Misukumo ya kisaikolojia kwa watu w...

Egypt's Dar Al-Ifta

Misukumo ya kisaikolojia kwa watu wa misimamo mikali (1)

Question

Misukumo gani muhimu zaidi ya kisaikolojia ya mtu wa msimamo mkali?

Answer

Kukata tamaa na kuhisi uduni vinazingatiwa ni katika misikumo muhimu ya saikolojia ya msimamo mkali.

Kukata tamaa ni katika mitazamo yenye umaarufu sana na kukubalika katika kutafsiri tukio la msimamo mkali, na hiyo hali ya kukata tamaa huzaliwa kutokana na ongezeko la mategemea ya mtu kwa upande wa kutosheleza mahitaji yake, lakini kutokana na hali halisi ya mtu na matatizo yake haiwezekani isipokuwa kujitosheleza kwa sehemu ndogo sana ya mategemeo yake, jambo linalopelekea uadui ambapo uadui huo sio mahala pake.

Kwa sura hii ukatishaji tamaa hupelekea mtu kuwa na tabia za matumizi ya nguvu, kisha huongezeka nafasi ya kujiunga kwenye vikundi vya misimamo mikali au kufanyia kazi fikra ambazo zinategemea matumizi ya nguvu ndio chaguo kuu.

Kuhisi uduni: Au kinachofahamika kwa Wanachuoni wa elimu ya saikolojia kama “Kikwazo cha upungufu”:

Tafiti nyingi za mambo ya saikolojia zimepeleka swala la kuhisi mapungufu na uduni wa hali ni moja ya motisha ya msimamo mkali, kutokana na kuzaliwa kwa hisia za kukosa amani, jambo linalompelekea mtu kujaribu kuifikia hiyo amani kwa njia ya kufuata moja ya vikundi vya msimamo mkali ambavyo vinamuimarishia hizo hisia, na anahisi kupitia vikundi hivyo kuwa na nguvu na utawala.

Mtu kama huyu amepatwa na hali ya maradhi makali yanahitaji kwake siku zote kupata nguvu zaidi, na siku zote kujaribu kulinda hali yake katika maisha kupitia kutoa juhudi si za kawaida na kutumia visasi vikali bila ya kusubiri na bila ya mazingatio yeyote ya wengine.

Share this:

Related Fatwas