Tahadahri kufurahia kifo na kuweka wazi mwisho matokeo yake
Question
Ni ipi hukumu ya anayefurahi kifo cha mtu mwingine?
Answer
Hakujuzu kisharia kufurahia masaibu ya mtu mwingine sawasa katika kifo au masaibu mengine; kwa sababu hilo ni jambo baya lisilokubalika katika nafsi zilizosimama sawa, hivyo basi, Sharia ya kiislamu imelikataza, hadithi kutoka kwa Al-Asqaa R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: “Usidhihirishe furaha kwa ndugu yako kwa masaibu yaliyomfika, akamhurumia Mwenyezi Mungu akakupa wewe mtihani” imepokelewa na Alirmidhy.
Na tunakumbusha wale wenye desturi hii mbaya na waja wa Mwenyezi Mungu kwamba kawaida ya maisha aliyoiweka Mwenyezi Mungu ni kwamba mwanadamu habaki katika hali moja, bali huishi siku za furaha na siku za huzuni, Mwenyezi Mungu Anasema: (Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu) [Aal-Imran:140].
Na katika yaliyotajwa limepatikana jibu la swali.