Kupaka Maji Juu ya Kandambili

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupaka Maji Juu ya Kandambili

Question

 Je, vipi tunapaka maji juu ya kandambili?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Kandambili zilikuwa katika zama za Mtume S.A.W. ni kama kitu kinachofanana na silipa au sabatu wakati wetu wa sasa.
2- Maswahaba R.A, walikuwa pindi wanapofuta soksi zao kwa maji "wakati mwingine walikuwa wakivaa na kandambili zilizotajwa na soksi, kwa hiyo katika hali kama hiyo, kupaka maji sio juu ya kandambili bali ni juu ya soksi kimsingi lakini ikatokea kupaka juu ya kandambili kwa kuwa kwake juu ya soksi mbili.
3- Katika zamu yetu sasa kandambili zinatofautia na zama zao, basi hukumu zao za kifiqhi zinazozitegemea hizo zilitofautiana.
4- Wewe unajua kwamba Wanachuoni wa Fiqhi wameshurutisha Kufuta juu ya Khufu ((Piopio) Ngozi ya kuvaa miguuni mfano wa kiatu) na mfano wake ambao ni soksi, vyote viwili viwe vimesitiri sehemu ya uoshaji wa faradhi mguuni na kinachokusudiwa hasa ni Nguyu mbili ambazo ni "Mifupa Miwili iliyojitokeza katika pande mbili za miguu" na kila kiatu katika zama zetu hakitoshelezi sifa za Sharti hili kwa maana ya kwamba viatu vya kisasa havifuniki mifupa hii miwili ya miguu. Na kwa ajili hiyo, haijuzu Kupaka juu yake peke yake kwa maana ya kuwa kama chini yake hakuna soksi nzito, na ikiwa kuna soksi nzito basi inajuzu Kufuta juu ya soksi hizo na ikiwa mtu atafuta juu ya kandambili ambazo ziko pamoja na soksi itajuzu kupitia mlango wa kwamba kinachokusudiwa Kukifuta juu yake ni soksi kwani soksi hizo ndizo zilizokamilisha masharti yaliyotajwa, nayo ni kuwa soksi hizo zinafunika sehemu ya mguu ambayo ni faradhi kuosha.
5- Na kuna aina ya viatu vya kijeshi viitwavyo buti, hivi viatu vinatimiza sharti lililotajwa ambalo ni kufunika sehemu ya lazima kuoshwa katika mguu, na kiatu hiki kinajuzu kufuta juu yake kwa masharti ya kufuta yanayozingatiwa ambayo kwayo vivaliwe katika hali ya Utwahara kamilifu na kwamba wakati wa kuvivua udhu utatenguka na haijuzu kuvuka muda uliowekwa kisheria wa kupaka na ulioruhusiwa nao ni usiku na mchana kwa mtu anaeishi sehemu na siku tatu kwa msafiri na masharti mengine uyajuayo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi


Share this:

Related Fatwas