Watu wa Rass

Egypt's Dar Al-Ifta

Watu wa Rass

Question

 Aya yenye kuleta shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani:
{Na tuliwaangamiza kina A'di Thamudi na watu wa Rass pamoja na vizazi vingi vilivyo kuwa kati yao} [AL-FURQAAN: 38].
Ni wakina nani hao watu Rass? Walikuwa ndani ya nchi gani? Wakati gani? Na ni kwanini Qur`ani haikutuweka wazi katika hayo ikiwa kweli watu hao walikuwepo?

Answer

 Hivi ndivyo walivyosema baadhi ya wapingaji wa ulianganiaji wa Mitume, nao ni watu wa Aad Thamudi na watu wa Rass, kwa watu hawa Mwenyezi Mungu anawapigia mifano watu wa Makka kwamba walikuwa ni wapingaji kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaangamiza, na huu ndio mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wapingaji, ili watu wa Makka na wengine wachukue mazingatio kwa yale yaliyotokea kwa hawa watu pale walipowapinga Mitume ya Mwenyezi Mungu, kisha Aya ikakusanya waliobaki na ikasema: {Pamoja na vizazi vingi vilivyo kuwa kati yao}.
Qur`ani kutaja kisa cha watu hawa kwa ufafanuzi wake na watu wake pamoja na muda wake sio kusudio la Qur`ani, lakini kusudio la kutaja visa hivi ni kutolea mfano tu, na Qur`ani Tukufu ni Kitabu cha uongofu.
Neno Rass katika lugha: Ni kisima kilichojengewa mawe ( ), wafasiri wamejaribu kufikia kuwaainisha na kuainisha sehemu yao na muda wao ili kufikia faida wakasema: Hao ni watu waliobakia katika watu wa Thamudi, na Suhaily wakasema: Hao ni watu walikuwa kwenye ardhi ya Aden walipelekewa Handhalah Ibn Sufian kuwa mtume na waliabudia masanamu na wakauwa Mitume yao ndipo Mwenyezi Mungu akawaangamiza, na ikasemwa: Hao ni watu wa Nabii Shuaibu, na ikasemwa tena: Hao ni watu walikuwa pamoja na watu wa Nabii Shuaibu, na akasema Mukatil: Kusudio la neno Rass ni kisima kilichopo huko Antokia na watu wa Rass ni watu wa Antokia ( ), na ikasemwa: Watu wa Rass ni watu wa mahandaki ambao wametajwa katika Suratul-Buruuj.
Na yaliyosemwa na Wafasiri ni kwa upande wa jitihada zao ili kuleta faida tu, ikiwa watapatia basi wana malipo ya aina mbili, na ikiwa hawatapatia basi wana malipo ya aina moja.

 

Share this:

Related Fatwas