Swala ya Mwenye Hedhi Baada ya Utwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Mwenye Hedhi Baada ya Utwahara wake

Question

 Wakati gani Mwenye hedhi anaswali baada ya kutwaharika kwake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanachuoni wa Fiqhi ya Madhehebu ya Shafi na wengine, wamesema kwamba Mwanamke akijitwaharisha kabla ya wakati wa Faradhi kwa namna inayotosha kutoa Takbiir ya kuhirimia Swala inamuwajibikia Faradhi hii kuiswali.
Na maana ya Twahara inatokusudiwa hapa ni yeye kujua kwa yakini kwamba Damu ya Nifasi na ya Hedhi zimekatika na hapo hapo achukue hatua ya kuoga na baada ya kuoga apate muda ambao haujamalizika na umebaki kiasi cha kuhirimia Swala.hapa yanamuwajibikia yale yaliyotajwa, hayo ni katika Swala zote.
Na kuhusu Swala ya Adhuru na Alasiri, hakika Wafuasi wa Madhehebu ya Shafi na Hanbali wanaona kuwa wakati wa swala hizi ni mmoja na kwa sababu hiyo, ikiwa mwanamke atajitwaharisha kabla ya Magharibi au kabla ya Isha kwa kiasi cha muda unaotosha Kuhirimia Swala, basi itamuwajibikia aswali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja, na aswali Magharibi na Isha kwa pamoja, na hii ni kwa njia ya kuwajibisha kwa Wafuasi wa Shafi na Hanbali kama tulivyotaja.
Na Wafuasi wa Madhehebu ya Maliki wao wanaona kuwa Swala sio wajibu kwake kama atakuwa aketwaharika kabla ya kumalizika kwa wakati kwa kiasi cha Kuswali rakaa moja kamili.
Na kwa upande wa Adhuri na Alasiri kama atakuwa ametwaharika kabla ya kumalizika wakati wake kwa kiasi kinachotosha rakaa tano kwa maana ya Adhuri kamili na rakaa moja ya Alasiri.
Na kwa upande wa Magharibi na Isha ikiwa mwanamke atatwaharika kabla ya kumalizika wakati wa sala kwa kiasi kinachotosha rakaa nne, tatu za Magharibi kamili na moja ya Isha basi Swala zote mbili zitamwajibikia kwa pamoja.
Na ninaona wewe utosheke katika kuwashereheshea wanafunzi wako rai moja ili wasivurugikiwe akilini mwao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas