Kitenzi Ata kuweka Wazi Kilicho Wazi
Question
Aya ya Qur`ani: {Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa mkizuiwa, basi (chinjeni) wanyama waliowepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakaye kuwa mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake basi atoe fidia kwa kufunga au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama. Na mtakapo kuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiye pata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakapo rudi; hizi ni siku kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu} [AL BAQARAH: 196].
Swali la mjenga hoja
Answer
Ni kwanini hakusema hizo ni siku kumi na kuondoa neno kamili ili kuepuka kuweka wazi kilichowazi, kwani ni nani anayedhani kumi ni tisa? ( )
Kuondoa shaka
1. Matumizi haya yaliyokuja kwenye Aya Tukufu ni matumizi ya lugha ya Kiarabu fasihi ambapo muulizaji ameshindwa kufahamu.
2. Na matumizi haya yana mwenza ndani ya Qur`ani Tukufu na katika maneno ya Waarabu Mwenyezi Mungu Amesema: {Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani} [AL HAJ: 46]. Na Mola Mtukufu Akasema: {Wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi} [AL AN'AAM: 38]. Na Mola Mtukufu Amesema: {Dari zikawaporomokea juu yao} [AN NAHL: 26].
Na katika mashairi ya Waarabu
Nimetembea kwenda kwao miezi ishirini
na minne na hiyo ni hija mbili.
Na kauli nyingine
Asubuhi tatu zenyewe zinanitosha
na sita pindi unaponikuta usiku.
Hivyo ni siku tisa Mola wangu
na kinywaji cha mtu baada ya kutema ni ugonjwa.
3. Ni katika makosa kulinganisha kati ya mfumo wa lugha ya Kiarabu na lugha zingine katika kusisitiza matamshi na jumla za kimaana na huo si mwenendo wa lugha zingine, kupinga mfumo huu kwa muulizaji kumekuja kutokana na kulinganisha kati ya lugha ya Kiarabu na lugha zengine kwa sababu ikiwa atahusisha mtazamo katika lugha ya Kiarabu basi itadhihiri kwake mfumo ambao umetanguliwa kutajwa.
4. Tamko la Aya Tukufu lina faida nyingi:
1- Kutajwa neno “Kamili” imebadilisha kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “Hizo ni siku kumi” na kuwa tamko lisilokubali uwezekano au maelezo( ).
2- Na faida ya kuleta funga siku zote hakupunguzi chochote, pamoja na kuelezea funga hiyo na yenyewe ni njia ya ukamilifu kwa mfungaji, hivyo ukamilifu hutumika kwenye uhalisia wake na kwenye ufupisho wake. Herufi ya Waw katika kauli yake “Na siku saba” huenda ikafahamika ni kuhalalisha, “Na neno siku saba ni sifa inayosisitiza siku kumi na kufidisha ufikishaji zaidi katika kulinda idadi au kubainisha ukamilifu wa siku kumi, kwani yenyewe ni idadi ya kwanza iliyokamilika ambapo yenyewe huishia umoja na kukamilika mpangilio wake unaonesha ukamilifu wake badala ya kuchinja mnyama” ( ).
Na faida yake ni kuwa maneno ambayo yanaelezea ibara nyingi na kufahamisha sifa nyingi, yana ukina zaidi kusahamu maneno ambayo yanaelezea ibara moja, ikiwa msisitizo umekusanya hekima hii basi kutajwa kwake kwenye sehemu hii inakuwa ni dalili ya kuchunga idadi katika kufunga ni katika mambo muhimu ambayo hayafai kupuuzia kabisa.