Motisha za kisaikolojia kwa watu wa misimamo mikali (3)
Question
Ipi athari ya ubinafsi wa fikra na migongano ya kiakili kwa mtu mwenye msimamo mkali?
Answer
Mtu anayesifika kwa ubinafsi wa fikra hawezi kupambana na mashinikizo ya kisaikolojia ambayo anakutana nayo, kwa sababu hamiliki matumizi ya njia za kiulinzi bali siku zote anafikiri kati ya pande za kinyume, wala hamiliki hukumu za mambo ya kati na kati, ima ni mwenye kufaulu au mwenye kufeli, ima mwenye kupingwa kwenye jamii yake au mwenye kupendwa, jambo ambalo linaandaa njia kwa huyo mtu kufuata fikra za msimamo mkali, kisha kujichanganya katika vikundi vya misimamo mikali kwa kuhisi kwake kuwa vikundi hivyo vinamiliki kile anachokosa katika jamii yake, na kuwa ndio tulizo lake na kimbilio la afya yake mbali kabisa na mazingira yake ambayo hawezi kuyaishi.
Ama mgongano wa kiakili ni maradhi huwafika baadhi ya watu, nao ni ibara ya mgongano unaomfanya mgonjwa wake kuamini kuwa msafi au kiongozi mkubwa ambaye anaongoza watu, jambo linalopelekea kwenye mgongano mkali wakati mtu anapofeli katika kuficha hizo imani au kujaribu kuonesha sawa na anachoamini, jambo linalo imarisha uwezekano wa fikra kali kwa huyu mtu na kufuata mwenendo wa matumizi ya nguvu kwenye jamii yake.