na kila sifa iliyokuja katika Qur'ani Tukufu kuhusu Taurati inaikusudia Taurati ya Kweli ambayo haikuguswa na mikono ya uvurugaji na haikukatika katika mapokezi yake na haikubadilishwa wakati wa kufasiriwa, na Taurati hii ya Kweli ndiyo Qur'ani imeelekeza ifuatwe na kuwahimiza watu kuifanyia kazi ipasavyo ambapo utagundua ya kwamba Qur'ani imewaelekeza watu wote wamfuate Mtume S.A.W, na wamwamini yeye na wakiamini kitabu chake alichoteremshiwa na Mwenyezi Mungu na yule asiyefanya hivyo sio katika Waislamu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema; {Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.} [AN NISAA 170]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas