Kitenzi Ata “Kimekuja” kwa Maana ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kitenzi Ata “Kimekuja” kwa Maana ya Uwingi Ambapo Imekusudia Uchache

Question

Aya ya Qur`ani: {Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: Mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu? Kweli Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyo yajua?} [AL BAQARAH: 80]
Na Mwenyezi Mungu Amesema: {Enyi mlio amini! Mmelazimishwa kufunga kama waliyolazimishwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha-Mungu * Mfunge siku maalumu za kuhesabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hesabu katika siku nyengine} [AL BAQARAH: 183, 184].
Swali: Ni nini alichokisema mjenga hoja?
 

Answer

Ilikuwa inapaswa kukusanywa kwenye uwingi wa uchache ambapo wao walikusudia uchache, anasema ni masiku machache( ). Akasema katika shaka ambayo inafuata baada ya Aya ya mia moja kumi na saba, na ilikuwa inalazimika kukusanywa kwa uwingi wa wingi idadi yake ni siku 30 na kusema siku chache( ).
Asili ya shaka
Ni kuwa katika lugha ya Kiarabu uwingi wa uchache na uwingi wa wingi ni kuwa uwingi wa uchache hutumika wakati kinachohesabika kinapokuwa kichache, na uwingi wa wingi hutumika pindi inapokuwa kinachohesabika ni kingi, na Qurani imekwenda kinyume na kanuni hii ikatumia uwingi wa uchache sehemu ya uwingi wa wingi na kinyume na hii inaondoa sifa ya Qurani kuzuiliwa kuwa na makosa.
Kuondoa shaka
1. Muulizaji amekosa ufahamu kwenye maswali haya mawili kuwa kadhia ya mizani ya mjumuiko wa uchache na uwingi unafungamana na uwingi mvunjiko, kwa mfano neno Maaduudaat la Kiarabu kwa maana ya “Siku chache” ni uwingi wa dhamiri ya kike iliyosalimika nayo inajengewa uwingi wake kwa kuongeza herufi ya Alifu na herufi ya Taa mwishoni ambapo inatafautiana na uwingi mvunjiko.
2. Neno la Kiarabu Ma’aduudah kwa maana ya “Siku chache” si katika uwingi wa wingi bali lenyewe ni umoja kama vile neno la Kiarabu Ma’aduudaat kwa maana ya “Masiku machache” si katika uwingi wa uchache bali ni uwingi wa dhamiri ya mwanamke iliyosalimika.
3. Uwingi wa uchache na uwingi huwakilishana wenyewe kwa wenyewe katika lugha pasi na kuwa muundo wenye makosa kilugha ( ).
4. Swali muhimu ambalo linajitokeza lenyewe katika hili ni namna gani muulizaji anashindwa kujua yote haya? Na ni vipi anazungumzia elimu ambayo hana ujuzi nayo?
5. Uchache ambao muulizaji anataka kuuthibitisha hapa unatokana na muundo wa Aya Tukufu.
Imekuja kwenye tafasiri neno Ma’aduudaat “Siku chache” kwa muundo wa uwingi tofauti na ilivyokuja kwenye Suratul-Baqarah neno Ma’aduudah kwa muundo wa umoja ikiwa ni ujuzi mkubwa wa kujieleza, na hilo ni kuwa uwingi mvunjiko kwa kitu kisicho na akili unafaa kufanya kazi kama inavyokuwa kwa mtu mmoja mwanamke kwa wakati mwingine na kufanya kazi katika uwingi wa wanawake, kwa mfano unaweza kusema milima hii imechimbika sana, na ukipenda unaweza kusema milima hii imejichimbia, au ukasema ngamia mwenye kutembea, na ukipenda unaweza kusema ngamia wenye kutembea( ).
Kusudio la neno masiku machache ni siku za ibada yao, na hapa limekuja neno masiku machache kwa muundo wa uwingi tofauti na ilivyokuja kwenye Suratul-Baqarah siku chache kwa muundo wa umoja ikiwa ni ujuzi wa kujieleza, na hapa imekuja kwa sifa maalum ya uwingi kutokana na kuwa na dalili ya uchache kama inavyoelezeka; na hilo linafaa zaidi kwenye hali ya kushangaza( ).
Masiku machache kwa maana yanayofahamika kwa idadi au machache kwa sababu uchache ni rahisi kuhesabika, na uwingi huchukuliwa bila mpangilio kwa mafano Mukatilu amesema: Kila masiku machache ndani ya Qurani au siku chache ni chini ya siku arobaini, na wala haisemwi hivyo pindi inapozidi idadi ya arobaini, na kusudio la haya masiku ima ni masiku ya mwezi wa Ramadhani na limepitishwa hilo na Ibn Abbas na Hassan pamoja na Abu Muslim Mungu Awe radhi nao na wahakiki wengine zaidi nayo ni moja ya kauli ya Imamu Shaafy, hivyo inakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametoa habari; kwanza ni kuwa amelazimisha kwetu funga kisha akabainisha kwa kauli yake: {Masiku machache yenye kuhesabika} hivyo akaondoa hali ya kutofahamika na kubainisha kwa kauli yake Mola Mtukufu kwa kusema: {Mwezi wa Ramadhani} ili kuiimarisha nafsi kwenye mwezi huo( ).
Na sifa ya chache inaruhusu uchache kwa sababu kusudio la neno uchache ambao watu wanaweza kuhesabu kwa wepesi pindi wanapoona au wanapozungumzia, kwani imeenea katika mazoea na kawaida kuwa watu hawahesabu vitu vinapokuwa vingi ili kuondoa uchovu au kwa sababu ya kazi ni sawa sawa wamefahamu hesabu au hawajafahamu kwa sababu kusudio kuhesabu ni kwa macho na ulimi na wala si kuhesabu kwa kujumlisha hesabu ambapo hapa sio kusudio, na kuja kwa herufi ya dhamiri ya kike kwenye neno Ma’aduudat likiwa ni sifa ya masiku limechunga ndani yake maelezo ya uwingi kwa wengi nayo ni njia ya lugha ya Kiarabu inayofahamika, hivyo uwingi katika sifa ya wingi pindi inapoingia dhamiri ya kike ni kuja kwa muundo wa umoja isipokuwa ikiwa wametaka maelezo ya uwingi kwa wengi, na hilo limekuja kwenye kauli ya Mola Mtukufu: {Ni siku chache}( ).
Na imesemwa kwenye kamusi ya Lisanul-Arab: Ni kuwa limefanywa uchache neno Ma’aduudat kwa sababu linapingana na kauli yako idadi kubwa haihesabiki, na miongoni mwa kauli nyengine: {Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa Dirham chache} kwa maana ya kidogo, Zujaj amesema kila ikiwa chache au nyingi hiyo inazingatiwa ni yenye kuhesabika lakini neno Ma’aduudaat kwa maana ya siku chache zinazohesabika inaonesha uchache kwa sababu kila kichache hujengewa uwingi wake kwa kuingizwa herufi ya Alifu na herufi ya Taa lakini pia inafaa kuwepo herufi ya Alifu na herufi ya Taa kwa ajili ya muundo wa wingi( ).

 

Share this:

Related Fatwas