Akili na Kumjua Mwenyezi Mungu Mtuk...

Egypt's Dar Al-Ifta

Akili na Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu

Question

Je, Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwa Akili? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanachuoni wa Akida za Kiislamu, wamethibitisha ya kwamba akili ni katika njia za kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu zinafuata mfumo wa kuiegemea Sharia na kuitegemea akili.
Na kumjua Mwenyezi Mungu kupitia akili kuna dalili zake mbalimbali:
Ya Kwanza: Kwamba akili inauendesha Ulimwengu na inatafiti Mwonekano wa Uwezo wa Mwenyezi Mungu ndani yake, kwani hakika Mbingu na Ardhi zote na Bahari pamoja na viumbe vingine vyote, ni dalili kubwa ya kwamba Ulimwengu huu una Muumba wake mwenye hekima na mwenye kuuendesha naye ni Mwenyezi Mungu Mkutufu.
Ya Pili: Hakika akili inapooneshwa dalili za Sharia Tukufu inakinaika nazo na haioni chochote cha kushangaza ndani yake, bali inaamini kwa kutumia akili na kupima.
Na hiyo haimaanishi kwamba Akili inakuwa peke yake katika kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini Sharia ya Qur'ani Tukufu na Sunna pia ni njia ya kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Share this:

Related Fatwas