Watu wa Kijiji.
Question
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu:
{Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipo wafikia walio tumwa * Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu * Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu…… Na hatukuwateremshia watu wake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha * Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa} [YASIN: 13: 29].
Na imepokewa katika baadhi ya vitabu vya tafasiri kuwa kijiji ni Antokia, na kauli yake Mola Mtukufu: {Walipowafikia waliotumwa} nao ni wajumbe wa Nabii Isa Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwake, na kauli yake:
{Pindi tulipowatuma wawili} nao ni Nabii Yahya na Nabii Yunus, na ikasemwa: Wengine wasiokuwa wao. Na kauli yake Mola Mtukufu: {Wakawakanusha basi tukawazidishia nguvu kwa mwiingine wa tatu} naye ni Shamauun, na kauli yake: {Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini} naye ni Habibu Najjar, na alikuwa anachonga masanamu yake, naye ni miongoni mwa aliyemuamini Muhammad na kati yao kukiwa na tofauti ya miaka mia sita, na ikasemwa tena: Alikuwa ndani ya pango akimuabudu Mwenyezi Mungu baada ya kufikiwa na habari za Mitume aliwaendea na kuonesha dini yake.
Basi ni namna gani Qur`ani inasema kuwa watu wa Antokia wana mfalme, na inafahamika kuwa Antokia ilikuwa chini ya utawala wa Roma? Na vipi Habibu Najjar akiwa mchonga masanamu anamuamini Muhammad S.A.W na Muhammad alikuja baada yake kwa miaka mia sita hivi hili linaingia akilini? Na Habibu Najjar si katika wanafunzi wa Shamauun wala Yunus kama ilivyotajwa, kwa sababu Shamauun ni mtoto wa Isaka Ibn Ibrahim, na Yunus au Yona ni mmoja wa Manabii wa Taurati ambaye alimezwa na samaki aina ya papa.
Answer
Kutoka kituo cha tafiti za Kisharia ofisi ya Mufti wa Misri.
Makusudio ya Aya hizi ni kuthibitisha ujumbe wa Mtume wetu Muhammad S.A.W kimekuja kisa hiki ikiwa ni mfano kwa watu wa Makka wa kutumwa Mtume mfano wa Mtume wao S.A.W kwenda umma, na watu hawa waliwapinga Mitume yao na Mwenyezi Mungu akawaadhibu, na sababu ya kutajwa kisa hiki ni kuwazuia kudumu kwenye makosa yao na msukumo kwao wa kuzingatia na kuamini ujumbe wa mbora wa viumbe ili wapate kuokoka na adhaba kama hizi.
Qur`ani haikutaja kuwa watu wa mji huu au kijiji hiki wana mfalme, wala jina la mji huu kuwa ni Antokia, wala jina la mtu ambaye alikuja akitokea maeneo ya mbali na mjini ni Habibu Najjar, na yaliyotajwa na baadhi ya wanatafasiri ikiwa ndani yake ni pamoja na kutajwa hayo ni kwa upande wa jitihada binafsi, haisemwi kuwa Qur`ani imesema hivi, hivyo kwanza tunapaswa kutenganisha kati ya maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na maneno ya yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, yaliyosemwa na baadhi ya wafasiri katika kutafsiri Aya hizi ni jaribio la ufahamu wao wa kusudio la Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha uwezo wa kibinadamu, wanajaribu kuonesha sababu za kisa na watu wake sehemu zake muda wake na mengine kwa njia ya mapokezi ya kihistoria yanayohusiana na kisa, na ndani yake yapo yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, na baadhi ya wafasiri wanategemea njia ya kukusanya kila kilichosemwa kuhusu Aya pasi ya kuangalia tofauti kati ya sahihi na dhaifu lengo likiwa ni kujumuisha yaliyopokelewa, wala hawawezi kutofautisha yanayokubalika isipokuwa wasomi wenye weledi, yaliyopitishwa na wao yanakubalika na yasiyopitishwa yanarejeshwa.
Ama kauli kuwa Antokia katika zama hizi ilikuwa chini ya utawala wa Roma, ni jambo la kuangaliwa kwa sababu linahitaji uthibiti wa kihistoria.
Ama kauli ya Habibu Najjar hakuwa mwanafunzi wa Shamaun wa Yunus bali alikuwa ni mtu anayefanya kazi ya kuchonga masanamu, tunasema: Qur`ani haikusema huyo mtu ni Habibu Najjar, wala haikusema kuwa alikuwa mwanafunzi wa Shamaun wala wa Yunus.
Ama kauli kuwa Habibu Najjar alimuamini Mtume wetu Muhammad S.A.W na kati yao ilipitia miaka mia sita – tuchukulie kuna ukweli waliyoyasema – tunasema: Huenda hili likawa kwa upande kuwa amesoma bishara za Mtume wetu Muhammad S.A.W ndani ya vitabu vya watu wa vitabu na akafahamu kuwa ni Nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu kisha akamuamini bila ya kumuona, na hili ni jambo linakubalika kiakili, au jina la Habibu Najjar linakuwa ni katika upande wa majina yanayofanana ambayo hutumika kuitwa watu mbalimbali.